CHADEMA tunalaani Sheikh Ponda kukamatwa, Kwanza Tv kufungiwa na kukamatwa viongozi wake; NI HOFU UCHAGUZI MKUU

CHADEMA

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
488
2,468
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimepokea kwa tahadhari kubwa na kinafuatilia kwa karibu mwendelezo wa vitendo vya Serikali kuendelea kudhibiti uhuru wa maoni, kutisha vyombo vya habari, huku vyombo vya dola vikitumika vibaya kuvunja sheria kwa kuzuia Viongozi na Wanachama wa Chadema kutekeleza haki na wajibu wao wa kisiasa kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Nchi, wakati huu ambapo nchi inajiandaa kwa Uchaguzi Mkuu.

Tukio la hivi karibuni zaidi ni kukamatwa na kushikiliwa kinyume cha taratibu za kisheria, Katibu wa Shura ya Maimamu, Sheikh Ponda Issa Ponda kwa tuhuma ambazo Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limedai ni uchochezi kupitia Waraka wa Shura ya Maimamu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, mwaka huu.

Hatua ya jeshi hilo kumkamata Sheikh Issa Ponda, imekuja muda mfupi baada ya Jeshi la Polisi mkoani Singida kuwakamata na kuwashikilia kinyume cha sheria na hatimae kuwafikisha mahakamani Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha), Nusrat Hanje, Mhamasishaji wa Bavicha Taifa, Twaha Mwaipaya na viongozi wengine 5 wa Chadema Jimbo la Singida Magharibi, wakituhumiwa kwa makosa ya kubambikiwa baada ya kukamatwa wakiwa barabarani wakitoka kwenye shughuli halali za kisiasa kwa mujibu wa taratibu za kisheria za nchi yetu.

Kabla ya hapo, jeshi hilo lilikuwa limemkamata na kumshikilia chini ya ulinzi, kinyume cha taratibu za nchi, mwanachama wa Chadema, Daniel Shillah, wakionekana kutekeleza amri iliyotolewa na kiongozi wa kisiasa Mkoa wa Morogoro.

Katika muktadha huo huo wa kuidhibiti Chadema, viongozi na wanachama wake katika wakati huu wa maandalizi ya Uchaguzi Mkuu, Jeshi la Polisi katika mikoa ya Mara na Shinyanga, liliingilia na kuharibu shughuli za mchakato wa urejeshaji wa fomu kwa watia nia wa ndani ya Chama, ambapo lilimzuia kwa muda Bi. Catherine Ruge alipokuwa anarudisha fomu zake Ofisi za Chadema Jimbo la Serengeti huku pia likimkamata kwa mahojiano Bi. Salome Makamba aliporejesha fomu zake Ofisi za Chadema Jimbo la Shinyanga mjini.

Wakati Serikali kupitia vyombo vya dola ikiendelea kutisha wanaotoa mawazo mbadala kuhusu hali ya kisiasa nchini, wakiwemo viongozi wa dini na wanasiasa hasa wa Chadema, kwa kuwakamata na kuwabambikia kesi, upande mwingine kupitia Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) imeendelea kudhibiti na kuminya uhuru wa vyombo vya habari nchini kwa kuviadhibu kwa kuvitoza fedha kuvifungia kwa muda mrefu kwa madai ya kukiuka Kanuni za Maudhui ya Mtandaoni za Mwaka 2018.

Tukio la karibuni zaidi ni kufungiwa kwa Televisheni ya Kwanza Tv (Online Tv) kwa muda wa miezi 11 na kutozwa faini ya jumla ya Tsh. Mil. 28 kwa vyombo vya habari vya Clouds FM (5mil.), Duma Tv (7mil.), East Africa Radio (3ml), Global Tv (7mil.), Sibuka Tv (3mil.) na Star Tv (5mil.).

Hatua ya TCRA ilifuata, siku chache baada ya Serikali kupitia Habari Maelezo, kulifutia leseni Gazeti la Tanzania Daima.

Katika hali hiyo, Chadema kinasema yafuatayo;

1. Tunalaani na kupinga vikali mwendelezo wa vitendo vya Serikali ya CCM, kupitia Vyombo vya Dola, hususan Jeshi la Polisi, kukamata na kuwashikilia watu mbalimbali, wakiwemo viongozi wa dini, viongozi wa Asasi za Kiraia (AZAKI), Wanaharakati, Wanasiasa na wananchi wa kawaida mmoja mmoja , kwa sababu tu ya kutoa maoni mbadala ambayo hayaendani na fikra za viongozi wa chama hicho walioko madarakani. Mwenendo huo si tu kwamba unavunja haki na uhuru unaotolewa na Katiba na Sheria za nchi, bali pia unadhihiridha kuwa chama hicho na viongozi wake, wana HOFU KUBWA kuhusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

2. Tunalaani na kupinga vikali kitendo cha Jeshi la Polisi kumkamata na kumshikilia kinyume cha taratibu Sheikh Ponda Issa Ponda. Tunalitaka jeshi hilo limwachie kwa dhamana au limfikishe mahakamani mara moja kwa mujibu wa sheria za nchi yetu.

3. Tunalaani na kupinga vikali vitendo vya jeshi hilo kuwakamata, kuwashikilia kinyume cha sheria, kusababisha usumbufu na kuvuruga shughuli za halali za kisiasa zinazofanywa na Chadema, viongozi au wanachama wake, wakati huu ambapo nchi inajiandaa kwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.

4. Tunalaani na kupinga vikali TCRA kutekeleza majukumu yake katika namna ambayo inalenga kutishia na kuminya uhuru wa habari nchini na hasa kuvinyamazisha vyombo hivyo visitimize majukumu yake kwa uhuru wakati huu wa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, mwaka huu. Adhabu zinazotolewa na TCRA, kama ilivyokuwa kwa Habari Maelezo, zote zinaibua maswali mengi, ikiwemo kwanini Serikali inaendelea kujipachika mamlaka yaliyo kinyume cha misingi ya utoaji haki, kwa kujigeuza mlalamikaji, polisi, mwendesha mashtaka na hakimu kwa suala/masuala yanayoihusu. Jambo hili halikubaliki na linastahili kuachwa mara moja.

5. Mahsusi katika suala la adhabu zilizotolewa na Habari Maelezo na TCRA dhidi ya vyombo vya habari mbalimbali, tunatoa wito kwa vyombo vya kitaaluma vya tasnia ya habari nchini, ikiwemo MCT (Baraza la Habari Tanzania), MISA-TAN na TEF (Jukwaa la Wahariri Tanzania), vifanye tathmini ya kina, kwa kupima ukubwa wa adhabu hizo dhidi ya makosa au maadili yanayodaiwa kukiukwa, kisha watoe taarifa ya kitaaluma iwapo maamuzi hayo ni sahihi au si sahihi.

6. Chama tayari kimewaelekeza wanasheria wake kuchukua hatua za kisheria ili kufungua shauri Mahakama Kuu, kuhusu uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida kuwanyima dhamana washtakiwa Nusrate Hanje, Twaha Mwaipaya na viongozi wengine wa Chadema 5, katika namna ambayo inastahili kuhojiwa na kutiliwa shaka, baada ya upande wa Serikali kuweka pingamizi dhidi ya dhamana yao, ambayo ilikuwa wazi kwa mujibu taratibu za kisheria.

Hitimisho

Mwenendo huu wa Serikali kuendelea kutumia vyombo vyake na mamlaka yake vibaya, katika namna ambayo inahusisha ukiukwaji wa Katiba, Sheria na misingi ya haki (inayoonekana ikitendeka), hasa wakati huu ambapo wadau mbalimbali wako kwenye maandalizi ya kushiriki Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba, unastahili kupingwa na kulaaniwa na kila Mtanzania mzalendo.

Ni mwenendo unaolenga kuminya na hata kuzima sauti kabisa sauti mbadala katika jamii dhidi ya hali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii inayoendelea nchini kuelekea Uchaguzi Mkuu. Hali hiyo ikiachiwa bila kuhojiwa, kukemewa na kupingwa vikali ili isiendelee, athari zake ni kubwa na zitaiweka nchi katika mkwamo mkubwa zaidi na kushindwa kupiga hatua sahihi za demokrasia na maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Imetolewa leo, Jumapili, Julai 12, 2020 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano

Chadema
 
Nilifikiri uzi niliousoma zamani sana humu, yaani miaka mingi, tele tele iliyopita.

Kumbe ni chadrama kukosa hoja!!!!.. wanatiana huruma hao, bora wamejitambua kwamba hawawezi kushinda. Mwaka huu kwasababu hawajajua kuwa wapinzani.

💚💛💚💛💚💛💚💥💥💥
 
Tamko limejitosheleza kuwatetea waTanzania wote bila kujali imani ya kidini, kundi gani liwe la wakulima, waalimu, wanasiasa n.k

Na Ndivyo inavyotakiwa waTanzania tuwe watetezi wa wote wanaoonewa bila kujali tofauti zetu. Kubwa ni kudai kufaidi bila ubaguzi Haki, Maendeleo, Demokrasia, kuwa Mtu-Huru na Furaha ya kuishi kama Mtanzania ndani ya Tanzania.

