CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

Wakuu zangu wenye akili kubwa na Great thinker msifanye kuyasoma yote haya kwa ushabiki kama mnavyojaribu kuchagua upande pasipo kupima maneno ya mtu na UKWELI ni upi?

Kwanza kabisa inakuwaje watu leo mnamwona Dr.Slaa mlomuamini hadi kumpa ridhaa zenu agombee Urais leo ndiye muongo kwa sababu gani, wakati alozungumza karibu nusu yake ni fact mnazozifahamu toka zamani mkiwa Chadema Asilia? Kipi kimewachukiza zaidi kusema ni UFISADI wa Lowassa ama makosa yalofanywa na Chadema kumteua Lowassa kuwa mgombea Urais!.

Labda mimi nikammue hili jipu alopasua Dr.Slaa ambaye sasa mtaitwa Msaliti kwa sababu tu kasema ukweli usokubalika! Maana katika mila zetu msema ukweli usotegemewa huitwa muongo!. Swala la Ujio wa Lowassa Chadema, mimi nimelijua toka nikiwa Tanzania mwezi December mwaka jana! kwa hiyo huyu Tundu Lissu anachoongea nini? na anafikcha nini ili iweje maana ya Mujini sisi wengine ndio huamka nayo!

Halafu ikiwa kweli Dr.Slaa ndiye alochaguliwa kuwa mgombea Urais wa Chadema sijui toka April ilikuwaje asitangazwe muda woteee hadi Lowassa katemwa CCM! Mlisubiri nini hiyo kamati kuu kumtangaza Dr.Slaa maana asingeweza jitangaza mwenyewe! Ikiwa kweli hatua zote zimeshapitiwa na kumchagua yeye kwa nini hakutangazwa kama CUF walivyofanya mwezi wa 6? halafu nasikia madai mapya ya kwamba Dr.Slaa ndiye alokuwa kiungo baina ya Lowassa na Chadema! jamani jamani toka lini Lowassa akawa na ukaribu na Dr.Slaa? yaani Dr.Slaa amtume Gwajima kwa Lowassa pasipo Mbowe kujua ana mzee Mtei? Dr. Slaa awe na mamlaka hayo basi ingekuwa rahisi kwake hata kumkataa Lowassa Chadema wote mungemuunga mkono maana yeye mshenga ndiye alomleta..Iweje leo mkatae maoni yake yeye alomleta kana kwamba nyie ndio wenye muafaka naye!

Na toka lini Katibu mkuu awe na mamlaka zaidi ya Mwenyekiti au hata mkamati kuu kufikiria na kuandaa ujio wa Mgombea Urais? Hata yale ya mwaka 2010 ya ujuio wa JK na mtandao hakuhusika wala ya mwaka 2005 ya kina Sitta hakuhusika, iweje leo yeye ndiye awe kiungo na mtu ambaye hawatazamani hata usoni? Hivi nyie watu mnamjua chuki ilokuwepo baina ya Lowassa vs Dr Slaa kweli au mnasimuliwa tu vibarazani?

Humu Humu JF tulielezwa mazungumzo baina ya Chadema na Lowassa yalianza toka mwaa 2011, iweje leo mshangae na kusikiliza uongo wa Tundu Lissu mfitini mkubwa alozoea vya kunyonga toka wakati wa Zitto akiwa Chadema. Kusambaratika kwa Chadema kote kunamhusu mimi najua hilo na kwa uhakika na kila wakati yeye amekuwa akipanda ngazi kutafuta nafasi ya juu ndani ya chama tena basi alitaka yeye achaguliwe kuwa mgombea!. Abishe hapa JF kama nasema uongo...

Na toka lini mtu yeyote uwe kiongozi wa Chama umepitishwa kuwa mgombea URAIS na baraza kuu au mkutano mkuu halafu wewe wende kumtafuta mtu mwingine toka chama kingine sijui awe badala yako hii inaingia akilini kweli? Yaani leo CCM wampitishe Magufuli halafu yeye aende kumtafua Dr.Slaa wa Chadema ambaye sii mwachama atawaambia nini wana CCM hadi waridhike! Dr. Slaa alijuaje kuwa Lowassa hatapitishwa CCM hadi atafute mbinu ya kumleta Chadema ilihali yeye ni katibu mkuu tu, Je, katiba inampa mamlaka hayo?

Halafu kumbukeni vizuri kuwa Mzee Mtei alifunga safari kutoka Moshi kuja Dar kumshawishi Dr.Slaa ikashindikana, halafu ikasemekana Slaa katumiwa watu wengine kina Hemed Seif na Profesa Safari nyumbani kwake kisha Mbowe akasema Dr.Slaa anajipumzika atakuwa nao atakapo kuwa tayari hii ni katika kutambulishwa Lowassa!. Leo hata kupumzika kwake walokutangaza wenyewe wanasema ni uongo angekuwa kaacha siasa asingekuwa anatumia mali za Chadema.

Sasa kama kweli Dr.S;laa alikuwa bado Katibu mkuu wa Chadema kwa nini mli hack twitter yake, ukiingia unamkuta Lowassa akjitangaza katika ukumbi wa Dr. Slaa! WHY? tena baada tu ya yeye kuandika juu ya kuhofia maisha yake na maelezo machache sana kuhusu kupingana nanyi?..

Kwa nini mlimnyima Jukwaa leo mtasema alitaka mwenyewe ilihali mlimkataza asizungumze na chombo chochote cha habari laa sivyo maisha yake yako hatarini? Mimi nilibahatika kuyasoma haya aliyaandika Twitter yake, kina nyie mkadai kuwa huyo sio yeye ni mkewe anayeandika haya! Ati Dr.Slaa yupo nanyi anapumzika tu atakuja kumkabidhi Lowassa fomu ya kugombea Urais mara atakuwepo ktk ufunguzi wa kampeni? sio nyie Chadema kina Yericko na Tumaini!. Sisi wengine hatusahau maneno tukisoma yanakaa kichwani..

Sasa ngoja nimsome vizuri Tundu Lissu mfitini mkubwa, halafu nitakuja na maelezo yangu kwa ufasaha zaidi maana UKWELI sisi wengine tunaujua japo kuna mambo mengine unayaminya hadi yanapokufika kooni inabidi utatapike..
 
TUJITEGEMEE ahsante maana point ziko straight na hizo ndizo tutaziangalia kama tulivyosema

Mkuu Nguruvi3,
Mm binafsi nimemsikiliza kwa makini sana Dr.Slaa, na kama ulivyosema ni haki yake kabisa kujieleza na kuonesha hisia zake binfsi kwanini yupo nje ya siasa kwa sasa, ila kuna kitu nilikinote kikaniuma sana kwa mwanasiasa wa aina yake, japo wengi watanipinga ila kiukweki Dr. Leo alikua ameongozwa na hasira kali, jazba kiasi cha kumfanya kdg apoteze muelekeo au busara.

kwa nini nasema hivyo? Kuna vitu vya msingi sana angeweza kueleza watu wakamuelewa ila sasa yeye kafanya yafuatayo ( selected few), ambayo kwa mtazamo angeweza tu kutoyazungumza na kutoleta picha hii ambayo hadi baadhi ya watu wanahisi labda kanunuliwa au labda kuna kitu nyuma yake, japo mm binfsi siamini kama kanunuliwa maana ni mtu mwenye integrity kubwa sana.

1. Kuzungumzia namna vikao vilivyokwenda, mpaka isu za vimemo, najua hapa alikua anajaribu kuweka msimamo wake kwamba hakukubaliana na process toka mwanzo, though kasema yeye ndie aliyepigiwa simu wakamshirikisha mwenyekiti. Kwa hapa alipaswa tu kusema kama Pro. Lipumba kwamba nilishiriki vikao ila sikukukubaiana na process na nimeamua kukaa kando. Story zingine zoote zinakua zinainyesha kama kuna hadaa fulani na kujifanya ww mtakatifu au mkuu than others.

2 . personal attacks, bahati mbaya sana ni kama vile press conference ilikua maalumu kwaajili ya kuja kumzungumzia mtu fulani na wapambe wake na kusahau mada kuu, hapa mnaweza kusema alikua anasisistiza why anamkataa, lakini ni yeye pia aliyesema mwanzoni kwamba aliweka masharti, ina maana angeyakubali asingemchana chana kama alivyofanya, mambo hadi ya kuchambua hotuba, na kukomalia richmond mwanzo mwisho, ina leta sintofaham nini haswa liliku lengo kuu, maana pia indrect unawapa ahueni watu wengine. Mbaya zaidi katika kusema Lowassa ni kama anacollude na akina Sitta na Mwakyembe kwenye maelezo yake,na hapa inakua inaleta shida kdg, is there any communication going on btn them?
Busara nadhani hata asinugfika mbali na Lowassa wala sumaye angeweza kama nilivyoeleza hapo juu kwamba sijaridhiswha naa so nakaa pembeni.

3. Kugusia isu ya udini, yaanu hapa ndio kabisa ni damage kwa reputation yake, kama mnakumbuka majuzi Amon Mpanju kule Songea kwenye kampeni za uraisi amegusia the same issue na tukaipinga hapa kwamba sio sahihi. Wale mashehe najua mnafuatilia kuna viongozi wa kiislam wakiwahi kumfuata Dr. Awasadie isu yao na akawaahidi kuwapa mwanasheria awasadie sijui ni nani so anafaham vizuri kabisa, sikuona umuhimu wa kuongelea hata kwa mbali.

na habari za tuhuma za kuhongwa hizo sio sawa kabisa bila uthibitisho maana nikuleta kashfa mbaya sana kwa viongozi wa dini ambao kimsingi ni baba wa wote, udini, ukabila, ukanda, umadhehebu na ubaguzi wa aina yyt ile upigwe vita kabisa na hautakiwi kabisa kuhusiswa kwa chochote kwenye siasa maana ni sumu mbaya sana.

Mwisho,
Binafsi namuunga mkono Dr.Slaa kutumia haki yake ya kujieleza na pia kutakasa dhamira yake, najua ametathimini vya kutosha kabisa nini kitatokea kwa mustakabali wake kisiasa na pia kwa harakati za upinzani nchini, najua wengi imewauma sana kwa yanayoendelea kwenye siasa za Tanzania hasa za upinzani, bt ndio kuelekea kwenye democrasianya kweli.
 
kuna vipengele vya maelezo ya Slaa ambavyo sievielewi bado, kwa ujumla inaonekana kaosha mikono na ameweka lawama zote za ujio wa Lowasa kwa wengine, hii itamcost sana baadaye kwa mtizamo wangu

16. Nilitaka kujua ni mtaji gani lowassa atakuja nao na ni viongozi gan atakuja nao.

17. Nilijibiwa kuwa anakuja na wabunge 50 wa CCM, wenyeviti 22 wa mikoa na wenyeviti 80 wa wilaya.

Hii nilivyoelewa mimi ni kwamba Lowassa angekuja na hao viongozi hapo juu, Slaa asingekuwa na tatizo, angemkaribisha, Je ufisadi wa lowasa usingekuwa issue? Sielewi tatizo la Slaa, ni ufisadi wa lowasa au kuja kwa makapi badala ya mitaji? Au kingine pembeni? Shutuma zote za nini kama aliona Lowassa ni mtu anayefaa hata kukaa chini na kumpangia vigezo vya kuingia Chadema na kuthamini "mtaji" atakaoleta? Kwa nini hakukataa kabisa hata kujadili suala la Lowasa kwenda Chadema?

Kwa nini atoe maelezo sasa? Kwa nini hakujitokeza kusema yote haya mara tu baada ya Lowasa kupokelewa, kwa nini hakusema kabla ya Lowasa kuchukua fomu za uraisi kupitia ukawa? Je alitaka Lowasa aende chadema/ukawa akawe mwanachama wa kawaida ila awaletee wabunge 50, wenyeviti 22 wa mikoa na 80 wa wilaya?

47. Siku moja kabla ya ripoti kusomwa, nililetewa Rushwa ya milioni 500 ili tukaupindishe ukweli bungeni lakini nilikataa

Nani alimpa Slaa hii rushwa, kwa nini hamtaji, kutoa rushwa kupokea rushwa na kumficha mtoa rushwa/mpokea rushwa yote ni makosa makubwa.

53.Nilifanikiwa kuijenga Chadema na ikawa tumaini jipya la watanzania.....Vijana wangu wa Chadema, naomba niwe mkweli propaganda imekivamia chama.

Hii sentensi zinaondoa credibility ya kiongozi bora, Chadema haikujengwa na mtu mmoja, wapo wengi tu ambao wamepigwa, wamekufa, wamefungwa, wamenyanyasika bungeni wote hawa na viongozi wengine na wananchi wamejenga Chadema na kuifanya tumaini kwa watanzania

....Bado sielewi Slaa anamaanisha nini
 
Mkandara nadhani tuwe fair katika majadiliano.Ulivyoandika hapo juu ni kwa mwelekeo wa kukusanya watu wote kwa pamoja. Kama unafuatilia uzi, watu wanapingana kwa hoja na wamekuwa fair kwa kila mmoja

Pili, si vema ukapandikiza maneno. Ukitusoma hapo nyuma hakuna mahali Dr Slaa alijadiliwa hadi leo.

Nipo katika rekodi ya uzi huu nikiandika hivi ' Uamuzi wa DrSlaa kukaa pembeni uheshimiwe. Ni mtu aliyekitumikia chama chake hata kufikiamahali pa kuweka maisha yake rehani. Vijana wanaoandika katika mitandao waachemara moja.
Hao iwe ni wa M4C au Team Lowassa. Dr Slaa anastahili kuheshimiwayeye na maamuzi yake. Apewe muda wa kutahmini hali yake ya baadaye. Uamuzi atakaouchukua uheshimiwe''

Hayo maneno tumeandika mwezi mmoja uliopita. Sasa unapokuja na tuhuma za watu kusema ni msaliti au mungo si kweli

Hapo juu tumesema, tutatumia maneno yake katika kupima alichosema bila kumuonea au kumhurumia.

jitegemee kaleta point, pamoja na za wengine kama akina Alinda n.k.
Tutazitumia si kutuhumu, si kujibu bali kufanyia uchambuzi.

Ni kama ule wa hotuba ya UKAWA jangwani

Tujadili issue kama zilizvyo na si kama tunavyowahisi wenzetu au hisia zinavyotutuma
 
Last edited by a moderator:
Kwa mambo yanayotokea sasa hivi inahitaji utulivu sana kuamini hizi kauli za wanasiasa...

Kwa kauli alizozitoa leo na alizozitoa kipindi cha nyuma kuhusu Lowassa ni vigumu sana kuamini kwamba Dk. SLAA alianza kuzungumza na Lowassa kuanzia May....Hata uso wake tu Dk. SLAA unaeleza kila kitu...

Binafsi tangu mchakato wa kumuingiza Lowassa CHADEMA/UKAWA nimekosa kabisa imani na Mbowe...Lissu et al....Si wa kweli...Hasa walipokanusha kwa nguvu zote Lowassa kuhushuria CC ya CHADEMA kwa mara ya kwanza...

Hivyo nashawishika kuamini kwamba kauli nyingi alizoongea Lissu leo ni za kutunga....Hazina mashiko kwa kweli...

Ni kweli tunahitaji utulivu kuamini nani anasema nini..

Lakini tukiunganisha kauli ya Dr. Slaa na kauli ya Lissu unaona kuna ukweli kuwa Dr. slaa ndiye aliyemleta Lowassa Chadema.

Lissu anasema kuwa Dr. Slaa alishachaguliwa na chama siku nyingi kuwa mgombea wa urais. Kama tunakumbuka vizuri tuliona mahusiano ya Gwajima na Dr. Slaa na Gwajima na Lowassa na baadaye kuulizwa kuhusu husiano wake yeye (Gwajima) na Dr. Slaa alisema ni rafiki yake wa siku nyingi na ni muhimu awe karibu na Dr. Slaa au Lowassa maana hao mmoja wao ndio rais.

Hivyo utaona kuwa Dr. Slaa, Gwajima na Lowassa wanafahamiana vizuri tu kupitia Gwajima (kitu ambacho ni jambo jema.)

Tukirudi katika maelezo ya Dr. Slaa anasema kuwa "alipigiwa simu na mshenga (ambaye ni Gwajima) akamwambia habari zilizopo ni Lowassa kakatwa na Dr. Slaa akasema mpaka aongee na Mwenyekiti..

Hivyo hapa utaona yale maneno ya Lissu yanaleta picha kuwa alishaongea na kuhusu Lowassa kujiunga na Chadema tangu May maana kama hisingekuwa hivyo basi hii simu ya Gwajima hisingekuwa Lowassa kakatwa bali ingekuwa ya kutakama maongezi ya Dr. Slaa kuhusu Lowassa.
Baada ya hapo kilichotokea ni Dr. Slaa kuongea na Mwenyekiti wake juu ya wazo la kumleta Lowassa...

Sasa basi kama huyu ndio kamtoa Chadema ni kitu kilichomfanya yeye alete ili wazo la Lowassa kujiunga nao? Kuna siri gani nyuma ya Dr. slaa kuhusu Lowassa?

Habari za uhakika ni kuwa Dr. Slaa alilala Serena Hotel, na kabla ya mkutano alikuwa na Dr. Mwakyembe.. (Tunajaribu kuunganisha dot tu)
 
HOTUBA YA DR SLAA

MTAZAMO KUHUSU HOJA, MAONI,TUHUMA, UKWELI

Sehemu ya I

Dr Slaa ametoa ya maoyoni baada ya kimya cha takribani mwezimmoja.
Slaa ametumia haki ya kutoa maoni kama mtu na kiongozi wajamii mwenye wafuasi

Slaa ana uhuru wa kueleza chochote anachoona hakubaliani auanakubaliana nacho.
Maoni yake hayapimwi kuwa sahihi au la, lakini yapo wazikupimwa usahihi na upotofu wake kwa mitazamo tofauti

Katika hotuba, Slaa ana sisitiza jambo muhimu la redibility, yaani ubora wa kujiamini na kuaminiwa.
Ametahadharisha kuhusu uongo na upotoshaji,

Yote hayo ni ukweli usio na shaka. Amejenga taswira yakekatika msingi huo

Tupitie kauli zake

1 Dr anasema alijiuzulu siasa tarehe 28 mwezi July. Kwa sikuya leo ni mwezi mzima'
Hoja yetu: Tarehe hii ni muhimu kwani inaeleza matukio mengine yanayofuata

2 Dr Nimeamua kujitokeza leo kukomesha upotoshaji na kuwekawazi ukweli
Hoja: Kipindi cha mwezi mmoja wa uKimya, ni muhimu sana ili kutoanafasi ya kutahmini, kupunguza jazba na kuweka ukweli katika muktadha mzuri.Hatudhani Slaa alipaswa kukomesha upotoshaji kwa kujitokeza.

Tunadhani ni muhimu alipojitokeza kuelezaupande wake. Hivyo, ni busara kutumia maneno ili yailete maana isiyokusudiwa

3 Sina ugomvi na kiongozi yoyote maana siasa si uadui
Hoja yetu: Unapjitokeza ‘kukomesha' kama ilivyo namba 2 juu, unajenga mazingira unatofautiana na maelezo ya namba 3

4 Niliamua kuachana na siasa tarehe 28.7.2015 saa sita usiku
Hoja:Lipumba alipoachana na siasa, siku hiyo aliita waandishi.Kwa mwezi mzima hujitokeza kueleza hilo.

Kama upotoshaji upo, pengine wakulaumiwa ni wewe. Ulikuwa na fursa ya kutoa sentensi moja tu ' Nimeacha siasa'iwe kwa twitter au waandishi wa habari

5 Dr. Ni kweli nilishiriki kumleta Lowassa lakini nilikuwana misimamo yangu iliyotufanya tuseielewane
Hoja: Dr Slaa anakiri mwenyewe kushiriki katika kumleta Lowassa.
Hoja hii ni muhimu kwasababu itajibu hoja zingine mbele ya safari au bandiko.

6 Dr Slaa , baada ya lowassa kukatwa, Gwajima alinipigiasimu kujua nini cha kufanya
Hoja: Gwajima alishakiri kuwa na uhusiano na Lowassa. Na hapa anatajwa na Slaa kuwa Mshenga.
Hakuna shaka yoyote kuwa utatu waLowass-gwajima-Slaa ni wa kweli

Jambo la kujiuliza, Gwajima mtu wa Lowassa wa CCM,anampigiaje simu katibu mkuu wa chama cha upinzani kujua nini cha kufanya?Inaonekana mawasiliano haya kuanza siku hiyo, bali kujua ninicha kufanya baada ya Lowassa kukatwa

7 Dr Slaa, nilimpigia mwenyekiti Mbowe na tukakubalianakuwasikiliza
Hoja ; Ni wazi kuwa Dr Slaa alikuwa tayari kuwasikiliza .Rejea hoja 5 Dr anapokiri kumleta Lowassa

Inaendelea
 
Sehemu II

8 Dr Slaa, kabla ya kuanza kuwasikiliza msimamo wanguulikuwa Lowassa atangaze kuhamachama,aweke wazi ni chama gani anakwenda na ajisafishe juu ya tuhuma

Hoja: Hata kabla ya kuwasikiliza, Dr Slaa alishajua wanatakakuhamia CDM ndio maana akaweka msimamo.

Rejea hoja namba 5 ya ushiriki wakumleta Lowassa, na namba 6 ya mawasiliano na Gwajima.

Ni fair kusema , kabla hajampigia simu mwenyekiti tayari allikuwa na msimamo aliouweka wazi kabla ya kuwasikiliza.

Hapa pia kuna hoja, kwamba Ufisadi wa Lowassa kama tutakavyoona mbeleni haukuwa tatizo.

Kilichotakiwa ni kujisafisha tu na kueleza umma anajiunga na chama gani.
Hivyo, ni fair kusema baada ya maongezi na Gwajima, hakukuwa na tatizo la Ufisadi, tatizo lilikuwa kujisafisha.

9 Dr Slaa, tangu akatwa Lowassa hakutangaza kuhama CCM au kujisaifisha na tuhuma kitu kilichonifanya nitofautiane naye
Hoja: Dr Slaa alikuwa hajaona ufisadi hadi hapo. Alichotakani kujisaifisha tu

10 Slaa, Niliwaulizawanachadema wanzangu, Lowassa anakuja kama mtaji au Mzigo?

Hoja: Hapa kuna tatizo. Kuanzia hoja yake namba 5 ya MshengaGwajima kumpigia,namba 7 ya kumpigia mwenyekiti, mhusika mkuu alikuwa Dr Slaa.Sasa vipi aseme ‘niliwauliza wenzagu' !

Anauliza nini wakati ndiye alikuwa kiungo? Lowassa anakuja kama mtaji au Mzigo?
Hapa yeye aliyekuwa na mawasiliano ndiye angepwaswa kuwaeleza wenzake, si kuwauliza

11 Slaa, nilitaka kujua ni viongozi gani na mtaji ganianaokuja nao Lowassa?

Hoja: Well, Dr Slaa alichotaka kujua ni mtaji na wa ukubwagani.
Kumbuka hapa suala la ufisadi lilikuwa halina mashiko kabisa

12 Dr, nilijibiwa anakuja na wabunge 50, wenyeviti 22 na 80wa wilaya
13 Baada ya hapo nilitaka kujua majina ya hao watu laikinihadi July 25 sikupewa

Hoja: Kumbuka kuwa Dr Lowassa aliacha siasa July 28. Siku 3 kabla alikuwa hajapata majina ingawa alijua Lowassa anakuja. (Rejea hoja ya 1).Hapa ufisadi hakuliona, alichotaka ni majina ya wanao ambatana naLowassa ili ayafanyie kazi

Ni ushahidi kuwa Dr Slaa alikuwa bega kwa began a wenzakehadi siku 3 kabla ya July 28

14 na 15 Dr Salaa, niliambiwa kuitisha kikao cha dharura nikagoma kwasababu sikupewa majina.
Katika kikao ( hicho hicho alichogoma)mabishano makali yalizuka , msimamo ulikuwa ule ule kujua mchango wa Lowassa

Hoja: Hadi hapo Dr alishakubali ujio bila kusafishika.
Kilichogomba ni kutaka kujua anakuja na nini, yaani atachangia nini katika chama kwa ujio wake.

Tunarudia, suala la ufisadi halikuwepo kichwani kwa Dr Slaa hadi muda huo.

16 Kesho yake nikaandika barua rasmi ya kujiuzulu
Hoja: Baada ya barua ya kujiuzulu Dr alipaswa pia kuutarifu umma ili kukwepa upotoshaji.
Hakufanya hivyo kwa mwezi mzima kuanzia tarehe 28July

17 Dr Slaa, Kikao kilivunjika na kesho yake picha zikaanzakusambaa mitandaoni tena viongozi wakikana

Hoja: Ni kweli na sote tulikemea upotoshaji huo. Tupo katika rekodi tukisema kama ni kweli lipo tatizo. Kwanini wafiche fiche ukweli waliokuwa wanaujadili?
 
sehemu ya II

18 Dr Slaa, Lowassana wapambe wake ni waongo maana hakuna kipengele hata kimoja walichotekeleza

Hoja: Kwa maelezo ya Dr hakukuwa na maafikiano. Lowassaangetekeleza vipi ikiwa wao wenyewe hawakukubaliana? Tunarudia hadi hapo sualala Ufisadi halikuwa tatizo kwa Dr Slaa, tatizo ni kutangaza kuhama chama nakujisafisha

20 Dr, tultaka hao wabunge 50 waje kwanza kabla ya mchakatowa CCM kuanza
Hoja: Kimsingi alikubaliana na yote, isipokuwa alitaka kuona huo mtaji.
Tunarudia , suala la ufisadi halikuwa tatizo kabisa kwa Slaa

21 Dr , napinga kuchukua makapi ya CCM kuyaita mtaji
Hoja: Ni kweli na wengine tupo katika rekodi tukileza hayo.
Tofauti na Dr Slaa, yeye ndiye alikuwa kiungo cha ujio wa makapi kupitiamshenga Gwajima.

Yeye ndiye aliyeweka masharti ya kutekelezwa kabla ya makapihayajawa ngano bora.

Dr Slaa hapa amejichanganya sana. Anawezaje kupinga shughuli aliyoratibu na Gwajima kuanzia mwanzo?

Gwajima alipomuuliza, nini chakufanya kwanini Dr asiseme ‘hakuna kupkea makapi?
Ilikuwaje akawasiliana namwenyekiti wake kujadili makapi?

22 Mtu kama Sumaye ni fisadi na nilikuwa siongei naye
Hoja: Hapa tunarudi kule mwanzo kabisa kwenye tarehe. Dr aliacha siasa July 28.

Sumaye amekuja UKAWA mwishoni mwa August. Dr hakujua Sumaye yumo.

Sumaye mwenyewe kasema aliwahi kukanusha hadi siku aliposema anahamia UKAWA

Leo Dr anapomshirikisha katika maamuzi aliyofanya takribanimwezi mzima si haki.

Akina Sumaye ni zao tu , labda angemuuliza Gwajima aliyeshirikiana naye nani watakuja. Hakumuuliza.

Hivyo Sumaye ni ‘out' katikahoja za Slaa

Kama ana ‘bifu' na Sumaye, hilo ni tatizo lililopo nje yatatizo analoongelea la chama chake.

Leo akitokea MCCM kaujiunga na UKAWA,haiwezi kuwa ndiyo sababu ya Slaa kuachia ngazi.

Hii ilikuwa personal attack yakuhalalisha hoja yake, kimsingi hakuna hoja. Huo ni ukweli

23 Dr ,Tulitaka mtaji kutoka kwa Lowassa na siyo makapi
Hoja: Lowassa mwenyewe ni Kapi. Ulitaka mtaji upi ikiwaulijua yeye ni kapi mwandamizi ‘senior kapi'?
Lakini pia inaonyesha Dr Slaaalikuwa tayari kumpokea Lowassa. Alishasahau ufisadi, tatizo ni mizigo ya Lowassa

24 Dr, Wenyeviti walioletwa na Lowassa ni mizigo. Akithubu tunamwaga uozo wake
Hoja: Dr Slaa wewe si ndiye uliyekuwa kiungo.

Hukuona uozohuo mapema hadi ulipoamaua kuwasiliana na mwenyekiti wao.
Leo kipi unachoonahakikuwa sawa ikiwa ulikuwa bega kwa bega na mshenga Gwajima?

25 Dr, Mimi nilikuwapo wakati wa sakata la Richmond linajadiliwa, nina ugomvi wa muda mrefu na Lowassa
Hoja: Maneno ya ufunguzi katika hotuba yake alisisitizasiasa si uadui .

Hapa anatueleza ana ugomvi na Lowassa kama adui yake kisiasa.

Lakini pia si Slaa huyu ndiye aliyekuwa kiungo muhimu cha ujio wa Lowassa?

Alikubali vipi kuongea na mshenga wa mgomvi wake?

Iaendelea
 
sehemu ya IV

26 Dr Siku moja kabla ya kujadiliwa, nililetewa rushwa yamilioni 50 kupindisha ukweli
Hoja: Dr na akina nani usioweza kuwataja ikiwa unawataja wahusika na akina Sumaye?
Kuna nini nyuma ya pazia kiasi cha kutuificha baadhiya wahusika, ukituaminisha ni watu wachache wanaoitwa mafisadi? Nani alileta hongo? Kwanini huwataji?

26 Dr, Lowassa haaminiki ni muongo na hapaswi kuwa Rais wanchi
Hoja: Ni Lowassa huyo huyo kupitia mshenga Gwajima ulikuwana maongezi naye tena ukitamka ajisafishe ili umukubali.

Vipi uongo unaanzia wapi ikiwa umekiri kushiriki kumleta na kutueleza kila hatua?
Hafai kuwa Rais lini ikiwa wewe ndiye uliyeulizwa na Gwajima ;tufanyaje'?

27 Dr Slaa Lowassa ni fisadi na kama anabisha ajitokeze
Hoja: Kama mtakumbuka tumeonyesha hatua zote ambazo Dr Slaa alikuwa anashiriki bila kuona ufisadi wa Lowassa.

Mwisho wa hotuba yake anaona ufisadi alioshindwa kuoona wakati anaongea na mshenga Gwajima , wakati anatoa mashrti, wakati anaeleza kushindwa kutekelezwa kwa mashrti

Hivi masharti gani yanaweza kumsafisha fisadi?

28 Dr, Lowassa kasema ataleta maji, mbona jimbo lake Mondulihalina maji
Hoja: Je hizi ndizo sababu zilizokuzuia kumkubali ingawaulishiriki kumleta?
Mambo ya maji yanahusiana vipi na kujiuzulu kwako kutokanana ugomvi na viongozi wenzako?

29Anasema kaanzisha shule za kata…
Hoja: Shule za kata zina uhusiano gani na kujiuzulu kwako?Je wakati ukiwa na mshenga Gwajima hukujua haya?
Mbona yameongelewa wakati anatafuta udhamini CCM? Uhusiano upo wapi kati ya kujiuzulu kwako na shule za kata?

30 Dr, Chadema inajaza watu kwa mabasi mkidanganya ni mafuriko
Hoja: Dr kama ulivyosema kuhusu credibility, je ukiambiwautoe ushahidi utatoa? Na huko kwingine mabasi yapo wapi?

Wakatiwa kuchukua fomu mbasi yaikuwepo? Una ushahidi wowote wa maana.

Kama wanabebwa na mabasi, hilo linahusiana vipi na kujiuzulu kwako?

31 Dr, RaiS hana mamlaka ya kumtoa Babu Seya, asiwadanganye
Hoja: Dr Slaa, haya yana uhusiano gani na maongezi yako na mshenga Gwajima,na ushiriki wako kumleta Lowassa?
Yametoka wapi ikiwa hukuyajali mapema?

Kulikuwa na haja ya kuongelea mambo hayo wakati unazungumzia hatma yako kisiasa na kilichotokea?

32 Dr, Sumaye aliamuru Polisi wavamie misikiti na Mbwa

Hoja: Lini ukiwa katibu mkuu ulizungumzia hili? Dr Slaa, una ushahidi wa kutosha na kwanini hukuusema nyakati hizo katika kutetea haki?

Sumaye ana uhusiano gani na kujiuzulu kwako nay ale yaliyotokea kati yako naviongozi wenzako

33 Dr, msikubali Rais muongo na mimi nitapiga kelele kilakona kumpinga Lowassa
Hoja: Kama utafanya hivyo hakuna tatizo kwasababu ni hakiyako. Lakini lazima uwe na NGO yenye malengo yanayoeleweka. Au uwe na chama chasiasa.

