CHADEMA toeni Tamko la kutangaza nia ya kugombea… | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA toeni Tamko la kutangaza nia ya kugombea…

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by amba.nkya, Oct 4, 2012.

 1. amba.nkya

  amba.nkya JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 417
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Habari wanajamvi,
  Nianze na ku "declare interest" kuwa mimi nimiongoni mwa wenye maono ya kugombea Ubunge, 2015 kupitia chama changu CDMkwenye jimbo langu ambalo sitalitaja kwa sasa. Sifa na vigezo vya kugombeaUbunge ninavyo; nikitaja baadhi ni kuwa mtanzania halisi, mwanachama mwaminifuna mzalendo, msomi, kiongozi, mpigania haki na usawa na kuweka mbele maslahi ya wanyonge juu ya kunufaika na raslimali luluki za Taifa hili. Aidha, nakubalikakwenye jimbo langu. Hata hivyo, pamojana sifa, vigezo nilivyotaja na kukubalika kwangu jimboni kwangu sijawahi kuwana kimbelembele cha kutangaza nia yangu mapema bali nafanya kazi kwanza ya kujengana kuimarisha chama changu kuanzia ngazi ya misingi.

  Vilevile, sababu yakutotangaza mapema ni kutokana na ukweli kuwa CHADEMA ni chama inayojiendeshakitaasisi kwa kuzingatia Katiba, taratibu, kanuni na miongozo yake. Miongonimwa taratibu, kanuni na miongozo hiyo ni pamoja na kupiga marufuku mwanachamayeyote kutangaza nia ya kugombea nafasi yoyote hususani udiwani, ubunge naurais kabla muda muafaka wa kufanya hivyo haujawadia maana itakuwa ni kampeni;mfano kuna waraka umetolewa na chama hivi karibuni unaoelezea suala hili. Lakini inanipa shidasana kwa viongozi wakuu kunyamazia mtu kutangaza kugombea nafasi nyeti kama yaUrais wakati wanachama wengine wamekaa kimya wakisubiri kipenga kipulizwe cha kutangazania.

  Ninashawishika kuamini kuwa Mh. Zitto Kabwe kutangaza nia ya kugombeaurais, 2015 pamoja na kuwa ana haki ndani ya chama; anatumika na CCM kwamaslahi yake binafsi, ni mroho wa madaraka, amelewa sifa ama anasukumwa na wapambena mamluki ili kuisambaratisha CDM. Nasema hivyo kutokana na jinsi nilivyoelezahapo juu hasa kwa kuzingatia kuwa Mh. Zitto ni kiongozi mkubwa wa chamaanayejua jinsi chama kinavyoendeshwa. Bado najiuliza kwanini anapata ujasiri wakuendelea kutangaza mara kwa mara kugombea urais hata kabla muda haujafika hukuwanachama wengine tuko busy kufanya shughuli za kukijenga chama na tukisubiritamko rasmi la chama kuanza harakati za kutangaza nia.

  Ushauri wangu kwa Mh.Zitto na wanachama wenzangu, kwa utafiti wangu na kuzingatia hali ya kisiasakwa sasa nchini Tanzania, ni kwamba Dr. Slaa ndio tegemeo na chaguo la wengikwa nafasi ya Urais, 2015 na watanzania wengi wana imani kubwa naye. Hata hivyo, Dr. Slaa hajawahi kutangazania hiyo hadharani au kwenye vikao vya chama ingawa wananchi wengi wanamwitaRais mtarajiwa kwa kuwa wamemuona anafaa kuwa Rais. Mh. Zitto pamoja na wapambewako mnapaswa kutambua, kukubali na kuheshimu ukweli huu kwa maslahi ya chamana Watanzania kwa ujumla.

  Mwisho, naomba chama kitoe tamko rasmi au warakamwingine iwapo mwanachama yeyote anaweza kuanza kutangaza nia ya kugombea kablaya muda kufika ama la.

  Nawasilisha………

   
 2. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 23,757
  Likes Received: 1,388
  Trophy Points: 280
  ya nini sasa wewe bongolala?subiri ibaki miezi kadhaa .
   
 3. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,490
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  Macho yanauma kusoma post yako mkuu, hebu fanya punctuation
   
 4. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,397
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Mkuu umeongea vitu vya maana sana tumekupata
   
 5. i

  iseesa JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa nini unamuingizia maneno mdomoni Dr Slaa? Ni lini alisema kuwa atagombea? Muacheni atasema muda ukiwadia
   
Loading...