CHADEMA tuondoleeni wasiwasi huu kama kweli mtaweza kuongoza Tanzania.! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA tuondoleeni wasiwasi huu kama kweli mtaweza kuongoza Tanzania.!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Molemo, Aug 10, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  WanaJF

  Ni ukweli ulio dhahiri kwamba chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA kwa sasa kimejijengea imani kubwa kwa watanzania kiasi kwamba wananchi wameanza kuamini kwamba kumbe hata bila CCM nchi inaweza kusonga mbele.Ni jambo la kuwapongeza viongozi wakuu wa chama hicho wakiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wake Dr Wilbroad Slaa kwa kufanikisha imani hiyo kwa chama chao.

  Hata hivyo kumeanza kujitokeza mashaka kutoka kwa wananchi mbalimbali kutokana na mashambulizi mbalimbali hasa ya kashfa dhidi ya viongozi wakuu wa chama hicho hususan Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa yanayotolewa na wanaodai ni watu walioko ndani ya uongozi wa CHADEMA.

  Watu hao wanaosambaza kashfa hizo kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii wamekuwa wakiongozwa na mtu anayejiita TUNTEMEKE anayedai yuko ndani ya uongozi na anafanya kazi makao makuu ya chama.Kwa vyovyote vile hili kundi kamwe haliwezi kuwa na nia njema na chama hicho kwa sababu katika hali yoyote kama wewe ni kiongozi una nia njema na chama chako huku ukiwa huridhishwi na matendo ya wenzako unapaswa kufanya mambo mawili kati ya yafuatayo:Kwanza kuyasema mabaya ya viongozi wenzako ndani ya vikao halali na Pili kama hatua zisipochukuliwa inakubidi utoke hadharani unajiuzulu nafasi zote na kutangaza kwa wananchi mabaya ya viongozi wako.Haiwezekani hata kidogo na wala haikubaliki katika demokrasia ukiwa hadharani kuwachekea viongozi wako na ukiwa gizani unatangaza kuwaangamiza.Huo ni UASI. Kamwe UASI haukubaliki katika chama chochote iwe ni CHADEMA,CUF,NCCR wala CCM

  Kilichotushangaza sisi wengine hata kuamua kulisemea hili ni ukimya wa viongozi wa CHADEMA.Vurugu hizi za kundi linaloongozwa na TUNTEMEKE zina karibu mwaka sasa na inafikia mahali baadhi ya wananchi wanaanza kuamini hizo tuhuma zinapoanza kusambazwa tena kwa ustadi mkubwa.CHADEMA imekuwa sikuzote ikijipambanua kama chama chenye Intelejensia ya hali ya juu sana ni kwanini wasitumie ukachero wao kuwabaini WAASI hawa wote na kuwafukuzilia mbali? Huyu TUNTEMEKE katika uchaguzi mdogo wa Arumeru alitoa siri zote za vikao vya CHADEMA kwenye mitandao mbalimbali na kujiapiza ni lazima chama chake anachodai kukitetea kishindwe! Matokeo ya uchaguzi ule sasa ni historia!

  Si nia yangu kutoa utetezi kwa mtu yeyote kama ana kosa lolote lakini katika demokrasia ya kweli haikubaliki watu kujificha ndani ya vyama kwa unafiki huku wakila njama za kuangamiza vyama hivyo kwa siri.CHADEMA wanapaswa sasa kuchukua maamuzi magumu haraka iwezekanavyo kama wanataka kuendelea kulinda heshima yao waliyojijengea kwa wananchi.Nina Imani CHADEMA wana uwezo wa kuwatambua WAASI wote na kuwaondoa kabla hawajaleta madhara makubwa kwa chama hiki ambacho sasa ni tegemeo kuu na ndiyo mdomo wa wananchi.

  Dr Wilbroad Slaa na Freeman Mbowe wanapaswa kuwathibitishia watanzania kwamba wako imara kwenye uongozi na kwamba hata wakikabidhiwa Taifa wanaweza kuliongoza bila kuruhusu UASI wowote ndani ya nchi.Ningependa kuwaambia waige mifano ya vyama vya CUF na NCCR ambavyo vimewatimua WAASI wao ambao walikuwa na nyadhifa kubwa za Ubunge sembuse hawa wa CHADEMA wanaoficha utambulisho wao chini ya TUNTEMEKE na kukiacha uchi chama chao huku wakipulizwa na viyoyozi vya chama hichohicho wanachokipiga vita makao makuu Kinondoni mtaa wa UFIPA.

  Sisi wengine kazi yetu ni kutoa tahadhari kwamba CHADEMA wanapaswa kulinda kwa nguvu imani waliyojiwekea mbele ya Watanzania na kuchukua maamuzi ambayo yatakuwa ni ishara njema ya kulinda heshima ya chama hicho pendwa cha Watanzania.Dr Wilbroad Slaa na Freeman Mbowe tunawataka watuondolee wasiwasi wananchi kwamba tukiwapa nchi wanaweza kutuvusha salama.!

  WanaJF karibuni kwa mjadala.
   
 2. M

  Molemo JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Hakika umeandika kwa ustadi mkubwa sana.Sina cha kuongeza hapo.Mungu akubariki Fmpiganaji
   
 3. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,780
  Likes Received: 6,114
  Trophy Points: 280
  Ustadi sio kwenye mantiki tu bali hadi kwenye font, mpangilio wa paragraphs, line spacing, etc. Inavutia.
   
 4. REMSA

  REMSA JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,569
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Good,maana kuendelea kumchukulia mtu kama Tuntemeke kwamba ni kichaa wakati anaendelea kuleta
  uharibifu kwa Chama ni kosa.
   
 5. only83

  only83 JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Nadhani naona kuna mambo kadhaa hapa...moja, inawezekana huyu TUNTEMEKE ni galasha fulani ambalo halina mahusiano kabisa na CHADEMA zaidi ya kuwa mropokaji kama wengine walivyo hapa JF na Tanzania kwa ujumla. Pili, Inawezekana hoja yako ikawa ukweli kuwa huyu TUMTEMEKE ni mwanachama wa CHADEMA na anafanya haya kwasababu zake binafsi, ama kwa kutaka madaraka au kulinda maslahi ya kundi lake. Lakini tunapaswa kutambua kuwa ukiwa mwanachama wa chama fulani halafu unaendesha mapambano ndani ya chama tena sio kukirekebisha ila kukiua ni udhaifu na upuuzi.
   
 6. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #6
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Atapatikana tuu muda si mrefu watu wa aina ya Tumtemeke wengi wao wapo CCM
   
 7. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #7
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Tumtemeke ni Sawa na wakina Dada Chama wa Gombo la mboto pamoja na dada majebere, wanaropoka kwa kuhisi
   
 8. Kesho Uanzia Leo

  Kesho Uanzia Leo Member

  #8
  Aug 10, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakina Tuntemeke ni aina ya viongozi wachumia tumboni ambao wako kwenye vyama vya siasa kwa ajili ya vyeo wakikosa vyeo ndio matokeo yake UASI..Viongozi wa Chadema wanamfahamu sana Tuntemeke na kuna kipindi waliahidi kumchukulia hatua za kinidhamu.sasa sijui walifikia wapi?
   
 9. m

  majebere JF-Expert Member

  #9
  Aug 10, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,522
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Hivi wakati Slaa alivyo wataja mafisadi alikua na nia ya kuharibia serikali au alikua anatuonyesha waovu yanayo fanyika? Sasa tuntemeke kututoa maovu ya CDM imekua kosa.
   
 10. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #10
  Aug 10, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Sina la kuchangia, nasubiri kuona reaction ya CHADEMA.
   
