CHADEMA toeni tamko kupinga DOWANS wasilipwe, nyie ni viongozi wetu, vp? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA toeni tamko kupinga DOWANS wasilipwe, nyie ni viongozi wetu, vp?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Wameiba Kura, Dec 19, 2010.

 1. Wameiba Kura

  Wameiba Kura JF-Expert Member

  #1
  Dec 19, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 390
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dr Slaa, Tundu Lissu, Marando, Mnyika, Mdee, nyie ni viongozi wetu, na wananchi wengi
  sana country wide depend on you, u r public voice, sauti ya wanyonge, sasa hadi sasa sijasikia mkipinga Dowans wasilipwe officially as leaders, vp? Mbona kimya? hizi ni pesa za
  wanyonge watanzania zinataka kuibiwa wazi wazi, nilitegemea mngejipanga within a week
  mtoe tamko kali, ila siku zinaenda nyie mko kimya? sikulitegemea hili, toeni tamko quickly na liwe kali na ikibidi maandamano yafanyike kuokoa wanyonge, bcoz hatuna imani na serikali kuhusu jambo hili, ni nyie basi mtungoze kulipinga kwa hali na mali, na huyu dowans hadi tumjue, kama yupo nchini hafai kuishi hapa kwetu TZ, si raia anaweza kufanya
  uwizi mkubwa hivi, plse CDM we beg u, it is a right time, naona kama mmechelewa kidogo
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Dec 19, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa wameiba kura,nami naku support naona kama chadema wamejisahau kazi yao ya kuwa wapinzani na chama tawala...kunyoosha mambo naona sasa wana upinznai wao kwa wao ndani.....au wanasubiria wakati wa uchaguzi...no way wanatakiwa wawepo kwenye ulingo wakati wote...hili la dowans watu wa ndani wamejaribu kukemea sita na nape wao kama upinzani wangesha stage kabisa kulipinga hili....chadema aibu jamani nguvu ya wanyonge iko nyuma yenu kama mlikuwa mna beep mjue mtawakwaza sana walala hoi wanaotaka mabadiliko!!!
   
 3. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #3
  Dec 19, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  you are wrong chadema huwa haikurupuki kwa hoja; subiri moto utawawakia vichwani mwao; mhimu wawe na evidence of whole scenario; mbona mnafanya kama chadema chama cha kutoa matamko tu; hiki sio cham cha kutoa matamko ni chama kinachojiandaa kuchukua dola; mna presha sana; dr slaa lazima apate muda kutafakari mambo mengine kitaifa; kwanza naona ilishatoa sasa ni muda wa vitendo tu; kumbuka hiki sio kitu kipya kabisa labda mnataka watu waseme seme tu hovyo mwishowe muwaite wasema hovyo; Richmond (Lowasa alijiuzuru) haitambuliki mmiliki wake, deni likanunuliwa na Dowans (RA, na wamiliki hawaklo wazi tuwajue mpaka sasa hatujui nani atakuwa analipwa hiyo check na kuibeba) sasa nini kipya hapo
   
 4. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #4
  Dec 19, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Na hofia maisha ya mtoto wangu vingivyo ningemtafuta EL na RA hata kwa mshale haewezekani tuwalipe mapesa yote haya, bil 185 hizi zikiingizwa kwenye elimu, afya itakuwa na mchango mkubwa sana...
   
