asante umemweleza vema kabisa.Mkuu, shetani ni shetani tu, hata ukimsifu na kumuabudu lengo lake kubwa ni kukuangamiza ili uishie kwenye mauti na kuzimu. Ndiyo! Anaweza kukupa burudisho kupitia anasa na raha za maisha ya kidunia lakini moyoni mwake anatambua fika unakwenda kuangamia.
CCM ni kama shetani tu, inajiona ndiyo pekee yenye hati miliki ya kushikilia dola, iwe kwa halali ama hata kwa njia batili. Starehe na "peace of mind" kwake ni kuona ikishindana na vyama dhaifu vya ushindani.
Hata kama Madam President akimaanisha kufanya mazungumzo na CDM, bado mfumo ndani ya chama chake hautakubaliana naye. Yeye ni "figurehead" tu ndani ya chama chake, na wala hana uwezo wa kufanya "ultimate decision" ijapokuwa yeye ndiye mwenyekiti taifa.
Visitafutwe visingizio kupitia CDM. CCM haina nia ya dhati ya kutaka kufanya mazungumzo na vyama vingine, inatambua vyema kuwa hakuna "fair political landscape" hapa nchini. Na jambo hilo ndilo pekee lenye kuihakikishia usalama wake wa kuendelea kushika dola.
Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app