CHADEMA: Tunasikitika kumkosa Maalim Seif, tulimtaka kweli!

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Chadema imesema ilitamani kumchukua aliyekuwa katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, lakini hawakufikia makubaliano, hata hivyo wameamua kushirikiana naye katika chama chake kipya cha ACT Wazalendo.

Maalim Seif alikuwa mmoja wa wanasiasa waliounga mkono kwa nguvu zote uamuzi wa vyama vinne vilivyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kumuunga mkono Edward Lowassa aliyeteuliwa na Chadema kugombea urais.

Msimamo wake ndio uliomfanya mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba kujivua uanachama, lakini akarejea takriban miezi nane baadaye akitaka arejeshewe madaraka, hali iliyoibua mgogoro ulioishia mahakamani na baadaye Maalim Seif na wafuasi wake kushindwa kesi na kuamua kujiondoa na kujiunga ACT Wazalendo ambayo haikuwamo Ukawa wala haikumuunga mkono Lowassa uchaguzi mkuu uliopita.

Siku moja baada ya Maalim Seif na wenzake kupokelewa ACT –Wazalendo, Chadema kimeweka bayana yaliyojiri kati yake na mwanasiasa huyo mkongwe nchini.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam, naibu katibu mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu amesema licha ya kumkosa Maalim Seif na kundi lake wataendelea kushirikiana naye kwa kuzingatia mkutano wa vyama vya upinzani uliofanyika Zanzibar Desemba 2018.

"Hakuna pigo, tulimtaka kweli. Viongozi wetu kwa hekima na busara waliona huyu mtu akija huku ni jambo jema na sisi tuliona tunusuru hadhi na heshima yake na mapambano ya demokrasia."

"Sasa kama amekwenda kwa mwenzio, ndugu yangu hajaolewa binti yako ameolewa binti wa baba mdogo, sasa si mulemule?"

"Kama ni tajiri utashindwa kwenda kuomba chakula? Maana una binti na mdogo wako ana binti, hajaolewa wako kaolewa wa ndugu yako, hayo si mule mule? Hutahudhuria sherehe?" amehoji.

Mwishoni mwa mwaka jana, Baraza la Wazee la Chadema lilitoa tamko la kumkaribisha Maalim Seif kwenye chama hicho wakati mgogoro wa CUF ukirindima.

Kuhusu nguvu ya Chadema Zanzibar, Mwalimu amesema chama hicho kitaendelea na programu zake, lakini hakitapambana na ACT-Wazalendo.

"Kuimarika kwa Chadema Zanzibar haimaanishi kukwamisha wale wanaoweza kusaidia mission ya mageuzi kule. Tunapambana ili tumsaidie yule na kumuimarisha yule mwenye nguvu. Kama itatokea na sisi tuna nguvu zaidi ni imani yetu watatokea wengine kuimarisha nguvu na si kutudhoofisha," amesema.

Alisema wataendelea na maazimio ya ushirikiano na vyama sita vilivyokutana Zanzibar mwaka jana.
 
Chadema imesononeshwa mno na kumkosa Maalim Seif.

Hiyo ni kauli ya Naibu Katibu mkuu wa Chadema Zanzibar Ndugu Mwalimu alipozungumza na vyombo vya Habari Jiji Dar es salaam.

Kauli hiyo ya Kiongozi wa ngazi ya juu wa Chadema inadhihilisha sasa kwamba ni kweli Chadema hawajafurahi hata kidogo kwa Act kuwazidi kete!

Ni suala la mda tu lakini mwisho wa uhusiano wa Vyama hivyo viwili utakuwa .....!
 
Wasome namba - Maalim Seif ni tycoon wa siasa za nchi hii - anafahamu kwa CDM ni chama kinachoenda kufa - sasa mwenye akili ataungana na CDM wakati huu kweli?
 
Wafitinishi kazini kama kawaida yao.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Alafu wanajaza nyuzi kuonekana kana kwamba wanafurahi yeye kwenda ACT,

Ukichunguza kwa Umakini CHADEMA wameumia sana, maana intentionally walitaka kuvimeza vyama vingine vyote,

Ndo maana nyuzi nyingi hapa za wana CHADEMA ni kujifariji kwamba wanaoumia ni CCM

Najiuliza hivi kwa akili ya kawaida kuna aliyetegemea Seif kwenda CCM?

Tuwe wakweli CHADEMA Waneumia,

Ila hata SEIF inabidi awe Makini na Kabwe maana kuna mbeleni Zitto kumpiga darizi Seif
 
Its senseless....porojoporojo tu unasema wew unawasingizia CHADEMA
 
Chadema imesononeshwa mno na kumkosa Maalim Seif.

Hiyo ni kauli ya Naibu Katibu mkuu wa Chadema Zanzibar Ndugu Mwalimu alipozungumza na vyombo vya Habari Jiji Dar es salaam.

Kauli hiyo ya Kiongozi wa ngazi ya juu wa Chadema inadhihilisha sasa kwamba ni kweli Chadema hawajafurahi hata kidogo kwa Act kuwazidi kete!

Ni suala la mda tu lakini mwisho wa uhusiano wa Vyama hivyo viwili utakuwa .....!
Wasome namba - Maalim Seif ni tycoon wa siasa za nchi hii - anafahamu kwa CDM ni chama kinachoenda kufa - sasa mwenye akili ataungana na CDM wakati huu kweli?
Wakati hausemi uongo mkuu - subiri uone yajayo
Bavicha wamekimbia uzi

Sent using Jamii Forums mobile app
Mataahira ya lumumba bwana....2020 mtataga na kuatamia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alafu wanajaza nyuzi kuonekana kana kwamba wanafurahi yeye kwenda ACT,

Ukichunguza kwa Umakini CHADEMA wameumia sana, maana intentionally walitaka kuvimeza vyama vingine vyote,

Ndo maana nyuzi nyingi hapa za wana CHADEMA ni kujifariji kwamba wanaoumia ni CCM

Najiuliza hivi kwa akili ya kawaida kuna aliyetegemea Seif kwenda CCM?

Tuwe wakweli CHADEMA Waneumia,

Ila hata SEIF inabidi awe Makini na Kabwe maana kuna mbeleni Zitto kumpiga darizi Seif
Hoja zako ni za witch doctor....unapiga ramli eti wew mchaw wa lumumba unajua watu wanawaza nn.Taifa linadumaa kwakua na vijana wenye mindset za kishirikina.
 
Kama hujui walio mshauri Maalimu kwenda ACT ni Chadema. Kwani jambo hilo litatanua wigo wa upinzani na kuwa na nyama viwili nyenye nguvu Tz bara. Hongerà chadema kwa wazo jema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maalim amekua kwenye siasa za nchi hii kwa miongo kadhaa sidhani kama kuna Jipya toka kwake.
 
Back
Top Bottom