CHADEMA V/S NAPE NNAUYE nana zaidi???? NAPE mkali kisiasa kama marehemu KOLIMBA nani anabisha??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA V/S NAPE NNAUYE nana zaidi???? NAPE mkali kisiasa kama marehemu KOLIMBA nani anabisha???

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chilisosi, Jun 16, 2012.

 1. Chilisosi

  Chilisosi JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 19, 2008
  Messages: 3,055
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Nimekuwa nikifuatilia mikutano ya chadema kwa karibu sana na kugundua kuwa hujaa watu wengi sana kwa sababu ndio wanaonekana kimbilio pekee la watanganyika , lakini kwa mbali namuona huyu Nnape anakuja kwa kasi sana na anafanya kazi bila kulala, yaani kama Dr SlAA ataenda mtwara basi nape yuko bomba mbili songea.

  Sikatai CCM wamebaki na watu wachache sana wanaoweza kuwashawishi wananchi, lakini katika hao wachache namuona huyu nape ni sawa na makamanda kumi wa chadema, nina maana nape mmoja ni sawa na MBOWE, SLAA, ZITTO, LISU, LEMA, MNYIKA, MSIGWA, SUGU, MDEE NA YULE DOMO KUBWA SHIBUDA

  Mie sina chama ila nawapenda chadema lakini tuwe tunaangalia kwa wapinzani wetu nani tishio,
  Wakati Chadema wanazunguka tanzania nzima full squad, NAPE ANAZUNGUKA PEKE YAKE NA MIKUTANO YAKE INAJAA KAMA YA FULL SQUAD YA CHADEMA.

  Mie binafsi namuona nape kama marehemu HORACE KOLIMBA, kijana ni mkali kisiasa na ndio hazina kubwa ya CCM. anayepinga na aseme
   
 2. Badu

  Badu JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2012
  Joined: Jun 2, 2012
  Messages: 363
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Huyo bado n kumbikumbi 2 kwa cdm
   
 3. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Nape ni mkali wa MIPASHO kama mzee Yusuph...

  Kwenye siasa Nape ni mchumba tu, alishindwa kwenye kura za maoni za ubunge wa Ubungo na Hawa Ng'umbi aliyeshindwa na Mnyika kwa kura kibao. Kwa maana hiyo kisiasa Nape hajafikia hata hadhi ya Mnyika, sasa kwa nini umpeleke kwenye CDM yote? Au ndo kujustify hela alizokupa, maana saizi anakampeni ya kuzunguka peke yake kote waliokopita makamata apatepate Per Diems maana makao makuu pagumu sana, lakini wananchi wamemkataa kabisa kama ilivyotokea Mafinga, Makambako na Njombe akaishia kupiga ngoma tu na kupiga picha na watoto wadogo eti ubora wa zizi ni ndama
   
 4. Chilisosi

  Chilisosi JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 19, 2008
  Messages: 3,055
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mnyalukolo,
  Kkura za maoni sio kipimo cha kukubalika kitaifa, Hawa ngumbi anaweza kuwa na ngome kubwa kwenye jimbo lakini yeye ni nani kitaifa??? Amini usiamini Jina la nape linakua kwa kasi sana na usije kushangaa kijana miaka ijayo akawa mwenyekiti wa CCM na baada ya hapo unajua maana yake nini?
   
 5. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,813
  Likes Received: 36,902
  Trophy Points: 280
  kwa hili unajitukana mwenyewe.
  re-think critically.
   
 6. Chilisosi

  Chilisosi JF-Expert Member

  #6
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 19, 2008
  Messages: 3,055
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kaka kwani ni kosa kumsifia mtu, mbona wewe unawasifia chadema sisemi unajitukana, kumbuka uhuru wa maoni. Usiwe sawa na mshabiki wa yanga akiona unaisifia simba kwa kucheza vizuri mashindano ya nje anakuona kama unajitukana kwa sababu na wewe ni yanga
   
 7. K

  KIMALIKE Member

  #7
  Jun 16, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sio kweli nape analolote kazi kuiga tu,na pia wananchi saizi awadanganyiki. R.I.P CCM
   
 8. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #8
  Jun 16, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Badala ya kumfananisha Nape na bi Kidude unamfanisha na CDM ahaaaaaa!!!!! Nimekumbuka sitakiwi kubishana na wewe kwasababu habari zako za kutoroka Mirembe nimzisikia juzi
   
 9. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #9
  Jun 16, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,028
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Waliokunywa maji ya bendera ya CCM wanakuaga kama wehu,
  yaani umeshindwa kutofautisha siasa na mipasho?
  Kwa taarifa yako Nape ni bingwa wa mipasho na matusi hajui kujenga hoja zaidi ya matusi na kebehi.
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  Jun 16, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Nape mmoja kwa CHADEMA nzima, halafu unauliza nani zaidi?

  Tunamwachia kijana awahenyeshe, sisi utatuona inapobidi.
   
 11. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #11
  Jun 16, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Huyo huyo Nape aliyewaambia ile Jumuiya yenu Huko Zenji ni ya Majambazi?
   
 12. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #12
  Jun 16, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Haiwezekani ushindwe kukubalika mtaani unakotokea halafu ukakubalika kitaifa. Muulize Nape kwa nini mikutano yake inaambatana na kukodi watu, kuwanunulia full tank madereva wa bodaboda, kugawa nauli na nguo za kulimia aka Tshirt za magamba?? Kwa nini asiende kavukavu kama Lema? Huyu jamaa hakubaliki kuanzia jimboni anakoishi, humu JF, FB wanadai wakimpinga anawaunfriend, na hata kwenye chama chake hakubaliki, only kwa kuwa kawekwa na MWENYEKITI ndio maana wanamuunga mkono kinafiki
   
 13. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #13
  Jun 16, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Huyohuyo ndiye anaewahenyesha, jumuia yetu au yenu? "mpaka kieleweke" Sheikh Farid - Uamsho Zanzibar.
   
 14. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #14
  Jun 16, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Aliwahi kuwatishia vijana wa Kirumba, Mwanza kuwa atawashikisha ukuta... Akiwa na jamaa yake aliyejipambanua kuwa ni kichaa, LUSINDE
   
 15. Chilisosi

  Chilisosi JF-Expert Member

  #15
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 19, 2008
  Messages: 3,055
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Duh! Wee kichomiz kweli una kichomi, hebu soma vizuri point Zangu kwanza, mie Sio ccm napenda chadema na sina chama
   
 16. n

  nyangasese Senior Member

  #16
  Jun 16, 2012
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ama kweli chadema ni kiboko. CCM sasa matumbo joto hawatulii,wamekuwa wapinzani wanafuata nyayo kila CHADEMA wanapopita. Wanapelekwa mchakamchaka,walizoea vyama vya msimu sasa wamekumbana na kiboko chao.

  Pamoja na propaganda zote chafu kwa kutumia vyombo mbalimbali kuichafua CHADEMA,bado uongozi shupavu wa mbowe ,slaa na wengine wameweza kukivusha chama.

  Msiyumbishwe na hao wanaoweweseka na M4C sisi wananchi tuko nyuma yenu na tunaunga mkono kazi yenu nzuri ambayo haina mfano tangu kuasisiwa kwa mfumo wa vyama vingi.Tunaomba mkaze uzi kujikita zaidi vijijini ili nape awafuate huko huko
   
 17. m

  mamajack JF-Expert Member

  #17
  Jun 16, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  katika majina ya vichaa,hata mie nimesikia linashika kasi balaaaaaaa.
   
 18. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #18
  Jun 16, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  siasa za tz bwana mi nilifikili utasema nani mtendaji kumbe unaangalia ujazaji watu mikutanoni.....!
  Hongera kwa mawazo.
   
 19. g

  gnsulwa Senior Member

  #19
  Jun 16, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 110
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  yeah unaona mbali sana. Big up
   
 20. Chilisosi

  Chilisosi JF-Expert Member

  #20
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 19, 2008
  Messages: 3,055
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Asante kwa kunisoma kaka,
  Mara nyingi watu wenye potential huwa hawakubaliki kwao, hata YESU wayahudi walimkataa
   
Loading...