CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
15,393
31,344
Sehemu ya I

MABADILIKO YA MWENENDO WA SIASA ZA NCHI

CCM WATUA, CDM/UKAWA WABEBA. LOWASSA 'FACTOR'

Mchakato wa wagombea Urais ndani ya CCM umebadili mwenendo wa siasa nchini
Kukatwa kwa jina la EL ni chimbuko la mbadiliko yanayoonekana

CCM wakionekana kutua' mzigo' uliowalemea , UKAWA wakiubeba kwa shangwe
Maswali ya kujiuliza, je, kuna aliyeondoa wawekezaji au aliyekaribisha wawekezaji?

Nini hatma ya siasa za nchi baada ya Oktoba 2015?

Tutafakari hoja tukiweka mbele maendeleo ya kuondoka na ujio wa Lowassa
Mtu anayeaminiwa kuwa na nguvu si tu kule anakotoka bali alikofikia

CCM NA KUONDOKA KWA EL

Hali ya kisiasa inaonyesha chama kikongwe kuelemewa.

Kuna hoja katika jamii iwapo CCM kipewe muda au ipumzishwe kama KANU na UNIP
Viashiria vya kuchokwa kwa CCM ni vingi,havihitaji akili ya ziada.

Vipimo kama chaguzi/serikali/mitaa unaosimamiwa serikali ya CCM vinaeleza hali ya CCM
Wingu la ufujaji na ufisadi ni gumzo la nchi, kidole huonyooshewa CCM

Kwa kutambua hilo, CCM ikawa njia panda.
Kukumbatia wanaoichafua au kukabiliana na ukweli wa kuwadhibiti bila kujali athari zake

Vikao vikaandaliwa kiufundi kukamilisha azma ya kujinasibu, chama kinavua gamba.
Kinachoitwa magamba ni nguvu kubwa iliyoachiwa ikastawi na kuchanua.

CCM ikachagua bega, kuwatosa ili kijinusuru mbele ya uso wa wananchi
Mwathirika mkubwa wa hatua za CCM ni EL, mwenye nguvu ndani ya chama

CCM ilitambua, kumuondoa Lowassa ni jambo la mawa 'risk'

Njia sahihi ya kurudi kwa wananchi ili kuwekeza tena kwa athari ndogo; Low risk investments' ni kumuondoa

Inaendelea..

CDM/UKAWA wambeba EL
 
Sehemu ya II

CDM/UKAWA WAMCHUKUA EL

Katika hali isiyotarajiwa, EL amejiunga na /UKAWA chini ya mwamvuli wa CDM

Halikuwa jambo la bahati mbaya, sita sita ya UKAWA kupata mgombea ni mkakati kujua nani atakuwa mgombea wa CCM

Hotuba ya EL akichukua kadi ya CDM inaeleza uwepo hai wa ndoto yake ya safari ya matumaini.

Hili linaashiria, makubaliano ni UKAWA/CDM kumtangaza kama mgombea upande wa upinzani

CCM wakiwa na uwekezaji usio na hati hati, UKAWA/CDM wamechukua hati hati yenye mawaaa kwa kiwango kikubwa ' High risk investments' wakitarajia kupata mafao

Kwa mtazamo wa haraka, shinikizo la uchaguzi limeahamia CDM/UKAWA

Hapa tunaitaji Chadema kwavile ndicho chama kikuu cha upinzani, na mwenyeji wa EL.

Mizigo au masurufu atakayokuja nayo mgeni EL , CDM itawajibika kwa taifa na dunia

Kwa mtazamo wa kawaida, CCM imetua mzigo licha ya athari wanazotegemea
Hii ni pamoja na kuondoka viongozi na kundi la wanachama. Ndivyo ilivyokuwa zama za Mrema

Uwezekano wa kupoteza dola, mhimili mmoja au ushindi dhaifu utakaozuia nguvu ya wingi wao katika maamuzi ya masuala ya kitaifa unazidi kuwa mkubwa

Kwa CCM kuondoka kwa lowassa kunatoa unafuu kuliko uwepo wake.

Upande wa CDM/UKAWA huu ni uwekezaji usio na uhakika nao.

Matarajio ni yale ya kanuni isemayo ''high risk investment" has a high amount of risk and usually a high potential reward''

Maswali ya kujiuliza

Uwekezaji wa CDM/UKAWA kwa EL ulikuwa na ulazima?

Je, ni uwekezaji unaotarajiwa kutoa matunda au historia ya Mrema kujirudia?

Kitu gani CDM/UKAWA wanachotarajia zaidi baada ya ujio wa mh EL?

Je, wamejiandaaje kubeba mizigo anayokuja nayo mh, tukijua aliungwa mkono ?

Je, wana agenda mbele ya mahamakama ya wananchi au sera zitakazoeleza uwekezaji wao?

Je, wana nguvu ya kushambulia au sasa ni nguvu ya kuzuia?

Inaendelea….
 
Sehemu ya III

CHANGAMOTO ZITOKANAZO NA UJIO WA Mh

Ujio wa mheshimiwa hauwezi kuwa shangwe isiyo na changamoto.
Miongoni mwa changamoto ni ile ya EL kuonekana kama taasisi.

Ujio wake hautakuwa peke yake, ana watu aliowaacha nyuma.
Katika mazingira ya sasa, watu hao wapo njia panda

1 Wengine watataka nafasi za ubunge/udiwani iwe kwa kushindanishwa na wale wa CDM.

Mchakato ndani ya CDM upo karibu kukamilika.
Wafuasi wa EL hawakubaliki tena ndani ya CCM. Njia imefungwa mbele na nyuma.

Je, waliochukua fomu CCM wapo tayari kuzitupa, waungane na mzee wakiwa' bench'
Kama jibu siyo, hicho kinachosemwa atakuja na watu wenye ushawishi kinaelezwaje?

2 Akiwa mgombea wa Urais, nafasi yake inakuwa kubwa ndani ya chama.
Ni kubwa pia, kwa kuzingatia kuwa ujio wake umechukuliwa kama ujio wa taasisi
.
Hoja, hivi hapo hatakuwa na mgongano wa masilahi kati yake na wenyeji?

3 Kwavile anaonekana kuwa 'mwiba' kwa CCM na serikali yake, CDM/UKAWA wamejiandaje na hatma inayoweza kujitokeza kumzuia kiufundi asiwe mgombea!

Tumeona suala la Escrow lilivyotumiwa na CCM kuondoa nguvu ya EL 'technical knock out' kwa kumuondoa mtu ndani ya kamati ya maadili,kamati kuwa na nguvu kuliko CC

Itakapotokea kukawepo suala la kisheria, likawekwa kiufundi kwa hila au kwa mbinu, CDM/UKAWA wana mbadala?

