CHADEMA unganeni na ACT Wazalendo

Usiwe MTUMWA wa historia

huu ni ushauri mzuri na Viongozi tunatafakari
Shikamoo Muheshimiwa.
Kwanza nimefurahi sana umereply comment yangu.Pili, Mimi ni shabiki wako kindaki ndaki na miongoni mwa wale ambao tuliumia sana kipindi kile unaitwa msaliti.
Tatu,.Nikutakie kila la kheri Mh.Mbunge.
 
Siku ya kufa nyani miti yote huteleza,hata kama wakiungana haitasaidia chochote kwa kuwa wote wako hoi kisiasa.Zitto na act-wazalendo yake ni bonge la mlaghai na mzushi mkubwa,mbowe na chadema yake the same na zaidi.Huo muungano wao utakuwa hauna afya na utakuwa chanzo wa migogoro zaidi kati yao hapo baadaye kwa kuwa wote ni wapenda madaraka na wabinafsi.
 
Ubinafsi wa mbowe anaiponza cdm,hapakuwa na sababu yakuwafukuza akina zitto,mwigamba,kitila wakati ule maana ile ndio ilikuwa reflection ya demokrasia ,mbowe kwa elimu yake ndogo akatafasri ni usaliti,akisaidiwa na wavuta mbagi wake akina lema
 
ACT ina nguvu mkuu. Kilichopunguza spidi ya ACT ni hili janga la corona ila ni chama ambacho kinakuja juu sana
Na ni chama ambacho kitakuja kuwa tishio sana kwa CCM endapo strategies fulani fulani wakizitumia..
Vyama vya upinzani hata wakijngana au ikawekwa Tume ya Uchaguzi kutoka Mbinguni, kamwe hawatashinda Uchaguzi Mkuu mwaka huu, labda 2025. Sababu ziko wazi kwani mwenye macho anaona na mwenye masikio anasikia.

Wakati viongozi wa upinzani wakiibeza, kuitukana, na kuizushia uwongo Serikali:-
√ Wapiga kura wanaona walivyo na wanavyo boreshewa miundo mbinu ya kukuza uchumi na huduma za jamii (afya, elimu, maji, umeme, nk);
^ Wapiga kura wanasikia kejeli za upinzani dhidi ya Rais na viongozi wenzake;
√ Wananchi majimboni wanaona jinsi wabunge wao wanavyoshiriki nao katika shughuli za maendeleo;
√ Wananchi wanasikia michango ya Wabunge Bungeni iwapo inawalenga au ni kwa mbunge kujijenga binafsi;
√ Na kadahalika.
 
Mpaka sasa kuna idadi kubwa ya Wabunge walioondoka CHADEMA kwa sababu mbalimbali. Lakini ni ukweli ulio wazi kabisa mpaka sasa chama kinadhoofu (Ikumbukwe kuondoka kwa hao wabunge haimaanishi kuwa wanaondoka na wanachama ila inasababisha sintofahamu kwa wanachama).

Unganiko lenu na ACT WAZALENDO ndio suluhu ya kukiokoa chama kisizame. Nina uhakika awamu ya 2020-2025 ndio itakuwa kuchakaa rasmi kwa CHADEMA na kuundwa chama kingine kikuu cha upinzani.

NCCR Mageuzi haiwezi kuwa tishio kwa CHADEMA. Mbatia hana ushawishi katika siasa za Tanzania ukilinganisha na Zitto Kabwe.
Siasa za upinzani zinahitaji muunganiko wa Lissu, Zitto na Maalim Seif. Hawa naweza kusema ndio wanaobeba upinzani kwa sasa. Mbowe ana siasa za matukio (kwenye ukweli tuseme).

Hii "combination" ya ZItto na Lissu ni hatari maana ni watu ambao wanajua kuanzisha hoja na kuisimamia na wana ushawishi mkubwa sana.

Mpaka sasa CHADEMA ishajua wasaliti wao ni akina nani. Zitto hakuwa msaliti na ndio maana hata alipofukuzwa CHADEMA alipoteza ubunge na hakuhamia CCM akaenda kuanzisha chama na huko akapita ubunge tena kwa kuhama jimbo (kitu ambacho Mbatia hawezi; alipigwa mtama na Mdee Kawe akaenda kwa Lyatonga Vunjo-Nguvu ya UKAWA ndio ikamuweka pale alipo). Hawa wengine mliowafukuza uanachama wamerudi CCM moja kwa moja.

Ushauri wangu achaneni na kujiona ndio mnaimarika bali fahamuni ya kuwa chama kinakufa na suluhu ni kuungana na ACT-Wazalendo hata kama hamtachukua dola lakini mtajiongezea idadi ya viti bungeni na hivyo kuipunguza monopoly ya CCM bungeni.

Achaneni na propaganda za kina Yericko wao siku zote wanamuona ZItto ndio adui namba moja wa CHADEMA. Unganeni na ACT mlete upinzani kwa CCM tofauti na hapo hiyo October mtapata wakati mgumu na mnaweza hata msipate wabunge (Sio kwa sababu watapigia kura CCM bali morale ya wanachama wenu itapungua sana na uwezekano wa wanachama wenu kutopiga kura ukawa mkubwa kutokana na kile kinachoendelea sasa).

Nawasilisha!
Waungane na NCCR mageuzi
 
Wazo zuri. Ila kuna ukweli watu wanaukwepa kuusema. Kudhoofika kwa CHADEMA ni matokeo ya CCM kutoa Rais mkristo! Wale wachungaji na maaskofu waliokuwa wanaipa CHADEMA nguvu sasa wanashabikia CCM. Kumbe na wao walikuwa na masai tofauti na ya CHADEMA ambayo sasa wanayapata CCM!
Pia kuna swala la kuhodhi na kujiona bora! Hili ndilo lilimfanya maaliim Seif achague kujiunga ACT badala ya CHADEMA! Huo muungano mnaouwaza utawezekana kama CDM itakubali kuwa "equal partner"!
 
Acha kushawishi watu wasipige kura mkuu, Kupambana ni muhimu kivyovyote vile.

Fahamu hili kuwa haitatokea kamwe CCM kuweka tume huru. Ni kupambana nao tu mpaka kieleweke
Upo sahihi mkuu.tume huru kwa ccm hawawezi kuruhusu wapo tayari kwenda motoni kuliko kukubali tume huru
 
Aliondoka Slaa mkakesha mnapayuka kuwa ndiyo mwisho wa cdm lkn hii ni miaka mitano Slaa yupo ccm na cdm bado inawanyima usingizini
Mbowe hana impact yoyote kwa CHADEMA awepo au asiwepo hana madhara.

Ukweli ni kwamba kwa sasa CHADEMA akiondoka Lissu basi chama kimekwisha.

In God we Trust
 
Mnajiliwaza ili kesho mkakeshe vizuri kwenye mkesha wa kuiaga corona
Chombo cha kuzama siku zote huwa hakina usukani!

Watatapatapa mwishowe wataungana hadi na CCM,ACT yenyewe ni Zanzibar tu bara imesimamia mguu mmoja kama jini.

In God we Trust
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom