CHADEMA, Tusitumie madai ya Katiba Mpya kumrudishia uhai wa Chama sio Matakwa ya Watanzania kwa sasa

JUMA JUMA

Senior Member
Jan 5, 2013
164
250
Naomba kuwakumbusha Wana jukwaa MCHAKATO wa Katiba Mpya ni Ajenda ya CCM wakati wa awamu ya nne Chini ya Rais Mstafu Jakaya Mrisho Kikwete Chini ya utashi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kutufikisha katika hatua ya Katiba pendekezwa.

Lakini kwa Sasa linaonekana Jambo jimpya kwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuifanya Ajenda hii Kama nguzo muhimu ya kumrudishia uhai wa Chama ambacho kimepoteza matumaini kwa Watanzania wanaotaka siasa za Maendeleo na si siasa za maneno na Matukio. Hivyo nitoe rai kwa vijana kutojiingiza katika maswala ya watu flani flani kwa maslahi yao na kufanya maslahi yaonekane ni takwa la Watanzania.

CHADEMA inapaswa kukumbuka kuwa maktaba ya Katiba Mpya hadi Sasa ipo na kwenye kabati lake Kuna Katiba PENDEKEZO. Hivyo wakati ukifika waliouanzisha wataumalizia.

CHADEMA nawakumbusha pia kurudisha uhai wa chama si kubeba kila Ajenda maana mmekuja na kila Ngoma mkademka nayo lakini mmegonga mwamba. Kaeni Chini mjiulize watanzania wanataka nini kwa Sasa. Si kingine siasa ya kuleta Maendeleo

Vijana msiingie katika huu mtego wa kukuza hizi Akaunti zao kwa manufaa yao kisiasa na si maslahi kwa watanzania usifollow wala kufungua hizo akaunti zao za KATIBA. MPYA TANZANIA MAANA NI USALITI KWA TAIFA
 

Kinoamiguu

JF-Expert Member
Nov 29, 2018
4,650
2,000
Msikilize Ally salehe Alberto . Soma barua yake juu ya TFF kama unaelewa utajua issue ya katiba mpya ilivyokuwa muhimu kwa sasa. Hilo ni suala la muda tyuu
 

LIMBOMAMBOMA

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
9,061
2,000
Mkuu pole, katiba mpya ni ajenda ya watanzania wote.Anayepuuza hitaji la katiba mpya huyo hajitambui..
 

Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
24,662
2,000
Tunataka siasa za Maendeleo sio kelele
Nadhani una elimu duni ,Siasa zipi za maendeleo unahitaji ikiwa katiba ina mapungufu ,maendeleo yanatokana pia na katiba ambayo inakidhi haja za wengi siyo kulinda maslahi ya wachache waliopo madarakani na kuwaruhusu kufanya watakavyo ,haiwezekani uiingizie taifa hasara halafu huguswi kisa kuna kinga.

Hizo porojo zako kahadithie familia yako wakati mnachoma mahindi
 

MZALAMO

JF-Expert Member
Jul 6, 2009
1,444
2,000
Tuanze na marekebisho ya katiba ya Chadema kwanza inayoruhusu mwenyekiti kukaa madarakani zaidi ya miaka ishirini, mkirekebisha katiba yenu kwanza tutawaona mko serious na tutawaunga mkono kwenye kudai katiba ya nchi.
 

Jp Omuga

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
4,508
2,000
Mkuu utanisamee lakini nawaalaumu wazazi wako kule kijijini kwa kukupeleka shule! Hela zote hizo ni bora wangenenepesha wale ng'ombe!!
 

Jp Omuga

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
4,508
2,000
Tuanze na marekebisho ya katiba ya Chadema kwanza inayoruhusu mwenyekiti kukaa madarakani zaidi ya miaka ishirini, na mkerekebisha katiba yenu kwanza tutawaona mko serious na tutawaunga mkono kwenye kudai katiba ya nchi.
Pengine hao wana CDM hawaoni shida kwenye Katiba yao kama ambavyo ccm hawaoni tatizo kwenye Katiba yao.
Lakini kwa wingi wao; Watanzania wanaona shida kwenye Katiba iliyopo. Na kwa uhakika wanataka Katiba Mpya!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom