Chadema: Tudai haki bila kumwaga damu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema: Tudai haki bila kumwaga damu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gumzo, Aug 14, 2012.

 1. G

  Gumzo JF-Expert Member

  #1
  Aug 14, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [h=3][/h] [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeitaka Serikali kuacha kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kuangalia upepo wa kisiasa, ili kuepuka kuwapa wananchi mateso na umaskini.

  Pia kimewataka wanachama wake, kudai haki zao kwa amani badala ya kutumia nguvu zinazoweza kusababisha umwagaji wa damu.

  Rai hizo zilitolewa juzi kwa nyakati tofauti na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Makamu wake wa Zanzibar, Said Issa walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari.

  Mbowe kwa upande wake, alitoa rai hiyo kupitia hotuba yake iliyosomwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Tanzania Bara, Zitto Kabwe, katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Mnadani Mjini Katesh.

  Zitto na wabunge wengine wa Chadema, walipita katika kijiji hicho wakitokea wilayani Rombo.

  Katika hotuba hiyo, Mbowe alisema Chadema imedhamiria kufa ikiwa katika harakati za kupigania haki za wananchi ikiwemo ya kumiliki ardhi na kupinga uonevu wa aina mbalimbali, unaofanywa na baadhi ya watawala wasiokuwa
  waaminifu.

  “Chadema imejipanga ili kuhakikisha kuwa haki za wananchi zinapatikana na wanatumia rasilimali zao kujinufaisha kiuchumi kuliko ilivyo sasa wanapoambulia kula makopa,” alisema Mbowe kupitia hotuba yake.

  CHANZO: GUMZO LA JIJI
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #2
  Aug 14, 2012
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  Haki haiji yenyewe bali hutafutwa na kupiganiwa. Mia
   
 3. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #3
  Aug 14, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Kichwa cha habari na content ni differ..mtoa mada ni gamba aloingilia masafa ya cdm.
   
Loading...