Hoja na maswali ni nyingi katika tafakuri.
Jambo moja tunaloweza kusema ni kuhusu uwekezaji wa CDM/UKAWA usiotabirika.

Ni uwekazaji wa hatari uliojaa tabia zote za kamari.
Hakuna anayeweza kusema kwa uyakinifu CDM/UKAWA wamelenga nini, kwa njia zipi na wanakabiliana na changamoto kivipi.

Huo ndio msingi wa kusema, huu ni uwekezaji usiotabirika
Ni njia panda itakayoamua hatma ya taifa kwa muda mrefu ujao

Njia panda inaweza kuwa ufunguo wa chapter nyingine ya uhai wa taifa hili.
Na pia yaweza kuwa rejeo la historia tuliyowahi kuisoma miongo michache ijayo


Tusemezane


Zakumi Mag3
 
Last edited by a moderator:
Wanaukumbi.

By John Mnyika:
TAARIFA KWA UMMA.


SERIKALI IACHE KUMLINDA LOWASSA.

• Ni mmoja wa mizizi ya ufisadi wa Richmond
• Akamatwe, ahojiwiwe na achukuliwe hatua za kisheria.



Tarehe 25 Februari, 2008 Vijana wa CHADEMA tulitoa taarifa kwa umma tukikemea jitihada zilizokuwa zikiendelea za Lowassa kujisafisha na kusafishwa na tukahimiza achukuliwe hatua za haraka kutokana na tuhuma za ufisadi na/ama matumizi ya madaraka katika kashfa ya RICHMOND. Pamoja na taarifa yetu hiyo kwa umma katika kipindi chote ambacho Serikali ilipewa na Bunge kutekeleza maazimio ya Bunge kuhusu suala hilo hatua tulizopendekeza hazikuchuliwa. Aidha tumefadhaishwa zaidi na Taarifa ambayo Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo ameiwasilisha Bungeni Alhamisi 28 Agosti, 2008 pamoja na kutaja hatua ambazo zimechukuliwa kuhusu watuhumiwa wengine ikiwemo kuandikiwa Barua za kujieleza na/ama kuanza kuchunguzwa na vyombo vya dola/usalama; Waziri Mkuu hakueleza hatua ambazo zimeaanza kuchukuliwa dhidi ya Bwana Lowassa.

Tunatambua kuwa Waziri Mkuu katika taarifa yake ameeleza kuhusu hatua ambazo serikali imeanza kuchukua ikiwemo za marekebisho ya Sheria ama mifumo ya uwajibikaji, ikiwemo ile ya manunuzi. Hata hivyo, tungependa kuweka bayana kwamba matatizo ya msingi ya taifa letu hayasababishwi na mapungufu katika sheria pekee, ila kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na kulegea kwa misingi ya utawala wa sheria na uwajibikaji miongoni mwa viongozi. Hivyo, tunapenda kuwajulisha Watanzania kuwa kama watuhumiwa wa ufisadi hawatachukuliwa hatua mapema, misingi ya utawala wa sheria itazidi kutetereka na matokeo yake ni kuwa mageuzi yoyote katika mifumo ya kiutawala hayatatekelezwa kikamilifu. Kwa ujumla tunaamini kwamba utamaduni huu wa kulindana katika serikali unatoa mfano mbaya kwa vijana wa kitanzania kuhusu uongozi na utawala bora.

Tungependa kusisitiza kuwa Bwana Lowassa, akiwa Waziri Mkuu wa nchi yetu wakati huo alikuwa mmoja wa mizizi mikuu ya ufisadi wa RICHMOND. Hivyo, tunaona kuwa Taarifa ya Utekelezaji ya Waziri Mkuu Pinda imejikita katika kushughulikia matokeo badala ya mzizi wa tatizo lenyewe na hivyo kama hali hii ikiendelea itaporomosha nidhamu na uwajibikaji katika taifa letu. Tunaamini kwamba kama Bwana Lowassa aliyekuwa kinara wa Serikali wakati huo, ataweza kuchukuliwa hatua kikamilifu basi itakuwa rahisi kwa waliokuwa chini yake kuweza kuchukuliwa hatua za haraka na hatimaye kurejesha maadili katika utawala. Lakini kama Serikali itaendelea kumlinda Bwana Lowassa na kuwatoa kafara maafisa wa chini, bado haitakuwa imetekeleza kikamilifu dhana ya uwajibikaji na utawala wa Sheria. Kujiuzulu kwa Waziri Mkuu na mawaziri wenzake kadhaa ni hatua ndogo sana katika kashfa iliyohusisha uvunjaji wa Sheria za nchi yetu, mazingira ya ufisadi na hasara kubwa kwa taifa.


Sisi tunaona kutotajwa kikamilifu kwa hatua zilizochuliwa juu ya Bwana Lowassa ni mwendelezo wajitihada za miezi ya karibuni za Bwana Lowassa(Mb) kupita akijitetea kuanzia katika hotuba yake alipokwenda Jimboni Monduli na kunukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari na hata mahojiano yake maalumu na Televeshioni ya Taifa(TVT).

Aidha, taarifa ya Waziri Mkuu Pinda imeakisi uamuzi wa Waziri Mkuu aliyejiuzulu Bwana Edward Lowassa kujitokeza miezi ya karibuni kujitetea kuhusu kuhusika kwake katika kashfa ya Richmond ambayo kwa ujumla ni ishara ya unafiki wa kisiasa. Itakumbukwa kuwa baada ya Kamati Teule kuwasilisha taarifa yake, Bwana Lowassa alipata nafasi bungeni takribani mara mbili kama kiongozi wa shughuli za serikali bungeni wakati akiwa Waziri kuzungumzia suala hili lakini hakutoa utetezi ambao Mwezi Februari alijaribu kuutoa kwa umma. Waziri Mkuu Pinda inabidi auleze Umma kama uamuzi wa kumtomtaja katika Taarifa yake ya utekelezaji kuhusu hatua ambazo amechuliwa ni ishara kuwa serikali imekubaliana na utetezi wa Bwana Lowassa.

Itakumbukwa kuwa Vijana wa CHADEMA tulieleza wazi kwamba katika kujitetea kwake mwezi Mei, Bwana Lowassa alithibitisha wazi uzembe na matumizi mabaya ya madaraka ambayo aliyafanya alipokuwa Waziri Mkuu wakati wa sakata zima la Richmond. Hivyo, tunarudia kutoa mwito kwa vyombo vya dola kuweza kumkamata, kumhoji na kumchukulia hatua za kisheria dhidi ya uzembe na matumizi hayo mabaya ya madaraka kwa mujibu wa sheria za nchi yetu. Badala ya Bwana Lowassa kuendelea kupita akijitetea kuwa Kamati Teule haikumuita kuweza kujieleza; vyombo vya dola vimkamate akatoe maelezo yake panapohusika. Vyombo vya dola vimekuwa vikiwakamata raia wa kawaida wenye taarifa za uhalifu kuweza kuisadia polisi, inashangaza Bwana Lowassa amejieleza wazi kuwa alikuwa anafahamu uhalifu uliokuwa ukitendeka lakini bado yuko nje akijitetea na pia Taarifa za kiserikali zikielekea kumlinda. Tunaamini akikamatwa yeye, atawezesha watuhumiwa wakuu wa kashfa ya Richmond kuweza kupatikana. Tulieza wazi katika tamko letu na Mwezi Februari kuwa , jitahada zozote za kumlinda na kumtetea zingeweza kuathiri mwekekeo wa hatua ambazo zitanatarajia kupendekezwa na Kamati ya Waziri Mkuu mpya Mheshimiwa Mizengo Pinda. Kutokana na Taarifa ya Waziri Mkuu Pinda aliyowasilisha Bungeni Alhamisi tarehe 28 Agosti, 2008 ni wazi kuwa kuna kila dalili kuwa mwelekeo huo umeanza kuathiriwa, hivyo tunarudia tena kutaka Bwana Lowassa achukuliwe hatua kabla ya Bunge la Mwezi Novemba, 2008.

Bwana Lowassa akiwa Waziri Mkuu amethibitisha kwamba maneno yake mwenyewe kuwa alikiuka Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995 na Sheria ya Makosa ya Udhibiti wa Uhujumu wa Uchumi wa nchi ya Mwaka 1984.

Bwana Lowassa alikiri kwamba alikuwa anafahamu kwamba Richmond ni kampuni ya kitapeli, lakini katika kipindi chote cha uongozi wake aliinyamazia hali hii na kwa kiasi kikubwa aliitetea kampuni hiyo mbele ya macho ya umma. Wakati wa Viongozi mbalimbali wa upinzani walipoweka bayana kwamba Richmond ni kampuni isiyo na uwezo, serikali ilitetea kampuni hiyo. Vyombo mbalimbali vya habari vilimtuhumu Bwana Lowassa mwaka 2006 na 2007 kama kiongozi wa Shughuli za serikali bungeni, kwamba alishiriki ‘kuwaziba midomo’ wabunge wa CCM wasijadili suala hili. Pia, ni Bwana Lowassa huyo huyo, alinukuliwa akiwa Arusha akiwataka watanzania wasiijadili kampuni ya Richmond baada ya mvua kuanza kunyesha. Kama Bwana Lowassa wakati wote huo alijua kama ni kampuni ya kitapeli kama anavyojaribu alivyojaribu kujitetea, uamuzi wake wa kuwaasa watanzania wasiijadili ulikuwa ni wa kulinda ufisadi ambao aliufahamu. Inashangaza pia ni Lowassa huyo huyo alisema alijua kuwa Richmond ni kampuni ya kitapeli; ni Lowassa huyo huyo alisema kwamba alishauriwa vibaya na watumishi wa umma aliowataja kuhusu uwezo wa Richmond; Ni Lowassa huyo huyo aliyesema kwamba alijua kuwa TANESCO chini ya Menejimenti ya Net Group Solution walitaka kuhujumu mchakato wa tenda na hivyo ‘kuwanyang’anya’. Lakini ni Lowassa huyo huyo aliyekuwa Waziri Mkuu ambaye angeweza kuviagiza vyombo vya dola kumwezesha kuthibitisha ‘utapeli wa Richmond’; hivyo, maelezo ya sasa yanayotolewa kuhusu ushiriki wake yanaonyesha kuwa sasa kuna mwelekeo wa kumlinda.


Tunaendelea kushangazwa na Serikali na Bwana Lowassa kutumia utetezi wake kueleza tu nia yake ya kutaka mkataba wa Richmond usitishwe; nia ambayo kama ni kweli alikuwa na uwezo wa kuitekeleza na hakuitekeleza. Tunaitaka Serikali na Bwana Lowassa kuweka bayana ni kwa vipi Richmond ilipewa tenda hiyo na kwa shinikizo la nani. Bwana Lowassa anakwepa kuyazungumzia haya kwa kuwa anajua kabisa kwamba ni yeye aliyetumia madaraka yake vibaya alipokuwa Waziri Mkuu kwa kukiuka Sheria na Taratibu za Ununuzi kwa ‘kupora’ mchakato uliokuwa ukiendeshwa na TANESCO, ‘kuunda kamati yake’ na kuzisukuma mamlaka za ununuzi hali iliyopelekea Richmond kupewa tenda ili hali haikuwa na uwezo uliotakiwa. Ni uzembe huu ambao umelisababishia hasara taifa kwa kulipa shilingi milioni 152 kila siku kwa kampuni ya Dowans iliyohamishiwa mkataba wa kitapeli wa Richmond; na takribani bilioni 172 kwa ujumla ambazo taifa linawajibika kuzilipa kutokana na kukodisha mitambo hiyo. Hvyo tunarudia tena rai yetu ya kutaka fedha zilizozilipwa kizembe mpaka sasa kurejesghwa serikalini. Kwa vyovyote vile, jitihada za Bwana Lowassa za kuhamasisha ujenzi wa Sekondari Kata, na utumishi wake kama Waziri Mkuu katika kipindi cha miaka miwili, haviwezi kuzidi hasara aliyosababisha katika uchumi wetu kipindi chote tulichokosa umeme wa dharura na wala hailingani na hasara ambayo tunaendelea kuilipa kila siku iendayo kwa Mungu. Maamuzi haya ya Bwana Lowassa yanaendelea kuwaumiza wananchi wote ikiwemo wa Jimbo lake la Monduli ambao wanataabika kwa mzigo wa gharama za umeme.

