• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Chadema uongozi balaa; CHAWEKA UTARATIBU MAALUMU KWA WANACHAMA WAKE KUGOMBEA

R.B

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Messages
6,299
Points
2,000
R.B

R.B

JF-Expert Member
Joined May 10, 2012
6,299 2,000
[h=3][/h]


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeitafutia dawa migogoro inayotokana na baadhi ya makada wake kuonyesha nia ya kuwania urais na ubunge mwaka 2015, baada ya kuanzisha utaratibu maalumu wa wanachama wake kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia gageti hili, mpango huo unakuja wakati Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe ametangaza nia ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao, kitendo ambacho kiliwashtua vigogo wa chama hicho akiwamo mwasisi wake, Edwin Mtei.

Mara kadhaa Mtei amekuwa akimwonya Zitto kuwa kitendo chake cha kutangaza nia yake ya kugombea urais kitasababisha mzozo na mpasuko ndani ya chama hicho.

Mtei amekuwa akisema kuwa Zitto anatakiwa kuwaunganisha wanaChadema na siyo kuwagawa, au kuwavuruga na kwamba siyo shida kuonyesha hisia za kuwania urais, lakini tatizo ni kuwa hali hiyo inatengeneza mzozo mkubwa.Mtei ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki Kuu (BOT) enzi za utawala wa Mwalimu Julius Nyerere, alisema wakati mwafaka ukiwadia, Chadema kitaamua ni nani mwenye sifa za kugombea urais akisema kina utaratibu wake wa kuwapata wagombea mbalimbali wa uongozi.

Akizungumza wakati akijibu hoja mbalimbali katika mtandao wa Jamii Forum katikati ya wiki hii, Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, alisema viongozi wa chama hicho walikutana mjini Morogoro hivi karibuni na kutengeneza utaratibu wa watu kutangaza nia wanapotaka kugombea nafasi yoyote ya uongozi.

“Nadhani huu ni uamuzi mzuri wa chama maana watu wengine wana wasiwasi usio na msingi wowote kwamba kuwa na wagombea wengi kwenye chama ni kuvuruga chama,” alisema Zitto na kuongeza:

“Lakini watu haohao wanashangilia kweli wakiona demokrasia inavyotekelezwa kwenye nchi nyingine kama Marekani. Alisema kuwa tatizo la Watanzania wanapenda kuona demokrasia inatekelezwa, lakini wao wanaogopa kuitekeleza, hivyo mwongozo kwa wagombea ambao walipitisha Morogoro utasaidia sana.“Uamuzi wa Morogoro kuhusu mwongozo kwa wagombea utatusaidia sana kuondoa mashaka kama haya,” alisema Zitto.

Mwananchi Jumapili lilipomuuliza Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho, John Mnyika kuhusu jambo hilo alionyesha kutofahamu lolote kuhusu utaratibu huo, wala ulipofanyika huo mkutano wa Morogoro.

“Mkutano upi wa Morogoro?” alihoji Mnyika. Alipoelezwa kuwa suala hilo lilizungumzwa na Zitto katika Mtandao wa Jamii Forum alisema: “Muulize kwanza Zitto akupe ufafanuzi ni kikao gani cha chama, pia juu ya huo utaratibu, akikueleza ndiyo urudi tena kwangu.”

Juhudi za kumpata Zitto kueleza kwa undani kuhusu utaratibu huo hazikuzaa matunda, kwani simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita bila majibu, baadaye kuzimwa kabisa. Akizungumzia azma yake ya kuachana na ubunge kama alivyoahidi mwaka 2005 kuwa, atagombea vipindi viwili pekee Zitto, alisema kuwa aliwaambia wapigakura wake kwamba nia yake ni kuwa rais wa nchi.

“Nia yangu ni kupisha wengine nao wakimbize kijiti cha maendeleo ya jimbo letu na mkoa wetu,” alisema Zitto na kufafanua, “ Nimeshasema mara kwa mara kwamba ukiachana na siasa kazi ninayoipenda zaidi ni ualimu.”

Alisema kuwa akiachana na ubunge atakwenda kufundisha kwa kuwa anapenda kufanya tafiti, kusoma, kuandika na kufundisha.

“Hivi sasa tunaandaa mpango wa kuanzisha Chuo Kikuu cha Ziwa Tanganyika (Lake Tanganyika) mkoani Kigoma, nitafurahi kama nitakuwa mmoja wa wahadhiri wa mwanzo wa chuo hiki,” alisema Zitto.

Katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe alisimama kugombea nafasi ya urais akishindana na Rais Jakaya Kikwete ambaye alikuwa akisimama kwa mara ya kwanza.

Mwaka 2010, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willbrod Slaa aligombea nafasi hiyo na kuibuka mshindi wa pili kwa kupata asilimia 26.34 nyuma ya Rais Kikwete ambaye alipata asilimia 61.17.

Hivi sasa tayari kumetokea maneno ya chinichini miongoni mwa wabunge waliopo madarakani wakiwatuhumu baadhi ya wanachama wa chama hicho ambao wameaanza kuingia katika majimbo yao kutaka kugombea viti hivyo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Wabunge hao wanahoji kama wanachama hao wanaofanya hivyo wanataka kugombea ubunge katika uchaguzi ujao ili kukifanya chama kiongeze idadi ya wabunge bungeni, kwa nini wasiende kugombea katika majimbo ambayo hayana wabunge wa chama hicho?Vilevile, chama hicho kilipata msukosuko katika mchakato wa kupata wabunge wa Viti Maalumu katika uchaguzi uliopita na kulazimika kuweka vigezo ambavyo viliondoa manung’uniko hayo.

Baadhi ya vigezo hivyo ni elimu, mchango wa mgombea katika chama, wanawake waliogombea katika majimbo na uzoefu katika ubunge.
 
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,869
Points
1,225
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,869 1,225
KITAIFA

Na Fidelis Butahe

Posted Jumapili,Novemba25 2012 saa 8:49 AM


KWA UFUPI


CHAWEKA UTARATIBU MAALUMU KWA WANACHAMA WAKE KUGOMBEACHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeitafutia dawa migogoro inayotokana na baadhi ya makada wake kuonyesha nia ya kuwania urais na ubunge mwaka 2015, baada ya kuanzisha utaratibu maalumu wa wanachama wake kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia gageti hili, mpango huo unakuja wakati Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe ametangaza nia ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao, kitendo ambacho kiliwashtua vigogo wa chama hicho akiwamo mwasisi wake, Edwin Mtei.

Mara kadhaa Mtei amekuwa akimwonya Zitto kuwa kitendo chake cha kutangaza nia yake ya kugombea urais kitasababisha mzozo na mpasuko ndani ya chama hicho.

Mtei amekuwa akisema kuwa Zitto anatakiwa kuwaunganisha wanaChadema na siyo kuwagawa, au kuwavuruga na kwamba siyo shida kuonyesha hisia za kuwania urais, lakini tatizo ni kuwa hali hiyo inatengeneza mzozo mkubwa.


Mtei ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki Kuu (BOT) enzi za utawala wa Mwalimu Julius Nyerere, alisema wakati mwafaka ukiwadia, Chadema kitaamua ni nani mwenye sifa za kugombea urais akisema kina utaratibu wake wa kuwapata wagombea mbalimbali wa uongozi.

Akizungumza wakati akijibu hoja mbalimbali katika mtandao wa Jamii Forum katikati ya wiki hii, Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, alisema viongozi wa chama hicho walikutana mjini Morogoro hivi karibuni na kutengeneza utaratibu wa watu kutangaza nia wanapotaka kugombea nafasi yoyote ya uongozi.

"Nadhani huu ni uamuzi mzuri wa chama maana watu wengine wana wasiwasi usio na msingi wowote kwamba kuwa na wagombea wengi kwenye chama ni kuvuruga chama," alisema Zitto na kuongeza:

"Lakini watu haohao wanashangilia kweli wakiona demokrasia inavyotekelezwa kwenye nchi nyingine kama Marekani."

Alisema kuwa tatizo la Watanzania wanapenda kuona demokrasia inatekelezwa, lakini wao wanaogopa kuitekeleza, hivyo mwongozo kwa wagombea ambao walipitisha Morogoro utasaidia sana.

"Uamuzi wa Morogoro kuhusu mwongozo kwa wagombea utatusaidia sana kuondoa mashaka kama haya," alisema Zitto.

Mwananchi Jumapili lilipomuuliza Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho, John Mnyika kuhusu jambo hilo alionyesha kutofahamu lolote kuhusu utaratibu huo, wala ulipofanyika huo mkutano wa Morogoro.

"Mkutano upi wa Morogoro?" alihoji Mnyika. Alipoelezwa kuwa suala hilo lilizungumzwa na Zitto katika Mtandao wa Jamii Forum alisema: "Muulize kwanza Zitto akupe ufafanuzi ni kikao gani cha chama, pia juu ya huo utaratibu, akikueleza ndiyo urudi tena kwangu."

Juhudi za kumpata Zitto kueleza kwa undani kuhusu utaratibu huo hazikuzaa matunda, kwani simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita bila majibu, baadaye kuzimwa kabisa.

Akizungumzia azma yake ya kuachana na ubunge kama alivyoahidi mwaka 2005 kuwa, atagombea vipindi viwili pekee Zitto, alisema kuwa aliwaambia wapigakura wake kwamba nia yake ni kuwa rais wa nchi.

"Nia yangu ni kupisha wengine nao wakimbize kijiti cha maendeleo ya jimbo letu na mkoa wetu," alisema Zitto na kufafanua, " Nimeshasema mara kwa mara kwamba ukiachana na siasa kazi ninayoipenda zaidi ni ualimu."

Alisema kuwa akiachana na ubunge atakwenda kufundisha kwa kuwa anapenda kufanya tafiti, kusoma, kuandika na kufundisha.

"Hivi sasa tunaandaa mpango wa kuanzisha Chuo Kikuu cha Ziwa Tanganyika (Lake Tanganyika) mkoani Kigoma, nitafurahi kama nitakuwa mmoja wa wahadhiri wa mwanzo wa chuo hiki," alisema Zitto.

Katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe alisimama kugombea nafasi ya urais akishindana na Rais Jakaya Kikwete ambaye alikuwa akisimama kwa mara ya kwanza.

Mwaka 2010, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willbrod Slaa aligombea nafasi hiyo na kuibuka mshindi wa pili kwa kupata asilimia 26.34 nyuma ya Rais Kikwete ambaye alipata asilimia 61.17.

Hivi sasa tayari kumetokea maneno ya chinichini miongoni mwa wabunge waliopo madarakani wakiwatuhumu baadhi ya wanachama wa chama hicho ambao wameaanza kuingia katika majimbo yao kutaka kugombea viti hivyo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Wabunge hao wanahoji kama wanachama hao wanaofanya hivyo wanataka kugombea ubunge katika uchaguzi ujao ili kukifanya chama kiongeze idadi ya wabunge bungeni, kwa nini wasiende kugombea katika majimbo ambayo hayana wabunge wa chama hicho?

Vilevile, chama hicho kilipata msukosuko katika mchakato wa kupata wabunge wa Viti Maalumu katika uchaguzi uliopita na kulazimika kuweka vigezo ambavyo viliondoa manung'uniko hayo.

Baadhi ya vigezo hivyo ni elimu, mchango wa mgombea katika chama, wanawake waliogombea katika majimbo na uzoefu katika ubunge.

E & P
 
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,869
Points
1,225
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,869 1,225
t's TIME... No POWER GRAB!!
 
OSOKONI

OSOKONI

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2011
Messages
10,981
Points
2,000
OSOKONI

OSOKONI

JF-Expert Member
Joined Oct 20, 2011
10,981 2,000
what is new in this text??
 
bornagain

bornagain

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Messages
3,384
Points
1,225
bornagain

bornagain

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2012
3,384 1,225
Kigoomaaaaaaa ewe Kigoma weeeeeeee reka dutigite uwutwanka ameneke
 
MNAMBOWA

MNAMBOWA

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2011
Messages
2,024
Points
1,225
MNAMBOWA

MNAMBOWA

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2011
2,024 1,225
ACHA ikulu bwana kila mmoja anapaota hakuna cha wana cdm au ccm.
 
WOWOWO

WOWOWO

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2011
Messages
586
Points
225
WOWOWO

WOWOWO

JF-Expert Member
Joined Aug 3, 2011
586 225
what is new in this text??
Read between the line. Kwenye mahojiano Zitto aliyoyafanya na AshaDii hapa jamvini alisema CDM ilifanya mkutano Morogoro na kuweka utaratibu wa jinsi ya makada wake kutangaza nia ya kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hasa ya Urais. Sasa Mnyika ambaye kimsingi ni msemaji wa chama hana taarifa zozote za kikao hicho. Sasa ni ama Zitto alidanganya hapa jamvini au Mnyika anaficha ukweli.
 
Last edited by a moderator:
MNYISANZU

MNYISANZU

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2011
Messages
7,050
Points
1,225
MNYISANZU

MNYISANZU

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2011
7,050 1,225
JamiiForum inaongoza wengine wanajikongoja.
 
Mlengo wa Kati

Mlengo wa Kati

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2011
Messages
2,732
Points
0
Mlengo wa Kati

Mlengo wa Kati

JF-Expert Member
Joined Feb 16, 2011
2,732 0
kilicho andikwa tofauti na heading ya gazeti!
 
Pancras Suday

Pancras Suday

Verified Member
Joined
Jun 24, 2011
Messages
7,765
Points
2,000
Pancras Suday

Pancras Suday

Verified Member
Joined Jun 24, 2011
7,765 2,000
Uandishi way habari siku hizi unatia shaka kwelikweli, yaani heading na content ni tofauti kabisa
 
Tumaini Makene

Tumaini Makene

Verified Member
Joined
Jan 6, 2012
Messages
2,619
Points
1,500
Tumaini Makene

Tumaini Makene

Verified Member
Joined Jan 6, 2012
2,619 1,500
Aisee! Hii habari inahitaji uchambuzi yakinifu.
 
TAMKO

TAMKO

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2011
Messages
1,072
Points
1,225
TAMKO

TAMKO

JF-Expert Member
Joined Oct 11, 2011
1,072 1,225
Yaani Waandishi wengi wa habari wanaidhalilisha sana tasnia hii.. Wavyojenga vichwa vyao vya habari Na habari yenyewe ni utumbo A-Z.

Mtu mmoja aliwahi sema ni vema Waandishi wetu Wa habari at least wahitimu F4 au hata SIX sio darasa la Saba as almost 75% of them now as this Butahe Sijui Kama anajua hata alikuwa anaandika Nini.. Ni aibu sana..
 
B

Bwaga ya moyoni

Senior Member
Joined
Aug 21, 2012
Messages
148
Points
195
B

Bwaga ya moyoni

Senior Member
Joined Aug 21, 2012
148 195
Tamko siyo sawa ulilosema. Headline huandikwa na Sub-Editor na siyo Mwanandishi wa Habari. Laani kosa lakini kosa kama hilo unalosema na elimu ya mtu ni vitu viwili tofauti. In fact, sidhani kama kampuni kama Mwananchi imeajiri mwandishi yeyote asiye na hata cheti cha Form Four au Six and in fact, siku hizi reporters wengi ni graduates na kwa kiasi kikubwa wapo hata wenye MAs. Ni kweli pia kuwa wapo wenye vyeti vya Form Four na Six haswa wale wa mikoani ambao wengi wao hufanya kazi na radio. Ktk research yangu ya MA, nili-base ktk ku-assess elimu za reporters and I came to realise that at least 60% ya wale walio-based Dar ni graduates na the remaining 40% wanadiploma na certificates za vile vyuo vya Ilala pale na waliingia baada ya kumaliza vizuri Forms Four na Six. Sikupata hata mmoja aliyekosa hata cheti cha Form Four na Six. Tulaani kosa jamani kama lipo genuine hata kama ni habari ambayo inaonekana kutokuipendeza kambi yetu kisiasa.

Yaani Waandishi wengi wa habari wanaidhalilisha sana tasnia hii.. Wavyojenga vichwa vyao vya habari Na habari yenyewe ni utumbo A-Z.

Mtu mmoja aliwahi sema ni vema Waandishi wetu Wa habari at least wahitimu F4 au hata SIX sio darasa la Saba as almost 75% of them now as this Butahe Sijui Kama anajua hata alikuwa anaandika Nini.. Ni aibu sana..
 
mirisho pm

mirisho pm

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2012
Messages
3,191
Points
2,000
mirisho pm

mirisho pm

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2012
3,191 2,000
leo nusura ninunue hilo gazeti kwa hiyo headline... ningepoteza tsh 800 buuureee....
 
WOWOWO

WOWOWO

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2011
Messages
586
Points
225
WOWOWO

WOWOWO

JF-Expert Member
Joined Aug 3, 2011
586 225
Aisee! Hii habari inahitaji uchambuzi yakinifu.
Tumaini Makene usipuuze hii habari unless kama hujui kinachoendelea.Kwenye mahojiano Zittoaliyoyafanya na AshaDii hapa jamvini alisema CDM ilifanya mkutano Morogoro na kuweka utaratibu wa jinsi ya makada wake kutangaza nia ya kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hasa ya Urais. Sasa Mnyika ambaye kimsingi ni msemaji wa chama hana taarifa zozote za kikao hicho. Sasa ni ama Zitto alidanganya hapa jamvini au Mnyika anaficha ukweli.
 
Last edited by a moderator:

Forum statistics

Threads 1,402,902
Members 531,005
Posts 34,409,055
Top