Uchaguzi 2020 CHADEMA teteeni nafasi yenu ya KUB na ACT Wazalendo watoe Makamu wa Rais Zanzibar. Nafasi ya Rais CCM haipingiki

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,616
141,447
Nitoe tu angalizo kama ambavyo maalim Seif wa ACT Wazalendo ameona ni heri akainyemelea tena nafasi ya makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar.
CHADEMA pambaneni muitetee nafasi mliyonayo Bungeni ya KUB kwa sababu bado hamjawa na uwezo wa kutoa Rais wa JMT.

Kwa sasa Rais Magufuli hapingiki kwa nafasi ya Rais wa Tanzania na kule Zanzibar tume aliyoisusia Maalim Seif ni ile ile hata kama Jecha amestaafu na kurejea CCM.

Maendeleo hayana vyama!
 
Hili la kwamba wapinzani hasa cdm wasisimamishe mtu wa kushindana na Magufuli naona linarudiwa mara kwa mara, na hili halirudiwi kwa bahati mbaya. Ni kuwa Magufuli kuna mambo kweli kafanya vizuri, lakini wanaCCM na Magufuli mwenyewe, hayuko tayari kuingia kwenye ushindani wa kisiasa kwani hana uwezo wa kushindana kwa hoja.

Hivyo anajua akiingia kwenye ushindani wa kisiasa, atajikuta kwenye wakati mgumu kama ilivyokuwa kwa JK vs Slaa uchaguzi wa 2010. CCM hawako tayari kuona aibu na fedheha hii katika uchaguzi huu.
 
Kwani hiyo nafasi ya kub si mpaka itokee miujiza!! Sioni dalili za kushinda wabunge wengi kwa lipi walilofanya labda wakarudi Tena wengi bungeni? Labda wakazane kupata wabunge wawili watatu!!!
 
hamjawa na uwezo wa kutoa Rais wa JMT.
John, kwani aliyepo ana qualities zipi za urais ambazo mtanzana mwingine hana? Jiwe anafanya nini ambacho wewe huwezi kufanya?Alipita kwa ngekewa ya tukose wote siyo kuwa he had wxceptional capabilities ambazo wengine hawana! Labda roho ngumu ya kukosa ubinadamu wa akina Ben, Mawazo, Azory, coco bech sandarusi,,... labda hayo!
 
Chadema wapo bize na urais badala ya kuwa bize kusimika wagombea ubunge ambao watakua rahisi kuuzika kwa.wananchi
 
Hicho chama kilishakufa, KUB hajulikani maana hakuna chama chenye nguvu. ACT ni wadini sana na Zitto ni mchumia tumbo wa mabeberu lazima akose kura na watu wake lazima waangukie pua
 
Umepata picha gani hapo baada ya kuona jinsi walivyopokea salamu za Prof J?

Watu wanawakubali wapinzani bila unafiki Ila hawapati nafasi ya kuwasikiliza. Magufuli anatumia ulaghai majukwaani na wakati wa kampeni ataaibika sana kwani kwa sasa ukimjibu unakumbana na "uchochezi" lakini hapo hatakuwa jukwaani kama Rais bali mgombea na hata weza kupambana na hoja za kina Zitto, Lissu nk.

Bila wizi wa kura na ulaghai yale ya Malawi yanakuja na Magu anagalagazwa.
 
Kwani hiyo nafasi ya kub si mpaka itokee miujiza!! Sioni dalili za kushinda wabunge wengi kwa lipi walilofanya labda wakarudi Tena wengi bungeni? Labda wakazane kupata wabunge wawili watatu!!!
Lipi walilofanya? We njinga nini?(kwa sauti ya Tabu wa Kitimtim) kwani wao ndio wenye serikali?
Hivi uliona alivyokubalika Jana Prof J mbele ya Magu? Panapo fuka moshi .....! Watu watawaonyesha wanataka nini ikifika octoba
 
John, kwani aliyepo ana qualities zipi za urais ambazo mtanzana mwingine hana? Jiwe anafanya nini ambacho wewe huwezi kufanya?Alipita kwa ngekewa ya tukose wote siyo kuwa he had wxceptional capabilities ambazo wengine hawana! Labda roho ngumu ya kukosa ubinadamu wa akina Ben, Mawazo, Azory, coco bech sandarusi,,... labda hayo!
Ila hiyo roho ngumu kashindwa kwa Mtela. Labda alijua JoJo akifahamu kamfanyizia anaweza kunyimwa sukari guru!
 
Hili la kwamba wapinzani hasa cdm wasisimamishe mtu wa kushindana na Magufuli naona linarudiwa mara kwa mara, na hili halirudiwi kwa bahati mbaya. Ni kuwa Magufuli kuna mambo kweli kafanya vizuri, lakini wanaCCM na Magufuli mwenyewe, hayuko tayari kuingia kwenye ushindani wa kisiasa kwani hana uwezo wa kushindana kwa hoja.

Hivyo anajua akiingia kwenye ushindani wa kisiasa, atajikuta kwenye wakati mgumu kama ilivyokuwa kwa JK vs Slaa uchaguzi wa 2010. CCM hawako tayari kuona aibu na fedheha hii katika uchaguzi huu.
Alisikika Muimba kwaya Akisema
 
John, kwani aliyepo ana qualities zipi za urais ambazo mtanzana mwingine hana? Jiwe anafanya nini ambacho wewe huwezi kufanya?Alipita kwa ngekewa ya tukose wote siyo kuwa he had wxceptional capabilities ambazo wengine hawana! Labda roho ngumu ya kukosa ubinadamu wa akina Ben, Mawazo, Azory, coco bech sandarusi,,... labda hayo!
Hebu taja qualities za mtu mbadala wa John Mkuu katika hao waliokuzunguka au Wewe mwenyewe?

John yes alipita kwa ngekewa ila ya tukose wote ila kwa alichokifanya 5 years hakuna mwingine anaweza kujaribu hata kumsogelea kwa 50%
 
Hicho chama kilishakufa, KUB hajulikani maana hakuna chama chenye nguvu. ACT ni wadini sana na Zitto ni mchumia tumbo wa mabeberu lazima akose kura na watu wake lazima waangukie pua
Tueleze udini wa ACT WAZALENDO mkuu?
 
Back
Top Bottom