Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,474
- 39,987
Are you implying that the guy can not speak? I wonder why he spends so much money to sell himself.
Of course he can speak; the question is, can he speak sense?
Are you implying that the guy can not speak? I wonder why he spends so much money to sell himself.
Naomba tuulizane, je tunavyoikomalia Ukawa na kuichambua chambua kama mchicha au mchele tunawaelewa wananchi wengi wapiga kura?
Maana kama ni kuichambua CCM, tumeichambua miaka nenda rudi na kila mwaka bila kujali scandal gani, umasikini wa kiwango cha medali ya dhahabu olimpiki, bado Watanzania waliendelea kukipigia kura CCM na CCM wameendelea kutudharau sisi "wachambuzi"!
What if Lowassa na wenzake nao wameibaini formula ya ushindi ya CCM? maana wakati tunahoji kuambiwa tukasome hotuba na ilani kwenye website ya Chadema, CCM wametoa PDF na ilani ya kurasa karibu 230 na hatuhoji ni nani huyo mwananchi mpiga kura wa kijijini au hata mjini atakayekaa chini kupitia kurasa 230 zenye majedwali na misamiati migumu ambayo haielewi?
Hatujiulizi ni vipi wananchi hawajuuliza ili kupata ufafanuzi wa hizo Milioni 50 kwa kila kijiji kama Mama Samia alivyosema, lakini leo tunamhoji Lowassa kusomesha elimu bure?
Nikiliangalia hilo la Shilingi Milioni 50 na lilivyopokelewa kwa shangwe (kwanza hiyo ni ahadi ya rushwa kupata kura), je shilingi hizi milioni 50 ni za kazi gani katika kijiji? ni wananchi kugawiwa fedha? ni za kununulia mabati ya shule? ni ya kununua magodoro ya zahanati? ni ya kuchimba mifereji? ni ya kununua ng'ombe wa mbegu? Hizi fedha ni za nini? je fedha zinazotolewa kila mwaka kwa shughuli za maendeleo na matumizi Wilayani haziendi huku vijijini?
Nikiongelea hili la Milioni 50 na rafiki yangu Mzee Mwanakijiji, akanikumbusha Mabilioni ya JK alipoingia madarakani na zile fedha za community fund, je uwiano wa kijiji chenye watu 100 na kijiji chenye watu 1,500 utapimwa vipi ikiwa kila kijiji kitapokea Milioni 50?
Nauleta huu mfano wa Milioni hamsini na ulivyopokelewa na wananchi kwa matumaini na vifijo kusema: Jamii ya Watanzania si wengi wanachambua mambo kwa kina na hata kuona mapungufu ya wazi.
Je Masha aliposema ameonewa na polisi na kuwekwa ndani kwa kuhoji, si ndivyo 50% ya walioko magerezani na jela wameswekwa kibabebabe? Hata la Babu Seiya na Mashehe si wananchi walilipuka kwa nguvu kabisa na limekuwa gumzo?
Sasa najiuliza ni nini sisi "wachambuzi" hatukioni miaka yote na CCM wanaendelea kujiamini hata kudiriki kuita wanaoihoji na kuipinga kuwa ni Wapumbavu na Malofa?
Nikikumbuka 1995 jinsi Mtikila na magabacholi au Mrema na mkwara wa kupambana na Rushwa akiingia ikulu na kisha wakaambulia kura za kubahatishabahatisha, je ni kitu gani wapiga kura wa Tanzania wanakiangalia kutoka kwa mgombea?
Jana na leo, Mwakyembe na Sitta wameudanganya umma tena kwa swala la Richmond huku wengine tunajua wao wawili walikuwa na uwezo mkubwa kuilazimisha Serikali kama Bunge kufuta mkataba huo mara moja na kuokoa mabilioni tuliyoyalipa kama Capacity Charge kwa Richmond, baadaye Dowans na sasa Symbion. Ikiwa waliweza mlazimisha Waziri Mkuu kujiuzulu, walishindwa nini kuilazimisha Serikali kufuta huo mkataba na wote walijua gharama tuliyoipata na IPTL na ubovu wa mkataba wa Richmond?
Hivyo lazima kuna kitu ambacho hatukielewi kwa kuwa tunapima na kuchambua kila anachokula bata na tunakuwa wepesi kutahamaki na kuonyesha mshangao huku Watanzania wanaimba korogakoroga zungusha zungusha Pipoz Pawa!
Alinda ndg yangu,
nimesikia tetesi mitandaoni,kesho Dr.Slaa anamwaga manyanga, sasa hii itakua pigo takatifu na demage kubwa sana kwa UKAWA na sijui watafanyaje iki kuniokoa, naombea tu atumie busara, maana kwa namna yoyote ile atarudisha nyuma mipango ya UKAWA kwa kiwango kikubwa mno na mambo nayaona yakienda mrama, only God knws wht willhappen after his damage, kiuhakika wajipange sas akina Mbowe.
