Chadema,Ufalume wa mbinguni na ibilisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema,Ufalume wa mbinguni na ibilisi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mshikachuma, Dec 19, 2010.

 1. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 19, 2010
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwa wale waliobahatika kununua gazeti la Tanzania daima la leo Jpili tar
  19 dec-2010. Kama ni mfuatiliaji wa mambo ya siasa hasa za chama cha Chadema,
  ukifungua ukurasa wa 12 [jahazi la Jpili] ndani ya gazeti hilo utakutana na kichwa cha
  habari -CHADEMA,UFALME WA MBINGUNI NA IBILISI. Mwandishi wa makala hiyo ni Prude
  nce karugendo. Nilipenda niiandike hapa kwa faida ya wale waliokosa kuisoma makala hiyo
  lakini ni ndefu sana! Lakini kwa wale walioisoma na kuielewa makala hiyo kwa faida ya
  Chadema maoni yao ni nini? mwandishi yuko sahihi kwa faida ya chama chetu au amekosea?

  Nawasilisha
   
 2. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #2
  Dec 19, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Kwa walioisoma tupeni maoni!
   
 3. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #3
  Dec 19, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  jamani tujuzeni maoni, sasa wewe umesoma hata kutoa tu dondoo hakuna? sasa unataka ushauri gani na kwa nani kama huwezi kutupa hata dodndoo kidogo, si wote watakao kuwa wameisoma.
   
 4. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #4
  Dec 19, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,435
  Likes Received: 2,310
  Trophy Points: 280
  CHADEMA, ufalme wa mbinguni na ibilisi

