Chadema tunataka ukombozi loliondo

Jasho la Damu

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
956
120
Ujumbe huu uwafikie wanachama na viongozi wa Chadema popote walipo. Loiliondo Tunahiatji ukombozi, sisi wananchi tumechoshwa na udhalimu unaofanywa na serikali ya CCM kupitia Halmashauri yake. Wilaya hii ndio wilaya ya pili katika kuchangia pato la taifa lkn ndiyo wilaya ya mwisho katika maendeleo. Wilaya hii ilianzishwa mwaka 1979 lkn mpaka leo hakuna maji yanayotoka ndani ya bomba, hakuna umeme, huduma mbovu za hospitali hata sehemu ya kuzikia mahiti ukifika waweza kutoa machozi.

Chadema karibuni loliondo tuwakomboe watz, majemedari waliopo huku hawatoshi kuimarisha nguvu japo mchango wao ni mkubwa katika kukitangaza chama, hv sasa katika nyumba nyingi za hapa loliondo zinapeperusha bendera ya Chadema na hii inatokana na ujio wa Mhe Mbowe mwaka jana watu walipata hamasa na wakahamasika mpaka kufikia hatua ya Dr. Slaa kuongoza kwa kura za uchaguzi mkuu katika vituo vya wasso na loliondo.
 
Usihofu tunakuja,tunajipanga kwa operesheni safisha Tanzania.........
 
Ndio huko wanakoibiaga kura lakini hakika Makamanda watafika na kuwa mpole kidogo majibu utapata.
 
Ukombozi wa nchi si wa Chadema pekee, kila mtanzania anawajibu wa kuikomboa nchi yake.
 
Kila mtu anawajibu lakini tunahitaji wa kutuongoza na kutuwakilisha na hii ndiyo sababu hatuendi raia wote pale katika nchi ya wagogo(mjengoni)!
 
Ukombozi wa nchi si wa Chadema pekee, kila mtanzania anawajibu wa kuikomboa nchi yake.

chama cha demokrasia makini=CHADEMA IS IMENOGA,chama cha mapinduzi=CCM is IMECHACHA.Bado hujaelimika tu!
 
Ama kweli CCM imepoteza dira nipo hapa Iringa naongea na wanafunzi wa vyuo maeneo ya Miomboni wote hawaitaki CCM, yaani mpaka Loliondo CHADEMA mnaitaka tumewasikia na tutawafikia.
 
Huu ni mwaka wa kukaba kila kona ya nchi hii,kila mzalendo wa kweli na anayejitambua anawajibu wa kutoa elimu ya uraia na uzalendo kila mahali alipo ili tuweze kuikomboa nchi yetu toka mikononi mwa manyang,au,mafisadi yaani ccm.muda huu si wakushangaa tena ni wakt wa kupambana kwelikweli.Mungu ibariki Tza,Mungu ibariki cdm
 
Tarafa ya loliondo kwa ujumla ni eneo ambalo kwa ukweli watu wake wameshaichoka ccm kutokana na hili tatizo la mwekezaji wa kiarabu aliyemilikishwa kitalu cha uwindaji bila ridhaa ya wanakijiji.Tatizo linalosababisha CDM isiwe na uimara hapa ni uwoga wa unaosababishwa na elimu ndogo kwa wakazi waishio huko pamoja na umaskini uliokithiri katika eneo hilo kiasi kwamba kiongozi yeyote wa serikali akisema kitu watu wote wanafyata mkia.Tatizo lingine ni kuwa wale wanaharakati wachache wanaojitokeza wanaambiwa kuwa si raia wa Tanzania bali ni raia wa Kenya na hii inawafanya wengi warudishe nguvu nyuma na wengi wao hubaki kuumia kimyakimya.
Ushauri wangu kwa viongozi wa CHADEMA Taifa ni kuwa waende Wilaya zote hizi za Wamasai wamwage elimu ya uraia kwani elimu hiyo imekuwa haba sana maeneo hayo.Wakifanikiwa kwa hilo basi CCM wahesabu kukosa kura za makabila yote ya wafugaji kwani wasukuma walishaanza.
 
Jambo kubwa la kuangalia ni usalama wa makamanda maana tumeona Igunga mauaji maana ccm Wameona hiyo ndo njia ya kuwafanya waogope.
Mi nasema songeni mbele makamanda ukombozi u karibu.

Huu ni mwaka wa kukaba kila kona ya nchi hii,kila mzalendo wa kweli na anayejitambua anawajibu wa kutoa elimu ya uraia na uzalendo kila mahali alipo ili tuweze kuikomboa nchi yetu toka mikononi mwa manyang,au,mafisadi yaani ccm.muda huu si wakushangaa tena ni wakt wa kupambana kwelikweli.Mungu ibariki Tza,Mungu ibariki cdm
 
Ujumbe huu uwafikie wanachama na viongozi wa Chadema popote walipo. Loiliondo Tunahiatji ukombozi, sisi wananchi tumechoshwa na udhalimu unaofanywa na serikali ya CCM kupitia Halmashauri yake. Wilaya hii ndio wilaya ya pili katika kuchangia pato la taifa lkn ndiyo wilaya ya mwisho katika maendeleo. Wilaya hii ilianzishwa mwaka 1979 lkn mpaka leo hakuna maji yanayotoka ndani ya bomba, hakuna umeme, huduma mbovu za hospitali hata sehemu ya kuzikia mahiti ukifika waweza kutoa machozi.

Chadema karibuni loliondo tuwakomboe watz, majemedari waliopo huku hawatoshi kuimarisha nguvu japo mchango wao ni mkubwa katika kukitangaza chama, hv sasa katika nyumba nyingi za hapa loliondo zinapeperusha bendera ya Chadema na hii inatokana na ujio wa Mhe Mbowe mwaka jana watu walipata hamasa na wakahamasika mpaka kufikia hatua ya Dr. Slaa kuongoza kwa kura za uchaguzi mkuu katika vituo vya wasso na loliondo.

CHADEMA ni chama cha mjini hawezi kuja Loliondo kijijini.
 
Back
Top Bottom