CHADEMA waelezea kilichotokea siku ya tukio la kuuwawa kwa Daudi Mwangosi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA waelezea kilichotokea siku ya tukio la kuuwawa kwa Daudi Mwangosi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 6, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145


  [​IMG]
  Mkurugenzi Wa Mafunzo Taifa Benson Kigaila akielezea tukio lilivyokuwa kwa waandishi wa habari leo.
  ---
  Na Francis Godwin, Iringa.


  Ikiwa ni siku tano zimepita toka kuuwawa kwa mwandishi wa habari wa channel ten na mwenyekitiwa klabu ya waandishi wa habari Iringa Daudi mwangosi katika vurugu baina ya polisi na CHADEMA huko nyororo mafinga.


  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo kupitia viongozi wake Iringa wameongea na waandishi wa habari kuhusu kile kilichotokea.


  Akiongea na waandishi wa habari Iringa leo Mkurugenzi wa mafunzo na operesheni ya Movement For Change Taifa Benson kigaila, ameeleza kuwa lengo kubwa la Chadema tarehe 2.09.2012 kule Nyororo walikuwa na lengo la kufungua matawi na kufanya vikao vya ndani na wanachama wao na sio kufanya mikutano ya hadhara kama inavyosemekana.


  Aliendelea kuleleza kuwa wakiwa katika ufunguzi wa tawi katika ofis ya kata Nyororo Polisi wafika na kutangaza kuwa watawanyike na wakamueleza RCO kuwa wapo kwaajili ya kufungua tawi na kufanya kikao cha ndani na kwamba polisi wakiingilia ndio watakao kuwa wanachochea vurugu.


  Aidha Kigaila ameongeza kuwa wakati huo huo wakifungua Tawi hilo vyama vingine kama CCM nchi nzima walikuwa wakifanya chaguzi katika ngazi za Wilaya lakini hawakuzuiwa kwa kile kinasemwa kuwa ni kuingilia zoezi la sensa.


  Baada ya kufanikiwa kufungua tawi walitangaza kuwa wanaelekea ofisi ya kata ili wakafungue tawi lingine lakini alipoingia RPC Kamuhanda ndipo alipoagiza na kusema kuwa hakuna kuzindua tawi ni kutawanisha watu na kufunga mkutano" alisema Kigaila.


  Wakati wakielekea katika ofisi ya kata Marehemu mwangosi alimueleza kigaila kuwa anawasiwasi alipokuwa akirekodi wengi wa polisi wanaonekana si wa Iringa jambo ambalo anaeleza kuwa ndicho chanzo kikuu cha kuuwawa kwake. Huku akihoji kuhusu kamera na laptop za marehemu kutoonekana na kutotolewa taarifa mpaka sasa.

  Naye katibu mkuu wa Zanzibar Hamadi Yusufu akielezea maneno ya mwisho ya marehemu alisema kuwa marehemu alikuwa akilalamika kuwa wamwachie kwani yeye yuko kazini wasimuue kwani anatekeleza majukumu yake " Jambo ambalo polisi hao hawakuliktilia maanani nakuendelea kumpiga mpaka umauti ulipomfika.  Aidha Hamadi ameeleza kuwa wao kama viongozi walikuwa katika tukio hilo wako tayari kutoa ushaidi mbele ya tume huru itakayoundwa na si Tume iliyoundwa na Jeshi la polisi au Waziri Nchimbi kwasababu kwa macho yao waliona polisi ambao wanasimamiwa na wizara yake wakitekeleza dhana hiyo.


  Katibu wa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) Deogratias Munishi ameeleza "Kuhusu kauli ya Msajili ya Vyama John Tendwa kuwa haina maana kwani alitegemea yeye kama mlezi wa vyama vya siasa angefika katika eneo la tukio ili aweze kuwa na ajionee hali halisi vyama anavyovilea yeye vikinyimwa fursa ya kufanya kazi zao kama vyama vya siasa"

   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  MZEE TENDWA AOMBE SANA MUNGU AMJALIE HEKIMA NA UJASIRI WA KUWEZA KUJITENGA NA U-KADA WAKE KULE CCM PINDI ANAPOTEKELEZA MAJUKUMU YAKE YA U-REFARII KWA VYAMA VYA SIASA NCHINI ILI OFISI YAKE IWEZE KUENDELEA KUHESHIMIKA NA WALA SI KULE KUTAFUT KUOGOPEKA KITU

  Mpaka hivi sasa mlezi wa vyama vya siasa nchini, John Tendwa, wala hajua hata kule kulikotokea mauaji na hata akapata taarifa za moja kwa moja toka kwa mashuhuda watukio lenyewe, yeye akiwa amekaa kwenye kiyoyozi ofisini Dar es Salaam tayari keshakimbilia kufunua ukurasa katika vitabu vya sheria na kutoa tamko la kukihuku CHADEMA.

  Taswira inayojengeka kwa umma hadi hapo tu ni kwamba yeye alikua anaendelea tu kuigiliza katika eneo ambalo alikabidhiwa na CCM atekeleze bila hata kujua kama kweli mwanamaigizo wa kwanza ambaye ni jeshi la polisi kama walikamilisha eneo lao murua bila kuondoka na masizi usoni kama ambavyo ilivyo hivi sasa kwa kashfa nzito huko mkoani Iringa, pengine tofauti na matarajio kwao.

  Hadi hapa ni vema ikafahamika kwa hii taasisi ya usajili wa vyama vya siasa nchini akiwemo mtendaji wake mmojawapo Mzee John Tendwa kwamba CHADEMA HAKITEKELEZI MAJUKUMU YAKE YA KICHAMA NCHINI KUTOKANA NA HISANI YA KUKARIBISHWA NA MTU YEYOTE WALA TAASISI.

  Ukweli waa mambo ni kwamba chama hiki (CHADEMA), sawa tu na vyama vingine vy siasa nchini, kina HAKI SAWA NA CCM PAMOJA NA VYAMA VINGINE nchini hivyo kuendelea kuundiwa mizengwe na kuzidi kutikisiwa kiberiti ni jambo ambalo kamwe halikubaliki hata kidogo kisheria.

  Kama Tendwa anaona kuna jambo CHADEMA kimekosea aidha wakijadili kwa uwazi au akipeleke mahakamani na wala si kubembelezana.

  Kama hoja ni kufanya shughuli ya kisisa (Mkutano wa ndani) siku za ziada za sensa basi hata CCM kilikua na jambo kama hilo hilo tena mkutano wa nje Bububu; kwanini hili la CHADEMA ndio ilete nongwa mezani kwake?????????
   
 3. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  Benson Singo Masalamakali Kigaila,mkuu wa oparesheni ya M4C akiongea na waandishi leo Iringa


  Ikiwa ni siku tano zimepita toka kuuwawa kwa mwandishi wa habari wa channel ten na mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari Iringa Daudi mwangosi katika vurugu baina ya polisi na CHADEMA huko nyororo mafinga.
  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo kupitia viongozi wake Iringa wameongea na waandishi wa habari kuhusu kile kilichotokea.
  Akiongea na waandishi wa habari Iringa leo Mkurugenzi wa mafunzo na operesheni ya Movement For Change Taifa Benson kigaila, ameeleza kuwa lengo kubwa la Chadema tarehe 2.09.2012 kule Nyororo walikuwa na lengo la kufungua matawi na kufanya vikao vya ndani na wanachama wao na sio kufanya mikutano ya hadhara kama inavyosemekana.
  Aliendelea kuleleza kuwa wakiwa katika ufunguzi wa tawi katika ofis ya kata Nyororo Polisi wafika na kutangaza kuwa watawanyike na wakamueleza RCO kuwa wapo kwaajili ya kufungua tawi na kufanya kikao cha ndani na kwamba polisi wakiingilia ndio watakao kuwa wanachochea vurugu.
  Aidha Kigaila ameongeza kuwa wakati huo huo wakifungua Tawi hilo vyama vingine kama CCM nchi nzima walikuwa wakifanya chaguzi katika ngazi za Wilaya lakini hawakuzuiwa kwa kile kinasemwa kuwa ni kuingilia zoezi la sensa.
  Baada ya kufanikiwa kufungua tawi walitangaza kuwa wanaelekea ofisi ya kata ili wakafungue tawi lingine lakini alipoingia RPC Kamuhanda ndipo alipoagiza na kusema kuwa hakuna kuzindua tawi ni kutawanisha watu na kufunga mkutano” alisema Kigaila.
  Wakati wakielekea katika ofisi ya kata Marehemu mwangosi alimueleza kigaila kuwa anawasiwasi alipokuwa akirekodi wengi wa polisi wanaonekana si wa Iringa jambo ambalo anaeleza kuwa ndicho chanzo kikuu cha kuuwawa kwake. Huku akihoji kuhusu kamera na laptop za marehemu kutoonekana na kutotolewa taarifa mpaka sasa.
  Naye katibu mkuu wa Zanzibar Hamadi Yusufu akielezea maneno ya mwisho ya marehemu alisema kuwa marehemu alikuwa akilalamika kuwa wamwachie kwani yeye yuko kazini wasimuue kwani anatekeleza majukumu yake “ Jambo ambalo polisi hao hawakuliktilia maanani nakuendelea kumpiga mpaka umauti ulipomfika.
  Aidha Hamadi ameeleza kuwa wao kama viongozi walikuwa katika tukio hilo wako tayari kutoa ushaidi mbele ya tume huru itakayoundwa na si Tume iliyoundwa na Jeshi la polisi au Waziri Nchimbi kwasababu kwa macho yao waliona polisi ambao wanasimamiwa na wizara yake wakitekeleza dhana hiyo.
  Katibu wa Baraza la Vijana Chadema(BAVICHA) Deogratias Munishi ameeleza “kuhusu kauli ya Msajili ya Vyama John Tendwa kuwa haina maana kwani alitegemea yeye kama mlezi wa vyama vya siasa angefika katika eneo la tukio ili aweze kuwa na ajionee hali halisi vyama anavyovilea yeye vikinyimwa fursa ya kufanya kazi zao kama vyama vya siasa”
   
 4. s

  sad JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2012
  Joined: Aug 26, 2012
  Messages: 295
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  huo ndio ukweli wana c.c.m wanatapatapa tu. wameua na kila mtu mitaani anajua hilo
   
 5. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #5
  Sep 6, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,199
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Tokea wamwage damu Igunga Arumeru morogoro na Iringa ni ishara tosha ya ccm kuaga
   
 6. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #6
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Uwezo Tunao MZEE TENDWA NI WAKALA WA NYINYIEM. MIE SINA HATA MUDA WA KUMSIKILIZA COZ HANA HOJA! TO HELL CCM! Bye!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #7
  Sep 6, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Inasikitisha sana kuona watz wasiokuwa na hatia wakiuawa kinyama, lakini ni funzo kwa watz kutumia silaha yao ya kura kuuweka uongozi bora madarakani tofauti na sasa ambapo wengi hatujitokezi kupiga kura nyakati za uchaguzi.
   
 8. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #8
  Sep 6, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Kuna picha ipo humu JF inamuonesha marehemu yupo pembeni ya gari ya Chadema Fusso watu wanagombania kupanda ilikuwa wapi? Fusso hiyo imebeba spika mbili kubwa.

  RIP Daudi Mwagosi.
   
 9. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #9
  Sep 6, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Makamanda naombeni mnifahamishe huyo kwenye picha aliyevaa kofia nyekundu ni nani.
   
 10. S

  SHEMGUNGA JF-Expert Member

  #10
  Sep 6, 2012
  Joined: Jan 13, 2012
  Messages: 653
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  chichiemu kwa heri!
   
 11. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #11
  Sep 6, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Tendwa futa futa hawa wachochezi
   
 12. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #12
  Sep 6, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hivi msajili wa vyama vya siasa anachaguliwa vipi!
   
 13. N

  NG'ONGOVE Senior Member

  #13
  Sep 6, 2012
  Joined: Apr 28, 2012
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unajua kwa umri wa mh Tendwa ukilinganisha na matamko yake unaweza kutenda dhambi bure, bora kum-ignore tu
   
 14. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #14
  Sep 6, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,583
  Likes Received: 1,949
  Trophy Points: 280
  Benson singo Masalamakali Kigaia ni kamanda wa ukweli.Kama yeye ndo anairatibu na kutoa mafunzo kwenye hii m4c,basi nampa zake hongera.Job well done kamanda,nchi hii kweli inakombolewa.Halafu kuna yule Simbaya,watu wamejitolea its just a matter of time.
   
 15. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #15
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,355
  Likes Received: 22,216
  Trophy Points: 280
  Hivi kweli Tanzania ni kisiwa cha amani?
   
 16. J

  JAPHETtumpa Senior Member

  #16
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mzee tendwa amefilisika kibusara hana hata uwezo wa kujisikiliza ukiona hivyo ujue tumefika pabaya swali alifikaje hapo kwa sababu kwa maneno yake haya na mengine aliyowahi kuyasema inadhihirisha wazi kwamba he is not of right mental capacity shem on him cant he afford any sense of objectivity? Tunamwitaje mtu kama yeye ni msaliti wa umma wa watanzania au ni mjinga. Tendwa na office yake ni sehemu ya matatizo tulionayo kama jamii
   
 17. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #17
  Sep 6, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,636
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Nilitegemea kusikia jipya,bado maswali yangu hayajapata jibu sahihi kuhusu maelezo kuwa marehemu aliwafuata polisi na nini ilikuwa dhamira yake,ukiondoa askari mmoja je kuna mwananchi mwengine aliyejeruhiwa katika purukushani hiyo?. Inaonekana pande zote zilizohusika(CDM+POLISI) katka tukio hazikuwa na nia njema na sasa hivi nafsi zao zinajuta na kuanza kutupiana mpira.
   
 18. h

  hans79 JF-Expert Member

  #18
  Sep 6, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Ukiisha mjua ili mmuuwe,endeleen tu kunyonya damu.
   
 19. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #19
  Sep 6, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndiyo maana nimegundua kwa nini yule jamaa wa Ivory cost aling'ang'ania madaraka pamoja na kushindwa. Yaani mfumo wa CCM ni wa kirafi kuanzia kwa balozi mpaka kwa rais. Siipendi nchi yangu, yaani siku nikipata uwezekano wa kutoka nje ya nchi si rudi ng'o. Labda mpaka CCM waondoke madarakani na JK afe. Maana ktk historia ya nchi huyu jamaa ni kituko!
   
 20. u

  utantambua JF-Expert Member

  #20
  Sep 6, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wana Nyololo wameingia kwenye historia ya ukombozi...kama Soweto ilivyo kwa South Africa
   
Loading...