 11. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #11
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Cha kufanya kwa viongozi wa chadema ni kumjibu huyu tuntemeke kwa kila kashfa au jambo atakaloleta na huo ndo utakuwa ukomavu wa kisiasa badala ya kumshushia matusi
   
 12. M

  Molemo JF-Expert Member

  #12
  Aug 10, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kabisa CDM wanapaswa kuonyesha misimamo
   
 13. M

  Molemo JF-Expert Member

  #13
  Aug 10, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Slaa hakuwa sehemu ya serikali na wala Slaa hakujificha kuongea yale,aliyaongea hadharani tena kwenye uwanja wa Mwembeyanga.Take my Point.
   
 14. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #14
  Aug 10, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,748
  Likes Received: 12,842
  Trophy Points: 280
  bila kumsahau mkewake Genda!
   
 15. T

  Tata JF-Expert Member

  #15
  Aug 10, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,741
  Likes Received: 661
  Trophy Points: 280
  Tunawataka akina Tuntemeke wengi zaidi CHADEMA, CCM, CUF, TLP na kwenye vyama vingine vyovyote. Isingekuwa akina Tuntemeke wa CCM habari za mafisadi wa CCM tusingewajua kamwe. Penye ukweli uongo hujitenga. Kama anayosema huyu ndugu Tuntemeke kuhusu CHADEMA ni ya uongo na uzushi kamwe hatafanikiwa ila kama yana ukweli basi anafanya jambo la muhimu sana kwenye ujenzi wa demokrasia imara nchini. Hatutaki kuiondoa CCM na kisha kuingiza CCM nyingine yenye jina tofauti lakini matendo yaleyale.
   
 16. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #16
  Aug 10, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  fmpiganaji umeliweka vizuri sana hili suala la hawa WAASI wanaotumia mgongo wa Chadema kuivuruga na kutaka kuismabaratisha.

  Nakubaliana na wewe kwamba umefika wakati sasa wa kufanya yafuatayo;
  1. Viongozi tajwa kuchukua hatua za dhati za kuisafisha nyumba yao kama kweli ni chafu kiasi hiki kinachoelezwa hapa.
  2. Kufanya uchunguzi wa kina na kumbaini muasi/waasi wanaovujisha mambo ya ndani ya chama na kuwachukulia hatua zinazostahili mara moja wahusika (hapa ni kuwafukuza uanachama tu)
  3. Kuweka udhibiti wa taarifa nyeti za chama ili kuondoa mianya ya taarifa hizo kuvuja na kuwafikia watu wasiohusika na wenye nia mbaya ambao huzitumia vibaya habari hizo kwa manufaa yao binafsi na kukidhalilisha chama.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. M

  Molemo JF-Expert Member

  #17
  Aug 10, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  You said well.CDM wachukue hatua naamini wanamjua yeye na kikundi chake.
   
 18. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #18
  Aug 10, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Ubarikiwe, wabarikiwe wazazi wako, wabarikiwe wote wanaokutakia mema! Wewe ni mmoja wa watanzania wachache sana wanaowafikiria wengine katika kupata mema ya nchi hii. Umeeleweka MTANZANIA & MZALENDO WA KWELI KWELI, bila ya shaka MBOWE NA DR SLAA wamekuelewa bara bara! Natamani kukurushia Tshs.50,000/= ili ununue angarau machungwa kwa afya yako nitakupataje????
   
 19. M

  Molemo JF-Expert Member

  #19
  Aug 10, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Kukaa ndani ya chama na kuendesha uasi wa kukiua ni sawa? Kuvujisha siri za chama za mikakati ya ushindi Arumeru ili chama kishindwe huko ni kupambana na ubadhirifu? Wake up man.
   
 20. N

  NG'ONGOVE Senior Member

  #20
  Aug 10, 2012
  Joined: Apr 28, 2012
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe 100%. Katika mazingira kama haya ambayo magamba wamebanwa mbavu kiasi hiki tutegemee kuwa na akina tuntemeke wengi ndani ya cdm.
  Cha maana hapa ni busara itumike ktk kuwashughulikia hawa dumuzi
   
Loading...