Chadema tumia mbinu mbadala, Arumeru East itakuwa msiba mkubwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema tumia mbinu mbadala, Arumeru East itakuwa msiba mkubwa!

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Lilombe, Mar 21, 2012.

 1. L

  Lilombe JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kampeni zikiwa zimepamba moto, CDM inaelekea kuendekeza siasa za maji taka za CCM:-

  CCM ikitumia mbinu na siasa CHAFU kupitia Mkapa, Mwigulu na Wasira wamesikika wakitoa maneno nje na sera zao;

  1. Vincent Nyerere siyo mwanaukoo wa Baba wa Taifa
  2.Dr. Slaa ni mchafu; kaiba mke wa watu, kafisadi michango ya ujio wa papa, katimuliwa upadre
  3.CDM kimeishiwa mapesa ya kampeni; kwa vile Serikali ya JK imekata bomba la misaada toka Conservative kwa kuwakatalia KUHARARISHA NDOA ZA JINSIA MOJA

  Inashangaza magwiji wa siasa ndani ya CDM imewaruhusu akina Vincent Nyerere, Msigwa, Mr. 2, na Dr. Slaa kuacha kupigia debe sera nzuri za CDM, BADALA YAKE wameingia kwenye mtego wa kujibu mipasho ya akina Wasira badala ya kuwaambia wananchi wa Arumeru East namna watavyowakomboa kutoka katika lundo la matatizo yalitokana na sera mbovu za CCM.

  Huu ni wakati muafaka akina Dr. Mkumbo na Profesa Baregu kufanya kazi za ziada kubadilisha mfumo wa kampeni ndani ya CDM ili ionekane ni chama kinajikita na namna ya kutatua kero za wananchi.
   
 2. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,703
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  unajua kama cdm watakuwa wananyamazia kizembe propaganda za ccm wananchi wanaweza wakadhan ni kwel koz ccm wana2mia ujinga wa wa2 kuombea kura.
   
 3. KirilOriginal

  KirilOriginal JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 1,920
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Nakubaliana na hoja zote ila watu wengi inabidi uwakanushie au uwatafsirie maneno ndipo uwaombe kura
   
 4. Freeland

  Freeland JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 14,468
  Likes Received: 6,761
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  CDM wanatumia mda mfupi sana kukanusha hizo siasa Chafu,mda mwingi wanatumia kwenye sera.CCM ndio wanatumia muda mwingi kuchafua CDM.Afteral hiyo ndo politics mkuu.Ni mchezo wa Timing
   
 5. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  cdm inauvaa mkenge wa mwigulu... Thenwananchi wataona ni haohao tu
   
 6. M

  Molemo JF-Expert Member

  #6
  Mar 21, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Huwezi ukaacha uongo uenee bila kuujibu.
  Kwa mfano Wassira alisema wazazi wa Nassari walimzuia kugombea Ubunge.Sasa kama asingekanusha na wazazi wake kupanda jukwaani si wananchi wangeamini huo uongo?
  Mkuu lazima ujue kwamba propaganda chafu kwenye majukwaa ya kisiasa ni lazima zijibiwe vilivyo.
  Mkuu nadhani huelewi siasa na kampeni ni nini? Ama ushauri wako unatoa kwa nia mbaya.
   
 7. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #7
  Mar 21, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  kwa wajinga sawa ila kwa anejuwa ataelewa.....hata hao ccm hawasemi wamefanya nini tangu uhuru zaidi ya kuuza mashamba kwa wazungu
   
 8. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #8
  Mar 21, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Propaganda hujibiwa kwanza ili wananchi waelewe then ndo unamwaga sera, ukinyamaza bas hata point zako zitapuuzwa wakijua kweli mchafu. Piga mabomu ya ukwel watanyamaza wenyewe, MUULIZEN YUSUF MAKAMBA YALIYOMPATA AKIWA MKUU WA MKOA KWE2 KIGOMA NA KILICHOMFANYA AACHE UALIMU, CHADEMA 4 LYF BWANA!!
   
 9. E

  Edwin Mtei JF Gold Member

  #9
  Mar 21, 2012
  Joined: Dec 13, 2008
  Messages: 181
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Pamoja na viongozi wa Chadema kujibu uzushi na taarifa za uongo zilizopikwa na Wassira akiongozwa na Mkapa, nashauri tuendelee na kusisitiza sera zetu zinazojali adha na matatizo ya wanyonge. Lazima tuendelee kupiga vita rushwa na uporaji wa mali ya umma ambavyo vinasababisha Serikali ya CCM kushindwa kutekeleza malengo yake.

  Ni sera kama za CDM zitaweza kuondoa mfumko wa bei ambao unafanya kila mwananchi ashindwe kumudu gharama za maisha. Mafisadi waliokwapua fedha za EPA wanaziingiza hizi fedha za dezo ktk uchumi sasa na kushindana na wavuja jasho. Hii ndio sababu moja wapo ya mfumuko wa bei Tanzania.

  Ni aibu kwa ex-Rais aliyegeuza Ikulu kuwa ofisi ya kuendeshea miradi kama ya benki binafsi; aliyekiuka miiko ya uongozi na kujaribu kujimilikisha Mgodi wa Makaa ya mawe ya Kiwira, kujitokeza ktk hizi kampeni za Arumeru Mashariki, eti atamfanya Mgombea wa CCM atatue matatizo ya ardhi yanayo wakabili Wameru tangu tupate uhuru. Mkapa angeeleza alifanya nini kuhusu suala hili kwa miaka kumi aliokaa Ikulu kama Rais.
   
 10. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #10
  Mar 21, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  I support what you have said it's the truth.
   
 11. P

  Praff Senior Member

  #11
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kukanusha uongo ni muhimu sana ukizingatia usipokanusha ni ngumu sana kwa watu kujua kama ni uongo au ukweli, baada ya kukanusha ndio muda muafaka wa kumwaga sera, siasa ni kamchezo kachafu sana usipokuwa makini ni hatari.
   
 12. d

  dada jane JF-Expert Member

  #12
  Mar 21, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono hoja. Pangua propaganda then endelea na sera
   
 13. kibakiking

  kibakiking Senior Member

  #13
  Mar 21, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unajua kama mtu hana la maana na msingi inakuwa ni tatizo sana kujua anafanya nini na nini anatakiwa afanye kwa sehemu hatuwezi kuwazarau kwa kuwa akili zao ni fupi kama joti.
   
 14. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #14
  Mar 21, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Mwanajeshi mzuri ni yule anayejua kupiga na kuokoa.

  Songa mbele chama la ukweeee.
   
 15. N

  NAMHALLAH New Member

  #15
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  umesema kweli cdm wanatakiwa kubadilimbinu kwa tunawategemea sana.
   
Loading...