Ukipiga kelele asichaguliwe una haki ya kupiga kelele nani achaguliwe,Dovutwa , Magufuli au Anna

Kumbuka, ukistaafu kisiasa hujihusishi na siasa. Hapa tutunahoji kauli yako, credibility ya maneno yako ipo wapi?
Unastaafu wakatiunazunguka kila kona kupiga siasa

34 Dr, Naomba nsiongee mengi maana nitakosa ya kuongea sikunyingine
Hoja: Siku ipi tena wakati umestaafu siasa?

35 Dr, Siku nyingine nitakuja kuongea kuhusu hisa za Lowassakwenye kampuni
Hoja: Mzee , si umesema unastaafu na uliacha tangu July 28?
Utarudi katika kampeni kama nani na mgongo upi? Dr Slaa lile neno credibilityunalitumia siku gani?

36 Dr, Nihitimishe kwa kusema sina chama na ninastafu siasa.Nitaendelea kutumikia nchi
Hoja: Kama utarudi katika kampeni utakuwa hujastaafu. Kama utapiga kampeni za utakuwa una chama.

Swali la kujiuliza ni chama gani hichousichokisema? Dr Slaa, maneno yako katika namba 2 ni kukomesha upotoshaji.

Bado unasimama na maneno hayo baada ya hoja hizo hapo juu?

37 Narudia tena sina chama na sitajiunga na chama chochote
Hoja: Ukipiga kampeni hata kama huna chama utakuwa na chama.

Ukipiga kampeni, hujastaafu bali umepunzika kutoka active politics.

Hapa narudia, credibility ya maneno iko wapi mzee wetu?

Wanajamvi, hayo ni kwa uchache. Inatosha kusema kuwa baadhiya hoja za Dr Slaa tumezijadili kwa mantiki hapa duru. Tulisimama kuhoji analysis na kama kulikuwa na uchambuzi wa kutosha

Kinachosikitisha, baada ya muda wa mwezi, tulitegemea busaraza Dr Slaa katika kueleza kile kinachotokea.

Akiwa na ‘credibility' Drameshindwa ku maintain credibility ya kuhifadhi mambo yaliyokuwa ya kiofisi.

Ametutia wasi wasi kuhusu motive ya hotuba yake. Haionekani kama alitaka kufafanua, bali alikuwa katika kampeni

Dr ameshindwa kutetea hoja zake. Haina maana hoja zake hazikuwa na mantiki, la hasha.

Kilichotokea ameongozwa na hisia na jazba nakupotea sehemu muhimu ya sifa zake, yaani busara.

Mambo mengine aliyoongea hayakupaswa kuwa katika public domain kama kiongozi.

Pengine anasababu zakufanya hivyo, muda utasema

Dr ana haki za kushiriki au kutoshiriki siasa. Haki zakuzungumza na kupanga anachokiamini.

Katika kufanya hivyo lazima asimame katika‘credibility' ili Slaa ‘preach what you practice'

Kwa muda huu tungemshauri atulie.

Heshima yake kwa mwezi mmoja uliopita ilikuwa kubwa sana.

Ana sifa za kipekee na ni wakati sasa aangalie anazungumza nini na kwa wakati gani ili kulinda hsehima yake.

Tusemezane
 
Wakuu zangu wenye akili kubwa na Great thinker msifanye kuyasoma yote haya kwa ushabiki kama mnavyojaribu kuchagua upande pasipo kupima maneno ya mtu na UKWELI ni upi?

Kwanza kabisa inakuwaje watu leo mnamwona Dr.Slaa mlomuamini hadi kumpa ridhaa zenu agombee Urais leo ndiye muongo kwa sababu gani, wakati alozungumza karibu nusu yake ni fact mnazozifahamu toka zamani mkiwa Chadema Asilia? Kipi kimewachukiza zaidi kusema ni UFISADI wa Lowassa ama makosa yalofanywa na Chadema kumteua Lowassa kuwa mgombea Urais!.

Labda mimi nikammue hili jipu alopasua Dr.Slaa ambaye sasa mtaitwa Msaliti kwa sababu tu kasema ukweli usokubalika! Maana katika mila zetu msema ukweli usotegemewa huitwa muongo!. Swala la Ujio wa Lowassa Chadema, mimi nimelijua toka nikiwa Tanzania mwezi December mwaka jana! kwa hiyo huyu Tundu Lissu anachoongea nini? na anafikcha nini ili iweje maana ya Mujini sisi wengine ndio huamka nayo!

Halafu ikiwa kweli Dr.Slaa ndiye alochaguliwa kuwa mgombea Urais wa Chadema sijui toka April ilikuwaje asitangazwe muda woteee hadi Lowassa katemwa CCM! Mlisubiri nini hiyo kamati kuu kumtangaza Dr.Slaa maana asingeweza jitangaza mwenyewe! Ikiwa kweli hatua zote zimeshapitiwa na kumchagua yeye kwa nini hakutangazwa kama CUF walivyofanya mwezi wa 6? halafu nasikia madai mapya ya kwamba Dr.Slaa ndiye alokuwa kiungo baina ya Lowassa na Chadema! jamani jamani toka lini Lowassa akawa na ukaribu na Dr.Slaa? yaani Dr.Slaa amtume Gwajima kwa Lowassa pasipo Mbowe kujua ana mzee Mtei? Dr. Slaa awe na mamlaka hayo basi ingekuwa rahisi kwake hata kumkataa Lowassa Chadema wote mungemuunga mkono maana yeye mshenga ndiye alomleta..Iweje leo mkatae maoni yake yeye alomleta kana kwamba nyie ndio wenye muafaka naye!

Na toka lini Katibu mkuu awe na mamlaka zaidi ya Mwenyekiti au hata mkamati kuu kufikiria na kuandaa ujio wa Mgombea Urais? Hata yale ya mwaka 2010 ya ujuio wa JK na mtandao hakuhusika wala ya mwaka 2005 ya kina Sitta hakuhusika, iweje leo yeye ndiye awe kiungo na mtu ambaye hawatazamani hata usoni? Hivi nyie watu mnamjua chuki ilokuwepo baina ya Lowassa vs Dr Slaa kweli au mnasimuliwa tu vibarazani?

Humu Humu JF tulielezwa mazungumzo baina ya Chadema na Lowassa yalianza toka mwaa 2011, iweje leo mshangae na kusikiliza uongo wa Tundu Lissu mfitini mkubwa alozoea vya kunyonga toka wakati wa Zitto akiwa Chadema. Kusambaratika kwa Chadema kote kunamhusu mimi najua hilo na kwa uhakika na kila wakati yeye amekuwa akipanda ngazi kutafuta nafasi ya juu ndani ya chama tena basi alitaka yeye achaguliwe kuwa mgombea!. Abishe hapa JF kama nasema uongo...

Na toka lini mtu yeyote uwe kiongozi wa Chama umepitishwa kuwa mgombea URAIS na baraza kuu au mkutano mkuu halafu wewe wende kumtafuta mtu mwingine toka chama kingine sijui awe badala yako hii inaingia akilini kweli? Yaani leo CCM wampitishe Magufuli halafu yeye aende kumtafua Dr.Slaa wa Chadema ambaye sii mwachama atawaambia nini wana CCM hadi waridhike! Dr. Slaa alijuaje kuwa Lowassa hatapitishwa CCM hadi atafute mbinu ya kumleta Chadema ilihali yeye ni katibu mkuu tu, Je, katiba inampa mamlaka hayo?

Halafu kumbukeni vizuri kuwa Mzee Mtei alifunga safari kutoka Moshi kuja Dar kumshawishi Dr.Slaa ikashindikana, halafu ikasemekana Slaa katumiwa watu wengine kina Hemed Seif na Profesa Safari nyumbani kwake kisha Mbowe akasema Dr.Slaa anajipumzika atakuwa nao atakapo kuwa tayari hii ni katika kutambulishwa Lowassa!. Leo hata kupumzika kwake walokutangaza wenyewe wanasema ni uongo angekuwa kaacha siasa asingekuwa anatumia mali za Chadema.

Sasa kama kweli Dr.S;laa alikuwa bado Katibu mkuu wa Chadema kwa nini mli hack twitter yake, ukiingia unamkuta Lowassa akjitangaza katika ukumbi wa Dr. Slaa! WHY? tena baada tu ya yeye kuandika juu ya kuhofia maisha yake na maelezo machache sana kuhusu kupingana nanyi?..

Kwa nini mlimnyima Jukwaa leo mtasema alitaka mwenyewe ilihali mlimkataza asizungumze na chombo chochote cha habari laa sivyo maisha yake yako hatarini? Mimi nilibahatika kuyasoma haya aliyaandika Twitter yake, kina nyie mkadai kuwa huyo sio yeye ni mkewe anayeandika haya! Ati Dr.Slaa yupo nanyi anapumzika tu atakuja kumkabidhi Lowassa fomu ya kugombea Urais mara atakuwepo ktk ufunguzi wa kampeni? sio nyie Chadema kina Yericko na Tumaini!. Sisi wengine hatusahau maneno tukisoma yanakaa kichwani..

Sasa ngoja nimsome vizuri Tundu Lissu mfitini mkubwa, halafu nitakuja na maelezo yangu kwa ufasaha zaidi maana UKWELI sisi wengine tunaujua japo kuna mambo mengine unayaminya hadi yanapokufika kooni inabidi utatapike..

hebu twende taratibu bila jazba.. Ni nani aliyemleta Lowassa Chadema? na kwanini?
 
Pale ambapo unapoamua kuchagua ukweli upi wa kuusema huku ukiweka akiba ya mengine sijui unafanya hivyo kwa maslahi ya nani? Kwa nini usiuweke ukweli wote hadharani once and for all? Pale ambapo mtuhumiwa wa ufisadi hajakamatwa wala kuchukuliwa hatua zozote za kisheria kwa miaka 8 huku nyaraka za ushahidi ziko mifukoni mwa watu wanazitumia kwa ajili ya vijembe tu mtaani and nothing more happens!
 
Kwa mambo yanayotokea sasa hivi inahitaji utulivu sana kuamini hizi kauli za wanasiasa...

Kwa kauli alizozitoa leo na alizozitoa kipindi cha nyuma kuhusu Lowassa ni vigumu sana kuamini kwamba Dk. SLAA alianza kuzungumza na Lowassa kuanzia May....Hata uso wake tu Dk. SLAA unaeleza kila kitu...

Binafsi tangu mchakato wa kumuingiza Lowassa CHADEMA/UKAWA nimekosa kabisa imani na Mbowe...Lissu et al....Si wa kweli...Hasa walipokanusha kwa nguvu zote Lowassa kuhushuria CC ya CHADEMA kwa mara ya kwanza...

Hivyo nashawishika kuamini kwamba kauli nyingi alizoongea Lissu leo ni za kutunga....Hazina mashiko kwa kweli...

Dr. Slaa alisema kabisa kuwa Gwajima alimpigia simu baada ya Lowasa kukatwa. Akataka kuongea kwanza na uongozi wa Chadema akimaanisha kabla ya hapo kulikuwa na mazungumzo ya awali kati ya Dr. Slaa na Lowasa kupitia Gwajima.
 
Kama nilimsikiliza vizuri Dk. SLAA na kama nimekuelewa vizuri ni kwamba Gwajima alimpigia Dk. SLAA baada ya Lowassa kukatwa...Na Lowassa alikatwa tarehe 11/07/2015...

Shaka yangu ni hilo la mwezi Mei lililoongelewa na Tundu Lissu....Sina shaka na kupigiwa simu na Gwajima baada ya Lowassa kukatwa...
 
Kwa jinsi tunavyomuelewa Dr. Slaa kwa swala la Lowassa hisingekuwa rais Gwajima ampigie simu tu from nowhere kumueleza kukatwa kwa Lowassa na Dr. Slaa ajibu mpaka niongee na Mwenyekiti..

Ndio maana kauli ya Lissu kwangu inaleta mantiki kuwa Dr. Slaa, Gwajima na Lowassa walikuwa na maongezi kabla ya Lowassa kukatwa inaweza kuwa ni May au June au hata July mwanzo...Sasa kama anafahamu uchafu wa Lowassa na huu uchafu wa Lowassa ndio ulimfanya yeye kuachana na siasa ni kwanini yeye kupeleka wazo la Lowassa kuhamia Chadema?
 
Urafiki wa Gwajima na Slaa si kitu kipya mkuu wangu...Kama ilivyo urafiki wa Gwajima na Lowassa...

Slaa amekuwa akihudhuria ibada kwenye eneo la kuabudia la Gwajima pale Kawe mara nyingi tu....Na hata Slaa mwenyewe jana amekiri kwamba Gwajima ni rafiki yake kwa muda mrefu....

Mantiki ya Gwajima kumpigia simu Dk. SLAA kumuomba wampokee Lowassa mbona iko dhahiri mkuu?...Usiniambie hata Sumaye aliyehamia CCM baada ya kukatwa ama Msindai,Masha na Mahanga waliohamia CHADEMA baada ya kushindwa kura za maoni CCM nao walikuwa na mawasiliano na CHADEMA kabla...

Sote tunajua kwamba Gwajima ni mfuasi/mtu wa karibu sana na Lowassa...Yuko tayari kufanya/kusema lolote kuhakikisha kwamba Lowassa anafanikiwa/anasonga mbele...Si ajabu kwa Gwajima kumpigia simu Slaa kumuomba wampokee Lowassa(kutokana na ukaribu wao)..Kwenye siasa lolote laweza kutokea (muda wowote)...Mara baada ya ujio wa Lowassa CHADEMA na mara baada ya Dk. SLAA kujiweka kando kuna vyama vingi tu vimemfuata Dk. SLAA ajiunge navyo na (vingine) vikimtaka awe mgombea wao wa Urais...Dk. Slaa angeweza kujiunga na mojawapo ya vyama hivyo, sina uhakika kama angejiunga na mojawapo ya vyama hivyo ingesemwa kwamba alikuwa na mawasiliano nao kabla...

Tukubali tu kwamba kwa hali ilivyo sasa lolote linaweza kuzungumzwa kwa lengo la kutuliza/kuondoa athari/hasara itayatokana na kauli za Dk. SLAA jana....Mengi yatazungumzwa lakini ukweli wanaujua Slaa, Mbowe, Gwajima na Tundu Lissu
 
Urafiki wa Gwajima na Slaa si kitu kipya mkuu wangu...Kama ilivyo urafiki wa Gwajima na Lowassa...

Slaa amekuwa akihudhuria ibada kwenye eneo la kuabudia la Gwajima pale Kawe mara nyingi tu....Na hata Slaa mwenyewe jana amekiri kwamba Gwajima ni rafiki yake kwa muda mrefu....

Hakuna niliposema Gwajina hasiwe rafiki wa Dr. Slaa ua Dr. Slaa hasiwe rafiki wa Lowassa.. nani awe rafiki wa Dr.Slaa na kwa vipi wawe marafiki hiyo ni haki yake na mimi ninafurahi niwaonapo wanasiasa wanashirikiana maana siasa si uadui.

Mantiki ya Gwajima kumpigia simu Dk. SLAA kumuomba wampokee Lowassa mbona iko dhahiri mkuu?...Usiniambie hata Sumaye aliyehamia CCM baada ya kukatwa ama Msindai,Masha na Mahanga waliohamia CHADEMA baada ya kushindwa kura za maoni CCM nao walikuwa na mawasiliano na CHADEMA kabla..
.

Ndio Sumaye, Masha au kiongozi yeyote yule anapotaka kuhamia chama fulani huwa kuna mawasilina kabla.. Hivi unafikri Sumaye aliamka asubuhi na kusema leo naamia Chadema bila kuwa na mawasiliano na viongozi?

Hivi inakuingia akili Gwajima anyanyue simu na kwambia Dr.Slaa kuwa jamaa ameishakatwa na Dr. Slaa ajibu kuwa akaongee na Mwenyekiti? Kama ni hivi nilitegemea Dr.Slaa ajibu kuwa amekatwa kwa sababu ya ufasidi wake au ajibu kitu chochote si kusema aongee na Mwenyekiti? Hii sentensi ya Dr. Slaa inazdhhirisha alichongea Lissu ni kweli kwamba kabla ya Lowassa kukatwa kulikuwa na maongezi kati ya DR,Slaa, Gwajima na Lowassa...

Na katika simu ya Gwajima Dr. Slaa hakusema kuwa alimuombea kujiunga na Chadema bali alimpigia simu kumpa taarifa ya kukatwa! na Dr, Slaa anajibu kuwa aongee na Mwenyekiti sasa kama hawakuwa na mazungumzo kabla basi hii kauli ya niongee na mwenyekti ilikuwa ya nini?

Sote tunajua kwamba Gwajima ni mfuasi/mtu wa karibu sana na Lowassa...Yuko tayari kufanya/kusema lolote kuhakikisha kwamba Lowassa anafanikiwa/anasonga mbele...Si ajabu kwa Gwajima kumpigia simu Slaa kumuomba wampokee Lowassa(kutokana na ukaribu wao)..Kwenye siasa lolote laweza kutokea (muda wowote)...Mara baada ya ujio wa Lowassa CHADEMA na mara baada ya Dk. SLAA kujiweka kando kuna vyama vingi tu vimemfuata Dk. SLAA ajiunge navyo na (vingine) vikimtaka awe mgombea wao wa Urais...Dk. Slaa angeweza kujiunga na mojawapo ya vyama hivyo, sina uhakika kama angejiunga na mojawapo ya vyama hivyo ingesemwa kwamba alikuwa na mawasiliano nao kabla...

Kwani wakati Gwajima anampigia Dr. Slaa simu ya kumpokea Lowassa, huyu Dr. Slaa hakufahamu kuwa Lowassa ndio yule yule ambaye alikuwa anatutangazia kuwa ni fisadi? na kama alipigiwa na Gwajima simu alishindwa kumwambia hapana sisi Lowassa ni kapi na sisi hatuchukui makapi?

Nitajaribu kuunganisha "dot" kulingana na maelezo ya Dr. Slaa na Lissu.

Ukisikiliza maelezo ya Tundu Lissu yanakupa picha halisi ya mchezo ulivyokuwa na mchezo ulikuwa hivi Dr. Slaa alishakubali kuwa Lowassa awe mgombe, kwenye vikao vya kamati kuu Dr. Slaa alishiriki na alikubali maelezo ya Lowassa. Siku moja kabla ya Lowassa kutangaza kujiunga na Chadema, walikaa vikao ambacho kiliisha usiku (nafikri saa 3) na wote waliagana kukutana kesho yake wakati Lowassa anatangaza kujiunga na Chadema.. Siku iliyofuata yaani siku ya Lowassa kutangaza kujiunga na Chadema Dr. Slaa bila taarifa zozote hakutokea, na alipotafutwa katika simu aliyekuwa anapokea simu ni Josephina.. na alipofuatwa nyumba kwake alitoa barua ya kujihudhuru, Prof. Safari alichana hiyo barua kwa sababu (nafikiri) hakuamini kuwa Dr. Slaa anaweza kujihudhuru bila sababu ya msingi na hapo ndio ukweli ulipokuja kujulikana kuwa Mama Josephina alikasirika na alikuwa amemlaza mzee wa watu kwenye gari kisa Lowassa..
 
Mkuu Nguruvi3, umekua mpana sana kwenye hoja zako, umejadili kila hoja kwa kina na kwa ufasaha bila ushabiki, soon tutachangia kuongeza uchambuzi kwa haki kabisa kama tulivyofanya kwa udhaifu wa Lowassa, mbowe, Zitto, na wengine wengi huko nyuma bila kupendelea upande
 
Back
Top Bottom