CHADEMA unganeni na ACT Wazalendo

Zitto kama akikubali kufanya hivo nitamuona hamnazo kabisa. Kwa jinsi walivyomnanga kipindi kile afu Leo watake kuungana nae tena.?
Zitto usikubali kufanya huo ujinga hao wote walitaka upotee lakini ulipambana kiume sana hadi leo hii heshima imeanza kurudi.
Mtakonda kisa cdm

In God we Trust
 
Usiwe MTUMWA wa historia

huu ni ushauri mzuri na Viongozi tunatafakari

Haya mambo ya muungano wa vyama tumeona madhara yake. Ccm wanapoona kuna muungano wenye nguvu, wanachota pesa hazina kuhakikisha umoja huo unasambaratika. Na sio kusambaratika tu, wanahakikisha haiba ya vyama vilivyoungana inachafuka, nadhani unaona anachokifanya Mbatia hivi sasa. Katika mazingira hayo unategemea tuunge mkono muungano wa aina yoyote?

Halafu ACT mnafikiria kuungana na Cdm, kisha mnataka Membe awe mgombea wenu wa urais! Hivi mnataka kurudia kosa la cdm la 2015? Hivi ni kweli wapinzani hamna uwezo wa kutoa mgombea imara wa urais, zaidi ya kusubiri hao wazee wa ccm waliochoka ili muwape nafasi? Au hao wazee wa ccm ndio wafadhili wa hivyo vyama vyenu?
 
Bila kujali malengo ya uzi wako, kwanza tumegundua muunganiko wa vyama ni tatizo sana kwa sasa kwani vyama vinaribunika kirahisi na kuishia kuchafua taswira ya chama kingine. Hiyo October wengi hatutashiriki uchaguzi maana tume ya uchaguzi sio huru, hivyo hoja kuwa cdm waungane na cdm ili cdm isife ni hoja mfu. Iwapo cdm itakufa kwa kukosa kura zetu hapo utakuwa na hoja, sio kufa kwa kufanyiwa hujuma.

Cdm na ACT kila mmoja apambane kivyake, sio umoja usio na mwisho mwema. Kitakachofanyika hiyo October unayotishia nayo watu sio uchaguzi, bali ujinga wa mtu mweusi kwenye kusaka madaraka. Wananchi tunajitambua na hatuko tayari kushiriki uhuni wowote uitwao uchaguzi, eti kisa tunaogopa cdm itakufa. Bila tume huru ya uchaguzi hatushiriki uhuni wowote. Waambie ACT wakaungane na NCCR maana wameahidiwa na rais kuhongwa kuwa chama kikuu cha upinzani.
Hivi ukawa ipo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vyama vya upinzani hata wakijngana au ikawekwa Tume ya Uchaguzi kutoka Mbinguni, kamwe hawatashinda Uchaguzi Mkuu mwaka huu, labda 2025. Sababu ziko wazi kwani mwenye macho anaona na mwenye masikio anasikia.

Wakati viongozi wa upinzani wakiibeza, kuitukana, na kuizushia uwongo Serikali:-
√ Wapiga kura wanaona walivyo na wanavyo boreshewa miundo mbinu ya kukuza uchumi na huduma za jamii (afya, elimu, maji, umeme, nk);
^ Wapiga kura wanasikia kejeli za upinzani dhidi ya Rais na viongozi wenzake;
√ Wananchi majimboni wanaona jinsi wabunge wao wanavyoshiriki nao katika shughuli za maendeleo;
√ Wananchi wanasikia michango ya Wabunge Bungeni iwapo inawalenga au ni kwa mbunge kujijenga binafsi;
√ Na kadahalika.

Wapinzani hawataki tume huru ya uchaguzi ili watangazwe washindi, bali wanataka tume huru ili mshindi halali ndio atangazwe, acha upotoshaji wa kijinga. Hizo mbwembwe ulizoweka kwenye bullets hapo chini, zote zitapimwa iwapo kuna uchaguzi wa halali fullstop.
 
Tunasubiri kusikia lugha hiyo ya matusi kwenye kampeni, maana mitandaoni tumeizoea.
 
Endeleen kujiongopea nitajie mikoa mitatu ambayo hko chama kina nguvu kwa huku bara
ACT ina nguvu mkuu. Kilichopunguza spidi ya ACT ni hili janga la corona ila ni chama ambacho kinakuja juu sana
Na ni chama ambacho kitakuja kuwa tishio sana kwa CCM endapo strategies fulani fulani wakizitumia..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka sasa kuna idadi kubwa ya Wabunge walioondoka CHADEMA kwa sababu mbalimbali. Lakini ni ukweli ulio wazi kabisa mpaka sasa chama kinadhoofu (Ikumbukwe kuondoka kwa hao wabunge haimaanishi kuwa wanaondoka na wanachama ila inasababisha sintofahamu kwa wanachama).

Unganiko lenu na ACT WAZALENDO ndio suluhu ya kukiokoa chama kisizame. Nina uhakika awamu ya 2020-2025 ndio itakuwa kuchakaa rasmi kwa CHADEMA na kuundwa chama kingine kikuu cha upinzani.

NCCR Mageuzi haiwezi kuwa tishio kwa CHADEMA. Mbatia hana ushawishi katika siasa za Tanzania ukilinganisha na Zitto Kabwe.
Siasa za upinzani zinahitaji muunganiko wa Lissu, Zitto na Maalim Seif. Hawa naweza kusema ndio wanaobeba upinzani kwa sasa. Mbowe ana siasa za matukio (kwenye ukweli tuseme).

Hii "combination" ya ZItto na Lissu ni hatari maana ni watu ambao wanajua kuanzisha hoja na kuisimamia na wana ushawishi mkubwa sana.

Mpaka sasa CHADEMA ishajua wasaliti wao ni akina nani. Zitto hakuwa msaliti na ndio maana hata alipofukuzwa CHADEMA alipoteza ubunge na hakuhamia CCM akaenda kuanzisha chama na huko akapita ubunge tena kwa kuhama jimbo (kitu ambacho Mbatia hawezi; alipigwa mtama na Mdee Kawe akaenda kwa Lyatonga Vunjo-Nguvu ya UKAWA ndio ikamuweka pale alipo). Hawa wengine mliowafukuza uanachama wamerudi CCM moja kwa moja.

Ushauri wangu achaneni na kujiona ndio mnaimarika bali fahamuni ya kuwa chama kinakufa na suluhu ni kuungana na ACT-Wazalendo hata kama hamtachukua dola lakini mtajiongezea idadi ya viti bungeni na hivyo kuipunguza monopoly ya CCM bungeni.

Achaneni na propaganda za kina Yericko wao siku zote wanamuona ZItto ndio adui namba moja wa CHADEMA. Unganeni na ACT mlete upinzani kwa CCM tofauti na hapo hiyo October mtapata wakati mgumu na mnaweza hata msipate wabunge (Sio kwa sababu watapigia kura CCM bali morale ya wanachama wenu itapungua sana na uwezekano wa wanachama wenu kutopiga kura ukawa mkubwa kutokana na kile kinachoendelea sasa).

Nawasilisha!
Kuna msemo unaosema ''HATA TAMU HUKINAI''. Msemo huu unamhusu Zitto kwa 100%. Watanzania wamemchoka sana zitto na ukitaka kuamini hilo fanya uchunguzi mdogo wa kufuatilia hoja anazozitoa zito kwa vyombo vya habari au katika mitandao ya kijamii. Zaidi ya asilimia 95 ya wachangiaji hawamuungi mkono. Hiyo ni dalili ya kuwa wamemchoka (amewakinai).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zitto kama akikubali kufanya hivo nitamuona hamnazo kabisa. Kwa jinsi walivyomnanga kipindi kile afu Leo watake kuungana nae tena.?
Zitto usikubali kufanya huo ujinga hao wote walitaka upotee lakini ulipambana kiume sana hadi leo hii heshima imeanza kurudi.
Siasa haina adui wa kudumu mpendwa. Kuna mtu alinangwa na cdm kama Lowasa? Lakini hukumbuki huyo Lowasa aliyasahau yote na akawa mgombea urais kwa tiketi ya cdm?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka sasa kuna idadi kubwa ya Wabunge walioondoka CHADEMA kwa sababu mbalimbali. Lakini ni ukweli ulio wazi kabisa mpaka sasa chama kinadhoofu (Ikumbukwe kuondoka kwa hao wabunge haimaanishi kuwa wanaondoka na wanachama ila inasababisha sintofahamu kwa wanachama).

Unganiko lenu na ACT WAZALENDO ndio suluhu ya kukiokoa chama kisizame. Nina uhakika awamu ya 2020-2025 ndio itakuwa kuchakaa rasmi kwa CHADEMA na kuundwa chama kingine kikuu cha upinzani.

NCCR Mageuzi haiwezi kuwa tishio kwa CHADEMA. Mbatia hana ushawishi katika siasa za Tanzania ukilinganisha na Zitto Kabwe.
Siasa za upinzani zinahitaji muunganiko wa Lissu, Zitto na Maalim Seif. Hawa naweza kusema ndio wanaobeba upinzani kwa sasa. Mbowe ana siasa za matukio (kwenye ukweli tuseme).

Hii "combination" ya ZItto na Lissu ni hatari maana ni watu ambao wanajua kuanzisha hoja na kuisimamia na wana ushawishi mkubwa sana.

Mpaka sasa CHADEMA ishajua wasaliti wao ni akina nani. Zitto hakuwa msaliti na ndio maana hata alipofukuzwa CHADEMA alipoteza ubunge na hakuhamia CCM akaenda kuanzisha chama na huko akapita ubunge tena kwa kuhama jimbo (kitu ambacho Mbatia hawezi; alipigwa mtama na Mdee Kawe akaenda kwa Lyatonga Vunjo-Nguvu ya UKAWA ndio ikamuweka pale alipo). Hawa wengine mliowafukuza uanachama wamerudi CCM moja kwa moja.

Ushauri wangu achaneni na kujiona ndio mnaimarika bali fahamuni ya kuwa chama kinakufa na suluhu ni kuungana na ACT-Wazalendo hata kama hamtachukua dola lakini mtajiongezea idadi ya viti bungeni na hivyo kuipunguza monopoly ya CCM bungeni.

Achaneni na propaganda za kina Yericko wao siku zote wanamuona ZItto ndio adui namba moja wa CHADEMA. Unganeni na ACT mlete upinzani kwa CCM tofauti na hapo hiyo October mtapata wakati mgumu na mnaweza hata msipate wabunge (Sio kwa sababu watapigia kura CCM bali morale ya wanachama wenu itapungua sana na uwezekano wa wanachama wenu kutopiga kura ukawa mkubwa kutokana na kile kinachoendelea sasa).

Nawasilisha!
Kumekucha mkuu, nimeona hii kwenye new ya leo. Ila ni kweli waungane hapo, membe asimame kama mshika bendera kwenye kampeni, babu duni awe makamu wa raisi, lissu wazir mkuu, zito ajenge chama na awe Kiongozi mkuu.

Wataweza pia unda baraza zuri la mawazir.
20200523_083202.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom