CHADEMA waache kabisa kuwa reactive wawe proactive kama awali katika siasa za nchi yetu

Hoja yako ni nini hapa? Huu uzi hauhitaji ushabiki, lengo letu ni kuirudisha cdm yetu ilivyokuwa na hata zaidi. Kwa hiyo tunajadili tumefikaje hapa na kipi kifanyike tutoke hapa. Bado una muda wa kutosha, hata baada ya idd una nafasi kwani huu uzi utaendelea kuwepo. Kama ccm inaendelea vizuri au vibaya sio sehemu ya mada hii.
Acha hasira logic ni kuwa if lowasa was bad with ccm ndio alikuwa anachafua chama. Je alivyohama alihama na uchafu wake na kuupeleka cdm!? Na ccm ikawa safi. Je hivi vyama ni taasisi au ni watu mpaka an individual abebe chama. Tujifunze kujenga taasisi ambayo bila mtu itaendelea kuwepo.
 
Hoja dhaifu, Lowassa alivyokuwa ccm, cdm ndio waliongoza kumchafua na ushahidi wa kuchafuliwa na cdm upo. Ccm ilikuwa ni chafu Lowassa akiwepo na hata alipoondoka bado ccm imeendelea kuwa chafu, ila Lowassa hakwenda cdm akiwa msafi na ccm wametumia mwanya huo kuifanya cdm ni chafu kama ccm na hata zaidi kwa kukumbatia mtu aliyekichafua chama chao. Nakubaliana na ww vyama ni taasisi, lakini hizo taasisi zimegeuka hazina nguvu kama viongozi wa hizo taasisi.

Kwa udhaifu huo wa taasisi hasa cdm, ndio hapo walipompokea Lowassa waliyemuita mchafu kwa zaidi ya miaka 8 bila ridhaa ya wanachama, na kuishia kumpa nafasi nyeti kabisa ya kugombea urais. Na kitendo cha kumpa nafasi Lowassa kilifanywa na k/viongozi wachache sana kwa faida ya matumbo yao. Matokeo leo hii ndio chama kimechuja na wala hakina ajenda inayojinasibisha nayo. Kwa maneno marahisi chama kimekuwa zilipendwa.
 
Mkuu hili jambo nimeliongelea sana humu kwamba ile cdm yetu imepotea chini ya Lowassa na Sumaye. Mbowe sasa hivi ana promote warembo akina Wema, katibu mkuu hata jina huwa namsahau, yeye yuko kwenye offline mode.

Amebaki Tundu Lissu wangalau namuona tena anapambana kwelikweli. Hili la kuwamwaga akina Lowassa na Sumaye wala halihitaji mjadala, hao wazee hawajui siasa za upinzani wamekuja kulisha watu ukondoo kwa faida ya ccm. Hata sijui cdm imekumbwa na balaa gani, imekuwa kama uji wa baridi usio na sukari. Kabla Ben Saanane hayajamkuta yaliyomkuta niliwahi kumuambia hilo hapa jukwaani. Aliona hoja yangu lakini bado chama kilikuwa kwenye usingizi wa uchaguzi. Lakini naona muda unaenda sioni hatua. Cdm amkeni hao wazee wameletwa hapo na ccm kuua chama.
Hata Lisu suala la makinika na utetezi wake kwa Accasia umempunguzia heshima
Labda tumshauri asiwe much know!
 
It
Hoja dhaifu, Lowassa alivyokuwa ccm, cdm ndio waliongoza kumchafua na ushahidi wa kuchafuliwa na cdm upo. Ccm ilikuwa ni chafu Lowassa akiwepo na hata alipoondoka bado ccm imeendelea kuwa chafu, ila Lowassa hakwenda cdm akiwa msafi na ccm wametumia mwanya huo kuifanya cdm ni chafu kama ccm na hata zaidi kwa kukumbatia mtu aliyekichafua chama chao. Nakubaliana na ww vyama ni taasisi, lakini hizo taasisi zimegeuka hazina nguvu kama viongozi wa hizo taasisi.

Kwa udhaifu huo wa taasisi hasa cdm, ndio hapo walipompokea Lowassa waliyemuita mchafu kwa zaidi ya miaka 8 bila ridhaa ya wanachama, na kuishia kumpa nafasi nyeti kabisa ya kugombea urais. Na kitendo cha kumpa nafasi Lowassa kilifanywa na k/viongozi wachache sana kwa faida ya matumbo yao. Matokeo leo hii ndio chama kimechuja na wala hakina ajenda inayojinasibisha nayo. Kwa maneno marahisi chama kimekuwa zilipendwa.
Ulikuwa ni mtihani ulioamuliwa na muda ukadhihiri nini lengo la cdm... Madaraka. Agenda za cdm sasa zimekuwa ni kiki reactive kama mtoa Mada. Kinachotakiwa Tanzania ni kile kilichotokea Kenya kusiwe na chama hodhi. Futa vyama tuanze upya tukiwa tuna dira angavu sio ujamaa kidogo ubepari kidogo.
 
Hata Lisu suala la makinika na utetezi wake kwa Accasia umempunguzia heshima
Labda tumshauri asiwe much know!

Kama umepitia post zangu za nyuma kuna mahali nimemtaja kabisa Lisu kwa jina kwamba wakati mwingine mitazamo yake binafsi inahusishwa ni ya chama. Nikasema kwa chama makini baada ya kuona mwanachama wake alichosema kimepata taswira tofauti kilipaswa kuja hadharani na kusawazisha kwa ripoti halisi ya kiofisi.

Cha ajabu jana Lowassa kaitwa kwa DCI leo, jana hiyo hiyo msemaji wa chama wala hakulala akatoa press release eti chama kimeweka vizuri suala la kisheria!! Hapo ndio nimejua kweli hela mwanaharamu. Manina wallah.
 
It

Ulikuwa ni mtihani ulioamuliwa na muda ukadhihiri nini lengo la cdm... Madaraka. Agenda za cdm sasa zimekuwa ni kiki reactive kama mtoa Mada. Kinachotakiwa Tanzania ni kile kilichotokea Kenya kusiwe na chama hodhi. Futa vyama tuanze upya tukiwa tuna dira angavu sio ujamaa kidogo ubepari kidogo.

Kila chama lengo lake ni madaraka, cha muhimu usiache agenda yako ya msingi uliyokubalika nayo. Hilo la Kenya limewezekana kwa kuwa Wakenya wengi wanajitambua. Hapa kwetu kama rais kakamatu tu mchanga lakini bado mikataba ni mibovu, wanaccm kibao mpaka rais mstaafu wanataka rais atawale milele kuna uwezekano wa kufuta vyama vyote hapo?
 
Chadema wanategemea nguvu ya umma ambayo ccm na serikali yao wameona athari yake na kuamua kuziba kwa kuweka pazia. Watu wameifahamu chadema kupitia mikutano ya kisiasa ya hadhara, makongamano na mijadala live bungeni. Baada ya kuifuta hiyo CHADEMA sasa haina sehemu ya kushika kuanza kurusha ngumi. Ujio wa Lowasa na Sumaye haujaififisha Chadema...wala hizo hoja za ufisadi hazijanyang'anywa na CCM. Kwa miaka 50 ambayo CCM imetawala na kufanya blander hata akija malaika hawezi kuipaisha CCM kwa hoja halafu wapinzani wakakosa cha kuongea, ni ngumu mno....ndio maana kinachofanyika ni kuhakikisha sauti za CHADEMA hazisikiki ila za CCM zinapaa...mwisho wa siku CCM hao hao wanatokea mbele na kusema CHADEMA hawana cha kuongea kwa sababu ya Lowasa. Lowasa mwenyewe tu bila hao vijana mnao wasema akiachiwa na Magu afanye mikutano ya hadhara hakuna mwanaCCM ambaye ataweza kum-win mbele ya public...Kikubwa wanachotakiwa kufanya CHADEMA ni kupigania haki ya kufanya mikutano ya hadhara basi....agenda zipo nyingi sana ambazo CCM hawataweza kuzimudu.
 
HAHAHAHA....comical Ali, salama? CHADEMA inaimirika kwa lipi, 17% au hukusoma taarifa week 2 zilizopita?

Tukurudi kwa mtoa mada ana point lakini amesahau jambo moja la msingi, ujumbe wake ameelekeza kwa CHADEMA ipi? Sasa hivi tuna CHADEMA nyingi, Kuna CHADEMA Mbowe, CHADEMA Lowassa, CHADEMA Ndesamburo (RIP) na kuna wakina Mnyika ambao wamapigwa ganzi, na kila kikundi kina malengo yake. Sasa ni CHADEMA ipi anataka iwe Proactive?
unavyoongea pumba Uwe unatoa na ufafanuzi
 
Unataka ushahidi gani wewe,Lowassa anatoa matamko na maelekezo hakuna wa kumpinga wala kumuonya
Madai yako kwamba Lowasa akitoa tamko hakuna wa kumpinga, siyo ushahidi kwamba amenunua Chama. Hiyo ni weakness ya mikakati ya kisiasa ambayo nimetolea mbadala wake kuwa vijana ndiyo kioo cha Chadema wala siyo Lowasa na Sumaye. Madai ya kununua majibu yake ni kwa wewe kuweka makabrasha ya maandishi ya kuuziana. Mengine ni porojo tu za kwenye kahawa ambazo hazihitaji ushahidi. Hapa JF tunahitaji ushahidi wa maandishi ya kuuziana chama.
 
Stabilaiza nakubaliana na wewe kuwa ni makosa makubwa kimkakati kwa Chadema kuwaweka Lowassa na Sumaye msitari wa mbele kwenye mapambano ya kisiasa. Lakini bila kwenda mbali ni lazima tukubaline kuwa tatizo kubwa la Chadema kwa sasa ni uongozi. Na hakika kwa sasa Mbowe is doing more harm than good to Chadema. He surely has outlived his usefulness as the "paramount party leader"!

Kwa upande mwingine sikubalini na wewe kwenye hoja yako ya agenda ya ufisadi. Ufisadi ni uhalifu na ni uvunjifu wa sheria. Kushamiri kwa ufisadi na kutokuchukuliwa hatua dhidi yake (impunity) ni kielelezo cha kukosekana kwa utawala wa sheria. Nchi inapaswa kuwa na mifumo imara na thabiti ya kitaasisi ya kupambana na uhalifu wa aina yoyote bila kuhitaji personal intervention ya viongozi wa kisiasa. Madai ya kupambana na ufisadi bila kuwa na hoja ya kubadili (transform) taasisi za kiutawala ili ziwe imara na huru ni utapeli mtupu............
...............................
................................
Narudia. Vita ya kupambana na ufisadi on ad hoc basis haipaswi kuwa agenda ya chama cha kisiasa. Huo ni utapeli. Agenda inapaswa iwe kuweka taasisi huru na imara (kwa mujibu wa katiba na sheria) za kupambana na ufisadi kwa njia endelevu. Na kwa taarifa yako hiki ndicho kitu ambacho wanasiasa wengi hawataki kusikia!

Nginana, umeongea mambo mengi mazuri na ya msingi sana kwamba mikakati ya kisiasa ijengwe katika kuingiza hoja kwenye taasisi na sheria zetu. Nakubaliana na wewe kwa hili. Lakini hizo unazoita ad hoc ajenda, ndizo zinazo-create awareness kwa umma juu ya direction ya chama na umuhimu wa ajenda hizo. Kinachotakiwa ni chama kuwa consistent na ajenda zake kama kupinga ufisadi maana ndizo zinazo-influence umma ili nao unatoa support kwa chama na mwisho wa siku ku-influence thinking na attitute ya serikali na wananchi kwa ujumla. Huwezi kuuza kuandika sheria na kuanzisha taasisi ikiwa umma bado haujajua umuhimu na ukubwa na tatizo. Hivyo CDM kuanza na ajenda ya ufisadi majukwaani ilikuwa ni njia sahihi na kinachotakiwa ni kumalizia kwa kutaka sheria na taasiasi za kusimamia mambo haya ikiwemo katika nzuri. Lakini ujio wa Lowasa kwa bahati mbaya kuna-dilute ajenda yao.
 
Madai yako kwamba Lowasa akitoa tamko hakuna wa kumpinga, siyo ushahidi kwamba amenunua Chama. Hiyo ni weakness ya mikakati ya kisiasa ambayo nimetolea mbadala wake kuwa vijana ndiyo kioo cha Chadema wala siyo Lowasa na Sumaye. Madai ya kununua majibu yake ni kwa wewe kuweka makabrasha ya maandishi ya kuuziana. Mengine ni porojo tu za kwenye kahawa ambazo hazihitaji ushahidi. Hapa JF tunahitaji ushahidi wa maandishi ya kuuziana chama.
Lowasa kununua chama ni hoja mfilisi low level mno. Sumaye and lowasa are retired officers
 
Lowasa kununua chama ni hoja mfilisi low level mno. Sumaye and lowasa are retired officers
Uko sahihi na bahati mbaya ni madaya ambayo yanatolewa bila ushahidi. Uko sahihi kuwa Lowasa na Sumaye ni retired wanatakiwa waone kuwa muda wao wa kuwa forefront katika siasa umepita waache na vijana wenye nguvu wachukue nafasi yao kama awali.
 
Hata Lisu suala la makinika na utetezi wake kwa Accasia umempunguzia heshima
Labda tumshauri asiwe much know!
Kwa vipi mkuu, kwa kuwa alisema wanashupalia michanga wakati real madini yanaendelea kuchukuliwa kutoka migodini kwa ndege zinazoruka kutoka viwanja vilivyojengwa huko migodini?
 
Back
Top Bottom