Chadema wadaiwa kuwapa rushwa viongozi jumuia ya watanzania waishio washington dc | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema wadaiwa kuwapa rushwa viongozi jumuia ya watanzania waishio washington dc

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Aug 27, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 27, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  CHADEMA WADAIWA KUWAPA RUSHWA VIONGOZI JUMUIA YA WATANZANIA WAISHIO WASHINGTON DC KUFANIKISHISHA MNUSO, JUMAMOSI HII  [TABLE="class: tr-caption-container"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption, align: center"]UONGOZI DMV[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  WASHINGTON DC
  MWENYEKITI, Katibu na Mweka hazina, wa Jumuia ya Watanzania waishio Marekani, wanashutumiwa na wanajumuia wa Washignton kuwa wamepokea rushwa kutoka kwa Chadema kwa ajili ya kufanyia pickic na party ya usiku, vitakavyofanyika Jumamosi hii, Agosti 25, 2012.

  Habari za madai za shutuma hizo zinasema kuwa Jumuia ilikuwa na fedha taslim zisizozidi Dola 2000 za Marekani zinazotosha kufanya party ya mchana ya picnic peke yake, lakini kwa cha kushangaza wakati wanajumuia wakiwa wanahoji kwa nini party ya usiku ifanyike wakati Jumuia haina fedha za kutosha, Viongozi hao wameweza kuja na fungu kubwa la fedha ambazo watazitumia kufanya party zote mbili kubwa na za kifahari zitakazoambatana na chakula na vinywaji mchana na usiku bure.

  Kama haitoshi kutokana na fungu hilo, pombe zitakuwa za bure hadi saa nane usiku, wakati ukumbi na muziki vikiwa vimelipiwa kwa Cash siyo mkopo.

  "Habari za kuaminika na ushahidi upo zinasema kuwa Katibu wa Jumuia Bwana Amosi Cherehani ni Mweka hazina wa Chadema Washigton na ndiye ambaye ameweza kuhamasisha fedha hizo kutoka Chadema iliziweze kufanya hafla hiyo", Imsema taarifa iliyotumwa kwa mtandao kutoka Marekani.

  "Wananchi wanahoji kwa nini Mwenyekiti ambaye alichaguliwa kwa kishindo ameweza kukubali kadia hii wkati Jumuia haifungamani na chama chochote cha siasa?" Imehojiwa katika taarifa hiyo.

  "Kutokana na kadhia hiyo, wakereketwa wa Jumuia wameipa Mamlaka Kampuni ya ERNEST & YOUNG kufanya "INDEPENDENCE AUDITING" ya Jumuia ili kujua "INCOME AND EXPENDITURE za Jumuia yao zometoka wapi na zimetumika vipi kabla ya hatua zaidi kuchukuliwa", Taarifa imesema.

  Tarrifa imesema wanajumuia wanaomba kuitisha mkutano ili kupiga kura a maoni ya kutokuwa na imani na uongozi kwakuwa bado mchanga. .."Na tuliuchagua kwa imani, hatutaki vyama vya siasa vituingile...Rushwa ni adui wa Haki"

  POSTED BY: BASHIR NKOROMO AT WEDNESDAY, AUGUST 22, 2012
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Aug 27, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  Kweli CCM wanajua kuchezea WANANCHI... Hawasemi JINSI wanavyopigania pesa za CCM - DMV?

  Wanaongelea ERNEST YOUNG AUDIT mbona hawafanyi hizo AUDIT nyumbani? AU KULETA PESA ZA USWISI?
   
 3. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #3
  Aug 27, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Wabongo rudini nyumbani tu kuna biashara za kutosha USD 2000(Sawa na Tshs 3,200,000) ni hela kiduchu na mtachezewa sana na hao jamaa wa CDM wanaopewa hela za bure na wafadhili wao.
  Ajabu ni kwamba hela zote wanazopewa ni za kufanya vurugu tu, maandamano na chaos.
  Leo wamewapeleka wafuasi wao machinjioni huko morogoro ili kupata political capital.
   
 4. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #4
  Aug 27, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ondoa ***** hapa,waulize wanamorogoro nani mwenye makosa leo?DAMU ILIYOMWAGIKA LEO IMEPANDA MBEGU KWA UZEMBE NA UDHAIFU WA CHICHIEEEEEEEEEM.
   
 5. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #5
  Aug 27, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Si kaandamane na wewe ili uonje joto ya jiwe.Peoplespower halafu vigogo wanaulaza walivyowaoga.
  Fuata sheria and everything will be allright.
   
Loading...