CHADEMA tunaomba mrushe Live wakati wa kupiga kura na kuhesabu za wagombea uraisi tuone demokrasia inavyafanya kazi

Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
9,356
2,000
Kukodi air time kwenye TV Ni gharama kubwa . Tunaomba chadema tuonyesheni tu live kipande kile Cha kupiga kura na kuhesabu tu mengine mwaweza acha kupunguza gharama
Sisi wanyonge wa ccm tuliomba mchapishe form 2 za urais kupitia ccm walau na Membe apate moja mkadai mashine ya kuprint imeharibika. Bure kabisa wanalumumba
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
24,829
2,000
Hivi mnapidhibiti vyombo vya habari, dola na vya maamuzi inawasaidia kukubalika miongoni mwa jamii ?!. Ukipata ushindi ktk mazingira hayo unapata wapi ushujaa wa kuwananga wapinzani wako ?!.
Kalipieni pesa media mtangazwe acheni uongo ohh Media zimedhibitiwa wao wanataka pesa tu

Ukisema pesa Ndio imewadhibiti Ni kweli sababu huhitaji walipwe wakutangaze ndio kazi yao wao sio NGO ya kujitolea bure. Lipeni pesa mtangazwe
 
Odhiambo cairo

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
13,010
2,000
Kalipieni pesa media mtangazwe acheni uongo ohh Media zimedhibitiwa wao wanataka pesa tu

Ukisema pesa Ndio imewadhibiti Ni kweli sababu huhitaji walipwe wakutangaze ndio kazi yao wao sio NGO ya kujitolea bure. Lipeni pesa mtangazwe
Yehodaya , kumbuka 2015 angalau ITV walikuwa fair kidogo tu. Ni nini kilichowakuta?! Mzee Mengi na Spencer Lameck waliishia kushambuliwa mawe, viatu pale Lumumba mpaka walipookolewa na gari la waziri Membe. Zaidi wakapigwa faini za kutosha na kutishiwa kufungiwa.

Leo unajifanya kipofu? Mtu wako hawezi ushindani
 
ndammu

JF-Expert Member
Apr 21, 2017
1,854
2,000
Kalipieni pesa media mtangazwe acheni uongo ohh Media zimedhibitiwa wao wanataka pesa tu

Ukisema pesa Ndio imewadhibiti Ni kweli sababu huhitaji walipwe wakutangaze ndio kazi yao wao sio NGO ya kujitolea bure.Lipeni pesa mtangazwe
Huku hakuna shida je mtaweza kuruhusu uchaguzi angalia matokeo ya Urais yahesabiwe vituoni maajibu yapatikane hapohapo?
 
stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
21,477
2,000
Hawataweza,

Hawataki aibu iwakumbe Hawa ndugu

Watakataa eti Mwaka 2005 Mbowe hakupata kura laki sita tu Nchi nzima.
 
owomkyalo

JF-Expert Member
Dec 26, 2017
4,195
2,000
Kukodi air time kwenye TV Ni gharama kubwa . Tunaomba chadema tuonyesheni tu live kipande kile Cha kupiga kura na kuhesabu tu mengine mwaweza acha kupunguza gharama

Sio vizuri kuingilia mambo ya chadema ayakuhusu wewe mataga.
 
Mr Tyang

JF-Expert Member
Sep 30, 2018
957
1,000
Mkuu unaiomba chadema ipi ifanye huo mchakato?

Kama ndo chadema hii ya kupitisha Wagombea wa ubunge kwa kura za ndio au hapana Kama uchaguzi wa viongozi wa TANU utasubiri Sana.
 
lee van cliff

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
2,860
2,000
Kukodi air time kwenye TV Ni gharama kubwa . Tunaomba chadema tuonyesheni tu live kipande kile Cha kupiga kura na kuhesabu tu mengine mwaweza acha kupunguza gharama
Unadhani kuna mtu anaweza kumshinda Lisu kwa nafasi hiyo ndani ya CHADEMA? Labda kama mmepandikiza wajumbe wenu.
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
19,804
2,000
Kukodi air time kwenye TV Ni gharama kubwa . Tunaomba chadema tuonyesheni tu live kipande kile Cha kupiga kura na kuhesabu tu mengine mwaweza acha kupunguza gharama
Ondoa gharama; jiulize ni TV gani isiyojipenda Tanzania irushe live mkutano wa CHADEMA. Hadi vitambaa (Bendera) hawataki kuziona kwenye eneo la Ukumbi wa mkutano.

Hapa ndipo tulipofikia watanzania
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom