CHADEMA waahirisha utoaji rambirambi

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelazimika kuahirisha zoezi la utoaji wa fedha kwa familia za marehemu, Ismail Omary na Denis Shirima, waliofariki dunia wakati wa vurugu za Januari 5, mwaka huu, baada ya walengwa halisi kutofika kwenye hafla hiyo. Waliofika ni baba wa marehemu Ismail, akiwa ameongozana na msemaji wa familia hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Manyerere, ambapo mke na watoto wa marehemu hawakuwepo, jambo ambalo viongozi wa CHADEMA walisema walitakiwa wawepo kwani ndio walengwa.
Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya City Link ya jijini Arusha, ambapo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CHADEMA akiwamo Mwenyekiti wa Mkoa, Samson Mwigamba na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.
Mwenyekiti wa Mfuko wa Maendeleo Arusha (ArDF), Elifuraha Mtowe, ambaye ndiye alikuwa na jukumu la kuratibu shughuli hizo alisema kuwa walifikia uamuzi wa kuahirisha zoezi hilo mpaka hapo watakapotangaza tena baada ya kuona wake na watoto wa marehemu ambao ndio walengwa wa fedha hizo hawakuhudhuria.
Alisema kila familia ilikuwa ipewe hundi ya sh milioni tano ikiwa ni rambirambi iliyotolewa na kada wa CCM, mfanyabiashara, Mustafa Sabodo, kwa familia zilizopatwa na msiba, ambapo tayari walikuwa wamewaandalia hundi namba 012617 na 012618 za CHADEMA Mkoa wa Arusha. “Tuliwaomba wafungue mirathi ili msimamizi wa mirathi ambaye ndiye mwenye jukumu la kutunza familia aje tumkabidhi, lakini naona hili halikutekelezeka, tunajua mwenye jukumu la kutunza na kulea familia si baba wala mama wa marehemu, bali ni mke, hivyo ni vema nao wangekuwepo hapa,” alisema. Hata hivyo, familia ya marehemu Shirima haikuwa na mwakilishi aliyejitokeza, ambapo Mtowe alisema kuwa wanaendelea kufanya mawasiliano kwa lengo la kumpata mtu sahihi anayetakiwa kupokea rambirambi hiyo.
 
Safi,kwanini apewe mtu asiye husika afu akajichane gongo huku mama na watoto wake wanateseka bila kupata chochote
 
Safi,kwanini apewe mtu asiye husika afu akajichane gongo huku mama na watoto wake wanateseka bila kupata chochote

Usiwe mwepesi wa kuhukumu,hoja hapa ni rambirambi iwafikie wàlengwa husika na si matumizi na hakuna gongo ya 5,000,000
 
Wangekuwa hawa jamaa zetu wangetoa tu, maana hat kusoma hawajuhi.

167541_1390032369824_1802575517_750317_699599_n.jpg
 
Back
Top Bottom