  Prudence Karugendo

  MWANAHARAKATI machachari na mzalendo wa aina yake, Anney Anney, ambaye ni mkazi wa Arusha, kanitumia ujumbe mfupi wa maandishi kwenye simu yangu akiuliza hivi: “ Aisee, mbona naona mambo ndivyo sivyo kule CHADEMA? Nahisi janga! Wananchi wanaona kuwa wapinzani daima ni ukorofi tu. Hii ni picha mbaya! Mzimu wa NCCR unahamia huko?”
  Ingawa hilo lilikuwa swali binafsi lililolengwa kwangu lakini kwa ridhaa yake nimeamua niligeuze swali la umma, hasa umma wenye mapenzi mema, si kwa upinzani tu bali kwa nchi na mustakabali wake. Nimeona swali la mwanaharakati huyu lililojaa kila vionjo vya uzalendo kuliacha libaki langu binafsi ni usaliti kwa muuliza swali, ni usaliti kwa wananchi wote waliobarikiwa moyo wa uzalendo na vilevile ni usaliti kwa nchi yangu ambayo nipo kuitukuza milele yote.
  Siku mbili kabla ya ujumbe huo nilikuwa na mdahalo na marafiki zangu wakereketwa wa siasa za nchi yetu mada ikiwa ni chama gani cha siasa kwa sasa chenye uongozi imara. Nilikuwa nawaambia kuwa sijaona chama chenye uongozi imara na makini kama CHADEMA, wao wakawa wanasema CCM.
  Niliwaambia kuwa imara wa uongozi wa CCM siwezi kuuona maana mara zote nakiona chama hicho kikiwa kimebebwa na nguvu za dola, hivyo sina uhakika kama kikiachiwa na nguvu hizo, ambazo hata mimi nashirikishwa nipende nisipende, sina uhakika kama chama hicho kinaweza kutembea chenyewe kama ilivyo kwa CHADEMA. Baada ya hapo ndipo nikapata swali kutoka Arusha.
  Kwahiyo swali hilo la mwanaharakati Anney Anney, ambaye kwangu ni mzalendo wa aina yake, kila mmoja wetu anaweza akalijibu kwa namna anavyoona inafaa, ila kwa upande wangu ningependa nilijibu kwa kutumia usemi wa wahenga wa Kihaya usemao kwamba “ bakuroga wakunda wagalya!”. Usemi huo una maana ya kwamba watu unaowajua kuwa ni wabaya wako, hawakutakii mema, wakikupa kitu ambacho unahisi ni uchawi usikubali kukila, lakini ukikubali kukila usimlaumu yeyote, hata wao wenyewe wachawi wako, ila uulaumu uzembe wako kwa yatakayokukuta.
  Ndipo Wahaya wanaposhangaa kwamba ‘Bakuroga naiwe wakunda wagalya!’, yaani unaletewa uchawi na wabaya wako unaowatambua nawe unakubali kuula!
  Nikijaribu kuyatafakari yanayojiri ndani ya CHADEMA, chama ambacho kwa sasa naweza kusema kwamba ndiko matumaini ya Watanzania yalikoegemea, ninayoyaona ni kama haya yafuatayo.
  Ukweli ni kwamba kwa wakati huu tulio nao siasa za Kiafrika kwa kiasi kikubwa zinalenga kwenye maslahi binafsi, ndiyo maana tunaona wale walio madarakani wanapigana kufa na kupona ili wasipokonywe madaraka. Isifikiriwe hata kidogo kwamba tamaa hiyo ya madaraka ina uzalendo ndani yake. Watu wenye uzalendo hawawezi kufanya mambo yenye viashiria vya kuziangamiza nchi zao ilimradi tu wao wabaki madarakani.
  Kwahiyo ni watu hao walio madarakani, ambao kwa maana nyingine ndio wanaoendesha vyama tawala, wasiopenda kuona vyama vingine vya siasa vikijiimarisha kiasi cha kutishia kuvipokonya madaraka vyama tawala. Watu hao, niwaite watawala kwa hapa, hawapendi kuona vyama vya siasa vilivyo imara, inapotokea chama cha siasa kikajaribu kujiimarisha ni lazima zifanyike kila juhudi za kukidhoofisha.
  Tena ikumbukwe kwamba juhudi hizi ziko nje ya uzalendo, ni juhudi zinazolenga maslahi binafsi lakini zikiwa zinafanyika kichama pasipo na malengo ya kukinufaisha chama wala nchi inayoitawala, ila watu binafsi hasa wale walio vinara wa chama.
  Kwa maneno mengine naweza kusema kwamba huu ni mradi wa watu binafsi unaoendeshwa kwa gharama ya chama tawala kinachofaidi unafuu wa aina mbalimbali kutokana na chenyewe kuushikilia usukani kwa kuendesha nchi.
