CHADEMA waanzishe na kumiliki News Media zao

Pamoja na kuzunguka na chopa, mie nashauri pia kufungua ofisi kwa kuanzia kila kata hapa nchini, ofisi hii itatumika pia kuelemisha umma elimu ya uraia. Wote tunajua ushindi wa CCM unategemea ukosefu wa elimu ya uraia vijijini. Watu wanatishwa wasichague upinzani eti kutakuwa na vita, watu wanatishwa shule zote zitafungwa, nk, na chama cha siasa ambacho kinategemea ujinga kutawala hakina muda mrefu, kitaanguka tu.

Naunga mkono hoja.
 
sio mbowe pekee yake,hata slaa asikabidhiwe make ataongeza mke wa tatu!

Kama una cha kuandika kaa kimya. CHADEMA ni chama makini, wivu tu unakusumbua. Unafikiri hiki ni chama cha magamba?? Nenda kwa magamaba wenzako mkadanganyane huko. Tena upotee na tusikuone tena katika thread zetu
 
Ndugu wana JF

wote mnajua kuwa CDM inakubalika mijini zaidi kwa sababu zifuatazo
1.mjini kuna wasomi wengi ambao ni wepesi wa kuchambua mambo
2. upatikanaji wa Vyombo vya habari vingi
3.Kampeni nyingi huwa zinaishia mijini hasa kwa sababu ya ufinyu wa budget

Ili CDM iweze kuchukua dola 2015 in wazi kuwa ni lazima iweke mkakati wa kwenda vijijini kwa muda huu ili kiweze kuweka mizizi huko kama ilivyo kwa CCM. Kazi hii ni ngumu na inaitaji fedha nyingi.
Napendekeza uongozi wa CDM waanzishe mfuko maalumu ambao wanachama na watanzania wote wenye mapenzi mema na wanaopenda kulikomboa taifa hill 2015 wachangie ili kufanikisha CDM kuenea vijijini. Pia mfuko huo uwezeshe CDM kuanzisha TV na Radio yake ili kiweze kunadi sera zake zaidi. katika kurahisisha uchangiaji utaratibu wa M-Pesa, Tigo pesa nk, etc utakua mzuri sana kutumika.

nawasilisha


Wazo zuri sana.
Lakini bila kuwepo na tume huru ya uchaguzi na utaratibu mpya wa upigaji kura (utakaolenga katika kufanya idadi ya wapiga kura iwe sawa na ile ya waliojiandikisha; angalia hapa kwa habari zaidi https://www.jamiiforums.com/katiba-...-compulsory-voting-for-2015-and-beyond.html); hakika huo mfuko hautasaidia chochote.
 
Huo ni ushauri unaotakiwa kufuatwa chama cha wananchi hugharamiwa na wananchi na sivinginevyo watu wako tayari kuchangia kazi kwenu kuanzisha na kutangaza kwa watu wote kupitia media mbalimbali
Naunga mkono kidogo sana. Huu ndio utakuwa mwisho wa CDM. Wenye fedha watachangia na watataka wawe na maamuzi makubwa kwa kuwa wana mchango mkubwa. PEOPLES POWER HAITAKUWEPO TENA itazaliwa RICHEST POWER. AMINI KAULI YANGU. ANGALIA KWENYE MPIRA WENYE MCHANGO MKUBWA NDO WENYE SAUTI.
 
Mtu kama si chadema inamhusu nini kuweka comment hapa ??? Watu wengine wanatumia Masaburi kufikiri mambo...
Naomba mwongozo: JF ni ya wana CDM ? sio ya wana JAMII? Huko vijijini mtahamasishaje kama mnabagua mawazo ya wanaojaribu kuwapinga/ Si ajabu watu makini wanawajaribu kuona ukomavu wenu katika kutetea hoja. Mnapo tukana mnaonekana CDM chama cha kihuni mliokosa kazi.TAKE CARE BUD.
 
