CHADEMA toeni vielelezo vyote halafu mtuachie wananchi

Eliphaz the Temanite

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
3,018
1,147
Uchaguzi uliopita umeacha mambo mengi ambayo watanzania tutaendelea kuyakumbuka! Kubwa zaidi ni kuitikisa ngome ya CCM to the core! Sasa nafahamu fika ya kwamba Tanzania bila CCM inawezekana. Mbinu walioyokuja nayo safari hii, ni kupaint picture Dr Slaa hakupigiwa kura wa Watz walio wengi. Kila mtu anafahamu walichoambulia kule Mz, Shinyanga, Arusha, Mara, Kilimanjaro, Mbeya, Rukwa (Sumbawanga) na maeneo mengine mengi!
Aidha nafahamu fika wazi kuwa JK anafahamu kile walichofanya na Chama chake. Watz wengi tunaimani na Dr Slaa na CHADEMA, vile vile hatuko tayari kuwa chimbuko la vurugu na umwagaji damu wa Wtz

Ushauri, tuwavue nguo hawa! CCM, tume ya uchaguzi! Ushahidi tunao na vielelezo vipo, Yawekeni hadharani matokeo ya halali ya mawakala, wezi wawekeni hdhari waliibaje, nani alihusika na wizi hii. Wtz wakiisha kuijua kweli itawaweka huru! 2015 TUTAIMARISHA ULINZI WA KURA ZETU.
 
Haswa, sisi ndio tutakao likomboa Taifa letu kutoka mikononi wa maharamia sisiemu wasio mthaminin mtanzania masikini, siku inakuja kila mwana sisiemu atalia na kusaga meno.

Naamini Chadema ni chama makini, kina watu makini, sera zake ni makina, na pia ni chama pekee chenye dira ya kuleta mabadiliko ya kweli, na pia Chadema hafagiliwi mtu, ukiwa vuguvugu tunakutema hatujali wewe ni nani unafanya nini, wapi ana wakati gani. Naamini 2015 hatoki mtu

Ama kweli hakuna TUPU iliyo na TUPU.
 
Uchaguzi uliopita umeacha mambo mengi ambayo watanzania tutaendelea kuyakumbuka! Kubwa zaidi ni kuitikisa ngome ya CCM to the core! Sasa nafahamu fika ya kwamba Tanzania bila CCM inawezekana. Mbinu walioyokuja nayo safari hii, ni kupaint picture Dr Slaa hakupigiwa kura wa Watz walio wengi. Kila mtu anafahamu walichoambulia kule Mz, Shinyanga, Arusha, Mara, Kilimanjaro, Mbeya, Rukwa (Sumbawanga) na maeneo mengine mengi!
Aidha nafahamu fika wazi kuwa JK anafahamu kile walichofanya na Chama chake. Watz wengi tunaimani na Dr Slaa na CHADEMA, vile vile hatuko tayari kuwa chimbuko la vurugu na umwagaji damu wa Wtz

Ushauri, tuwavue nguo hawa! CCM, tume ya uchaguzi! Ushahidi tunao na vielelezo vipo, Yawekeni hadharani matokeo ya halali ya mawakala, wezi wawekeni hdhari waliibaje, nani alihusika na wizi hii. Wtz wakiisha kuijua kweli itawaweka huru! 2015 TUTAIMARISHA ULINZI WA KURA ZETU.

mimi nilishakugongea thanks nilijua kuwa tunawaletea noma ,ila kama ni 2015 hapo umeniangusha chalii, kwa sababu hata mwaka huu watu walikuwa wanajua kuwa kura zitaibiwa sasa hazikuibiwa ila zimechakachuliwa sijui tofauti yake hapo....ila nnacho jua kura wamehamishia kwao ...
 
Naunga mkono hoja, Chadema makao makuu tupeni taarifa na ikiwezekana tupate data ili tuanze mchakato.
 
Dr. Slaa kubaliana na uamuzi ila si matokeo,kwani uamuzi umefanywa na NEC kinyume na matokeo. Ushauri unaotoka hapa ni mzuri ili CCM wasipate sababu. Kama ulivyotushitakia ufisadi, tushitakie matokeo tunajua namna ya kutoa hukumu.
 
Nipo na wewe mkuu.
 
Dr. Slaa toa ukweli hadharani usiende mahakamani kwani kesi haitasikilizwa, weka wazi kwa umma ili 2015 watu wajue, CCM wakitaka waende mahakamani ili we uende na ushahidi wako wakinyamaza watanzania watajua kuwa kumbe ni kweli, halafu jibu ni uchaguzi ujao, tutapiga kura na tutalinda kura zetu, tutapika na kula kituoni hadi matokeo yatangazwe.
MUHUMU KULIKO YOTE. Wabunge wa chadema wapeleke muswada bungeni kuwa wakurugenzi wa halmashauri waondolewe kuwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wakati wa uchaguzi. Hawa ndiyo chanzo cha tume kutoaminika kwasababu hawawajibiki hata tume bali kwa serikali ya chama tawala.
OMBI kwa Rais wetu mtukufu, Jakaya Mrisho Kikwete: Tusaidie kubadili tume iwe huru, waondoe wakurugenzi wa halmashauri kuwa wasimaizi wasaidizi ili wewe ukapumzike kwa amani Bagamoyo na watanzania wakukumbuke kwa hilo.
 
Ndio Naunga Mkono.

Wananchi wengi sana tulikupigia kura Dk Slaa, tunaomba Chadema muweke wazi kuhusu Kura zetu.

Lini Dk Slaa ataongea na Waandishi wa habari tujue yaliyojiri kuhusu uchakachuaji?

Je na Hawa Viongozi wa Dini wanamwomba Dk SLaa akubali yaishe, yaisheje??

Viongozi wa dini wanatakiwa waikemee NEC hadharani, NEC ivunjwe na Katiba Mpya iandikwe.

Pia Serikali itakayoundwa itekeleze baadhi ya sera za chadema kama Elimu bure, afya bure, Kupunguza kodi kwenye vifaa vya ujenzi, pia kupunguza kodi kwenye bidhaa muhimu kama sukari, mafuta ya kupikia
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom