SPACED
Senior Member
- Jun 7, 2016
- 137
- 132
Wanabodi
Nianze na pongezi kwa shughuli pevu inayofanyika humu katika ujenzi wa taiga letu.
Ndugu wapenda mabadiliko, haki na demokrasia ya kweli; inavunja sana moyo pale tunapopambana kwa hoja maridhawa na chama dola (na kwa kiasi kikubwa sana tunawashinda na kuzidi kukubalika zaidi kwa umma) lakini jitihada hizo zinafifishwa na watu wachache. Inakera sana.
Wapo watu wachache ambao kwa sasa wanadandia matukio na kuyarun kwa hoja cheap na za kitoto kwa mgongo wa upinzani wenye vinasaba na chadema. Hii inatujengea taswira mbaya mtaani.
Chadema inakubalika kwa hoja zake madhubuti (statistical & researchable) zikihusishwa na approach pamoja na presentation yake kwa jamii. Huu ndio uchawi wa chadema unaowanyima usingizi CCM. Lakini umahiri huu sasa umeharamiwa na watu wenye chuki binafsi wanaotumia mitandao ya kijamii kuattack personalities za watu na sio hoja na agenda za chama.
Watu hawa imekuwa sasa kila tukio (hata kama ni zuri kwa kiasi fulani katika jamii, maana lisipo-solve shida zako limesolve tatizo la jamii fulani) wao wanalizungumzia kama msimamo wa upinzani tena kwa hoja zisizo na mashiko zilizojaa matusi na chuki binafsi dhidi ya watu fulani/kada fulani inayojaribu kupingana na mitazamo yao. Kitu hii ni mbaya sana maana wabaya wetu wanatumia loop hii kuiaminisha jamii jinsi upinzani wetu usivyoitakia mema jamii hiyo, hatimaye huonekana sasa kama ni upinzani uliokosa dira.
Kuna mambo watanzania hawajayazoea kabisa na ndio yanayotuchafua mtaani tunapoyashabikia bila kuyakemea kwa namna inavyotofautiana na wenzetu wa CCM. mambo ni kama, hoja za matusi ya nguoni, kutetea ufisadi wa wazi, unafiki, usaliti, kupinga miradi ya maendeleo inayotekelezwa na mtu usiempenda, ubinafsi, upotoshaji wa wazi, uchonganishi, na mengine mengibmithili ya hayo.
Rai yangu kwa upinzani hasa Chadema yenye jina kubwa, tujitenge sana na masalia ya CCM hasa yaliyokosa uelekeo na kuja kujifichakwetu kisha kukichafua chama kwa kujua au bila kujua.
Mwisho kama chama naomba tuwakane watu hawa kuwa sio mtandao wetu ama tuwakubali kuwa ni wenzetu na tuwarejeshe kwenye misingi ya chama chetu bila kubeza jitihada zao wanazozionesha katika jamii kupitia mitandao ya kijamii.
1. Ni huyu msichana anaejiita Mange Kimambi, anatuharibia sana brand yetu licha ya harakati zake zilizojikita kwenye personalities to whomever criticises her. Matusi hayajengi yanakuonesha what kind of a person you are. ( a rejected leader)
2. Tanzagiza, hawa ni wazuri ata kama sio wetu. Tuwaimarishe zaidi kwenye hoja na sio personal attacks
3. Wachangiaji wenye malengo sawa na yetu hasa wanaochipukia zaidi katika siasa. Tuwaelekeze namna ya kupambana bila kuiudhi jamii tegemeo lao. Tuwakumbushe katika hoja zao kuwa dola haishikizwi kwa mihemuko bali hoja zinazogusa na kulinda maslahi yao. Tuwashauri wasitukane na kukejeli vyombo vyetu vya ulinzi na usalama bali kuwapa taarifa na mbinu bora zaidi kulilinda taifa, nao watatupenda na kutuamini daima, watakuwa marafiki na wanachama wetu na kwa roho safi watatusaidia sana kuishika dola tunayoitafuta.
Maadili, uzalendo, amani, demokrasia na ajenda thabithi ndizo silaha zetu siye wasaka Dola.