CHADEMA tumeshinda katika kura - tunataka kushinda katika uongozi

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
8,972
2,000
Wapenda mabadiliko na maendeleo,

Karibuni niliwaambieni juu ya mchango wangu ambao ningependa kila mmoja ajitahidi kuUIGA KUFANYA vizuri zaidi. Katika kata ambayo kijiji changu cha kuzaliwa kimo, CHADEMA ilikuwa chini sana. Nilichukua likizo, na ndani ya siku 10 tulizopiga kampeni usiku na mchana kwa kushirikiana na makamanda wa huko kijijini, zilitosha uongozi wa wilaya kuchanganyikiwa.

Katika kipindi hicho cha siku 10, CCM walimleta Naibu Waziri Pindi Chana, Mkurugenzi wa Wilaya, Uongozi wa UWT wilaya, Polisi waliletwa mara 3, na mara ya mwisho wakiwa katika idadi kubwa. Jitihada zao zilihitimishwa na ugawaji pesa usiku wa kuamkia tarehe 14, siku ya upigaji kura.

Hapa naongelea KATA YA MAVANGA, WILAYANI LUDEWA, JIMBO LA MBUNGE DEO FILIKUNJOMBE. Mwisho wa jitihada zote za CCM katika kata hii yenye vijiji viwili ilikuwa kama ifuatavyo:

MAVANGA

MWENYEKITI
CHADEMA - 594
CCM - 414

VITONGOJI
CHADEMA 4
CCM 1

WAJUMBE
CDM 8
CCM 3

VITI MAALUM
CHADEMA 4 (wote tuliowasimamisha)
CCM 4 (walifuatia baada ya top 4 ya CHADEMA)

KIJIJI CHA MBUGANI
MWENYEKITI
CHADEMA - 272
CCM - 296

VITONGOJI
CHADEMA - 2
CCM - 3 (kimojawapo walipita bila kupingwa)
WAJUMBE - WOTE CCM ( Mtendaji wa kijiji aligoma kutangaza matokeo usiku wa 14 Desemba, jana amepita kila kitongoji kutangaza matokeo. Matokeo yaliyotangazwa ni tofauti na yaliyopatikana vituoni. Tunaendelea kufuatalia).

Matokeo mabaya ya kijiji cha Mbugani yamesababishwa na uzembe wa watu wetu kutolinda matokeo kama tulivyokuwa tumepanga. Kijiji cha Mavanga tumefanikiwa kutokana na kuweka mtandao mpana na madhubuti wa ulinzi wa kura kiasi ambacho hawakutarajia. Tuliwabana hasa, mkurugenzi alipoona imeshindikana aliondoka, na saa 7 usiku tukatangaziwa matokea.

Baada ya matokeo haya, makamanda tunaendelea na kampeni japo kwa staili tofauti. Sasa tunaanza kampeni ya utekelezaji wa tuliyowaahidi. Katika kata hii kuna tatizo la maji na umeme ingawa kuna maji ya bomba na umeme wa maji, huduma ambazo zililetwa na Kanisa Katoliki. Huduma hizi zimetupwa na serikali ya CCM, kwa sasa maji na umeme vinapatikana kwa mgao.

Kwa kuanzia tunataka kuondoa mgao wa maji ambapo tunaweka pampu mpya ya maji kutoka kwenye chanzo kingine cha maji ili kuongeza kiasi cha maji. Sahizi naenda kufanya survey, na kazi hiyo itakamilika mwezi February 2015. Gharama ya kazi hii inakadiriwa kufikia TZS 10 milioni. Mimi na marafiki zangu tuishio mjini tutachangia milioni 4, wafanyabiashara wa kijijini watachangia milioni 2, nguvu za vijana makamanda kijijini zitaokoa milioni 4. Tukikamilisha mradi wa maji tutaenda mradi wa umeme na baadaye kwenye viwanda kidogo.

Tunataka kata hiki ijiendeshe kama nchi ndogo ndani ya wilaya, na iwe chachu ya kusambaza ujumbe mzito kwa kata zilizo chini ya CCM. Viongozi wetu wote kwa nusu mwaka watafanya kwa kujitolea bila ya kulipwa posho yoyote. Wataanza kupata posho tutakapokuwa tumeweza kuzalisha. Tulichosisitiza ni kuwa mwananchi asichangishwe kwaajili ya kupata posho za viongozi wa kijiji kama ilivyokuwa imezoeleka.

Natambua kuwa mazingira ya kata nyingine ni tofauti na kata hii lakini wito wangu kwa wote wapenda mabadiliko, hakikisheni maeneo tulioshinda yanakuwa ya mfano katika kutunza haki za raia (wanakijiji wanaonewa sana, hapa kwetu kuna watu wamekuwa wakifungwa kamba na kucharazwa fimbo kwa kutotoa michango ambayo pesa zinazochangwa zililiwa na viongozi). Tuwe mfano wa kutoa uongozi wa mfano, na uongozi wenye ubunifu.

Katika kijiji cha Mavanga, mwishoni mwa wiki kabla ya kurejea jijini Mwanza natarajia kuendesha mafunzo ya uongozi na utendaji kazi wenye tija kwa viongozi wote. Nimefurahia sana kushiriki katika jitihada hizi. Vijana mori yao ipo juu sana, wanasema wapo tayari hata leo hii kwenda kufanya kazi zozote za kutumia nguvu na akili zao bila malipo alimradi kama zina faida kwao na wazazi wao.

Nina hakika CHADEMA ikiingia madarakani, tukiwa na miongozo mizuri, nchi itabadilika haraka. Wananchi wamechoka na umaskini, wapo tayari kufanya lolote ili kupata maendeleo. Tatizo kubwa ni mchwa CCM unaokula mkeka ambao kila mmoja anajitahidi kuusuka.
 

respect wa boda

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
4,536
2,000
Suluti kwako ndugu Bams nimependa sana mawazo yako pamoja na kujitolea kwako bila shaka wananchi wa hapo Mvangaw wataenzi na kuuthamini mchango wako. Bravo

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
33,756
2,000
Nakupongeza sana ndugu Bams. Hii kitu niliisema jana, hizo sehemu walizoshinda upinzani ndio Kingi kwa wale waliocheza draft wananielewa. wahakikishe wanatumia nafasi hii ndogo kuleta mabadiliko chanya ambayo yatatumika kama shamba darasa kwa watu wengine. Ni lazima kutoka sasa waliochaguliwa wachape kazi kwani hawajapata madaraka kwa hongo bali kukubalika na wananchi. Tunataka ikifika wakati wa uchaguzi mkuu ujao maeneo tuliyoshinda iwe ni kumalizia kazi tubakie na sehemu za watu wenye labdalabda na tukifika na mifano halisi ya sehemu tunazoongoza mbona ushindi ni lazima.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom