Chadema tulifanya makosa kuzindua kampeni zetu kistaarabu kule arumeru mashariki.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema tulifanya makosa kuzindua kampeni zetu kistaarabu kule arumeru mashariki....

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by only83, Mar 18, 2012.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  ....Kwa hali navyoiona kwenye kampeni kule Arumeru Mashariki nasikitika kwa CDM kuzindua kampeni zake kistaarabu.Lakini pia nasikitika kwasababu magamba wametumia nafasi hiyo kutukashifu na kututukana..mifano ni mengi,ukisikia wanachofanya Lusinde,Mwigulu,Wassira,Mkapa nk..unaweza ukaona jinsi hawa jamaa wanavyotumia upole na ustaarabu wetu kutupiga mawe kwelikweli..Mbaya zaidi nimeshangaa hata kwenye mitanado ya kijamii kama Facebook,Twitter nk vita hii ni kubwa sana..Lakini tuna mifano pia hapa JF kuwa threads zinanyanyuka kama uyoga kwasasa kumkashifu Dr Slaa na Kamanda Mbowe...Kwangu mimi nadhani hii inatokana na sisi kukubali kuwa wapole kwa uchaguzi huu...na CCM wanatumia nafasi hii kutuchafua na kutufanya kama wajinga..Nashukuru kwa kamanda Vincent aliyegundua hili mapema na kuanza mashambulizi...Nashauri kwa kusema CCM sio watu wastaarabu,huwezi ukawa mstaarabu kwa mtu asiye na akili kama CCM na watu wake.Na nikisema haya sina maana kuwa tuanzishe vurugu no,nasema tuwape vidonge vyao wanaostahili..nasikia Lowasa anataka kwenda huko,akishuka apewe vidonge vyake...
   
 2. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Akili za wanamagamba ziko ICU ya Milembe. Unataka tuziige?
   
 3. N

  Ngoiva JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tulianza na mungu, tutamaliza na mungu. Never give ur prayer to god. Chadema we shall win.
   
 4. Chilli

  Chilli JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2012
  Joined: Jul 17, 2011
  Messages: 1,638
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Tusitake kufanana na wajinga ambao wanajifunza mipasho na majungu. Tunachotaka kubadili ni ile imani watu walioaminishwa kwamba CDM ni chama cha fujo na ghasia, tutachukua ushindi kwa amani kabisaa, we acha tu wapige majungu.
  Naipenda sana hii "Tulianza na Mungu, tutamaliza na Mungu"
   
 5. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Wiki ya Mwisho watakimbia wenyewe
   
 6. chitalula

  chitalula JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,307
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  tena nngependa dr. slaa angeenda ile wiki ya mwisho ile akafunge kazi
   
 7. M

  Makupa JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Ndio maana siku zote hawa wanazi wa cdm wana matatizo tena ya kujitakia
   
 8. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #8
  Mar 18, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Misingi ya Taifa hili ilijengwa katika utu wa mwanadamu. Sasa usawa, ustaarabu, umakini, kuheshimiana ... ni sehemu ya utu huo. Kwa hiyo kama kampeni za CDM zilifunguliwa kwa kuzingatia hayo hakuna ubaya wowote, wala madhara yoyote

  Wenyewe (CDM) waendelee kutoa hoja zao na sera zao, huku wakiwaelimisha wananchi nguvu halisi waliyonayo kwani wananchi wengi hawajui nguvu halisi waliyo nayo. Halafu utaniambia matokeo yake
  View attachment 49595
   
 9. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #9
  Mar 18, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,793
  Likes Received: 36,806
  Trophy Points: 280
  CCM wameamini sana kwenye siasa za maji ya chooni na kujisahau kuwa wako kwenye nyumba ya vioo na wameanzisha vita ya mawe.
  CDM ina uwezo mkubwa wa kujinadi kwa sera,hoja za msingi na za namna yeyote ile ya kidemokrasia.
  Kuchagua CCM ni kujichagulia maisha magumu.
  Twendeni kazi.
  Tulianza na Mungu, tunamaliza na Mungu.
   
 10. Unyanga

  Unyanga JF-Expert Member

  #10
  Mar 18, 2012
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 402
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  mi nafikiri ulipaswa kusifia kitendo hicho kuliko kulaumu, wenye akili watachagua wastaarabu.
   
 11. MNAMBOWA

  MNAMBOWA JF-Expert Member

  #11
  Mar 18, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,983
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  kati ya cdm na ccm nani wastaarabu? Mlianzisha wenyewe siasa za kuchafuana ccm wakawa kimya mkaonekana kweli mna hoja na mnavutia wa2 kwenye mikutano yenu .sasa ccm nao wanajaribu angalau kwa ustaarabu kujibu mapigo mnaona cyo fair hv mnatufanya cc ni watoto? Pambaneni huko tutatoa uamuzi we2 kwenye sanduku la kura
   
 12. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #12
  Mar 18, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Get well soon MUAMBA!
   
 13. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #13
  Mar 18, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  ungekuwa mkoa wa pwani na wilaya zake labda coz una vichwa maji wengi wasioelewa, huwezi shawishi chadema wakajivue nguo kwa watu wa arusha ambao ni werevu. Nyerere alijibu kwa vile kuna mtu alitaka kuchukua sifa kupitia kwake. Wasira naye inabidi anyamazishwe na vijana wa kazi ndio saizi yake. Kuongea matusi kama kina kusinde ni sawa na wewe kujifananisha naye. NO!
   
 14. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #14
  Mar 19, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Tulianza na mungu, tutamaliza na mungu.
   
 15. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #15
  Mar 19, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mbona hamna tofauti ya kile wanachokifanya ccm na chadema. au wewe unaangalia upande mmoja tu?
   
 16. E

  EmeraldEme Senior Member

  #16
  Mar 19, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Watu wa Arumeru wanahitaji sera zitakazowasaidia kutatua matatizo yao makubwa kama ardhi,na maji! Na nyingine kama ajira na vitu kama hivyo. Suala la siasa za maji machafu wala sio kitu cha kuwa proud nacho, CCM wanaweza kuwa wameshapoteza mvuto kwa hiyo wanautafuta kwa sasa. Nyie pia mkifanya hivyo mtakua kama wao. Ni kitu kizuri kuwa mlifungua kampeni kistaarabu, hongereni na mjitahidi kumaliza kistaarabu. Wana Arumeru wataamua fate yao panapo siku ya kura.
   
Loading...