CHADEMA tv

kwa hilo jina sijui kama watapata masafa labda wajiite tanzania daima tv.
 
Confirmed, Mh Regia kaweka habari hii kwenye page yake facebook
 
Regia Estelatus Mtema
Wapendwa CHADEMA tumezindua TV yetu kupitia mtandao haijazinduliwa officially..Tembelea mtandao wa Chadema.tv ujionee na kusikia yanayoendelea kwenye Kampeni Igunga..Kila siku tunaongoza njia wengine wanafuata..
 
Du!hiyo link nashidwa kuifungua kwenye mchina wangu, tafadhal wenye sim zenye uwezo/wanaotumia laptonga mtujuze zaid
 
CHADEMA Televishen ni chombo kilichotarajiwa kwenda hewani tangu mwaka juzi.

Tafadhali msitufanye tukasubiri sana kwa chombo hiki na kuendelea kunyanyaswa na TBC Ujima kwa kutelekeza majikumu yake wakati wa msiba uliogusa taifa zima na badala yake kuamua kuburudisha baadhi ya viongozi wa CCM kwa mirindimo ya taarab.

Jambo hilo la kusikitisha sana lilikua likitokea huku taifa zima likihangaika kutafuta habari juu ya hatima za ndugu zetu kwenye ajali baharini. CHADEMA tusaidieni haraka kuziba pengo hilo kwani sisi wengine tulishajiamulia tangu Tido aondoke pale kujifanya kama vile TBC haikuwahi kwepo hata siku moja kwa ajili yetu na kwa kodi zetu katika taifa hili.
 
Iko poa CTN Chadema Television Network

Ni Idea Nzuri....sema kwa vile TV lengo lake ni kuhabarisha watu wa itakdi zote, ni vyema Chadema wakafanya utafiti wa JINA litakalokuwa na mvuto kwa wote. Ukiita Chadema, hardly mtu wa CUF au CCM atapenda kuangalia.
Mfano mzuri ni vyombo vyenye majina kama Tanzania Daima, Uhuru, Mzalendo etc.....ambavyo vinafuata mlengo wa vyama husika bila kuonyesha waziwazi.
 
Back
Top Bottom