Elections 2010 CHADEMA uraisi tunachukua? CCM chaliiii Nipeni Nifaidi

silver25

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
743
44
CHADEMA mpaka Sasa wanaongoza kwa Majimbo,, na sijui hayo yaliyo baki kwani CHADEMA ilisimamisha asilimia 45 tu ya majimbo yote Tanzania,, lakini ninaimani kuwa Watanzania now wamekubali mabadiliko na wameamua kuchange system ya ufisadi kuja kwa system ya Democrasia,

nikifuatilia kwaukaribu sana humchakato,, Kwanza Safari hii hakuna mchakachua utakao tokea mimi namini hivyo kwani kunamajimbo ambayo CCM wameanguka chaliii

Nimesikia Ubungo,, Kinondoni,, Mbeya mjini na Iringa sinauhakika please twendeni pamoja wanajamii Uraisi tunachukua?

Vunjo jamani Mrema amepeta,,
 
ubungo​
CHADEMA​
kawe​
CHADEMA​
iringa mjini​
CHADEMA​
mbeya mjini​
CHADEMA​
moshi mjini​
CHADEMA​
kigoma kaskazini​
CHADEMA​
tanga mjini​
CUF​
mtwara mjini​
CUF​
hai​
CHADEMA​
vunjo​
TLP​
rombo​
CHADEMA​
Karatu​
CHADEMA​

Haya Ndo niliyo yapata wajameni
 
ubungo​

CHADEMA
kawe
CHADEMA
iringa mjini
CHADEMA
mbeya mjini
CHADEMA
moshi mjini
CHADEMA
kigoma kaskazini
CHADEMA
tanga mjini
CUF
mtwara mjini
CUF
hai
CHADEMA
vunjo
TLP
rombo
CHADEMA
Karatu
CHADEMA

Haya Ndo niliyo yapata wajameni

Jamani mbona matokeo yanayokuja ni ya upinzani tu?? Naogopa isijetokea kama kule Zamibia 2006, matokeo yalipotoka upinzani walikuwa wanaongoza. Kumbe wenzao waliwatangulizia hayo matokeo ili wakati wanasherekea wao wanachakachua kwenye ngome zao then mwishoni kabisa matokeo yanabadilika.

Kwa hiyo Chadema lazima wawe makini kwa hili ili wasiibiwe. Kuna mtu ameposti matoke ya Kinondoni mpaka nimeshangaa!! Yaani turn out eti ilikuwa ni 30 % tu!! Hivi kwa mwamko uliokuwepo inawezekan kweli turn out ikawa that low?? Au ndiyo wanajaribu kupunguza kura za wapinzani sehemu walizoshinda??
 
Sasa Tazama na haya uongee mengine

MATOKEO ya awali ya kura za urais, ubunge na udiwani yaliyoanza kutolewa jana kwenye vituo mbalimbali nchini, yameonyesha kuwa nyota ya mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, imeendelea kung'ara huku wagombea ubunge wa chama hicho nao wakionekana kufanya vizuri.
Habari kutoka Jimbo la Iringa Mjini, zinasema matokeo ya urais katika kata saba, mgombea wa urais wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alikuwa akiongoza dhidi ya mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete.
Vituo hivyo ni stendi, Dk. Slaa (146), Kikwete (114), Ndiuka Dk. Slaa (133), Kikwete (272), Soko Kuu 2, Dk. Slaa (114), Kikwete (84), Zimamoto 1, Dk. Slaa (93), Kikwete (84), Zimamoto 2, Dk. Slaa (84), Kikwete (108), Hazina Dk. Slaa (138), Kikwete (97), IDYC Dk. Slaa (75) na Kikwete (72).
Katika Jimbo la Mbeya Mjini, matokeo ya ubunge vituo vya Block T- A, CHADEMA (140), CCM (33), kituo B, CHADEMA (115) na CCM (15).
Mbeya Mjini, katika Kata ya Mwakibete, Dk. Slaa (3,564), Kikwete (950), Kalobe Sekondari 1 Dk. Slaa (109), Kikwete (97), Kalobe Sekondari 2 Dk. Slaa (107), Kikwete (76), Kalobe Sekondari 5 Dk. Slaa (93) na Kikwete (85).
Geita kura za urais Kikwete (376), Dk. Slaa (341), kwa upande wa ubunge CCM (396), CHADEMA (322) na CUF (10) na kwa udiwani CCM (315), CHADEMA (474) na CUF (0).
Jimbo la Kyela matokeo ya urais katika kituo cha Nsesi, Kikwete 150, Slaa 119, kituo cha Katumba shuleni Kikwete 150, Slaa 120, Kilasilo, Slaa 36, Kikwete 205, Community Centre Slaa 125, Kikwete 56, Itungi Slaa 76, Kikwete 54. Katika kituo cha Bunge, jijini Dar es Salaam, Slaa 225, Kikwete 189.Arusha Mjini, katika Kata ya Kaloleni A1, Dk. Slaa amepata kura (112), Kikwete (59), Kaloleni A2, Dk. Slaa (119), Kikwete (76), Profesa Lipumba (2), Kaloleni A3, Dk. Slaa (104), Kikwete (61), Lipumba (1), Kaloleni A4, Dk. Slaa (109) na Kikwete (165).
Kituo B1, Dk. Slaa (118), Kikwete (67), Profesa Lipumba (0), kituo B2, Dk. Slaa (102), Kikwete 64, B3, Slaa 92, Kikwete 50, B4, Slaa 87, Kikwete (67) na Lipumba (3).
Jimbo la Segerea, Kata ya Kipawa, kituo Minazi mirefu A1 urais, Kikwete (79), Dk. Slaa (75), Profesa Lipumba (7), kituo A6, Dk. Slaa (69), Kikwete (62), kituo A2, Dk. Slaa (102), Kikwete (52), Profesa Lipumba (1), kituo B3, Kikwete (64), Dk. Slaa (78) na Profesa Lipumba (3).
Katika matokeo ya ubunge wa kata hiyo, mgombea wa CHADEMA, Godbels Lema alionekana akiongoza ambapo katika Kata ya Kaloleni A1, (113), dhidi ya mgombea wa CCM, Dk. Batilda Burian (54), Kaloleni A2, Lema (120), Burian (71), Kaloleni A3, Lema (109), Batilda (62), Kaloleni A4, Lema (111) na Batilda (63).
Jimbo la Ukerewe katika vituo vitatu, Mtoni, Nansio, Bwisya, mgombea wa CHADEMA, Salvatory Namuyaga wa CHADEMA alikuwa akiongoza akifuatiwa na mgombea wa CCM, Gertrude Mongela.
Katika Jimbo la Musoma Mjini, CHADEMA ilikuwa ikiongoza kwa madiwani katika kata nane, CCM ikipata kata tatu na CUF ikipata madiwani wawili.
Taarifa za awali zimedokeza kuwa Vincent Nyerere, alikuwa akiongoza kwa tofauti kubwa dhidi ya mgombea wa CCM, Vedasto Manyinyi.
Jimbo la Moshi Mjini, CHADEMA ilikuwa ikiongoza kwa kiti cha urais na ubunge huku upande wa madiwani ilikuwa ikiongoza kwa kupata viti 15 kati ya 21.
Hali hiyo, ilijitokeza katika majimbo ya Kigoma Mjini na Kigoma Kaskazini, ambako upinzani mkubwa ulikuwa kati ya vyama vya CCM na CHADEMA.
Katika Jimbo la Kigoma Mjini, Peter Serukamba wa CCM anachuana na Ally Mleh wa CHADEMA, huku katika Jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe wa CHADEMA anachuana na Robinson Lembo wa CCM.
Jimbo la Mbeya Mjini, mpaka tunakwenda mitamboni mgombea wa CHADEMA, Joseph Mbilinyi, ameonekana kuongoza dhidi ya mgombea wa CCM, Benson Mpesya. Kituo Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (DARUSO), urais Dk. Slaa (454), Kikwete (71), ubunge, John Mnyika wa CHADEMA (473) na Hawa Ng'umbi wa CCM (45).
Maswa, Magharibi, ubunge

Mgombea wa CHADEMA, John Shibuda, alikuwa akiongoza dhidi ya mgombea wa CCM, Peter Kisena, ambapo katika kituo cha Bukigi, Kata ya Malampaka Shibuda 113, Kisena 65, Sokoni Shibuda 68, Kisena 46, Sokoni B Shibuda, 61, Kisena 56, Mahakama A, Shibuda 66, Kisena 47, Mahakamani B, Shibuda 65, Kisena 50.
Shule ya Msingi Malampaka, Shibuda 54, Kisena 55, Chekechea A Shibuda 79 Kisena 5, Chekechea B, Shibuda 74, Kisena 53, Oil Mill, Shibuda 56, Kisena 36.
Jimbo la Nyamagana, inadaiwa mgombea wa ubunge Ezekiel Wenje, ameonekana kuongoza dhidi ya mgombea wa CCM, Lawrence Masha, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katika jimbo hilo CHADEMA inaongoza kwa kupata madiwani katika kata 12 kati ya 14. Katika Jimbo la Iringa Mjini, hadi tunakwenda mitamboni mgombea wa CHADEMA, Peter Msigwa, alikuwa akiongoza katika vituo vingi dhidi ya mgombea wa CCM, Monica Mbega.[/QUOTE]
 
CAHEMA tumeshashinda sasa tujiandae kushiriki katika uhapisho wa Dr. Slaa
 
kama mchakachuo hamna CHADEMA oyee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! na CCM bye bye :doh:
 
Back
Top Bottom