Tunarudia tena kumkumbusha Rais Kikwete kwamba Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma inamtaka Rais kuhakikisha kwamba taratibu zinatengenezwa zitakazojenga maadili na kuongeza imani ya wananchi kwa uadilifu wa viongozi wa umma na katika taratibu za utoaji maamuzi ndani ya Serikali na katika sekta ya umma. Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma vile vile imeweka kanuni zinazotakiwa kuongoza utendaji wa viongozi wa umma: kwamba wanapokuwa madarakani, viongozi wa umma watakuwa waadilifu, wenye huruma, utulivu, umakini na watakaoendeleza viwango vya juu vya maadili ili kujenga na kuendeleza imani ya umma kwa uadilifu wa Serikali. Kuhusiana na utoaji wa maamuzi, viongozi wa umma watatekeleza wajibu wao kufuatana na sheria na kwa maslahi ya umma. Hivyo, taarifa ya Waziri Mkuu Pinda kutokueleza bayana hatua ambazo Bwana Lowassa ameshachukuliwa au atachukuliwa ni ishara kuwa kauli ya Rais Kikwete aliyoitoa wakati akizungumza na Wazee wa CCM mkoani Dar es Salaam kwamba Bwana Lowassa amepata tu ‘ajali ya kisiasa’, na kumsifu kwa utumishi wake imechangia kumlinda mhusika huyu mkubwa katika sakata zima la RICHMOND. Vijana wa CHADEMA tulitarajia kuwa, baada ya Bwana Lowassa kukiri mwenyewe hadharani kuhusu uzembe wake na matumizi mabaya ya madaraka Rais Kikwete angelekeza hatua za kuchukuliwa dhidi yake badala ya kuendelea kumpamba kama “shujaa wa uwajibikaji’, kinyume na hayo tutaamini kwamba serikali yake inaendeshwa kwa ‘ubia wa kulindana’. Aidha tunarudia kutoa rai kwamba Rais Kikwete kuwafukuza kazi watumishi wote wa umma waandamizi ambao wametajwa na Bwana Lowassa kushiriki uzembe na matumizi mabaya ya madaraka; watumishi ambao walitajwa pia na Kamati Teule ya Bunge lakini mpaka sasa wanaendelea kutumikia nafasi zao mbalimbali. Kwa kuwa Waziri Mkuu Pinda ameshatangaza kwamba kwa wale wateule wa Rais, Kamati yake imeshapeleka suala zima kwake, tunategemea Rais atachukua hatua za haraka ili kuonyesha mfano kwa viongozi wengine wa chini yake wanaotarajiwa kuchukua hatua kwa watumishi wa chini.

Kadhalika tunapenda kuvikumbusha tena vyombo vya dola kwamba Sheria ya Udhibiti wa Makosa ya Kuhujumu Uchumi ya mwaka 1984 inatamka makosa yafuatayo kuwa baadhi ya makosa ya kuhujumu uchumi ni pamoja na yale yote yenye kusababisha hasara kwa mamlaka ya Serikali. Pia Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007 inatamka kuwa ubadhirifu na/au ufujaji wa mali ya umma unaofanywa na watumishi wa umma na Matumizi mabaya ya madaraka kwa ajili ya manufaa binafsi, ni sehemu ya ufisadi. Bwana Lowassa alithibitisha kwamba maneno yake kwamba wapo viongozi waandamizi wa Serikali ambao amewataja kwa majina wamefanya maamuzi ya kifisadi, kitendo chake cha kunyamazia ufisadi huo- kinafanya iwe vigumu kwa yeye kutenganishwa na tuhuma za ufisadi zilizomo katika mchakato mzima wa kupewa tenda kwa kampuni ya Richmond na mambo yote yaliyotokea baada ya Mkataba huo kuhamishiwa kwa kampuni ya Dowans.

Aidha tumefadhaishwa na Taarifa ya Waziri Mkuu Pindi kwamba kujiuzulu kwa Waziri Mkuu na Baadhi ya Mawaziri ilikuwa ni ishara ya hatua ambazo serikali imechukua kutekeleza maazimio ya Bunge kuhusu suala husika. Tunarudia kukumbusha kwamba toka sakata la Richmond lilipoanza zaidi ya mwaka mmoja uliopita tulimtaka Bwana Lowassa kujiuzulu kulinda heshima yake lakini alikaidi na kuitetea kampuni ya Richmond. Uamuzi wa yeye kujiuzulu baada ya kashfa yote kuwa hadharani, umesaidia tu kuilinda serikali ya CCM lakini katu hauwezi kumpatia heshima ya uwajibikaji na wala hakuwezi kuwa ishara ya kwamba Maazimio ya Bunge yameshatekelezwa.

Kwa niaba ya Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA), kwa taarifa hii tunarudia kukemea jitihada zozote za kumlinda na kumtangaza Lowassa kuwa shujaa katika taifa letu kwani hali hii ikiachwa kuendelea inatoa mfano mbaya kwa vijana wa Tanzania. Tusingependa kwa namna yoyote katika taifa letu, mtuhumiwa wa ufisadi aliyetajwa pia katika orodha ya mafisadi(list of shame) kulindwa na kuenziwa kama shujaa wa Taifa letu kwani ni kuharibu maana nzima ya ushujaa katika uwajibikaji.

“Inasikitisha kwamba vijana wezi wadogo wadogo wakijazana magerezani. Vijana wamachinga kuendelea kukosa mitaji na maeneo ya kufanyia biashara; wanafunzi wa elimu ya juu wakipandishiwa ada na wengine kukosa mikopo- huku fedha za walipa kodi zikiendelea kuteketea kwa ufisadi na watuhumiwa wa ufisadi wakiendelea kutamba hadharani. Hali hii ikiachwa, itaharibu utawala wa sheria na kuleta matabaka katika taifa letu. Vijana tusingependa kuona nchi yetu inatumbukia kwenye migawanyiko kwa sababu ya kuwalinda watu wachache kwa kisingizio cha haki za binadamu”

Imetolewa tarehe 31 Agosti 2008 safirini Kenya na:


John Mnyika
Mkurugenzi wa Vijana
0754694553

Cc; Mag3, Waberoya, Alinda, Ngongo, JokaKuu Mkandara, Zakumi, Kapwela The Boss, Mchambuzi TujiTEGEMEHE, ZeMarcopolo,
 
Last edited by a moderator:
Ritz,

..that is old stuff.

..kuna USHAHIDI MPYA.

..Lowassa anadai mamlaka ya juu yake ilitoa amri wasaini mkataba wa richmond.

..kinachotakiwa kufanyika sasa hivi ni kuwahoji wale makatibu wakuu ambao walikuwa pamoja na Lowassa ktk kikao ambacho walipewa maagizo hayo na mamlaka ya juu.

Cc Mag3, Nguruvi3, Mkandara
 
Last edited by a moderator:
Ritz,

..that is old stuff.

..kuna USHAHIDI MPYA.

..Lowassa anadai mamlaka ya juu yake ilitoa amri wasaini mkataba wa richmond.

..kinachotakiwa kufanyika sasa hivi ni kuwahoji wale makatibu wakuu ambao walikuwa pamoja na Lowassa ktk kikao ambacho walipewa maagizo hayo na mamlaka ya juu.

