Chadema Wafanye Mkutano mkubwa Dar Haraka maana karibia wakamatwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema Wafanye Mkutano mkubwa Dar Haraka maana karibia wakamatwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ta Muganyizi, Mar 4, 2011.

 1. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #1
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Kwa vile dalilizote zinaonesha kuwa serikali ina lengo la kuwakamata Chadema kwa uhaini, ni vizuri wafanye mkutano mkubwa Dar es Salaam, wahamasishe peoples power ili pindi tu akikamatwa kiongozi yeyote wa Chadema, maandamano yaanzie hapohapo, vilevile naona serikali ya ccm inajiyafutia kifo chake yenyewe. Kwani Chadema hawajafanya uhaini wowote, wanachokiongea ni cha kawaida kabisa, sasa uhaini umetoka wapi? Hali ni mbaya kila mtu anaona. kwa hiyo ni dhambi kusema na kuwaeleza watanzania kuwa hali ni mbaya? Kwa nini watu hawataki kukosolewa? Anayesema hivyo nadhani hajaudhuria mkutano hata mmoja wa CDM. Mie sijaona baya lolote.

  Sasa peoples powerrr iko hivi, mkijidanganya mkawakamata CDM, tunaanzia hapo kuingia barabarani nchi nzima. Naomba ufanywe nkutano mkubwa Dar fasta maana mambo yote yanaweza kuanzia hapo. Serikali muache vitisho ....... sasa wakamateni CDM muone .................cha .........moto.
   
 2. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #2
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Kwanini serikali mnaogopa kama mna uhakika kwamba hamjawakosea wananchi??? ahaghgggggggggggghh
   
 3. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,143
  Trophy Points: 280
  Ikiwa viongozi wa Chadema turufu yao wanayoitumia ni maandamano basi wajuwe hawana ubunifu wala muelekeo.

  Kwa upande wangu, naona hata JK bado anawabembeleza sana. Laiti ningekuwa mimi ndie nnaongoza, saa hizi kusingekuwa na kiongozi wa Chadema anatembea mitaani kuhamasisha uvunjifu wa amani.

  Ingekuwa kweli wanayoyasema yote yana ukweli wangetumia njia za amani na si hizi za kuandamanisha watu kwa majungu.

  Nasema, serikali iwashughulikie kisheria hawa waanzisha fujo haraka iwezekanavyo. Kwa nini inawaona wanaanzisha maandamano yasiyo na maana yoyote halafu inawaacha tu waendelee? Serikali iwafungulie mashitaka ya uvunjaji wa amani haraka iwezekanavyo.
   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  serikali yenu omba-omba haina ubavu wa kukamata na kuwaweka vizuizini viongozi wa upinzani. labda mtu wenu awe ameacha mchezo wake wa kusafiri kila wiki kwenda kucheka-chaka na kina Sarkozy
   
 5. m

  mob JF-Expert Member

  #5
  Mar 4, 2011
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 509
  Trophy Points: 280
  kuna quote moja kwenye gazeti la mtanzania la leo ni nzuri sana (iko kwenye ukurasa wa mbele)nikilipata nitaanzisha thread. ok by the way kila mtu ana haki ya kutoa mawazo yake,hivyo basi kwa kuwakamata viongozi wa chadema kutachochoa machafuko zaidi na kusababisha vurugu zisizo na maana,kwa kuwa chadema wanaongelea hali halisi ya watanzania kwa nini viongozi wetu wanakwepa hoja na kujaribu kukemea na kukurupuka.
   
 6. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwani ameonana na Sarkozy....!!!!!!,sidhani.....huyo rais Sarkozy ana kazi nyingi sana siyo kuhudhuria mikutano ya NGOs
   
 7. M

  Marytina JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Dar ni sehemu yenye siasa za kinafiki sana, siwatukani wakazi wa Dar ila ukweli ni kwamba ni vigeugeu hata ndani ya sanduku la kura,
  Kuna jirani aliwahi kuniambia ukitaka kupigwa kubali kuwa wakala wa CUF kwenye uchaguzi lazma utaambiwa umeuza kura kumbe wana CUF wenyewe (Mbagala na Temeke) wakiingia ndani hawawapigii kura watu wao.

  Hamshangai CUF hawajai kuwa na mbunge Dar, Dar is all about CCM VOTERS hasa kwa wanaojiita wazawa, ubungo na Kawe kuna upinzani kwa kuwa kuna wahamiaji wengi wa miaka ya karibuni.