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  Dec 19, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hakuna tamko la kutoa..DOWANS lazima walipwe maana CCM na serikali yake inafanya mambo bila kutumia akili..hakuna tamko hapo..Serikali ya JK ni kuilipa DOWANS tu..period!!! hatuwezi kuonea huruma upumbavu wa watu wachache wanaofanya mambo kwa influences za siasa na kaucha proffesions zao katika kufanya maamuzi
   
 6. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #6
  Dec 19, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Niliona taarifa kwenye gazeti, Waziri mkuu akisema lazima serikali iilipe DOWANS kwa sababu serikali ya CCM ina heshimu utawala wa sheria. hapo unategemea nini huyu pinda sina imani nae tena kama wana zingatia utawala wa sheria, sheria ipi iliyotumika kumpiga mbunge wa Godbless Lema mpaka kuzimia.....Pinda wewe ni mnafiki tu na unafiki wako ulijionyeshea ulipo kataa gari halafu ukasema serikali itafute mtu mwingine alitumia hapo ulisaidia vipi pesa ya wakulima ambao wewe unajiita eti mtoto wa mkulima huku tukikumbuka kauli yako ya kushauli serikali isinunue magari ya garama leo nchi iko taabani mnanunua gari 65 ya mil 280 kwa kila hivyo ndivyo ulivyo washauli, je umewachukulia hatua gani walio nunua hayo magari...na kuchukia siku hizi yaani wewe na kina Mkwere, Lowasa, Rostam na mafisadi wengine lenu moja halafu ukome kutuzunga na jina la mkulima na kulia lia bunge....
   
 7. Keynes

  Keynes JF-Expert Member

  #7
  Dec 19, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 499
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  kwa kweli tunaomba TAMKO KALI CDM....mi kwa hili nipo tayari kwa lolote
  nipo tayari kuishia jela
  nipo tayari kujitoa mhanga
  nipo tayari kukesha pale nje ya IKULU kila anayetoka alambe bakora
  nipo tayari kwa ajili ya manufaa ya wajukuu zangu.

  "There's no way I'm going to put myself through Sandhurst and then sit on my arse back home while my boys are out fighting for the future generations.
  CORRUPTION IS MORE THAN WAR WE NEED TO JOIN EFFORT.
   
 8. m

  mjombajona JF-Expert Member

  #8
  Dec 19, 2010
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 262
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wasilipwe mpaka kwanza walipa kodi wajue Dowans ni nani, na kama ni mchongo wa mmojawapo wa mafisadi tuliowataja Mwembeyanga mwaka fulani uliopita basi nguvu ya umma itumike accordingly,hatuwezi angalia hazina inakaushwa halafu tunakenua meno!
   
 9. Wameiba Kura

  Wameiba Kura JF-Expert Member

  #9
  Dec 19, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 390
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tamko kali halina gharama yoyote, immediately Uongozi wa CDM led by Dr. Slaa or their Chief whip watoe tamko hatutavumilia huku PM anasema
  eti serikali itafuata taratibu za kisheria while huu ni uwizi wa macho, PM hana majibu as usual, back & forth, plse waokoeni wananchi msisahau nyie ni viongozi na ndio mliopata kura nyingi mno kila mtu anajua, be quick plse
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Dec 19, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,609
  Trophy Points: 280
 11. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #11
  Dec 19, 2010
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,784
  Likes Received: 2,681
  Trophy Points: 280
  Nadhani malunde-malundi yuko sahihi, labda "wao" wanaanza vita ya kipropaganda kwa kutoa kauli zenye utata ili CDM wakurupuke kuzijadili bila tafakuli waanzie hapo kuwabomoa kipropaganda, kwa sababu kauli ya " tutalipa deni la DOWANS kwa mujibu wa utawala wa sheria" nahisi imekaa kimtego.
   
 12. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #12
  Dec 19, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,077
  Likes Received: 4,662
  Trophy Points: 280
  There is no utawala wa sheria wala kauli za mtego hapa, hela hizi ni zangu na zako, za walipa kodi maskini wengi, CDM ndio wahusika as our representatives, they must respond kupiga hili, si swala la serikali isiyoaminika, isiyomtetea mnyonge na inakumbatia mafisadi, luxury life, etc, CDM ndio pekee
  watoe sauti kuu na ikibidi maandamano yawepo makubwa countrywide kama jamaa alivyosema, huu ni uwizi mkubwa sana
   
Loading...