CHADEMA Tumpe uenyekiti Prof Safari Na ukatibu mkuu apewe Mh John Mnyika.

Mbundumale

Senior Member
Dec 30, 2013
150
0
Kheri ya mwaka mpya mwaka 2014.

Ninaomba kupendekeza safu mpya ya viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika uchaguzi mkuu ndani ya Chama.

Napendekeza wafuatao na nyadhifa zao

1/PROFESSOR SAFARI-Napendekeza Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimchague kwa kura za kutosha Prof Safari kuwa mwenyekiti wa CHADEMA taifa.

Hii,itasaidia propaganda ya ccm na washirika wake kwamba ni chama cha wakristo itakufa kifo cha mende. Hii pia itasaidia kuua hoja ya ccm na washirika wake kwamba CHADEMA inaongozwa na mwenyekiti mwenye elimu ndogo na hivyo wanakopa usemi wa mh Msigwa kwamba akili ndogo kuongoza akili ndogo.

2/JOHN MNYIKA-Huyu ni kijana machachari, mwepesi na flexible sana. Mara zote amekuwa mwenye hoja nzito, mpanguaji wa propaganda za ccm,anayeweza kufafanua mambo kwa weledi. Pia ni kijana aliye na social capital kwa vijana, wazee,wanawake na watoto. Binafsi nimemshuhudia Mnyika akilala sakafuni na wanafunzi wa Chaso katika usiku wa kuamkia kupiga kura uchaguzi mdogo wa madiwani mwezi juni 2013 kata ya mianzini jijini Dar es salaam.

3/MARRY MSABAHA-Huyu ni mbunge wa viti maalumu kutoka Zanzibar.Napendekeza huyu apewe unaibu katibu mkuu .Hii itasaidia kuua propaganda tatu za maccm. 1/Ukanda, 2/udini na 3/ubara,4/gender balance. Huyu dada ni machachari kweli kweli na ana uwezo mkubwa wa kujenga hoja na kuzipangua.

4/PHILIPO MWAKIBINGA-Ni kijana mwenye maono na uwezo mkubwa wa kufikiri, mwenye ushawishi mkubwa, ujasiri na utayari wa kujitolea. Ni kijana mwenye kupenda wapate wengine yeye akose na hilo nilithibitisha akiwa rais wa Udom kupigania wanafunzi wenzake wapate mafunzo kwa vitendo na fedha za field wakati yeye hakuwa na mkopo na hivyo asingepata pesa hizo. Napendekeza apewe uenyekiti wa BAVICHA taifa. Hii itaua propaganda ya ukanda kwani MWAKIBINGA anatokea Nyanda za juu kusini jimbo la lupa wilaya ya Chunya.

5/ZAINABU MUDHIHIRI ASHIRAF-Huyu ni dada mchapakazi mahiri sana na ameonesha uwezo mkubwa kwa chama. Amekuwa mwanzilishi wa Chaso TIA-Mbeya mjini, amemnadi mgombea wa Udiwani huko Tanga kwa weledi mkubwa sana na pia anafanya vizuri sana makao makuu na sasa yuko katika utekelezaji wa CHADEMA ni msingi. Napendekeza apewe umakamu mwenyekiti BAVICHA taifa.Hii itasaidia kuuawa propaganda ya udini na mfume dume.

6/BEN WA SAA NANE-Huyu ni kijana mwenye uwezo mkubwa katika teknolojia ya habari na pia ni msomi mzuri katika diplomasia na ushirikiano wa kimataifa. Napendekeza apewe ukatibu wa BAVICHA taifa.Nashauri hivi kwa kuwa Ben saa 8 Sio msemaji sana jukwaani bali mtendaji zaidi.

8/DK SLAA-Huyu ana siri nyingi sana za chama na serikali, ana busara, uwezo mkubwa wa kufikiri nk.Napendekeza apewe uenyekiti wa Baraza la Wazee taifa.

Nafasi nyingine nitashauri siku nyingine .

Zingatia ,haya ni mawazo ama maoni yangu binafsi .Pia hao niliowataja wagombee na Demokrasia ichukue nafasi yake.Ninamaana wachaguliwe kidemokrasia na si kuteuliwa.

************* Nawasilisha ***************
 
aminangalo

JF-Expert Member
Aug 31, 2013
974
0
Hanasifa dini yake na kabila analotoka

MNyika nimfuasi wa Zitto kwa siri nyendo zake tunafuatilia
 
Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,414
2,000
Umekubali ila kwa sasa uko na CHADEMA NI MSINGI kwanza ..unaionaje?
 
OSOKONI

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
10,973
2,000
Tusubiri muda ufike wanachama kidemokrasia kabisa tutaamua nani aongeze CHADEMA, kwa sasa kazi kubwa mbele yetu ni kujiandaa vilivo kwa mambo matatu 1. Kupata katiba safi (kumbuka hii ni agenda yetu CCM waliparamia tuu) 2. Uchaguzi wa serikali za mitaa 3. Uchaguzi mkuu 2015,, Hizo ndio agenda za ku adress kwa sasa swala la kutaja majina hilo lije pale uchaguzi ndani ya chama ukitangazwa!
 
tofyo

JF-Expert Member
Jul 18, 2013
2,690
2,000
hicho kiti kimesha fisha watu. Kama unataka kufa gusa hicho kiti.
 