Maneno yako yanafikirisha sana na ni ukweli ambao ni mchungu.
Sisi tulio humu jamvini twaweza kuchambua kila linaloendelea kwenye ulingo wa siasa lakini bado hatuwakilishi asilimia kubwa ya wapiga kura ambao wako mtaani na vijijini. Ndio hawa hawa ambao waliipa kura kuirejesha CCM madarakani 2010 pamoja na kashfa lukuki zilizokuwapo, ndio hawa hawa waliwarejesha majimboni wabunge watuhumiwa wa kashfa za ufisadi mwaka 2010 na hata sasa wamewapitisha kwenye kura za maoni!
Kuna wakati huwa najiuliza kama ni kweli kwa siasa zetu za kiafrika hizi hususan hapa Tanzania chama kinaweza kushinda uchaguzi kwa sera pekee? Najiuliza kama wananchi wanaohudhuria mikutano ya kampeni wanaenda kusikiliza seraza vyama na wagombea ili kuzichambua au wanaenda kusikiliza porojo, vijembe na tambo za wagombea majukwaani? Nini kinachowavutia?
Ili kuweza kuelewa haya lazima tufike mahali tufanye tathmini juu ya mindset ya watanzania inapofikia masuala ya siasa na uchaguzi... sababu hiki ndicho CCM wanakitumia kujipatia ushindi miaka nenda rudi. Ndio maana tunasikia kauli hizi "Mchagueni Rev Kishoka sababu ana MVUTO na ANAKUBALIKA"... lakini swali ni kwamba mvuto na kukubalika vinahusiana vipi na sera?? Lakini mwisho wa siku ndicho wananchi wanakikubali!
Watanzania tumekuwa wasahaulifu mno na tunapokea mambo bila kuhoji ndio maana watu kama kina Mwakyembe wanaweza kusimama leo jukwaani kusema ati Lowassa anaweza kushtakiwa kuhusu Richmond na akapigiwa vigelegele! Wala hatumhoji kwa nini aliamua kuficha madudu mengine kwenye ile ripoti yake ili kuisitiri serikali ya chama chake isianguke! Na hii ndio mindset ya watanzania ninayoiongelea...
Mwanzoni UKAWA walipoamua kumsimamisha Lowasa nilishtuka na sikuelewa kwa nini. Lakini baada ya kuona mwitikio kwenye mikutano ya kampeni sasa naanza kuelewa. UKAWA safari hii wameamua kukalibiana na CCM "using their own game"
Slaa amejitokeza...Amezungumza
Ngoja nitulize kichwa nitarudi kujadili.. Ila siasa kwa Tanzania ni ngumu jamani..CCM wapo tayari kutumia njia yeyote ile kuleta mgawanyiko.. Katika maongezi ya Dr. Slaa kuna mgawanyiko aliyougusia dah kweli tusiwaamini wanasiasa by Zitto Kabwe
Mwanasiasa mmoja wa Uingereza aliwahi kusema 'siku moja ya siasa ni muda mrefu sana'Miezi michache iliyopita hakuna mtu angeweza kwa kutumia akili timamu kuja na analysis yenye kueleza kinachotokea kwenye siasa za Tanzania leo hii. Nani angeweza kuja na analysis ambayo ingemuweka Membe, Magufuli, Lowasa, Dr Slaa, Sumaye na Prof Lipumba Hapo walipo sasa.
Pia ni vigumu kabisa kwa kutumia ujuzi wowote unaopatikana kwenye akili zetu kutabiri baada ya wiki tatu nini kitakuwa kinajiri ndani ya siasa za Tanzania.
Dr Slaa leo kakamilisha kile kisichotabirika kwa siasa za uchaguzi wa mwaka huu.
Mungu Ibariki Tanzania.
Ukweli anaouzungumza mwanasiasa ni salamu tu mkuu....
Binafsi sikuwahi kutegemea kama Lowassa atakuja kuwa mwana CHADEMA kwa ghafla...Hasa nikirejea kauli za Lema..Slaa...Mnyika..Mbowe na Sugu kuhusu Lowassa
Nguruvi3,
..hivi mbona mambo haya hayatokei CCM?
..yaani CCM wanaweza kufanya chochote, kwa yeyote, na hakuna mtu wa kuleta ubishi-ubishi.
..kuna mtu kama Salim Salim. kwa jinsi alivyochafuliwa ungetegemea angemwaga mboga na ugali kama alivyofanya Dr.Slaa. Au, Mzee Malecela alivyokata bila maelezo ya kuridhisha.
..Kwanini CCM wanaonekana kuwa wavumilivu na watiifu kwa chama chao, kuliko hawa walioko vyama vya upinzani?
cc Mkandara, betlehem, Mzee Mwanakijiji, Alinda, Mwalimu
Mkuu za siku tele. Bila kupoteza muda, najikita kwenye hiyo redbold......
Shida ya Dr. Slaa si ufasadi wa Lowassa shida yake ilikuwa ya wabunge 50 aliyosema hivyo kama angeleta wabunge 50 basi leo hii angekuwa anakula "tapishi lake" and after all hivi baada ya miaka 8 bado kunakufa na Richmond na kuacha Dowans na Escrow??
Mkuu za siku tele. Bila kupoteza muda, najikita kwenye hiyo redbold.
Nimemsikiliza Dr. Slaa, toka anaanza mpaka anamaliza kujibu maswali. Leo sikutaka kuhadithiwa wala kuwekekewa clips zilizokatwa katwa, ilinifanye tathimini sahihi.
Nadhani si kweli kusema Dr. Slaa hakuwa na shida na ufisadi wa Lowassa. Ninadhani hivyo kwa sababu wakati anaanza kutoa maelezo juu ya kumkaribisha Lowassa alitoa masharti ya kimsingi ambayo alitaka Lowassa ayatekeleze. Baadhi ya masharti hayo ni haya:
1. Lowassa atamke hadharani kuwa ameachana na CCM
2. Lowassa ajibu tuhuma hadharani tena kinagaubaga kwa kusema wazi nani alihusika na Richmond na kashfa nyingine zianzomuhusu yeye Lowassa (Badala ya kusema mwenye ushahidi apeleke mahakamani ama mfunge midomo. Pia suala mahakamani haliwezekani kwa raia wa kawaida , Dr Slaa kasema, kesi za jinai ni serikali ndiyo ufungua mashitaka)
3. Akisha maliza kujisafisha (Lowassa), atangaze anaamia chama gani(Chadema ama chama kingine!);
4. na kisha kama ameamua kuamia chadema, basi chama(Chadema) kiamue kumpokea ama la...!Baada ya kujiridhisha kama Lowassa ni Asset kisiasa(atakuja na viongozi na wabunge wa CCM ambao nao watafuata utaratibu wa 1-3 hapo juu) ama ni Liability kisiasa.
Hivyo nadhani Mkuu, Alinda, si sahihi kumuhisi Dr. Slaa hivyo(redbold).
Binafsi, nadhani kwa kiasi fulani Dr. Slaa alikuwa nafanya siasa sahihi zisizo za kilaghai (siasa za ukweli). Siasa zisizo za kilaghai ndizo zilizonivutia kufatilia maadishi mengi ya Nguruvi3, ya kwako(Alinda) na wengineo hapa jukwaani.
Nadhani kwa leo Dr. Slaa kazitendea haki siasa nilizoziamini na ninazozidi kuziamini yaani siasa za ukweli na wala si siasa za kitapeli.
Mapambano bado yanaendelea kutafuta na kisha kuupata ukombozi wa kweli kwa kufuata siasa za ukweli.
-TUJITEGEMEE.
..... hivi baada ya miaka 8 bado kunakufa na Richmond na kuacha Dowans na Escrow??
Hizo ndizo siasa za Tanzania.. Hivi ulifkiri kuwa leo hii Dr. Slaa angekuwa hero wa CCM? kuna mtu mbaya aliyekuwa upinzani kama Dr. Slaa? yako wapi? leo Dr. Slaa anakuja na propogada za udini? hivi ndo huyu Dr. Slaa aliyekuwa anasimangwa kuwa ni padre? Siasa za Tanzania ni mgumu jamani.
Nimekupa mkuu..na nime"edi" hapo.. shukurani kwa maelezo yako...
Kama umemsikliza vizuri hivi ameongea nini kuhusu "udini" maana mie nilikuwa nafatilia update za watu wa hapa JF. Inawezekana kuna upotoshaji wa aina fulani..
Mkuu katika bandiko 2015-391 hapo juu nilisema naishia pale makusudi kabisa. Ukisoma vizuri nimeandika 'collateral and colossal damage' naomba nifafanunueKuhusu udini kausemea, lakini hasa kajikita zaidi kwenye maadili ya viongozi wa dini. Amesema alielezwa na 'mshenga' .... kuwa kunabaadhi ya maaskofu wa maadhehebu ya kikristo(katholiko likiwemo) wamehongwa na 'wanasiasa' kuanzia kati ya mil.50 na kuendelea. Akamalizia kwa kusema kama maelezo yale (ya mshenga) yalikuwa ya kweli amesikitika sana.