CHADEMA: Viongozi wa mikoa na wilaya (Chadema) ambao wanashindwa kufanya kazi zao waondoke. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA: Viongozi wa mikoa na wilaya (Chadema) ambao wanashindwa kufanya kazi zao waondoke.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkwawa, Oct 30, 2012.

 1. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  Chaguzi baada ya chaguzi, ipo mikoa tunaona jinsi inavyotamalaki ushindi wa CDM kila chaguzi zinapofanyika, na zile ambazo zina bank kura nzuri pamoja na kwamba tunashindwa na zile ambazo zinaonyesha kudorora kwenye kila chaguzi.

  Chama hiki cha siasa ni chama kinachokuwa kwa kasi kina hitaji viongozi makini, wasomi, na wenye uwezo mkubwa wa kuona mambo, kupambanua na kutenda. Natumaini viongozi wetu wa chama wa mikoa na wilaya, tarafa na kata ni wale wenye weledi wa kuthubutu na kufikia viwango halisi vya viongozi.

  Uongozi unaonekana kwa kiwango cha kuweza kufikia malengo uliyopewa, kiongozi wa kisiasa wa mkoa na wilaya ndio wana hakikisha ukuzi wa chama ngazi husika wakishirikiana na viongozi wa kata na vijiji. Kuna haja ya kufanya tathimini kama hawa viongozi wana fanya kazi zao ipasavyo. haiwezekani wilaya nzima tukakosa hata kata moja kwa Udiwani au mkoa mzima tukakosa ubunge.

  Viongozi wanaotegemea mpaka viongozi wa taifa wafike ndio wafanye kazi hawatufai. lazima chama kijikite na kujijenga ngazi ya kata, wilaya na mkoa ili kuweza kuwafikia wengi kwa wakati muafaka.

  Chaguzi zinatoa mwanga wa kukua kwa chama kwani kura zinaonyesha chama kinakuwa, sasa umakini unahitajika zaidi kuliko wakati wowote. Hakuna wa kulaumiwa 2015.

  Chief Mkwawa wa kalenga
  Hatukumshinda mkoloni kwa imani, bali kwa vitendo.
   
 2. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,694
  Trophy Points: 280
  Mkwawa,

  Huo ni ushauri mzuri mkuu.Ofcourse kila kukicha Team ya Chadema inajifunza na hasa kitengo cha sera na Utafiti.

  Zaidi ya kwenda field hata ushauri kama huu wa kwenye mitandao kutoka kwa wataalamu mbali mbali ni sehemu muhimu ya kujifunza zaidi

  Mikoa ambako kumekuwa na irregularities oflate tumeshuhudia chama kikifanya maamuzi magumu by aidha kuuvunja uongozi eneo husika au kuchukua measures ambazo vyama vingine havina ujasiri wa kufanya hayo
   
 3. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Je tatizo ni Viongozi?
   
 4. Bartazar

  Bartazar JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 805
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Bado chama kina kazi kubwa zaidi ya kufanya! Kwa upande wa mawilayani vitendea kazi ni muhimu sana kwa watendaji, hasa vyombo vya usafiri na kwa kuanzia walau piki piki! Tukumbuke kuwa ili kuyafikia maeneo mengi sana na kwa wakati wilayani ni muhimu sana kuwa na nyenzo hizo. Pia tunahitaji kuwa na walau mtendaji mmoja ndani ya wilaya ambaye uenezi kwake ndio itakuwa kazi ya msingi, mwenye commitment ya hali ya juu na mwenye maono! Walau nafasi hii iwe ni ajira ya kudumu ambapo mhusika atakuwa alalapo, aamkapo na kila afanyacho concentration yake iwe kwenye siasa tu!
   
 5. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Ben chukua 5,umemjibu.CHADEMA IMETHUBUTU..MFANO hapa arusha katibu wa ccm CHATANDA ana bifu na kambi fulani ila wanamlea,kama cdm 2ngeshamfurusha na kumpoka kadi.
   
 6. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  Mimi siongelei migogoro kuna viongozi wazuri tu na wanamapenzi makubwa sana na chama ila hawana uwezo wa uongozi. Natambua fika tumetoka mbali wapo wengi waliogopa kuwa hata na kadi ya chama chetu, ila leo wapo wengi wanaotuunga mkono na kuwa na wengi wenye upeo na uwezo mkubwa wa kufanya kazi na wabunifu.

  Nakubaliana kabisa kuwa na watendaji wa wilaya wenye kupata angalau ka posho ili waweze kufanya kazi ya chama tu. Na sie wanachama tujitahidi kuchangia chama ili kiweze kuwawezesha watendaji hawa. Tuna wilaya zaidi ya 150 TZ na mikoa 30+ kuna haja ya kuongeza kwenye payroll zaidi ya watumishi 200 sio kazi ndogo tunahitaji ushuriki wa kweli wa kila mmoja.

  Mkwawa
  Changia walau miguu na mdomo wako tutafika.
   
 7. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Kabla ya kuwataka waondoka, lazima kwanza uwapatie nyezo za kufanya hiyo kazi yako unayoitaka.

  Viongozi wengi wa Mikoa na Wilaya wanafanya kazi za CDM kwa mapenzi yao, kwa kujitolea na kutumia resources zao. Kama utawataka waachie ngazi because Mikoa/Wilaya zao hazifanyi vizuri, basi itakuwa sawa na kumnyima mtu kunde!
   
 8. S

  Sagamikotdt Member

  #8
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakuunga mkono mkuu Ben
   
 9. M

  Mundu JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Na hapo Sisiem wanajiona hawana mfarakano..ngoja wachakachuane watakapo fanya uchaguzi wa ndani kuteua wagombea wa nafasi mbalimbali mwaka 2015...

  CCM kwishney...
   
Loading...