Chadema wabadili msimamo wa kuingia bungeni kumshinikiza Makinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema wabadili msimamo wa kuingia bungeni kumshinikiza Makinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JIULIZE KWANZA, Jun 7, 2011.

 1. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Monday, 06 June 2011 20:59

  0digg Ally Mkoreha, Dodoma


  KAMBI Rasmi ya Upinzani Bungeni, imesema itaingia kwenye mkutano wa Bunge unaoanza leo, ikiwa na hoja nyingi lakini kubwa ni kumng’ang’ania Spika wa Bunge, Anne Makinda, kueleza umma kama wabunge wana kinga ya kutokakamatwa au la.

  Msimamo wa kambi hiyo inayoongozwa na Chadema, ulitolewa jana na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, alipokuwa akizungumza kwa simu saa chache baada ya kuachiwa kwa Kiongozi wa kambi hiyo, Freeman Mbowe.

  Mbowe alikamatwa juzi na polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, kufuatia amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, kutaka akamatwe kwa kosa la kudharua chombo hicho cha sheria kwa kutohudhuria usikilizaji kesi dhidi yake.


  “Tutaingia Bungeni, lakini safari hii tukiwa na hoja nyingi kweli, kubwa ni ya kumtaka Spika aueleze umma wa Watanzania kama wabunge wake wana kinga ya kutokamatwa au hawana. Hii inatokana na ukweli kwamba wabunge na hasa wa upinzani, wamekuwa wakimatwa ovyo tena kwa masuala ya kisiasa wakati wa CCM hawakamatwi,” alisema Lisu na kuongeza:

  “Kuna mbunge mmoja wa CCM aliwahi kutuhumiwa kwa makosa ya mauaji, lakini hakukamatwa, hii ni sahihi kweli.”
  Alisema wakati umefika kwa Makinda, kufahamisha umma ili kuwezesha wapiga kura kutambua kwa wazi kama wabunge wao wanapaswa kuwa na kinga au kinyume chake.

  Mbunge huyo ambaye siku chache zilizopita alitiwa mbaroni wilayani Tarime, mkoani Mara, akituhumiwa kuchochea wananchi kwenye tukio la mauaji ya wananchi sita yaliyotokea mgodi wa North Mara, alisema kambi hiyo isingeingia bungeni kama Mbowe asingeachiwa huru.“Kama mwenyekiti wetu (Mbowe) asingeachiwa huru leo (jana), tusingeingia Bungeni na tungeitisha maandamano makubwa nchini kote, kupinga unyanyasaji huu dhidi ya wabunge wa Chadema,” alisisitiza.


  Na katika hatua nyingine, Kamati ya Uongozi ya Bunge, jana ilikutana mjini Dodoma bila kuwapo kwa Mbowe na Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe.

  Akizungumza kutoka Dar es Salaam kwa simu, Mbowe alisema alipaswa kuja Dodoma jana kushiriki katika kikao hicho, lakini kukamatwa kwake kulimfanya ashindwe kusafiri.


  Hata hivyo, Mbowe alisema ili kuepuka kuvuruga shughuli muhimu za serikali na zenye maslahi kwa umma, aliridhia kikao hicho kiendelee bila ya kuwapo kwake.


  “Niliwajulisha wenzangu kwamba waendelee na kikao hicho ili kuepuka kuvuruga shughuli muhimu za serikali,” alisema Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai.

  Spika wa Bunge na Naibu wake, hawakuweza kupatikana ili kuzungumzia mambo yaliyojadiliwa katika kikao hicho, ambacho kwa kawaida ndicho kinachotoa mwelekeo wa shughuli za Bunge.


  source
  Gazeti la habari za kiswahili la kila siku Tanzania, linaongoza
   
Loading...