CHADEMA wachoma khanga za rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA wachoma khanga za rushwa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by BASIASI, Oct 20, 2010.

 1. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2010
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,116
  Likes Received: 351
  Trophy Points: 180
  CHADEMA wachoma khanga za rushwa
  • Zilitolewa na Mama Kilango kwa wananchi

  na Grace Macha, Same


  [​IMG] CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimechoma khanga zinazodaiwa kutolewa bure kwa wananchi na mgombea ubunge wa jimbo Same Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Anne Kilango Malecela.
  Khanga hizo za rangi nyekundu, njano na nyeusi zenye maandishi “upendo ni nuru ya maisha” zilikabidhiwa kwa uongozi wa CHADEMA na kina mama wanne ambao walidai pamoja na wananchi wengine waligawiwa na Kilango kwenye kata yao ya Maore kama rushwa, ili wampigie kura siku ya uchaguzi.
  Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki kwenye kijiji cha Mafigiro, kata ya Mtii wakati wa mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia CHADEMA, Nagenjwa Kaboyoka.
  Akizungumza kwenye mkutano huo, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA), mkoani Kilimanjaro, Deo Munishi, ambaye ndiye aliyezichoma khanga hizo alisema kitendo hicho kitampelekea ujumbe sahihi Kilango kuwa wananchi wa jimbo hilo kwa sasa hawadanganyiki.
  Alisema kitendo cha Kilango kutoa rushwa kwa wananchi ili wamchague inaitia doa hata tuzo aliyopewa na ubalozi wa Marekani kama mwanamke jasiri anayepambana na vitendo vya rushwa nchini.
  Munishi alisema wameshapeleka malalamiko yao mara kadhaa kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini, (TAKUKURU) juu ya vitendo vya rushwa vinavyafanywa na Kilango ambapo mbali ya kugawa khanga, lakini pia amekuwa akitoa fedha taslim kwa wananchi yeye binafsi na kupitia mabalozi wa CCM lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
  “TAKUKURU wanafanya kazi kama taasisi ya CCM kwa sababu tunawapelekea malalamiko tunawaita waje wamkamate Kilango wakati akigawa kanga na fedha taslim shilingi elfu tano na elfu 10 lakini hawatokei badala yake wanatushauri twende kwenye kamati ya maadili ya tume ya uchaguzi sisi tunahoji mbona wakati wa uchaguzi ndani ya CCM walikuwa wanawakamata?” alisema Munishi.
  Aidha alilaani kitendo cha mgombea huyo wa CCM kutoa ishara za matusi ili kuikejeli ishara ya vidole viwili inayotumiwa na CHADEMA, jambo alilosema kuwa kama mzazi hawakumtarajia kufanya hivyo.
  Naye mgombea ubunge wa jimbo hilo, Kaboyoka aliwataka wananchi hao wampe kura ili aweze kushiriki kikamilifu katika kuwatatulia matatizo ya maji pamoja na kuwainua kiuchumi kwa kuwaibulia miradi ya maendeleo.
  Alisema kama aliweza kushirikiana nao katika shughuli hizo ikiwemo kuwafungulia vijana karakana ya useremala kabla hawajampa uongozi basi wakimchagua watarajie kuibuliwa miradi mingine mingi.
  Kwa upande wake Kilango akijibu hoja hizo alikiri kugawa khanga kwa vikundi vyake vya hamasa kwa kile alichoeleza kuwa kuna ugeni wa mgombea mwenza, Dk Gharib Bilali, anayetarajiwa kufanya mkutano kwenye jimbo lake kesho kwenye kata ya Miamba.
  “Nimeshapeleka malalamiko yangu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa wamechoma khanga ambazo ni mabango ya CCM, zimeandikwa chagua Kikwete, chagua CCM na yeye kama anataka si akatengeneze zake aziandike chagua Slaa, chagua CHADEMA sijamnyima,” alisema Kilango . Kuhusu suala la kugawa fedha alisema suala hilo ni la TAKUKURU, hivyo awape taarifa wamkamate na kukanusha suala hilo kujadiliwa kwenye vikao vya maadili vya Tume ya Uchaguzi.
   
Loading...