  Mfano yapo madai yenye ushahidi kwamba baadhi ya makada wa chama tawala hapa nchini ambao, mbali na mashaka ya wazi ya kuhusu uimara wao katika siasa za nchi yetu vilevile uraia wao unawasuta, wamekuwa wakijisogeza karibu na makada wa ngazi za juu wa CHADEMA.
  Kuna kila hisia zinazopambwa na ushahidi usiopingika kwamba watu hao wa CCM wanajaribu kutumia nguvu zao za kiuchumi kuwarubuni baadhi ya makada wa CHADEMA ili wawageuze misukule na kuanza kuwatumikisha kukiharibu CHADEMA kwa unafuu na manufaa ya chama tawala.
  Nayasema haya nikiwa naamini kabisa kuwa kila mmoja wetu anaufahamu ukweli huo. Kwahiyo katika kulijibu swali la msingi juu ya mtafaruku ndani ya CHADEMA kila mmoja wetu atakuwa na namna yake ya kuutafsiri ukweli huo kulingana na jinsi anavyoiona hali halisi ndani ya CHADEMA.
  Mfano mwanaharakati Anney baada ya kuwa ameuliza swali lililonichochea kuandika makala haya, katoa mtazamo wake. Anasema kwamba hili linalotokea ndani ya CHADEMA kwa sasa inabidi litufunze kutegemea wanachama wetu wenyewe badala ya kutegemea makapi wanaohamia katika chama dakika za mwisho.
  Anasema vyama viandae mapema watakaogombea nafasi mbalimbali kwa tiketi za vyama hivyo kabla ya uchaguzi. Nadhani alichotaka kukimaanisha hapa ni kwamba chama kinapaswa kuondokana na hali kama hii ambayo inakifanya kionekane kama kimbilio tu la kisiasa baada ya wanasiasa, hasa wale toka chama tawala, kuwa wamezidishiana mizengwe kwenye vyama vyao.
  Sisemi kwamba CHADEMA hakipaswi kuwapokea wanachama wapya na wale wanaohamia kutoka vyama vingine, ila zoezi hilo linapaswa lifanyike kwa umakini mkubwa ili kuwabaini wanachama wanaoletwa na mapenzi ya kweli na kuwatenganisha na wanaokuja kwa mbinu za ugaidi ili baadaye wakisambaratishe chama.
  Sidhani kama zoezi hilo ni gumu kulitekeleza kwa watu walio makini. Mfano CCM kiliweza kufanya hivyo huko nyuma kabla ya uchovu wa sasa uliokifanya kuiacha milango yake wazi kwa kila mwenye uwezo kuingia anavyotaka.
  Chama cha siasa kinapaswa kiwe na itikadi yake kinayoiamini kuwa ndiyo inayofaa kuendesha nchi kwa ufanisi na kiwe tayari kuisimamia na kuilinda kwa nguvu zote, kimaneno na kivitendo. Isiwe kama chama tawala, CCM, ambacho itikadi yake haieleweki kwa sasa kutokana na nadharia ya itikadi yake kukinzana na matendo ya kada wake. Wananadi itikadi ya chama huku nyuma wanatenda tofauti kabisa na yale wanayoyanadi!
  Kwa sababu hiyo mtu anayetaka kujiunga na CHADEMA ingebidi kwanza aonyeshe kwamba amevutiwa na itikadi ya chama na yuko tayari kuifuata na kuitekeleza kivitendo. Na mtu wa aina hiyo anaweza akaaminika anapoanzia chini kwenye shina ili kukihakikishia chama kwamba ameota mizizi ya chama.
  Siyo Yule anayekuja moja kwa moja anatua kwenye matawi na kuanza kudai kuwa naye ni CHADEMA, mtu wa aina hiyo anakuwa amesubiri tu upepo ili uje kumpeperushia kwingine kwa maana hana mizizi kwenye chama.
  Upo mfano mzuri wa hili ninaloliongelea. Majuzi mheshimiwa mmoja kwa tiketi ya CHADEMA alisikika akitaniana na mwenyekiti wa chama alichokikimbia baada ya chama hicho kumfanyia ufisadi ili asigombee ubunge, kwamba kwa sasa yuko likizo huku CHADEMA!
  Ni vigumu kuamini kwamba kwa kauli kama hiyo mtu huyo ni muumini wa kweli wa itikadi ya CHADEMA. Huyu ni mkimbizi tu wa maslahi, kayakosa kwenye chama chake kaamua kuyafuata CHADEMA, mambo yakitulia kidogo kwenye chama chake anarudi kwao. Ni kama ule wimbo wa zamani wa watumwa usemao “kumbuka tai afugwapo, akiota mabawa yake, hasahau kwake hewani, mikono ya mfugaji mitupu”.
  Kwahiyo CHADEMA kama kinataka kujihakiki uimara wake kisijiangalie tu kwenye matawi na kujiridhisha na ushamiri unaoonekana huko juu, kinapaswa kijiangalie kuanzia kwenye shina na kuhakikisha kama mizizi yake imekaa sawasawa. Chama ni mizizi si matawi, na daima kushamiri kwa matawi kunategemea uhai wa mizizi vinginevyo hakuna mti.
  Tatizo lingine ninaloliona katika CHADEMA ni ile hofu ya kwamba mtu fulani akiguswa basi chama kitayumba au kusambaratika. Kwahiyo baadhi ya watu wanaitumia hofu hiyo kuugeuza umaarufu wa chama kuwa mradi binafsi. Wapo wanaoonekana kuutumia umaarufu wa chama kama mali binafsi na hivyo kutaka kujifanya watu wasiogusika. Wanaonekana kutaka kuitumia nafasi hiyo kufanya biashara haramu ya usaliti.
  Rai yangu ni kwamba chama kinapaswa kiikatae hali hiyo kwa nguvu zote, ijengwe hali ya kila kada kujiona sawa na mwingine kwa maana ya kwamba anaweza akasemwa au kuguswa inapobidi, umaarufu wa kutokuguswa ubaki ni wa chama pekee. Huo ndio mfumo unaotumiwa na vyama vyote vya siasa ulimwenguni vilivyotokea kujijengea uimara. Chama kama taasisi hakipaswi kuyumbishwa na mtu mmoja au kundi la watu ndani yake.
  Chama ni taasisi, na taasisi iliyo imara haiwezi kuendekeza kitu kinachoitwa kwa lugha ya kigeni “one man show”. Tunapaswa kujifunza kwa chama kikongwe Barani Afrika, ANC cha Afrika Kusini. Chama hicho hakikuona ugumu kumvua uenyekiti Thabo Mbeki ambaye pia ndiye aliyekuwa rais wa nchi baada ya kubainika kuwa anakiendesha ndivyo sivyo. Na baadaye chama hicho, kwa vile ndicho kilichokuwa kimempatia tiketi ya urais wa nchi, kikaamua pia kumuondoa Mbeki kwenye urais wa nchi. Sisi tunashindwa nini?
  Kwa sasa Wanachadema wanahisi usaliti ndani ya chama chao, wanajiona wanasalitiwa. Na kila dalili za usaliti zinajionyesha wazi. Ila kuna hofu ya kuukabili usaliti huo kwamba chama kitayumba au kusambaratika. Tunaiona saratani iliyouingilia mwili wetu ila tunaogopa kuipeleka kunako husika ili ikadhibitiwe kwa hofu ya kwamba kitaondolewa kiungo ilikoingilia na kutuachia ulemavu!
  Lakini si bora ulemavu tukabaki na uhai? Maana saratani ikisha sambaa mwili mzima kinachofuatia ni kifo. Kuzuia hilo ni kuwahi ilipoingilia saratani na kukiondoa kiungo husika.
  Katika sakata hili mimi naona bora kuwashughulikia wasaliti wote ndani ya CHADEMA bila ya hofu yoyote, hata kama chama kinasambaratika. Heri kutokuwa na chama kuliko kuwa na chama kilichojaza wasaliti wanaoonekana kuwatumikia wapinzani wa chama.
  Hali hii inaonekana kuwachosha wanachama. Tujikumbushe kilichotokea Mwanza wakati wa Uchaguzi Mkuu pale wananchi walipokuwa wamezilinda kura zao za majimbo ya Nyamagana na Ilemela zisichakachuliwe.
  Serikali ilimuomba mmoja wa wagombea, Wenje, awatulize wananchi, kwa hapa niwaite wanachama. Wanachama walimjibu mgombea kwamba katika hali kama hii hata wewe hatukuamini. Hiyo ni hofu iliyojengwa na tabia ya usaliti.
  Kama wanachama walifikia kumwambia hivyo mgombea wao waliyeamini kashinda ila wakihofu kuwa anaweza kushawishiwa akakubali kushindwa, wanaonyesha ni kiasi gani walivyo tayari kufanya kazi kitaasisi kuliko kumtegemea mtu mmoja “one man show”. Hivyo wasaliti wote katika CHADEMA wanaweza wakatupwa nje na chama kikaendelea na uimara wake. Hata wasanii wa muziki waliwahi kuliona hilo katika kibao cha MV Mapenzi 2 cha Mlimani Park.
  Msisitizo wangu ni kwamba inapaswa ieleweke kuwa hatuwezi kuupata ufalme wa mbinguni tukishaelewa kwamba kiongozi wetu ni ibilisi. Kwahiyo ili tuwe na matumaini ya kuuona ufalme wa mbinguni kitu cha kwanza ni kumkana ibilisi, hata kama kwa ushawishi wake, tutakuwa tumetokea kumpenda kwa kiasi gani.
  CHADEMA bila usaliti inawezekana. Hofu ya kwamba wakiguswa watu fulani chama kitayumba itatufanya tuendelee kucheza mahepe, ngoma inayochezwa gizani, kiasi cha watu kudai kwamba ni ngoma ya wanga. Kwa kuyapuuza haya CHADEMA itakuwa inajifanyia usaliti yenyewe kama Wahaya wasemavyo, “Bakuroga naiwe wakunda wagalya!”

  CHADEMA, ufalme wa mbinguni na ibilisi
   
 5. B

  Bull JF-Expert Member

  #5
  Dec 19, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chama cha kidini na kikabila, kinaonekana kwa terminology zake. kisipewe nafasi tanzania.
   
 6. Halfcaste

  Halfcaste JF-Expert Member

  #6
  Dec 19, 2010
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 973
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  waafrica hawana dini ndo maana viongozi wake uanguka anguka majukwaani kwasababu huamini nguvu za giza.ila utumia madhehebu kupata kura za wajinga na walevi wa dini za wauza watumwa(arab) na wakoloni
   
 7. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #7
  Dec 19, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  macho_mdiliko
  heshima kwako, nimekugongea ka thanx hapo juu. Sina cha kucoment hapo kwa Prudence Karugendo makala imegusa sehemu zote nyeti
   
 8. B

  Bull JF-Expert Member

  #8
  Dec 19, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Nadhani wanao amini nguvu za giza ni wale wanaolawitiana na kubaka watotot kwa jina la bwana, ningependa ufahamu waafrika wengi wan dini takatifu zisizo fuata sheria za kishetani
   
 9. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #9
  Dec 19, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180


  Amka brother, achana na mawazo mgando, Tanzania bila CCM inawezekana! Kuendelea kuikumbatia ccm inaonyesha jinsi ulivyo na mawazo mgando.
   
 10. M

  Molemo JF-Expert Member

  #10
  Dec 19, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Huyo BULL anaonekana ni udini unamsumbua.Siku CCm itakapoweka mkristo kugombea urais atakimbia na kuanza kuwatukana.Watu wenye akili finyu siku zote huhangaika na mambo ya kidinidini.
   
 11. B

  Bull JF-Expert Member

  #11
  Dec 19, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Mkuu mimi si ccm, ni think tank on my own, lakini sikubaliani na udini, ukabila ulioko chadema, simply siwezi isaliti nchi yangu

  I am independent observer
   
 12. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #12
  Dec 19, 2010
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  Nimeipenda comment yako mkuu, siku CCM wakimsimamisha mgombea urais mkristo, bull nawenzake wataitukana CCM, nawewe utakimbilia huko kutoa support, will that signal the end of CDM?
   
 13. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #13
  Dec 19, 2010
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  Nimeipenda comment yako mkuu, siku CCM wakimsimamisha mgombea urais mkristo, bull nawenzake wataitukana CCM, nawewe utakimbilia huko kutoa support, will that signal the end of CDM?
   
 14. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #14
  Dec 19, 2010
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Bull pole sana na hizo tongotongo zako machoni hadi ubongoni.
  Uzuri ni kwamba hujui kama mimi ninakufahamu kuanzia unyayoni
  hadi utosini! kwahiyo huwezi sumbua akili yangu wala ya mtanzania
  yeyote yule mwenye akili timamu zidi ya hizo pumba zako mgando.
  wewe hujui kuwa UDINI na UKABILA ni kaulimbiu ya CCM katika chaguzi
  zote? Eti unadai wewe si CCM,wakati wewe ni zuzu la ccm.Hata mda wa
  kula chakula unaomba dua kwa katiba ya ccm ndipo uanze kula.shame on u
   
 15. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #15
  Dec 19, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  sasa wote mmeacha kujadili mada mnamjadili huyo bull, yeye hataki mjadili mada wewe mgongee kale kadubwasha kekundu utaeleweka.

  Shibuda nakumbuka alisema source:mwananchi anaondoka ccm ila ipo siku atarudi kwani hajagombana na mtu ccm. Ni kweli Karugendo tuandae wagombea wetu na hapa ndipo linakuja swala la umuhimu wa kuwa na chuo cha maadili CHADEMA
   
 16. B

  Bull JF-Expert Member

  #16
  Dec 19, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Chuo cha maadili ya chadema kwanza apelekwe Mchungaji Slaa alievunja maadili yote, Mfano;

  1. Aliowa wakati mchungaji mkatoliko haruhusiwi kuowa, alivunja maadili ya kanisa katoliki

  2. Alipo owa akamuacha mwanamke talaka, nikinyume na kanisa

  3. Kaowa tene mara ya pili tena mke wa mtu, La hawla wala kuwata.

  4. Kafukuzwa ukatibu mkuu wa kanisa, sababu ya utovu wa nidhamu na ubadhirifu

  5. Alijiunga ccm baada ya kunyimwa nafasi ya ubunge akaenda chadema, hana msimamo wala haaminiki.

  6. Habari chafu ndani ya kanisa katoliki, ni miongoni ya wachungaji wanaohusishwa na maswala machafu, ushahidi utatolewa hivi karibuni

  Chuo hicho ni muhimu kwa viongozi wenu, watakapo faulu ndio tuwafikirie kama wataweza kuendesha nchi hii takatifu
   
Loading...