Wakuu,
Niliyasikia maneno ya Mbunge na Mwakilishi wa Zanzibar Bungeni, kweli tunakoenda si kuzuri, mbunge alifikia hadi kusema haya mapinduzi tunayoyaongea wao waliyafanya 1964. Kafika mbali kuanza kumshamblia Lissu as a person. Watu kama hawa ni hatari sana kwa muungano wetu. Sisi watanzania tuna wajibu wa kuhoji muundo wa muungano wetu, sasa si kuanza personal attacks na matusi ambayo si utamaduni wa mtanzania - Bisha kwa Hoja si kwa matusi - Wanzanzibar msameheni huyu mwakilishi wetu kajiaibisha yeye na familia yake si ninyi.
Ninavyopendekeza mimi CHADEMA warudi kwetu watueleza nini hasa Lissu aliongea na nini hasa anamaanisha, sababu duniani kila mtu ana upeo wake wa kuelewa, kuna wengine pia ni wagumu wa kuelewa na wepesi wa kusahau. Kuna wengine mpaka uongee kwa lugha nyepesi ili dhana nzima uliotarajia kueleza iweze kueleweka.
Kama ni pumba au mchelle sisi wananachi tutajua baada ya ufafanuzi kufanyika, siamini na sidhani LISSU ana nia mbaya juu ya Tanganyika, Zanzibar na Tanzania kwa ujumla laa hasa, nafikiri ni upeo wa kuelewana ndiyo kikwazo hapa.
Jingine watanzania tusiwe waoga kama mtu anajitokeza kusema ukweli, hakuna mtu atanibishia kwamba tuna matatizo mengi sana katika muungano wetu lakini matatizo haya tunayaficha uvunguni. Akitokea mtu kuyasema anaonekana msaliti.
Watanzania wenzangu kama sisi tu waoga hivi kuongelea matatizo yetu ya ndani sasa kuna haja kweli ya KATIBA MPYA? katiba mpya haitakuwa na jipya kama mtaogopa kuyasema yote hata haya ya muungano ambayo wengine huwa wanafikiri kuyasema ni uhaini.
Mimi kwa sababu ni Mtanzania nina haki ya kuhoji original copy ya haya makubaliano ya awali ya muungano wetu yapo wapi, je ni mchakato gani ulitumika kuyapata, je kina nani walishirikishwa? nk ili tuanzie hapo kuona kipi tukiondoe, kipi tukiboreshe na kipi hakitufai kwa manufaa ya sisi sote yaani bara na visiwani.
Wanaombeza Lissu kwa hili ni wanafiki wakubwa na hawaupendi muungano huu.
CHADEMA nawaomba mrudi kwetu wananchi, kwa lungha nyepesi kabisa mtueleze ni nini hasa mantiki ya mawazo ya Lissu hasa katika masuala ya muungano sababu navyojua mimi huo ndio msimao wa CHAMA ila Lissu alitumika kuufikisha kupitia Bunge.