CHADEMA tumieni busara

kamtesh

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
1,395
512
Chama sio mwenyekiti wachama. Mwenyekiti ni mtendaji aliepewa mamlaka na wanachama kuiongoza chama kwa hekima na busara.

Hekima na busara vikikosekana, chama kinapoteza dira na mapenzi toka kwa wafwasi wake. Licha ya watanzania kutamani chama kingine kuongoza dora, ila sio kwa mfumo huu unaojitokeza hivi karibuni was Fukuza fukuza. Wazee wachadema, waongozeni vijana wenu kwenye chama hicho, kinapotea njia.

Ifike mahali pawe sababu za msingi kabisa za kumfukuza mwanachama mkongwe ndani ya chama. Na chama kijiridhishe, kwamba manufaa ya hatua hiyo ya kumfukuza nimakubwa kuliko hasara zake.

Ni mwaka wauchaguzi, Chadema munahitaji wanachama wengi zaidi.

Vitabià vya mwenyekiti kila Leo kukuruuka na maazimio, au misimamo yake binasfi na kuitengenezea njia kua mismamo ya chama, viachwe. Mwenyekiti asiwe mungu mtu. Demokrasia iko wapi? Uhuru waku kukubaliana au kusokubaliana nawe, isiwe adhabu kwa wale wanao pinga. Chadema kiwe mfano wa hiyo demokrasia. Charity begins at Home.

Tusiwalaghai wa Tanzania kwa demokrasia feki munayo hubiri. Msemo wa 'Kiongozi akikaa sana madarakani, anageuka dictator.' Ndo ya chadema! Hakuna wakumpinga mwenyekiti, yeye ni nani asipingwe?

Sasa ninaanza kuwa na mashaka na uwezo wa wambuge wa Chadema na wanachama wake, pasipo kukemea tabia za mwenyekiti wao.

Swala la korona ni la mtu binafsi, akiugua ni yeye na akifa ni yeye na akipona ni yeye. Wangapi wamepona jameni? Musilazimisha vitu vingine nakufikia kufukuzana kwenye chama, kisa korona. Kwani wa CCM hawaoni korona. Leo hii nchi zote zinaanza kufungua milango tens baada yakuona lockdown inaumiza watu.

My take, futeni maamuzi yakufukuza wambunge, fwateni taratibu za kinadhamu zinazo faa kwa afya a chama chenu.
 
Ume andika nini sa na wewe
clementsanga-20200512-0001.jpg


sijui itakuaje
 
Klia kitu kina taratibu zake na sheria na vile vile ukikiuka kuna adhabu yake acha wasimamie sheria n funzo kwa watu wengne pale sio sehemu kila mtu anajiamulia cha kufanya
 
Klia kitu kina taratibu zake na sheria na vile vile ukikiuka kuna adhabu yake acha wasimamie sheria n funzo kwa watu wengne pale sio sehemu kila mtu anajiamulia cha kufanya
Ni sawa Kuna taratibu lakini inatia Shaka Sana Kama kweli lockdown kwa wabunge wa chadema ilikuwa ni makubaliano ya wabunge wote kwenye kikao rasmi na kilichokuwa na uhuru wa kutoa maoni.
 
Chama ni msimamo kama wanataka Chama legelege waende CCM na jumuia zake za Nccr na Tlp
 
Back
Top Bottom