MALUNGU

JF-Expert Member
Jun 2, 2011
250
0
Ni mawazo mazuri ila muda si mwafaka wa kuwa na timu hii kwa sasa, itakuwa timu imara sana kunzia baada ya uchaguzi mkuu hasa nafasi ya Mwenyekiti na Katibu mkuu taifa ila nafasi zingine mawazo yako yafanyiwe kazi.
 
Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
26,553
2,000
Kheri ya mwaka mpya mwaka 2014.

Ninaomba kupendekeza safu mpya ya viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika uchaguzi mkuu ndani ya Chama.

Napendekeza wafuatao na nyadhifa zao

1/PROFESSOR SAFARI-Napendekeza Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimchague kwa kura za kutosha Prof Safari kuwa mwenyekiti wa CHADEMA taifa.

Hii,itasaidia propaganda ya ccm na washirika wake kwamba ni chama cha wakristo itakufa kifo cha mende. Hii pia itasaidia kuua hoja ya ccm na washirika wake kwamba CHADEMA inaongozwa na mwenyekiti mwenye elimu ndogo na hivyo wanakopa usemi wa mh Msigwa kwamba akili ndogo kuongoza akili ndogo.

2/JOHN MNYIKA-Huyu ni kijana machachari, mwepesi na flexible sana. Mara zote amekuwa mwenye hoja nzito, mpanguaji wa propaganda za ccm,anayeweza kufafanua mambo kwa weledi. Pia ni kijana aliye na social capital kwa vijana, wazee,wanawake na watoto. Binafsi nimemshuhudia Mnyika akilala sakafuni na wanafunzi wa Chaso katika usiku wa kuamkia kupiga kura uchaguzi mdogo wa madiwani mwezi juni 2013 kata ya mianzini jijini Dar es salaam.

3/MARRY MSABAHA-Huyu ni mbunge wa viti maalumu kutoka Zanzibar.Napendekeza huyu apewe unaibu katibu mkuu .Hii itasaidia kuua propaganda tatu za maccm. 1/Ukanda, 2/udini na 3/ubara,4/gender balance. Huyu dada ni machachari kweli kweli na ana uwezo mkubwa wa kujenga hoja na kuzipangua.

4/PHILIPO MWAKIBINGA-Ni kijana mwenye maono na uwezo mkubwa wa kufikiri, mwenye ushawishi mkubwa, ujasiri na utayari wa kujitolea. Ni kijana mwenye kupenda wapate wengine yeye akose na hilo nilithibitisha akiwa rais wa Udom kupigania wanafunzi wenzake wapate mafunzo kwa vitendo na fedha za field wakati yeye hakuwa na mkopo na hivyo asingepata pesa hizo. Napendekeza apewe uenyekiti wa BAVICHA taifa. Hii itaua propaganda ya ukanda kwani MWAKIBINGA anatokea Nyanda za juu kusini jimbo la lupa wilaya ya Chunya.

5/ZAINABU MUDHIHIRI ASHIRAF-Huyu ni dada mchapakazi mahiri sana na ameonesha uwezo mkubwa kwa chama. Amekuwa mwanzilishi wa Chaso TIA-Mbeya mjini, amemnadi mgombea wa Udiwani huko Tanga kwa weledi mkubwa sana na pia anafanya vizuri sana makao makuu na sasa yuko katika utekelezaji wa CHADEMA ni msingi. Napendekeza apewe umakamu mwenyekiti BAVICHA taifa.Hii itasaidia kuuawa propaganda ya udini na mfume dume.

6/BEN WA SAA NANE-Huyu ni kijana mwenye uwezo mkubwa katika teknolojia ya habari na pia ni msomi mzuri katika diplomasia na ushirikiano wa kimataifa. Napendekeza apewe ukatibu wa BAVICHA taifa.Nashauri hivi kwa kuwa Ben saa 8 Sio msemaji sana jukwaani bali mtendaji zaidi.

8/DK SLAA-Huyu ana siri nyingi sana za chama na serikali, ana busara, uwezo mkubwa wa kufikiri nk.Napendekeza apewe uenyekiti wa Baraza la Wazee taifa.

Nafasi nyingine nitashauri siku nyingine .

Zingatia ,haya ni mawazo ama maoni yangu binafsi .Pia hao niliowataja wagombee na Demokrasia ichukue nafasi yake.Ninamaana wachaguliwe kidemokrasia na si kuteuliwa.

************* Nawasilisha ***************

Sio timu mbaya,
But muda ukifika!!
 
Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
42,309
2,000
Mwenye chama Mbowe umemtosa pamoja na kijana wake Lema.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom