CHADEMA, tuelimisheni nini hasa Lissu alikusudia kukisema!

FUSO

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Messages
16,646
Points
2,000

FUSO

JF-Expert Member
Joined Nov 19, 2010
16,646 2,000
Wakuu,

Niliyasikia maneno ya Mbunge na Mwakilishi wa Zanzibar Bungeni, kweli tunakoenda si kuzuri, mbunge alifikia hadi kusema haya mapinduzi tunayoyaongea wao waliyafanya 1964. Kafika mbali kuanza kumshamblia Lissu as a person. Watu kama hawa ni hatari sana kwa muungano wetu. Sisi watanzania tuna wajibu wa kuhoji muundo wa muungano wetu, sasa si kuanza personal attacks na matusi ambayo si utamaduni wa mtanzania - Bisha kwa Hoja si kwa matusi - Wanzanzibar msameheni huyu mwakilishi wetu kajiaibisha yeye na familia yake si ninyi.

Ninavyopendekeza mimi CHADEMA warudi kwetu watueleza nini hasa Lissu aliongea na nini hasa anamaanisha, sababu duniani kila mtu ana upeo wake wa kuelewa, kuna wengine pia ni wagumu wa kuelewa na wepesi wa kusahau. Kuna wengine mpaka uongee kwa lugha nyepesi ili dhana nzima uliotarajia kueleza iweze kueleweka.

Kama ni pumba au mchelle sisi wananachi tutajua baada ya ufafanuzi kufanyika, siamini na sidhani LISSU ana nia mbaya juu ya Tanganyika, Zanzibar na Tanzania kwa ujumla laa hasa, nafikiri ni upeo wa kuelewana ndiyo kikwazo hapa.

Jingine watanzania tusiwe waoga kama mtu anajitokeza kusema ukweli, hakuna mtu atanibishia kwamba tuna matatizo mengi sana katika muungano wetu lakini matatizo haya tunayaficha uvunguni. Akitokea mtu kuyasema anaonekana msaliti.

Watanzania wenzangu kama sisi tu waoga hivi kuongelea matatizo yetu ya ndani sasa kuna haja kweli ya KATIBA MPYA? katiba mpya haitakuwa na jipya kama mtaogopa kuyasema yote hata haya ya muungano ambayo wengine huwa wanafikiri kuyasema ni uhaini.

Mimi kwa sababu ni Mtanzania nina haki ya kuhoji original copy ya haya makubaliano ya awali ya muungano wetu yapo wapi, je ni mchakato gani ulitumika kuyapata, je kina nani walishirikishwa? nk ili tuanzie hapo kuona kipi tukiondoe, kipi tukiboreshe na kipi hakitufai kwa manufaa ya sisi sote yaani bara na visiwani.

Wanaombeza Lissu kwa hili ni wanafiki wakubwa na hawaupendi muungano huu.

CHADEMA nawaomba mrudi kwetu wananchi, kwa lungha nyepesi kabisa mtueleze ni nini hasa mantiki ya mawazo ya Lissu hasa katika masuala ya muungano sababu navyojua mimi huo ndio msimao wa CHAMA ila Lissu alitumika kuufikisha kupitia Bunge.
 
Junius

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2009
Messages
3,183
Points
1,170

Junius

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2009
3,183 1,170
Tatizo lipo hapa kwa Viongozi wote wa Tanganyika wa CCM na Vyama vya upinzani:

Wanapenda kuufanya uwongo kuwa ukweli:

Leo hii wanakataa hakuna Tanganyika, eti imefutwa, wapi imefutwa, nani kaifuta hawasemi,leo tunaambiwa kuna "..Maazimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania bara...", Mkoloni gani alitawa nchi inayoitwa Tanzania bara? ipo wapi hiyo nchi? hapa si kuufanya uwongo kuwa ukweli?

Wanapenda kuwapotosha wananchi makusudi:

Leo wanakataa hata historia ya muungano kwa upotofu wa makusudi, wanajifanya tatizo la muungano huu ni katiba wakati muungano huu umeundwa kwa mkataba na matatizo yameanzia huko, wanafanya hivyo makusudi kwa nia ya kuwafanya watu waamini kuwa nchi hizi tokea hapo zilikuwa moja, huu ni upotofu.

Wanapenda siasa za "dharau" na " ubabe".

Viongozi wa bara wanawadharau wananchi wao wa bara kwa kuwatia umasikini wa kujitakia huku wao wakineemeka na familia zao na mara zote wamekuwa na maamuzi ya ubabe zidi ya Zanzibar, haya yote na mengine wameyarithisha sasa hata kwa vyama vya upinzani kwa upande wa Tanganyika. Leo tusingelitegemea Chadema kubeza na kudharau hatua ya Wazanzibari kuunda serikali ya umoja wa kitaifa(GNU) na hata kuwatenga wenzao CUF katika serikali ya kivuli ya upinzani kwa kisingizio hicho hicho, na kwa kuonyesha kuwa wametihishwa hata "dharau" hata wapinzani wenzao wa NCCR-Mageuzi, ambao hawakuwa na kisingizio cha wenzao, pia wamewadharau na kuwatenga. Leo kina Tundu Lissu wanaendele na kauli za dharau kwa Wazanzibar, eti "...wanaonewa huruma...rais wao aambiwe ambiwe tu...siasa za rehani.." n.k
 
Mkiliman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2011
Messages
967
Points
225

Mkiliman

JF-Expert Member
Joined Jun 8, 2011
967 225
kweli kwa mtu makini hawezi kushangaa ukweli na hali halisi ya mambo yanavyotakiwa kufanyika hapa Tanzania. Kisheria Muungano wetu ni kama ni kidonda ambacho hakijapata tiba sahihi coz kuna upande wanalalamika zaidi ya wengine. Tatizo ni kutokuonekana kwa mambo ya Tanzania Bara ktk Muungano, lakini hili halizuii hoja kuwa ni kweli kuna mambo wazanzibar hawatakiwi kuamua juu ya mambo ya watu wa bara,,, thats what Lissu alijaribu kusema ktk hotuba yake.
Kama itatokea wazanzibar wataruhusiwa kujadili kila kitu basi wabara tutakuwa zuzu wa kujua mambo yatu,,hoja kuwa hakuna serikali ya Tanganika haitoi mwanya kwa Wazanzibar pekee kuwa na haki kila jambo ktk Muungano na wakati huo huo mambo ya Z'bar wanajadili wakiwa peke yao. Huo utakuwa ni uonevu mkubwa ambao unatumika vibaya kutokana na udhaifu wa sheria na mkataba wa Hati ya Muungano.
Kuna haja ya kuweka mipaka kwa uwazi kabisa kuwa Wazanzaibar na Wabara wajadili mambo kadhaa tuu katika Muungano na yaliyobaki yajadiliwe na serikali Zanzibar pekee while yale ya bara exclusively yawe chini ya Serikali ya Muungano bila kuingiliana na mambo ya Zanzibar.
 
Henry Kilewo

Verified Member
Joined
Feb 9, 2010
Messages
898
Points
250

Henry Kilewo

Verified Member
Joined Feb 9, 2010
898 250
mkuu: umeongea kwa busara ya hali ya juu sana bila kuweka ushabiki umesimama kwenye haki. hakika hata mimi nilisikiliza hutuba ya Lissu alihoji mambo ya msingi sana ambayo watanganyika tunao jiita watanzania bara tulikuwa tunatamani yasemwe na yakasemwa na lissu. sasa mimi na shangaa sana hii nongwa ya wazanzibar pale watanganyika wanaposimama na kuhoji uhalali wa muungano huu na kuonekana si wazalendo nongwa hii inatoka wapi? mimi mwenye huwo muungano siujui maana niliishia kuuona kwenye vitabu nyerere akichanganya mchanga huwo je huu ndiyo haswa ulikuwa muungano wa nchi hizi mbili kati ya zanzibar na tanganyika? je! ni watanganyika wangapi na wazanzibari wangapi waliyoshiriki kwenye kura za maoni juu ya muungano wanaoutaka? wapi alikokosea lissu kwenye kuhoji juu ya mambo ya msingi kama haya?
 
Henge

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2009
Messages
6,917
Points
1,250

Henge

JF-Expert Member
Joined May 14, 2009
6,917 1,250
tatizo lipo hapa kwa viongozi wote wa tanganyika wa ccm na vyama vya upinzani:

wanapenda kuufanya uwongo kuwa ukweli:

leo hii wanakataa hakuna tanganyika, eti imefutwa, wapi imefutwa, nani kaifuta hawasemi,leo tunaambiwa kuna "..maazimisho ya miaka 50 ya uhuru wa tanzania bara...", mkoloni gani alitawa nchi inayoitwa tanzania bara? Ipo wapi hiyo nchi? Hapa si kuufanya uwongo kuwa ukweli?

wanapenda kuwapotosha wananchi makusudi:

leo wanakataa hata historia ya muungano kwa upotofu wa makusudi, wanajifanya tatizo la muungano huu ni katiba wakati muungano huu umeundwa kwa mkataba na matatizo yameanzia huko, wanafanya hivyo makusudi kwa nia ya kuwafanya watu waamini kuwa nchi hizi tokea hapo zilikuwa moja, huu ni upotofu.

wanapenda siasa za "dharau" na " ubabe".

viongozi wa bara wanawadharau wananchi wao wa bara kwa kuwatia umasikini wa kujitakia huku wao wakineemeka na familia zao na mara zote wamekuwa na maamuzi ya ubabe zidi ya zanzibar, haya yote na mengine wameyarithisha sasa hata kwa vyama vya upinzani kwa upande wa tanganyika. Leo tusingelitegemea chadema kubeza na kudharau hatua ya wazanzibari kuunda serikali ya umoja wa kitaifa(gnu) na hata kuwatenga wenzao cuf katika serikali ya kivuli ya upinzani kwa kisingizio hicho hicho, na kwa kuonyesha kuwa wametihishwa hata "dharau" hata wapinzani wenzao wa nccr-mageuzi, ambao hawakuwa na kisingizio cha wenzao, pia wamewadharau na kuwatenga. Leo kina tundu lissu wanaendele na kauli za dharau kwa wazanzibar, eti "...wanaonewa huruma...rais wao aambiwe ambiwe tu...siasa za rehani.." n.k
kumbe wewe mpemba! Kwanini siku hizi cuf mnajifanya kutetea sana ccm haaaa!??
 
SMU

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2008
Messages
8,694
Points
2,000

SMU

JF-Expert Member
Joined Feb 14, 2008
8,694 2,000
Wakati Mh Lissu wakitaka kuomba mwongozo/kutoa taarifa spika alitoa kauli fulani ambayo ndani yake (kwa mtizamo wangu) inabeba ujumbe mzito.

Alisema 'tuvumiliane' na akimwacha mbunge yule aendelee kutoa lugha isiyofaa. Kwa haraka inaweza kuonekana kawaonea CDM (hasa Lissu) lakini ukitizama kwa mapana ni kama vile alikuwa anamwacha mbunge yule aendelee 'kujiaibisha' na kuonesha 'uwezo wake wa kufikiri na kutoa hoja'.

Hiyo 'tuvumiliane' ukiitizama sana na hasa katika context ya jana bungeni, inaashiria 'what else can we expect from him?' (maana mwanzo alikwisha mwambia ajikite kwenye kutoa hoja...lakini badala yake akaendelea kutoa matusi).
 
ntagunga

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2011
Messages
630
Points
250

ntagunga

JF-Expert Member
Joined Aug 13, 2011
630 250
Mambo ya muungano ni suala TETE sana. linatuumiza watanganyika.

Mbunge wa zanzibar, lazima amwone Lissu ni mbaya kwani angusa maslahi yake moja kwa moja. Mi nadahni na nakubali wabunge walitoka zanzibar kuja kwenye bunge la muungano, wanafaidi kuliko hata wa kule zanzibar.

Maslahi wayapatayo, hawataki hata kuyaachia kwa kuruhusu muungano kuhojiwa. Ni wabunge maslahi.

Ukweli ni kwamba, muungano unawafaidisha zaidi wazazimbar kuliko watanganyika tunavyofaidika nao. Tanganyika tuungane ili kama wanataka tuendelee na sisi tuwe na bunge letu la Tanganyika, na tuchague wabunge wa muungano. hapo tutaenda sawa.
 
Consigliere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
10,237
Points
2,000

Consigliere

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
10,237 2,000
Tatizo lipo hapa kwa Viongozi wote wa Tanganyika wa CCM na Vyama vya upinzani:

Wanapenda kuufanya uwongo kuwa ukweli:

Leo hii wanakataa hakuna Tanganyika, eti imefutwa, wapi imefutwa, nani kaifuta hawasemi,leo tunaambiwa kuna "..Maazimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania bara...", Mkoloni gani alitawa nchi inayoitwa Tanzania bara? ipo wapi hiyo nchi? hapa si kuufanya uwongo kuwa ukweli?

Wanapenda kuwapotosha wananchi makusudi:

Leo wanakataa hata historia ya muungano kwa upotofu wa makusudi, wanajifanya tatizo la muungano huu ni katiba wakati muungano huu umeundwa kwa mkataba na matatizo yameanzia huko, wanafanya hivyo makusudi kwa nia ya kuwafanya watu waamini kuwa nchi hizi tokea hapo zilikuwa moja, huu ni upotofu.

Wanapenda siasa za "dharau" na " ubabe".

Viongozi wa bara wanawadharau wananchi wao wa bara kwa kuwatia umasikini wa kujitakia huku wao wakineemeka na familia zao na mara zote wamekuwa na maamuzi ya ubabe zidi ya Zanzibar, haya yote na mengine wameyarithisha sasa hata kwa vyama vya upinzani kwa upande wa Tanganyika. Leo tusingelitegemea Chadema kubeza na kudharau hatua ya Wazanzibari kuunda serikali ya umoja wa kitaifa(GNU) na hata kuwatenga wenzao CUF katika serikali ya kivuli ya upinzani kwa kisingizio hicho hicho, na kwa kuonyesha kuwa wametihishwa hata "dharau" hata wapinzani wenzao wa NCCR-Mageuzi, ambao hawakuwa na kisingizio cha wenzao, pia wamewadharau na kuwatenga. Leo kina Tundu Lissu wanaendele na kauli za dharau kwa Wazanzibar, eti "...wanaonewa huruma...rais wao aambiwe ambiwe tu...siasa za rehani.." n.k
Unajaribu kufanya kile unachodhani kitatupandisha hasira.....hatuhitaji inputs zenu, tunafahamu tufanyalo na tunajua tunakachokihitaji, hatuhitaji msaada wa mawazo yako/yenu....
Tundu Lissu amewakilisha kikamilifu kile ambacho tulihitaji mtu akiongee kwa uwazi, mnapenda sana kujifanya mnapiga simu kwenye suala la muungano, tukipokea mnalalamika.
 
ntagunga

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2011
Messages
630
Points
250

ntagunga

JF-Expert Member
Joined Aug 13, 2011
630 250
SMU, CCM wanaamini kwamba kuwatukana CHADEMA/UPINZANI, KUWAFINYA BUNGENI, ni kuwapaka matope waonekane si lolote mbele ya wapiga kura.

Lakini wanasahau kuwa wapiga kura wameshawachoka CCM, na wana mkakati wa kuwaondoa kwenye uuongozi na kuwakabidhi upinzani.

Utawasikia wakijikosha kwa maneno, MIAKA MITATO SI MINGI kwa nia ya kuwatisha Upinzani.

Swali langu ni JE, MIAKA MITANO ITAKAPOISHA NA BADO WANANCHI WAKAONESHA KUWAAMINI UPINZANI NA KUWAONGEZEA VITI VYA UBUNGE, CCM WATASENMA NINI?

MADUDU WAYAFANYAYO VIJANA TUNAYAONA, NA NI SISI WENYE UCHU WA MABADILIKO. KIZAZI CHA KINA WASIRA, SIKU ZAKE ZINAHESABIKA. CHADEMA/NCCR-MAGEUZI ENDELEZENI KUWEKEZA KWA VIJAN, TUTASHINDA TU
 
HT

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2011
Messages
1,899
Points
0

HT

JF-Expert Member
Joined Jul 29, 2011
1,899 0
Wakati Mh Lissu wakitaka kuomba mwongozo/kutoa taarifa spika alitoa kauli fulani ambayo ndani yake (kwa mtizamo wangu) inabeba ujumbe mzito.
Alisema 'tuvumiliane' na akimwacha mbunge yule aendelee kutoa lugha isiyofaa. Kwa haraka inaweza kuonekana kawaonea CDM (hasa Lissu) lakini ukitizama kwa mapana ni kama vile alikuwa anamwacha mbunge yule aendelee 'kujiaibisha' na kuonesha 'uwezo wake wa kufikiri na kutoa hoja'.
Hiyo 'tuvumiliane' ukiitizama sana na hasa katika context ya jana bungeni, inaashiria 'what else can we expect from him?' (maana mwanzo alikwisha mwambia ajikite kwenye kutoa hoja...lakini badala yake akaendelea kutoa matusi).
I love this :)
 
Angel Msoffe

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2011
Messages
6,795
Points
1,225

Angel Msoffe

JF-Expert Member
Joined Jun 21, 2011
6,795 1,225
Kwenye katiba Rais wa zanzibar anapaswa ashirikishwe kwenye mambo yanayohusu muungao tu asishirikishwe kwenye mambo mengine ya tz bara ikumbuje Wazanzibar wametunga katiba yao bila kumshirikisha mtanzania bara ht m1. NA kuhusu muungano wananch waseme km wanauhtaji muungano na wanahtaji muungano wa aina gani. Maneno haya aliyaongea TUNDU LISSU. Maoni yng: haiwezekani upande 1 utunge katiba yk bl kushrikisha upande wa 2 hlf wkt upande wa 2 unapotaka kutunga katiba yk upande wa 1 ung 'anie kushiriki kwa lazima, hii si sawa kbs kila upande utunge sheria zake kwa nch yk hlf kuwe na sheria/ katiba ya muungano ninamaa kuwe na katiba 3. wazanzbar wanamambo ya udini sn wanataka kuleta udini wao hk bara mf. Wanasema lazima sheria ya ndoa irekebishwe iruhusu watoto wakishapevuka waolewe kwa kawaida watoto wanapevuka 10-12yrs when they are std 5/6 hvy mchumba(mbakaji) akijitokeza sheria imruhusu kuoa, mi naona huu ni upumbavu,unyanyasaji na ukatili kwa watoto wa kike.
 
luhwege

Member
Joined
Sep 17, 2010
Messages
90
Points
95

luhwege

Member
Joined Sep 17, 2010
90 95
Asante kwa kutoa mawazo yako chanya haiwezekani wabara kuonewa kiasi hicho.Muungano wetu hauko wazi kwani hata usome madarasa yote hutaweza kukutana na Topic inayohusu Muungano wetu.Tuamke na tufanye yale tutakayo yafanywe kwa maslahi ya wote.
 
fige

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2010
Messages
376
Points
0

fige

JF-Expert Member
Joined Jul 4, 2010
376 0
Katika muungano wetu kuna mambo mengi ambayo hayajakaa sawa kama wachangiaji wengine hapo juu walivyoonyesha ,mfano mmojawapo ni wizara ambayo ina mambo ya muungano na yasiyo ya muungano kuongozwa na mzanzibari naona haijakaa sawa.
 
Ringo Edmund

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2010
Messages
4,889
Points
0

Ringo Edmund

JF-Expert Member
Joined May 10, 2010
4,889 0
Tatizo lipo hapa kwa Viongozi wote wa Tanganyika wa CCM na Vyama vya upinzani:

Wanapenda kuufanya uwongo kuwa ukweli:

Leo hii wanakataa hakuna Tanganyika, eti imefutwa, wapi imefutwa, nani kaifuta hawasemi,leo tunaambiwa kuna "..Maazimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania bara...", Mkoloni gani alitawa nchi inayoitwa Tanzania bara? ipo wapi hiyo nchi? hapa si kuufanya uwongo kuwa ukweli?

Wanapenda kuwapotosha wananchi makusudi:

Leo wanakataa hata historia ya muungano kwa upotofu wa makusudi, wanajifanya tatizo la muungano huu ni katiba wakati muungano huu umeundwa kwa mkataba na matatizo yameanzia huko, wanafanya hivyo makusudi kwa nia ya kuwafanya watu waamini kuwa nchi hizi tokea hapo zilikuwa moja, huu ni upotofu.

Wanapenda siasa za "dharau" na " ubabe".

Viongozi wa bara wanawadharau wananchi wao wa bara kwa kuwatia umasikini wa kujitakia huku wao wakineemeka na familia zao na mara zote wamekuwa na maamuzi ya ubabe zidi ya Zanzibar, haya yote na mengine wameyarithisha sasa hata kwa vyama vya upinzani kwa upande wa Tanganyika. Leo tusingelitegemea Chadema kubeza na kudharau hatua ya Wazanzibari kuunda serikali ya umoja wa kitaifa(GNU) na hata kuwatenga wenzao CUF katika serikali ya kivuli ya upinzani kwa kisingizio hicho hicho, na kwa kuonyesha kuwa wametihishwa hata "dharau" hata wapinzani wenzao wa NCCR-Mageuzi, ambao hawakuwa na kisingizio cha wenzao, pia wamewadharau na kuwatenga. Leo kina Tundu Lissu wanaendele na kauli za dharau kwa Wazanzibar, eti "...wanaonewa huruma...rais wao aambiwe ambiwe tu...siasa za rehani.." n.k
ndoa gani mke hataki uingie chumbani kwake ila kwako anataka aingie wakati wowoteatakao na aamue kila kitu cha chumbani kwako,huko kwake hata akiingia mwanaume mwingine usihoji.
kwanza signature yako inafanana na akili yako na chama chako kasome kokote duniani hakuna kitu kinaitwa haki sawa kwa wote,quran,bible,vitabu vya dini zote na hata vya wanadamu wenye akili timamu.
kila mtu anahaki yake na anastahili kuipata,anayefanya kazi kwa bdii ana haki sawa na bidii yake na asiyefanya kazi nae ana haki yake,sasa hiyo haki sawa maana yake ni nini?
cuf haiuziki kwa watu wenye akili timamu (samahani kama nimekugusa)kwa sababu ya hiyo kauli mbiu ya kidikteta,isiyojali maagizo ya mungu(wa kweli)na iliyoasisiwa na watu ambao sidhani kama walienda shule kuelimika au walienda kutafuta vyeti.
hata hilo jina ulilojiita sijui ila sishangai kwani hata kiongozi mkuu wa chama chako amenunua udk.
pole lakini kwani inaonyesha ndivyo mlivyoumbwa.
 
Junius

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2009
Messages
3,183
Points
1,170

Junius

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2009
3,183 1,170
wazenji wamekuwa wakibip sasa leo wabara wanataka kupokea inakuwa nongwa
Mnapokea vipi? bara wanasema Zanzibar haiwezi kwenda bila ya wao, hapo hapo wanasema wanaibeba, wao wenyewe wanasema hawataki, hivi niulize, wapi duniani umepata kumuona mtu analazimisha kutoa msaada au kumsaidia mtu ambaye hataki??
 
Jobo

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2008
Messages
587
Points
195

Jobo

JF-Expert Member
Joined May 15, 2008
587 195
Tuna alisema kweli! Hivi Rais wa Zanzibar atahusishwa vipi kutoa maamuzi ya Katiba ambayo kwa asilimia 90 inahusu mambo yasiyo ya Muungano? Hata kwa akili ya kijinga tu, huwezi kuweka wajumbe 15 Bara na wajumbe 15 toka Zanzibar kujadili Katiba hiyo. Hapo utakuwa umeacha sekta muhimu za Bara katika mchakato huo na kutoa nafasi ya wajumbe wengi wa Zanzibar kwenda kupiga usingizi na kupata posho. Inatosha kuwa na wajumbe 20 toka Bara na watano tu au basi hata 10 wa Zanzibar. Rais wa Zanzibar anapaswa kupewa tu taarifa na ashirikishwe katika kuteua wajumbe wa kutoka Zanznibar na si vinginevyo. Nadhani haya matatizo ya Muungano tumeyalea wenyewe kwa kuwa soft mno kwa Wazanzibari. Tundu alisema ukweli, na ukweli siku zote ni msumari mchungu!!!!!!
 
Forum statistics

Threads 1,353,373
Members 518,297
Posts 33,076,309
Top