  STATERGICALLY DAR SIO MAHALI PA CDM wala CUF kuwekeza nguvu nyingi.
   
 8. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #8
  Mar 4, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Ni kweli wewe sio JK lakini akili kama mnafanana vile

  Pili tuambie wapi kanda ya ziwa umesikia uvunjifu wa amani baada ya polisi kukubali kulinda mkutano badala ya kuanzisha vurugu.

  Chadema hawajaanzisha fujo popote na ushahidi upo, serikali ikijifanya kuwashugulikia yenyewe ndio itaanzisha fujo. Ni haki ya kikatiba ya chama cha siasa kufanya maandamano na mikutano ya siasa, ulikuwa hujui hilo tutakucheka.

  Ni lipi kati ya wanayosema Chadema halina ukweli? Naomba unitajie. Dowans kampuni ya Kikwete na akina Rostam mtanzania gani anapenda ilipwe? , gharama za maisha hazijapanda?, uchumi haujaporomoka? ufisadi haujaongezeka?.

  Wewe ni mtanzania kweli? Endelea kulala tukifika tutakuamsha.
   
 9. s

  smz JF-Expert Member

  #9
  Mar 4, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wewe naona ni wale wale, Chama cha siasa chochote makini kama kilivyo CDM ni kuhuhubiri siasa. Kwa chama cha cha upinzani kazi yake kubwa ni kuikosoa serikali iliyoko madarakani. Siyo kazi ya upinzani kuisifia serikali iliyoko madarakani.

  Ili uongee na wanachama huwezi kuwafuata mmoja mmoja nyumbani, ni lazima uwakusanye, uwahamasishe na uwaeleze madhaifu ya serikali iliyoko madarakani. Taabu chama tawala kilizoea siasa za wakati wa uchaguzi tu, kinaachwa kipindi chote hiki kinafanya kinavyotaka. Uwajibikaji kwa waajiri wao - yaani wananchi unakuwa hakuna.

  Siasa ni kuvumiliana, na hasa kwa chama kilichoko madarakani lazima wakubali kukosolewa na yule anayewakosoa asionekane kama mhaini, kwanza anawasaidia kujirekebasha.

  Hayati Mwl Nyerere aliwahi kusema enzi za uhai wake kwamba: Vyama vya Upinzani ni VIOO vya ccm. Inajiangalia kupitia ukosoaji na kutumia muda huo kujirekebisha.

  Vyama vya upinnzani ni sawa na mcheza mpira aliyeko Benchi. Ukivurunda tu unaona mtu "ana-troti",(anapiga jaramba), ndivyo CDM wanavyofanya, cha msingi ccm wakaze buti kutatua kero za msingi za waTZ, wanaweza wakacheza hadi dk ya 90. Vinginevyo wachezaji wa akiba tunao wengi, na pengine ni wazuri kuliko waliomo uwanjani kwa sasa.
   
 10. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #10
  Mar 4, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,595
  Likes Received: 4,709
  Trophy Points: 280
  Akupe nani uongozi wakati wewe ni kipofu?
   
 11. M

  Mabulangati JF-Expert Member

  #11
  Mar 4, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 779
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Mpaka sasa sijaona mtu wa Dar anayeweza kuandamana kisa kiongozi fulani kakamatwa Arusha sawa sababu mnazijua. Kingine sioni chadema inachofanya katika maandamano kama kafulila alivyosema serikali inaifagilia chadema bure. chadema wanachojua ni lawama, dowans, epa na kutafuta kuonewa huruma, nasema hivi kwa kuwa sijawahisikia wakihamasisha watu kufanya kazi, wakihamasisha vijana kupambana na uhalifu hasa wanapokua wameajiriwa sehemu yoyote bila kujali itikadi zao, vijana kuungana kuikomboa nchi kutoka utumwani.

  CHADEMA wajipange upya waje na new strategies za kupambana na malaghai yanayoiangamiza nchi yetu. Strategy ya kucheza na hisia za watanzania zinaanza kuwachosha watu na kuwafanya ccm wawe sugu. Waje na mbinu nyingine kuaibisha madhalimu. Mfano mzuri ni kutumia fedha wazotumia kwa maandamano kutunisha mifuko ya maendeleo katika majimbo yao kama walivyoanza Mh. Lema na baadhi ya wabunge wengine.

  Muda wa majungu ya siasa umepita sasa tutumie majungu ya kisayansi kuijenga nchi na kuaibisha madhalimu. kwa mfano tufanye liwezalo kumsahuri rais katika kupata wakurugenzi wa idara nyeti kwa kutumia misingi ya kitaalamu na siyo kisiasa kama kiongozi wa TAKUKURU, Usalama wa Taifa (CID), Tume ya mipango, tume ya haki za binadamu, tume ya uchaguzi, msajili wa vyama vya siasa nk pia kuondoa taasisi zisizokua na sababu ya kuwepo yaani zinazofanya kazi zinazoingiliana kama mkukuta, mkurabita nk. pia kwa maslahi ya nchi katika kupanga muundo wa serikali, muundo wa mahakama. Haya yote ni hujuma kwa madhalimu na mwisho wake ni kuwadhalilisha bila kujali wanatokea chama gani cha kisiasa maana wanasiasa wote lao sawa ila mipango ndiyo tofauti.
   
 12. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #12
  Mar 4, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Hakuna kitu kama hicho kwani wakamatwe kwa kosa gani? dar tutafanya maandamano tu kufuatana na ratiba yeu!
   
 13. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #13
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  Kila siku ccm na viongozi wake wanahubiri kwamba watanzania si wajinga, sasa vipi tena wanaandamana kwamba maisha magumu. Tafakarini tafadhali. Basi waheshimu waerevu wanaoandamana
  .
   
 14. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #14
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  duh kwa hali hii mie naona watz wakubali tu kwamba ni maskini basi. Msijitingishe kaeni hivyo hivyo. Acheni wenye kula wale, ukipata nafasi pa kuitafuna nchi tafuneni maana watu kama wameridhika na hali iliyopo aghhhhh.
   
 15. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #15
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Katika yoote uliyoongea nimekuheshimu sana penye red. Kikwete ndo anataka kuvunja amani ya nchi hii, sisi tuna sheria zetu akitokea mtu anahatarisha amani yetu apelekwe mahakamani kujibu makosa yake kisheria siyo malalamiko utadhani mwimbaji wa taarabu, kikwete ana ni-let down mwanaume mwenzake
   
 16. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #16
  Mar 4, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  dar cha mtoto bana kwenye kupiga kura hawana lolote hakuna umuhimu wa kufanya mkutano dar vijijini ndo wanahitaji kuamshwa sasa maana bado kuna watu wanajua ccm ni ya nyerere ndo mana wanaichagua so big up cdm kazeni buti kuwaamsha hao wa mashambani kitaeleweka tuuu!!
   
 17. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #17
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180


  Nadhani umejaza maneno mengi tu...ngoja nikusasahishe, hayo hayo uliyonena kwa ujumla wake ndio katiba mpya ambayo CHADEMA ndio vinara wa kuilazimisha serikali ifanye mchakato wa kuipata kwa manufaa ya wananchi wote...we vipi bana!!!!
   
 18. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #18
  Mar 4, 2011
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,212
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  Kwani kazi ya chama cha upinzani ni nini? Sio kuikosoa serikali, na pale inapoonekana haiwezi, kuishinikiza ijiuzulu?

  CDM ina wajibu, wa kikatiba, kuikosoa serikali ya CCM, na pale inapoonekana serikali haikosoleki, kuishinikiza ijiuzulu.

  Njia ya kawaida ya amani, ya chama cha upinzani kuishinikiza serikali iachie ngazi (kama serikali ikionekana kushindwa kuongoza), ni ipi? Sio maandamano ya amani?

  Naona wanaopinga maandamano ya amani ya CDM wana lao. Wanataka kuleta vurugu.
   
 19. f

  furahi JF-Expert Member

  #19
  Mar 4, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 947
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Its true, hata mimi nimesikia huo mkutano haukuhudhuriwa na Rais yeyote zaidi ya JK!
   
 20. M

  Mchili JF-Expert Member

  #20
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  CDM wakamatwe kwani wamekosa nn?? Wanaongea na wananchi kuhusu natatizo yao na jinsi serikali inavyotakiwa kuyashughilikia. Mbona ccm mnaogopa kivuli chenu?? CCM wamezoea kuwadanganya wananchi sasa wanapoona wanaelezwa ukweli wanachachawa.
  Go go gooooooooooo CDM
   
Loading...