Chadema: Wafanye nini baada ya shambulio la bomu arusha

makoye2009

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,638
1,218
Ndugu Wana-JF na Watanzania wote wapenda haki,

Nimeguswa sana na nimehuzunishwa sana na tukio la mlipuko wa Bomu kwenye mkutano wa CHADEMA tarehe 15/06/2013 katika kuhitimisha kampeni za Uchaguzi katika Jiji la Arusha. Napenda niwape pole sana ndugu zetu Watanzania(sizungumzii Wanachama wa CHADEMA)waliofiwa na ndugu zao kutokana mlipuko huu wa kinyama ambao kila mtu mwenye akili timamu anaweza kubaini nani yuko nyuma ya mlipuko huu.

Kila mtu anasema lake na yamesemwa mengi,Viongozi wa CHADEMA wamesema na Viongozi wa Serikali ya chama Twawala CCM wamesema ya kwao. Watu wenye hekma wamesikia,wamepima,wametafakari na hatimaye mwisho wa siku ukweli mejitenga.Ni mwendawazimu au kichaa tu ndiye anaweza kukubaliana na kauli ya kwamba CHADEMA walipanga kujiua wenyewe ati waweze kupata huruma ya Wananchi kwenye kura za udiwani!!!!

Nipende tu kuwaomba viongozi wa CHADEMA ngazi ya Taifa kuchukua hatua za haraka,za maksudi au dharura kutokana na tukio hili la Kinyama ambalo hakuna mtu anayeweza kulivumilia.Mambo yafuatayo yanatakiwa yafanyike sasa na haraka ili kwanza kuweka ukweli hadharani lakini kubwa kabisa kuzuia na kukomesha kabisa huu ujinga na upuuzi unaofanywa na Serikali iliyoko madarakani.

  1. Kuanzia sasa Mikutano yote ya CHADEMA iwe ni Kampeni,ya M4C au harambee iwe kwenye mtandao wa kamera za CCTV(Closed Circuit TV) ili kuweza kuangalia kila tukio linalotendeka tangu mwanzo wa mkutano mpaka mwisho. Hii itasaidia kuimarisha ulinzi na kuzuia watu waovu wanaoweza kutumiwa na maadui wa CHADEMA. Naamini kama mtandao huu ungelikuwepo juzi pale Soweto, kesi ingelikuwa imekwisha zamani!
  2. Kuanzia sasa Ulinzi binafsi uimarishwe kwa Viongozi wote wa chama Kitaifa na Wabunge kwa kuwa na Walinzi mahiri(tarined bodyguards)kwa ajili ya Usalama wa Viongozi hawa. Bomu la Soweto liliwalenga Viongozi wa CHADEMA. Tushukru Mungu ameepusha hilo lakini bado likawauawa ndugu zetu Watanzania.
  3. Mwenyekiti wa Taifa,Mhe. Mbowe amezungumzia kuhusu kuwepo mkanda wa Video unao mwonyesha Askari wa FFU aliyerusha lile Bomu na baadaye kukimbia na walw waliopiga risasi raia.mimi nashauri ile Video kwanza ipelekwe kwenye Balozi za USA(Marekani),UK(Uingereza),China,Ufaransa,Ujerumani,Russia,Italy na nchi nyingine zinazotoa misaada kwa Tanzania ili nao waone aina ya Serikali wanayoipa misaada na inachowafanyia raia wake.Lakini pia picha hizi zipelekwe kwenye Taasisi za Kimataifa kama UN,AU,EAC,Umoja wa Nchi za Ulaya n.k. ili dunia ijue nini Serikali ya CCM inafanya.
  4. Mwisho tunaomba uongozi wa CHADEMA Taifa ile picha ya Video ya yule askari wa FFU aliyerusha Bomu pale Soweto akabidhiwe IGP Mwema na wakti huohuo iweke hadharani kwenye mitandao ya kijamii kama YouTube, JF, FaceBook na Twitter ili Watanzania na dunia yote ijue.

CCM wametangaza vita kwa hiyo hakuna kuoneana aibu. Kama wao CCM waliweza kuweka Video fake ya Lwakatare, sasa ni wakati wa CHADEMA kuweka kitu halisi ambacho kimechukuliwa LIVE toka kwenye tukio.

(Tafadhali Moderator usiifute thread hii wala kuichanganya na nyingine,treat it differently please)

Naomba kuwasilisha.
 
Tunalaani kwa nguvu zote watu waliofanya hiki kitendo cha kipuuzi ila tunamwombe Mbowe aache mara moja kuingiza siasa kwenye maswala mazito
 
Kwani kinachoendelea Arusha kina msukumo wa kisiasa au nini? Mambo mazito yepi yako arusha kama sio siasa za kimabavu zinazoendeshwa na ccm?
 
Makoye2009 hakuna haja ya kutafuta msaada kutoka nje katika kukabiliana na hali hii.acha tuendelee hivihivi tutapata majibu tu.
 
Kwanin tusikae na mabango akitua tu huyu Obama anatuona na mabango kibao! Me langu litakua na picha ya kikwete likicheka na ile ya askari akimfwatua Mwangosi bomu la tumbo na itasema! He is smiling and We are dying!
 
ofcause naunga mkono hoja mawazo hayo hata mimi nilifikiria sana kama uwezekano upo bas iko haja ya kwenda hapa walipofikia yatosha sasa
 
Makoye obeja sana guku.

Hata mimi nakubaliana na wewe kabisa.ukipatwa janga kama hili ni lazima ndugu na jamaa wa karibu uwaeleze chanzo cha janga, nakubaliana mkanda huo upelekwe kwa wafadhili wa hii serikali, kama ulivyotaja no.3 na kuhusu namba 2 ni vema sasa cdm iingie gharama ku-train vijana wake katika vyuo makini duniani.
 
Back
Top Bottom