Geza Ulole
JF-Expert Member
- Oct 31, 2009
- 64,416
- 90,495
Kwa maehsabu ya haraka inaelekea CUF wanawania kuongoza kambi ya upinzani wakiwa na fikra ya kuwa watashinda viti vinne vya visiwani na ukichanganya na vinne vya NCCR-Mageuzi na TLP; Wataweza kuunda serikali ya upinzani maana watakuwa na zaidi ya vya CHADEMA; ila nathani katiba inasema chama kinachopaswa kuunda serikali ya upinzani ni kile kilichopata kura zaidi ya 12% na nathani hapa CUF watashindwa kubadilisha hili! Na pia ni ushauri wa CHADEMA kuhakikisha viti vilivyokwapuliwa kiutata (10+) na CCM vinashughulikiwa mahakamani naona Mh Mpendazoe ameanza kuonyesha njia!