Cc Mag3, Nguruvi3, Mkandara

Ndio maana Mwenyekiti wa chama alikuwa mstari wa mbele kumsafisha rafiki yake kwamba ile ilikuwa ni "ajali ya kisiasa". Kisha akaenda MOnduli kumpigia kampeni 2010. Na mwishowe jusi wakati anafunga bunge akashindwa kujizuia na kumsifu na kumshukuru kwa utumishi wake!

Ngoma inogile!
 
''POLITICAL BASE'' KUDUWAA (PARALYZE) NA HAMASA (EXCITEMENT)

Kuondoka kwa EL CCM kumezaa hali mbili. Moja, wapo walioduwaa ndani ya CCM kwa kukatwa jina, na wapo wanaoshangilia kwa chama kujisafisha.

CCM ilinasibishwa na ufisadi ikutuhumiwa kushindwa kuvua magamba.

Hoja ya kushindwa kuvua magamba ilienezwa na CDM/UKAWA kama kichocheo cha hasira. Imezizima sana masikioni

Baada ya kuondoka EL, CCM watarudi kwa wananchi wakiwa na hoja ya kuvua gamba.

Kwa maneno mengine wana mada 'theme' inayozunguka vichwani mwa wananchi.

Hili linawapa nguvu kwasababu ile 'slogan' yao tayari ipo sasa wanaifanyia ukarababti iwe na mashiko 'Kuvua gamba'

Kwa wale wakereketwa wa CCM ambao ndio political base ya CCM, hili limeleta hamasa sana 'fired up''


CDM/UKAWA

Kwa upande wao hawana slogan kwasababu ile ya ufisadi tayari imeshakuwa na sura mbili.

Hakuna siri , political base ya CDM/UKAWA imeduwaa 'paralyzed'' kutokana na mabadiliko ya ghafla na haraka yaliyotokea.

Ujio wa EL umepelekea kile kinachosemwa 'Pandemonium' kutokana na conflicting information(habari kinzani)

Tunarudia kuandika kwa uhakika, political base ya CDM/UKAWA imeduwaa na theme yao kuelekea uchaguzi imegeuka

Katika kipindi kifupi cha miezi 2, uongozi wa CDM/UKAWA una kazi ya kwenda kueleza nini kimetokea na kisha kuweka mada 'theme' halafu kueleza sera. Hii ni confusion kubwa sana inayoambatana na 'high risk'

CDM/UKAWA hawana rasilimali za kugeuza hali ya kisiasa kwa muda mfupi, muda hauwapi nafasi na hawana mada 'theme' kwenda mbele huku 'infrastructure' zao zikiwa zimeduwaa na kuchanganyikiwa

CDM/UKAWA wana wakati mgumu sana wa kukabiliana na hali iliyopo hasa kwa wanachama wao

Uamuzi wa kumpokea Lowassa umetoka juu kwenda chini. Je, yalikuwepo maridhiano ya dhati kuhusu hilo?

Kama hayakuwepo maridhiano, CDM ijiandae tena kukabiliana na hali nyingine.

Katika kipindi cha miezi 2, si muda wa kuweka viti sawa, ni muda wa kuwa uwanjani na kucheza.
Ndivyo ilivyo ndani ya CDM/UKAWA leo hii?

Kwa CCM kumuacha mwekezaji aondoke ni kutoa nafasi ya kupumua

Kwa CDM/UKAWA hii ni uwekezaji hatari sana na sasa wapo njia panda.

CDM/UKAWA wana wakati mgumu kuliko inavyoonekana haraka haraka.

Inahitaji maridhiano na nguvu ya pamoja, vinginevyo ''taasisi ya EL'' inaweza isiwe na mchango wa maana katika uwekezaji zaidi ya kuua jitihada za uwekezaji zilziofanywa miaka mingi

Tusemezane
 
Ahsante, nikisoma maswali yako mazito kama kawaida, naona kichwa cha mada kina fit kabisa

Kwamba, hii ni gambling inayoweza kuwa na 'dividend au disaster'

Tutaangalia tena approach iliyotumika, vigezo na hoja zilizowashawishi CDM/UKAWA kuchukua uamuzi huu very delicate!

Binafsi ni muumini wa changes, naamini mabadiliko yanayofuata hekma yana mwisho mzuri kulliko radical changes zisizo na plan

Ninajaribu kusoma values, convictions, wisdom, logics na stat, hakika sijapata jibu

Ni moja kati ya investment nisizozielewa hata kidogo kwa mantiki. Nasimama kuamini ni kosa ambalo halikupaswa kutendwa
 
Wasiwasi wangu kuhusu ujio wa Lowassa:

1. Je, atakuja na genge la mafisadi wakina Chenge, Karamagi na Tibaijuka? Au anakuja peke yake?
- Je, kama atakuja na marafiki (finaciers) wake, Ukawa wamejipangaje kuwapokea? Au watarudishiwa mlangoni?

2. Ukawa wamejipangaje kuwapokea watakaohama toka CCM? Wale waliokosa tiketi ya kugombea kwa tiketi ya CCM wakija Ukawa watapewa nafasi au watachinjiwa baharini?
- Je, Ukawa wamejipangaje kuwaenzi wanachama wao waliosimama na chama toka mwanzoni?
Sitaki kuamini kama Ukawa watawapa nafasi hao wagombea watakao kuja Ukawa toka CCM.
Mfano; Bulaya & Lembeli.
Na hao watakaotoka CCM watakubali kuja kukaa Ukawa na kuwa washangiliaji? Au wataanza kuanza kuleta fujo kama walipotoka?

3. CDM wana sheria gani kuhusu hayo makapi toka CCM? Hayo makapi yatazoea kufuata na kutii sheria ndani ya chama? Au ndo itaanza fujo za kufukuzana kama yalivyokuwa ya Zitto?
- Hofu yangu isije kusababisha CDM kuwa chama cha fujo. Viongozi washindwe ku-control wanachama.

Natamani CDM ibaki na amani kama ilivyokuwa awali. Watakaokuja wafuate sheria kama ilivyokuwa awali.
 
HOFU HII INA ULAZIMA ?

Hofu ya CCM kupasuka imepaita, na ni vema kusema sasa wanahangaika na mtikisiko. Wamepita kipindi cha mawimbi makali

Hofu iliyopo ni ya UKAWA kupoteza wanachama sawa sawa na kupasuka. Hiyo ndiyo iliyotanda ingawa haisemwi wazi

Mpasuko au mtikisiko wa CCM ilikuwa uzae ujio wa wanachama UKAWA.
Hilo lisingeathiri wanachama wa UKAWA kwani hakukuwa na sababu za wao kumfuata Lowassa au kwenda CCM.
CDM/UKAWA walikuwa na 'net gain'

Ujio wa Lowassa kwa wale wanaoamini hivyo, unasemwa ni kuongeza nguvu.
Nguvu hutokana na wananchi wanaopiga kura katika majimbo na hatimaye Urais

Tumeeleza, mchakato wa kura za maoni kwa UKAWA umekamilika.

Kilichobaki, wanaokuja, kuwa wanachama wa kupiga kura pengine za hasira dhidi ya CCM. Je, ndivyo inaweza kuwa?

Tumesikia kauli za Tundu na nyingine zikinong'ana kuhusu kuondoka kwa wanachama wa CDM wanaotengeneza UKAWA kwa asilimia kubwa. Athari kama zitakuwepo zitaikumba kambi nzima ya Upinzani.

Maana yake , Lisu anasema kama wapo watakaondoka na waondoke

Hapa kuna hali mbili kuu za kujadili

1 Ina maana kama Lowassa ataleta 600 na 550 wakondoka chadema, kwa akina Lisu hiyo ni 'net gain' Fair enough!

Wasichokijua ni kuwa hao 550 ni 'infrastructure' tayari kwa vile wanakielewa chama chao na wanakitumikia.
Thamani yao na wale wa Lowassa katika ubora hailingani

2 Mabadiliko yakitokea kwa watu kuondoka, uwezekano wa kupoteza wapiganaji wanaokijua chama chao upo

Katika mazingira hayo mawili, haieleweki wale wanaosema Lowassa anakuja na watu wanaangalia nini
Hao wanaosema atakaye aondoke wanafikiria nini.

Hofu ya CCM sasa imehamia UKAWA, Je, hofu hiyo ilikuwa na ulazima?

Itazaa matunda ya uwekezaji wa hatari kama walioufanya?

It remains to be seen'

Tusemezane
 
Ritz,

..that is old stuff.

..kuna USHAHIDI MPYA.

..Lowassa anadai mamlaka ya juu yake ilitoa amri wasaini mkataba wa richmond.

..kinachotakiwa kufanyika sasa hivi ni kuwahoji wale makatibu wakuu ambao walikuwa pamoja na Lowassa ktk kikao ambacho walipewa maagizo hayo na mamlaka ya juu.

Cc Mag3, Nguruvi3, Mkandara


Nisaidieni hapo kwenye red. Waziri Mkuu anaweza kuridhia mkataba wa mabilioni ya fedha ya umma kwa mambo ya 'kuambiwa? Serikali aliyokuwa anasiamimia Lowassa ilikuwa inafuata mtindo gani, hakuna documentation? Ingekuwa mahakamani hapa kesi ingechukuwa sura gani?

Pili, Na siku zote Lowassa ametuaminisha kuwa yeye na Kikwete hawakukutana barabarani, sasa kilimshinda nini kunyanyua simu na kujiridhisha kweli mamlaka ya juu imetoa amri? Pengine huyo mgonja alikuwa anangoea na mkewe!

Tatu, kama Lowassa aliamini kampuni ilikuwa na utata, na akasema ina utata, lakini 'akaambiwa' mamlaka ya juu imetoa amri, kwanini yeye Lowassa aliendelea kusimamia jambo ambalo anaamini lina utata? Kwanini asingejiuzulu pale pale kuonesha jinsi ambavyo hakuridhishwa na jambo hilo?

Nne, kule mwaka huu akiwa Dodoma kabla ya kutangaza nia Lowassa alisema Richmond haikuwa na shida, tatizo ilikuwa ni uwaziri mkuu. Leo hii tuamini lipi?
 
Ritz,

..that is old stuff.

..kuna USHAHIDI MPYA.

..Lowassa anadai mamlaka ya juu yake ilitoa amri wasaini mkataba wa richmond.

..kinachotakiwa kufanyika sasa hivi ni kuwahoji wale makatibu wakuu ambao walikuwa pamoja na Lowassa ktk kikao ambacho walipewa maagizo hayo na mamlaka ya juu.

Cc Mag3, Nguruvi3, Mkandara
Mkuu mimi nadhani huyu Lowassa akili zake sio nzuri! huyu mtu inabidi apimwe kwanza maana maamuzi yake ni ya ajabu ajabu kabisa. Haya madai ya kwamba amri ilitoka juu ndio mwanzo wa kujichimbia kaburi lake kwa sababu hili swala ataliamsha upya na litakula kwake.

Yeye akiwa waziri mkuu kuna ushahidi wa kutosha juu yake kuna signature zake, kuna mazungumzo baina yake na makatibu wakuu ambao nina hakika JK hakuwepo katika mikutano hiyo, hivyo hata kama JK alimwambia deal lipitishwe ilikuwa kwa simu baina yao wawili tu kwa sababu walikuwa wakilipa fadhila ya mfadhili wao.

Kumbuka Dowans ilikuwa chini ya Rostam na address ya shirika lake hivyo wameweza kuficha machafu yote kwa kuirithisha shirika la Ujasusi la Marekani waloingia kwa jina la Symbion na ndio maana swala zima limezimwa hadi leo. na mwisho JK kama rais wa JMT ana kinga wakati Lowassa hana kinga hiyo kikatiba, kwa hiyo mimi naona anacheza na Upanga.
 
Ninakubaliana na nina amini Mh. Lowassa ana wafuasi wengi wether ni kwa ushawishi, nguvu ya fedha au sababu nyingine yeyote iwayo ile.

Pamoja na haya ameamua kuhamia CHADEMA,
1. Je, uhamiaji huu ni kutokana na kukiukwa kwa taratibu za uchaguzi wa majina TU "kukatwa" kama atuaminishavyo?
2. Ni wapi nguvu yake katika malalamiko kabla ya kupitishwa mgombea Mh. Magufuli?
3. Jitihada gani zilizofanywa na yeye mwenyewe au wafuasi wake juu ya hili?



Katika uwekezaji kuna vitu viwili muhimu
1. Kuchukua hatua ambayo inaweza kuwa hatarishi 'Risk'
2. Kumthamini mwekezaji.


Hofu kubwa ni uwekezaji huu uliofanywa na CHADEMA ni ku_risk miaka takribani 20 ya vuguvugu la maendeleo nchini kwa miezi mitatu ya 'siku za usoni'. Hii ninaisema kwani umaarufu huu ilionao CHADEMA leo ni kutokana na kuwekwa wazi kwa mambo mengi yaliyojificha hasa mikataba feki, mikataba halali yenye kuletea Taifa hasara, n.k mojawapo ya hii ilimhusisha Mh. Lowassa moja kwa moja, ingawa leo wanatuaminisha kuwa pengine hawakuwa sahihi(anbayo yaweza kuwa sawa lakini kwa upande mwingine kuonekana kazi wazifanyazo si sahihi(legit).

Pili katika kumthamini muwekezaji, Mh. Lowassa amepewa "heshima kubwa" (refer maneno ya Mh. Tundu Lissu. katika chama, yaani kuwa mwakilishi/mgombea Urais kupitia CHADEMA na hatimaye UKAWA. Pengine hapa ndipo waliposema "Tanzania ni yetu sote", "CHADEMA ni chama cha watanzania wote" na "Nchi kwanza u_chama baadae"
Lakini tukumbuke mwekezaji huyu amekuja na watu wake, na kwasababu ya kuwekeza "vyema" atakuwa na masharti yake tunayoyajua bayana au yale yaliyo nyuma ya pazia. Tukumbuke mwekezaji asipothaminiwa/usipomjali atatafuta mahali pengine pa kuwekeza(lengo ni kupata faida tu). Hii yaweza kuwa kuhama kutoka CHADEMA kuelekea chama chochote kile ndani au nje ya UKAWA mf. ACT-Maendeleo.


Wakati fulani kama nchi/mwenye mali inabidi kuwa na msimamo pamoja na ahadi lukuki za mwekezaji. Kuna msemo unasema 'mfa maji haishi kutapatapa' hii ninaiona kama vile iko kwa Mh. Lowassa kwa heshima yake ndani ya chama kwa muda sasa na akitaka kushika popote kulinda hili(heshima binafsi ndani/nje ya chama).

Hofu kubwa ni kwamba ndani ya miezi michache hii, je CHADEMA itaweza kuimarika au kwa sababu kubwa ya wimbi la "wahamiaji" kuwavuruga na kupoteza mwelekeo.Ikipoteza mwelekeo sasa nguvu ya kuirudisha pamoja, kuweka dira, nguvu ya ushawishi itakuwepo au ndiyo vuguvugu la maendeleo litapotea.


Binafsi, nina amini na nitasimamia hili haikuwa sahihi kumpokea "mwekezaji" ( Mh. Lowassa) kwa sasa, angalau si haraka namna hii. Muda bado watosha katika kubadilisha mtazamo/mwelekeo/dira na kupata mwelekeo. Lakini ingawa CHADEMA wamefanya kosa hili(kwangu) na kumpokea bado kunataka kuwepo kwa muendelezo wa makosa (kumfanya agombee Urais).

'Wazungu' wanasema "Do not pick any fight not worth fighting for" na pia "Do not pick a fight with someone who has nothing to loose" Mwekezaji huyu has nothing to loose, absolutely nothing atapambana atavyoweza akishindwa ATAHAMA TU, and if so i don't think is the fight worth for us to take/gamble.

Kuna watu waliopoteza maisha, waliofungwa magerezani, waliojeruhiwa na damu kumwagika kwa ajili ya CHADEMA. Mwekezaji huyu hayajui haya, anahitaji faida, ni sisi wenye kuthamini mchango wao na si mwekezaji.Tulipaswa kuweka masharti magumu kwa mwekezaji katika kuthamini hili, mojawapo ninaamini ilikuwa ni muda wa kumpokea ikiwa umekaribia kabisa na Uchaguzi mkuu kumfanya asipate nafasi ya kwenda sehemu nyingine kuwekeza.
 
Akhsante Nguruvi3 kwa kuanzisha mlolongo huu wa mawazo. Kama sijachangia mawazo yako, ningependa kutoa maoni yangu binafsi.

Kama mtu ninayependa uhuru wa kutoa mawazo, kushiriki katika shughuli za kisiasa, na kuchagua mwelekeo wangu wa maisha bila kulazimishwa na watu, nilikata tamaa sana na jinsi CCM walivyoendeleza mabadiliko ya mfumo wa vyama vingi mwanzoni mwa miaka ya 90.

Miaka hile nilimshabikia sana Mrema. Sio kwamba alikuwa kiongozi mwenye sifa za uongozi, bali nilikuwa na iman kuwa umaarufu wake kwa kipindi kile ungeweza kuwavuta watu kwenye upinzani. Lakini kwa bahati mbaya CCM waliweza kutumia rasimali zao kama vile wazee wa chama (Nyerere, Kawawa, etc) kubadilisha mawimbi ya mageuzi.

Na vilevile nimekaata tamaa na jinsi CCM walivyoendesha mchakacho wa kupata katiba mpya. Rasimali nyingi zilitumika katika mchakacho huu, lakini hakuna matokeo muhimu ya kuridhisha.

Toka tumepata uhuru CCM imetoa elimu duni kwa sehemu kubwa ya umma. Na kwa mtaji sina tegemeo kubwa kwamba CCM wanaweza kufanya mabadiliko kwa shinikizo la kutoka kwa wananchi. Sehemu kubwa ya Tanzania bado inaridhika na kile CCM inachotoa. Kundi hili alijiulizi hata kidogo kuwa kwa rasimali za nchi, serikali ingeweza kutoa zaidi ya kile kinachotolewa sasa. Kwa mfano, watu wanafurahia ujenzi wa shule za bure lakini hawajiulizi kama shule hizo zina viwango vya kuridhisha na vya kubadilisha maisha ya binadamu.

Kama umma umeshindwa kusaidia vyama vya upinzani kuleta mabadiliko basi migogoro ya ndani ya CCM ambayo itafanya chama hicho kupunguza nguvu zake, ninaikaribisha kwa mikono miwili. Wanasema adui yako muombee njaa. Kama juhudi za vyama vinavyounda UKAWA hazipokelewe na sehemu kubwa ya watanzania, basi hatua za Lowassa za kujiunga CDM/UKAWA nazikubali.

Nazikubali kwa lengo moja tu. Kudhoofisha CCM. Kwa upande wangu, ujenzi wa taifa au demokrasia ni mradi ya muda mrefu. Na kwa Tanzania unadhoofishwa na CCM.

Lengo la CCM katika uchaguzi wa 2015, ni kushinda uchaguzi kwa kumpata rais na wabunge wengi. Lengo la upinzani liwe kudhoofisha CCM. Hili ni lengo la muda mfupi. Kama Lowassa ataupa upinzani nguvu ya muda mfupi, apokelewe lakini asisafishwe.
 
Mkuu:

Labda tutenganishe maana ya wafuasi na washabiki. Nadhani Lowassa ana washabiki na sio wafuasi. Wafuasi wako tayari kukuchangia kwa hali na mali na hata kwa kutoa roho zao. Sidhani kama kuna mtu anaweza kujitolea kufa kwa ajili ya Lowassa. Au kutoa pesa zake mfukoni kwa ajili yake.

Mwaka 1995, Mrema alikuwa na wafuasi.
 
Mkuu mimi nadhani huyu Lowassa akili zake sio nzuri! huyu mtu inabidi apimwe kwanza maana maamuzi yake ni ya ajabu ajabu kabisa. Haya madia ya kwamba amri ilitoka juu ndio mwanzo wa kujichimbia kaburi lake kwa sababu hili swala ataliamsha upya na litakula kwake.

Yeye akiwa waziri mkuu kuna ushahidi wa kutosha juu yake kuna signature zake, kuna mazungumzo baina yake na makatibu wakuu ambao nina hakika JK hakuwepo katika mikutano hiyo, hivyo hata kama JK alimwambia deal lipitishwe ilikuwa kwa simu baina yao wawili tu kwa sababu walikuwa wakilipa fadhila ya mfadhili wao.

Kumbuka Dowans ilikuwa chini ya Rostam na address ya shirika lake hivyo wameweza kuficha machafu yote kwa kuirithisha shirika la Ujasusi la Marekani waloingia kwa jina la Symbion na ndio maana swala zima limezimwa hadi leo. na mwisho JK kama rais wa JMT ana kinga wakati Lowassa hana kinga hiyo kikatiba, kwa hiyo mimi naona anacheza na Upanga.

Mkandara:

This is the thing. Kwa sababu upinzania umemkubali Lowassa, Richmond sio issue katika uchaguzi huu. Kama Lowassa angekuwa mgombea kwa kupitia tiketi ya CCM, Richmond ingekuwa issue. Hivyo Lowassa hakujibu swali, alichofanya ni ku-deflect.

Mambo ambayo Lowassa atapata taabu kuyajibu ukimuuliza, ni zile shutuma alizotoa Nyerere 1995. Sasa hivi ukimuuliza Richmond atasema kama una ushahidi nenda mahakama. Lakini 1995 alishindwa kumwambia Nyerere aende mahakama kama anao ushahidi.
 
Bavaria , Kwamba EL atakuja na watu wake, sidhani ni kosa. Mgeni akifika na mizigo, utaikataaje na kwasababu zipi?
- Kwamba, UKAWA wamejiandaaje, hilo nalo ni swali linaloeleza uwekezaji usiotabirika
- Kwamba, wanachama wa CCM watapewa uongozi, hilo halina mjadala. Ukishakuwa mwanachama una haki zote

FJM
1.Anachojaribu kusema mh EL ni kuwa alikubali mikataba, kinyume chake ingekuwa ''dereliction of duty ya military code'' ingawa alichokifanya ni ''dereliction of duty'' Nadhani utakuwa umenipata

2.Kwanini hakunyanyua simu kumpigia mkuu akiwa PM na badala yake kukubali kauli ya PS! swali gumu

3. Alisimamia si kwa simu bali bungeni kwa kukubali taarifa ya PCCB.
Hilo linathibitishwa na hoja ya 2 kuwa alijua nini kinaendelea hata alipokuwa 'under duress ys PS''

Kutokana na hayo, zipo hoja mbili tofauti. Kwanza, kama alishiriki inayohitaji vithibitisho na pili, uzembe uliopelekea hasara kwa taifa. Sina uhakika kama anapoongelea hoja hii anajua haya

Mkandara #12 Kwamba kuna ushahidi na anacheza na upanga, sidhani kama upo ushahidi wa kutosha
Hata hivyo, alipokuwa waziri mkuu alikula kiapo cha nafasi hiyo ikiwa ni pamoja na kutunza siri za serikali.

Hofu, akiendelea kuongea bila wanasheria kumshauri, hoja ndogo kama hii inaweza kutumika katika 'tech knock out' hapo ndipo tunaposema uwekezaji huu ni risk na usiotabirika

Zakumi #14
Sikubaliani na hoja kuwa wapinzani ni dhaifu. Kuanzia Mtei, Mbowe, Mrema, Slaa ni muda wa kutosha kujiufunza

Mwisho wa uchaguzi ni mwanzo wa uchaguzi mwingine. Kipindi cha miaka 10 hakuna maandalizi ya kumpata kiongozi?

Je, huyo aliyekuja akiwa mwanadamu kama wewe na mimi, likitokea jingine analojua mwenyezi, upinzani nio basi tena.

Tuna uhakika CCM imechokwa na dalili zipo. Akiwa katika sherehe za CCM mwaka huu, Kikwete alisema uchaguzi wa mwaka huu ni wa kihistoria. Anajua historia ni ipi, na upepo ulikuwa unavuma vipi

Baada ya kufukuzwa bungeni, tuliwaambia waende kujenga hoja zaidi. Hakuna aliyefanya hivyo, sasa udhaifu unaolalamikiwa ni upi? Hii hoja kaisema Lisu kama excuse , ukweli haina mashiko

Ujio wa EL haieleweki ulipangwa au ni tukio tu kutokana na hali.
Anapokuja kama taasisi na si mtu, akiaminiwa ana wanachama wengi , ni investment yenye risk sana

Hippocratesocrates
Tunaposema investment yenye risk tunamaanisha baadhi ya uliyosema.

Uwekezaji wa wapinzani umechukua muda mrefu

Je, kulikuwa na tathmini ya kutosha ya mwekezaji vs time and resources zilizotumika?

Kulifanyika risk assessment ya kutosha?
 
Mkuu:

Labda tutenganishe maana ya wafuasi na washabiki. Nadhani Lowassa ana washabiki na sio wafuasi. Wafuasi wako tayari kukuchangia kwa hali na mali na hata kwa kutoa roho zao. Sidhani kama kuna mtu anaweza kujitolea kufa kwa ajili ya Lowassa. Au kutoa pesa zake mfukoni kwa ajili.

Mwaka 1995, Mrema alikuwa na wafuasi.

Haswaa Mkuu.

Na hapo ndipo naposema this was wrong step to be taken by CHADEMA, na hata kama wapo si wote watamfuata, bado wengi walidhani anafaa kwa saba u yuko CCM akiwa kama kondoo aliyebeba dhambi ya wengine(Huruma), wengine kyona ana maamuzi magumu ya kidikteta lakini ya maendeleo(Kiongozi asiyetetereka) n.k.

Sidhani hawa "washabiki' wataenda wote UKAWA.
 
Wanajukwaa uchaguzi wa mwaka huu una changamoto kubwa kwa chama tawala na wapinzani.

Tumeambiwa kuwa leo lowassa anachukuwa fomu ya kugombea urais kwenye ofisi ya makao makuu ya chadema ufipa DSM, swali, je anachukua fomu kupambanishwa na nani? kama kuna kushindanishwa kwa mchujo je atakuwa tayari kukubali matokeo endapo yatakuwa tofauti na ilivyotegemewa? na kama inajulikana wazi kuwa yupo upinzani ili kupeperusha bendera ya urais kupitia ukawa kwanini achukue fomu?
 
Back
Top Bottom