wazo lako nzuri kabisa, kwani CDM ikiweza kupata mabalozi wa shina kama ilivyokua wakati wa nyerere yani kila nyumba kumi ikawa na balozi mwanachama wa chadema tunaweza kuongeza wanachama kama ifuatavyo, Tanzania inakadiriwa kuwa na watu 45million, hii ni sawa na kaya million 9 kwa wastani wa watu watano katika kila kaya, that means kaya kumi zikitoa balozi mmoja ina maana tutakua na mabalozi 900,000 nchi nzima. hizo ni kura 900,000, bado wake zao au waume zao marafiki nk. Hivyo hinyo ngazi ya kijiji, kata, tarafa n,k tukiwa na safu za uongozi ngazi zote hizo utajikuta tuna wanachama wakutosha kuibwaga CCM
hakuna hesabu hiyo. Unawajumlisha na watoto chini ya miaka 18. Unawajumlisha na wagonjwa waliolazwa, wafungwa, watu wanaosafiri.Unataka kusema tanzania nzima watAKUWA WANACHAMA WA cdm VYAMA VINGINE VIFE? UNATAKA KUJENGA GHOROFA KWA MATOFALI YA MATOPE MABICHI. CDM mnajidanganya sana wekeni mikakati inayotekelezeka na kupimika.
 
ccm wana wanachama hai zaidi ya milioni 5, chadema mna wanachama wangapi?; nimgechangia naogopa wajanja wasizitafune!!!!!!!
 
Naomba mwongozo: JF ni ya wana CDM ? sio ya wana JAMII? Huko vijijini mtahamasishaje kama mnabagua mawazo ya wanaojaribu kuwapinga/ Si ajabu watu makini wanawajaribu kuona ukomavu wenu katika kutetea hoja. Mnapo tukana mnaonekana CDM chama cha kihuni mliokosa kazi.TAKE CARE BUD.

Umekuja na kasi mpya, ari mpya na nguvu mpya kuleta kichefuchefu, poa tu kwani ndivyo ulivyojaliwa.
 
Naomba wazo ilo lipite. Ili magamba wasiwe na cha hapa tz mimi mwnyewe nmesha wai kuwa balozi wa nyumba kumi kuptia magamba. Hawa jamaa wanyonyaji sana. Hawa mabalozi hawalipwi hata senti moja ya mshahara, mimi nimmoja kati ya watu ambao wata kuwa kipaumbele katka mpango uo.
 
Huo mfuko msimkabidhi Mbowe kwasababu mtakuta hela zote zipo counter Bilicanas

wana JF hili ni wazo zuri sana, na litakomboa taifa hili na vizazi vyetu vijavyo.

mbowe hana umaskini huo, kwan hata sasa chama anakisaidia sana kifedha. tuacheni majungu tuangalie jinsi ya kuikomboa hii nchi ccm imeshashindwa kabsaaaaaa.

wazo zuri nalisuport 100%
 
Chadema ifungue vyombo vya habari vyake naomba wananchi wenye uelewa tuichangie CHADEMA ili iwe na redio, Tv na magazeti. Hakika nawaambia 2015 tutaikomboa Tanzania toka mikonon mwa magamba. Seriously, JF ni chanzo kizuri sana cha habari lakin Watanzania weng hawaijui JF tena wengne wako vyuo lakin hawana access na JF. Naomba mwenye mawazo mapana kuliko haya achangie hapa.
 
Nadhani tatizo si pesa. Labda ni mawazo na mipango. Nadhani Mzee Ndesamburo (na wengine) anao mtaji wa kutosha wa kuanzisha kituo cha TV na Radio. Tatizo linaweza kuja katika kupata vibali na leseni kutoka serikali ya magamba.
 
Nadhani tatizo si pesa. Labda ni mawazo na mipango. Nadhani Mzee Ndesamburo (na wengine) anao mtaji wa kutosha wa kuanzisha kituo cha TV na Radio. Tatizo linaweza kuja katika kupata vibali na leseni kutoka serikali ya magamba.

mkuu, mbona mzee ndesamburo anayo redio tayari ,.... Moshi FM
 
Naunga mkono hoja hiyo na niko tayari hata familia yangu ikose mambo machache lakini nichangie. hakiyamungu nawaambia anzisha kaka na ongea na viongozi wa chadema kama wako tayari.
 
Hapo tatizo litakuja kwa waandishi wa habari tena ......... wanapenda sana pesa.
 
Back
Top Bottom