CHADEMA Tujiandaekulinda kura za 2015 na katiba ya sasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA Tujiandaekulinda kura za 2015 na katiba ya sasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tuko, Apr 14, 2011.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Apr 14, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Sorry kwa wale ambao sio wahusika,
  Haihitaji tena kufikiria sana. Ni wazi kuwa probability ya kufanyika uchaguzi wa 2015 kwa katiba tuliyo nayo sasa ni zaidi ya 90%.

  Naamini kuwa kwa kiasi kikubwa ubovu wa katiba yetu ulipanua mwanya wa CHADEMA kuibiwa kura katika uchaguzi wa 2010. Tukijua wazi kuwa sio salama tena kwetu wala kwa vizazi vyetu kuendelea kuiachia CCM itawale baada ya 2015, ni vizuri tukatumia fursa ya muda tuliyo nayo hivi sasa, kujipanga kwa uchaguzi wa 2015. Haipaswi na sio sifa za mwanaharakati yeyote kukata tamaa. Hivyo nawaomba wanaharakati wote wanaoamini na wanaopenda Tanzania ikombolewe mikononi mwa mafasadi kwa kupitia CHADEMA, tuanze kuumiza vichwa, ni kwa vipi 2015 tutapambana kwa maslahi ya nchi yetu.

  Wakati mwingine tumekuwa tukidhani kuwa hii ni kazi ya viongozi wa chama, lakini ukweli sio. Nilipata kuwa kwenye jimbo mojawapo waliloshinda CDM kwenye uchaguzi ulipita. Kwa kweli, ni akili na ujasiri wa hali ya juu unahitajika kupambana na CCM, kwa kutumia katiba iliyopo, lakini inawezekana.

  Nawahamasisha, lakini siku sio nyingi nitakuja na paper hapa, nikitoa mapendekezo yangu ni vipi tuanze kujipanga, na kuomba michango ya wadau. Jukumu ni la kila mmoja wetu.
   
Loading...