Chadema tunaomba DVD's na VCD's za uzinduzi wa Kampeni

Domhome

JF-Expert Member
Jun 28, 2010
3,197
3,930
Naamini ya kuwa siku ya leo itaingia kwenye historia ya nchi hii. Hivyo basi, ni vyema Chadema mkazalisha DVD's na VCD's au pengine VHS nyingi sana za uzinduzi wa kampeni hapo Dar (Jangwani) ili ziweze kuuzwa nchi nzima kwa malengo yafuatayo:
  • Matangazo yenu ya moja kwa moja yanahujumiwa na TBC TV na kwahili najua watadai ni hitilafu za mitambo, na baadaye wata-edit hotuba na waturushie ili kujinafikisha.
  • Mauzo ya kanda/tepu hizo yatauzwa nchi nzima ili kuwa chanzo cha mapato, tena itakuwa ni vyema mkawa mnatembea nazo wakati wa kampeni na kuziuza.
Nimuhimu kufanya hivyo kwasababu leo ndo mwanzo wa ukombozi kwa Mtanzania. Naomba pia hebu jaribuni kuweka kipindi maalumu Chanel ten baada ya uzinduzi wenu ili watanzania wote waweze kujionea mwanzo-mwisho wa uzinduzi wenu.

Binafsi nitakuwa mmoja wa wanunuzi wa kubwa wa tape hizo!!!!!!! Wakati wa Ukombozi ni Sasa:clap2:
 
Yah on a serious note kuna haja ya kutengeneza ivyo vitu,makatizo ya TBC tumechoka nayo
 
Back
Top Bottom