CHADEMA Vumilieni, Rais pekee atakayeunga mkono suala la Katiba Mpya ni Samia Suluhu, na hatotokea mwingine CCM

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,050
4,904
Sioni haja ya Vyama pinzani hususani CHADEMA kulazimisha upatikanaji wa katiba mpya kwa kutumia vitisho na nguvu, eti iwe kwa Shari ama kwa shwari.

Kuna haja ya kujifunza kwa Vyama vya wafanyakazi nchini, pamoja na kwamba haki zao kimsingi ziliminywa awamu ya tano, lakini walivumilia, na wote tunakumbuka katika sherehe za may mosi mwaka huu pale mwanza , Raisi aliomba suala la kupandishwa madaraja na mishahara apewe muda, lakin leo tunajua ni watumishi wangapi wamepandishwa madaraja.

Suala la Katiba mpya ni matakwa ya msingi kabisa katika nchi yetu kulingana na hali iliyopo kwa Sasa, kimsingi sikumsikia Mama akisema hatoweza kutengeneza mazingira ya upatikanaji wa katiba mpya, ila aliomba apewe muda, kwa waungwana kulingana na mwenendo wa uongozi wa Mama Samia, hatupaswi kuweka vitisho na maneno makali ili tupate tunachokitaka, Bali tuwe na lugha za kukumbusha , Kama jinsi ambavyo CHADEMA walivyoandaa kongamano lao lililohusu katiba mpya.

Ninaunga mkono upatikanaji wa katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, lakini wakati huu ni wakati wa kuenenda kwa akili na busara, sio kukurupuka, mwishowe Mama abadili mtindo wa utawala tukarudi kwenye mfumo original wa HAPA KAZI TU.

Ikumbukwe hata miezi minne bado haijatimia toka Mama Samia aingie madarakani, nchi hii ipo kwenye kipindi Cha restoration, kwa hyo Kuna transition period inapaswa tupitie.
 
Back
Top Bottom