More :

13 Julai 2020

This is really bad. Yaani Mwaka huu ni wa kushuhudia “ibada” za CCM pekee kwenye media zote.

Kwa miaka mingi nilikuwa nikihangaika kuelewa kilichojiri kuwafanya Wajerumani, taifa la watu makini sana kielimu, kitaaluma na kinidhamu, wamkabidhi Hitler uongozi na kumuachia abadili katiba kidogo kidogo hadi kuwa na madaraka yasiyodhibitika! Mtu aliyekuja kujidhihirisha kuwa na hulka ya udikteta na ukatili wa kinyama sana kwa binadamu wenzake. Mtu aliyeliingiza taifa lake kwenye vita kuu ya maangamizi.

Baada ya kusoma vitabu na machapisho kadhaa ya watafiti wa ujerumani ya karne iliyopita na ujio wa Hitler, nimesikitika mfanano na hali zetu. Jamaa aliingia na gia kubwa ya kurejesha “ukuu” wa Ujerumani iliyokuwa imedhibitiwa na mataifa mengine baada ya kushindwa Vita ya Kuu ya Kwanza. Pia aliahidi kuwang’oa mabeberu/mafisadi (Wayahudi) waliokuwa wakidhibiti uchumi nchini na duniani na kusafisha taifa la Ujerumani liwe na “watu bora” tu.

Ingawa tunatofautiana viwango, naona mianya inaachiwa katiba ichezewe kwa kisingizio cha kudhibiti “wapiga dili”, “mabeberu na vibaraka wao”, “kutekeleza miradi ya kimkakati”, na “kurejesha ukuu wa Tanzania (MATAGA)”. Ukisikiliza ibada na mapambio ya sifa yanayovuma kwenye media siku hizi, unabakia kujiuliza kama hatuelekei kwenye kuimarisha utawala wa kidikteta usiokuwa na chembe ya utu. Na mtu awaye yeyote asijidanganye kuwa yupo kwenye “chama sahihi”. Hakuna guarantee popote. Wakati wa Hitler kuna Wajerumani waliosota kwenye makambi ya maangamizi (concentration camps) yaliyolenga hasa Wayahudi”.
 
Mkuu nchi imeshashikwa na magaidi. Twafaa!
 
Kuna tofauti mkuu.

Hitler alikuwa 'sophisticated' na alikuwa na mvuto mkali sana kwa watu wake. Huyu wa hapa ni 'crude', anachojua ni mabavu tuu kwa kila analofanya.

Kwa bahati mbaya, matokeo yake kwa hao wawili pamoja na tofauti zao ni yale yale.

Nina hofu sana na huyu wa hapa, huenda hali itakuja kuwa mbaya sana kwa jinsi anavyolipelekesha taifa.
 
Mungu mbariki Sheikh Ponda
Naomba msaada rafiki.

Hivi haya "Matamko" yanapotolewa, kama hili la leo, huwa yanaelekezwa wapi? Nani hupewa haya matamko?

Kuna sehemu yoyote nchini, mbali ya ofisi kuu ya CHADEMA yanapopelekwa haya matamko, kwa mfano kwenye kofisi za kanda...., hadi kwenye mashina ambako wananchi hupata fursa ya kupata taarifa zake?

Hili litakuwa somo zuri sana kwangu, mkuu wangu Erythrocyte kama utakubali kunifundisha, na hata pengine wengine ndani ya jukwaa hili la siasa.

Karibu sana.
 
CHADEMA mnasikitisha sana kwa kudakia mambo

Shehe Ponda na taasisi yake (Shura ya Maimamu) ni wakupigwa vita
 
Huu ni utoto

Yaani unasemaje wanakamatwa kinyume na sheria?

Kama wamekamatwa kinyume na sheria kwanini unasema wapelekwe mahakamani?

Kwani unamtetea Ponda kwa lipi,hujui tulipitisha hapa sheria ya takwimu?

Mimi natamani watu wa aina ile hata wafe tu.

Ni Mimi
Stesheni
 
Simple logic:
Anaye mtetea Shehe Ponda na (Shura ya Maimamu kwa ujumla) maana yake pia naye anaunga mkono Uamsho na vurugu za Zanzibar, mauaji ya Kibiti, Mkuranga, Rufiji, na nk.
 
Back
Top Bottom