Uncle Jei Jei
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,684
- 2,157
Mwanzoni wakati Rais Samia anapokea madaraka makundi mengi yalionekana kumuunga mkono wakiwemo CHADEMA
Bahati mbaya sana baadhi yetu tulitaka mabadiliko ya ghafla kwenye kila kitu kana kwamba nchi ilikuwa imetoka kwenye mapinduzi ya uongozi
Walioteswa na urais wa Magufuli hasa CHADEMA walitaka madiliko ya ghafla sana hata kabla msiba haujaisha kitu ambacho kilikuwa kigumu sana
Rais Samia alichukua madaraka baada ya msiba wa Rais hakuchukua madaraka kwa mapinduzi! Kama binadamu, Magufuri alikuwa na familia, wafuasi, waliompenda na waliomchukia! Alikuwa mwanachama wa CCM ambapo walikuwemo waliompenda na waliomchukia.
Hayo yote yalitosha kuwapa changamoto CHADEMA ya kwenda taratibu katika kutafuta mabadiliko kupitia Rais Samia
Haiwezekani na isingewezekana Rais Samia ndani ya kipindi Kifupi kuwaponya wote waliojeruhiwa na Magufuri! Huu ungeonekana Kama usaliti! Labda angekuwa ameingia kimapinduzi
Yanasemwa mengi kwamba hata utaratibu wa kutaka kuonana na Rais ili kufanya mazungumzo waliovuruga ni CHADEMA wenyewe! Kutaka kujipangia na kulazimisha kila kitu
Tangu Magufuri afariki hata mwaka haujapita lakini ndani ya kipindi hiki Kifupi tayari CHADEMA walianza kukimbizana barabarani kudai Mambo mengi sana ambayo hawakuyafanya kipindi Cha Magufuri! Unadhani system ingekubali tu Mambo yaende hivyo?
CHADEMA walishindwa nini kujipa na kumpa muda Rais Samia ili wapimane?
Wangeweza kutumia busara ya kawaida tu kwa kujipa muda angalau wa mwaka mmoja huku wakifanya juhudi za kimya kimya kurekebisha Mambo halafu waone Kama mabadiliko yangetokea au laa!
Kuna wakati unaweza kukosa unachostahili kwasababu ya style uliyotumia kuomba au kudai kitu hicho! Hiki ndicho kilichowapata CHADEMA!
Wanakurupuka kwa kila Jambo! Hawako smart kudai haki! Wanataka kulazimisha ili tu waonekane washindi. Wanasahau kwamba hata ukidai haki kistaarabu bado jamii itakutambua tu!
CHADEMA wanatukosea sana watanzania, wanaendesha Mambo yao kana kwamba wao ndo wanajua kila kitu, kila wanachowaza ni sahihi tu, wanaweza kujipangia wafanye nini na kumpangia Rais afanye nini na asifanye nini. Hii sio sawa!
Naamini Kuna watu wenye busara ndani ya CHADEMA! Hawajachelewa. Watumia mlango wa nyuma kurekebisha mambo. Sio lazima kila kitu kiletwe kwenye public! Mambo mengine wakubwa hawapendi kuyaona hadharani! Mnamalizana huko huko sisi wananchi tunaona mabadiliko tu!