Chadema Tengeneza utaratibu mzuri wa kuchangiwa fedha na Watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema Tengeneza utaratibu mzuri wa kuchangiwa fedha na Watanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by rosemarie, Apr 14, 2012.

 1. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,743
  Likes Received: 832
  Trophy Points: 280
  Wakuu nipo Pretoria South Africa,hapa tumekutana na watanzania wengi sana wanaoishi huku,tumetembelea miji ya Johannesburg na Capetown kwa shughuli zetu za biashara,Watanzania wanaoishi hapa wamependa jinsi Chadema inavyotoa matumaini ya kuikomboa tanzania,Watanzania wengi wapo connected na television na radio zetu hasa ukizingatia technologia inakuwa haraka sana,maswali tuliyoulizwa ni vipi chadema itachangiwa fedha na Watanzania waishio nje ya nchi ambao wanashindwa kushiriki kwenye shughuli za mabadiliko moja kwa moja kwa kuwa wapo mbali,kwa mtazamo wangu binafsi nimeona hiyo ni point nzuri,Chadema itachangiwa vipi hela??system ya Chadema bado haijakaa vizuri,kuna haja ya Chadema kuangalia upya jinsi ya kutengeneza database itakayosaidia kuchangiwa fedha na watanzania wapenda mabadiliko na kuweka yale majina na michango kwenye system,kama mambo yatakwenda kama tunavyotegemea Chadema itashinda uchaguzi 2015 na kwa vyovyote vile itahitaji watanzania wa kufanya nao kazi,system nzima ya ccm lazima iondoke waingie watu wapya kabisa,naomba chadema iangalie hili,ikiwezekana kuna haja ya ku copy au kuiga walicho fanya ANC wakati wa ubaguzi,walichangiwa fedha nyingi wa wananchi wao waliokuwa wamesambaa dunia nzima na baada ya uchaguzi mkuu 1994 waliitwa kufanya kazi na serikali ya weusi,Chadema naomba mmbadilike ili chama kiweze kupanuka zaidi na kupata watu wenye idea nyingi na tofauti,kumbukeni ccm ikitoka kutakuwa na kazi kubwa ya ku-rebuild taifa letu lililoharibiwa na hao wasaliti wakubwa wa nchi yetu,Mungu bariki Tanzania Mungu bariki Chadema
   
 2. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,054
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Well said. Ngoja tumsubiri Dr Slaa aje alitolee ufafanuzi.
   
 3. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,187
  Likes Received: 4,541
  Trophy Points: 280
  Watanzania wengi wanaishi J,burg na Pretoria ni vibaka wa simu na laptop pamoja na kuuza unga kuweni makini sana napafahamu vizuri South Africa.
   
 4. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,716
  Likes Received: 955
  Trophy Points: 280
  umeshajiuliza kwa nini wamehama Bongo? Akili yako ndogo
   
 5. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Good idea. Viongozi wa CDM kama mnapita humu, chukueni haya mawazo na kuyafanyia kazi.
  Si lazima utoe strategy zenu kwa umma, lakini vitendo vitaonyesha ni jinsi gani mlivyo wasikivu wa kilio chetu sisi wananchi.
   
 6. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kila siku nakuambia, jifunze kutoka kwa watoto wa mzee mkapa, hawakuwa na kimbele mbele cha politics kama wewe, kipindi baba yao yuko rais walikuwa COOL, hatukuwasikia UVCCM au dodoma kwenye vikao vya chama, na mpaka leo wapo COOL... Mbona unakuwa mgumu kujifunza?
  Lkn 2015 si mbali, utatueleza tu huo ubilionea wako umeutoa wapi.
   
 7. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #7
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,187
  Likes Received: 4,541
  Trophy Points: 280
  Kwani South kuna wa Tanzania peke yao? wapo wa Nigeria, Mali, Senegal, Ghana, Kenya, Uganda, jiulize wamekwenda kufanyaje South Africa.
   
 8. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #8
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 11,827
  Likes Received: 1,273
  Trophy Points: 280
  Mbona chama chenu ni cha majambazi
   
 9. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #9
  Apr 14, 2012
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 891
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  "kuchangiwa fedha na watanzania wapenda
  mabadiliko na kuweka yale majina na michango
  kwenye system,kama mambo yatakwenda kama
  tunavyotegemea Chadema itashinda uchaguzi
  2015 na kwa vyovyote vile itahitaji watanzania
  wa kufanya nao kazi".
  Ndugu yangu unataka watu wapewe nafasi kwa sababu wametoa michango ya fedha!!!?
  Hii ni hatari sana na ndio imetufikisha hapa.
  Kuna watu hawana fedha lakini mawazo wanayo
  mazuri sana kuliko Hao wenye fedha, kwa mtizamo wako,wasipewe safari.
  Umejipambanua vizuri kuwa wewe ni mfanyabiashara,hivyo mkakati wako ni kuchangia Chama ili baadae ulipwe fadhila!!!
  CHADEMA ni chama cha ukombozi kwa masikini wa Tz.
  Kinahitaji fedha kujiendesha,lakini kwa utaratibu
  wako chama kitakufa siku Si nyingi.
   
 10. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #10
  Apr 14, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,240
  Likes Received: 233
  Trophy Points: 160
  Pia Joburg na capetown Watanzania wengi waliopo ni wauza mboga mboga na matunda. Ukienda mitaa ya rissik, long street, harrison na waterfront utawasikia wanavyokigonga kishwahili. Wabongo wanadharauliwa sana kule, bora hata wazimbabwe ambao ni madereva tax. Labda director1 atuambie hizo rand chache anazozipata kwenye kuuza mboga mboga zitakisaidiaje chadema.
   
 11. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #11
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,595
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ni kweli kabisa tunaomba chama muwe wabunifu watu wanawapenda sana tunataka tuwachangie kwa hali na mali tengeneze njia nzuri watu wako tayari. Halafu mnapaswa muwe na ofisi rasmi wilaya zote za tz, wanapeoble tupo tayari kwa kazi 1 kuing'oa ccm.
   
 12. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #12
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 11,827
  Likes Received: 1,273
  Trophy Points: 280
  Baba zenu ambao ndio wezi wa rasilimali zetu ndio wamefanya wazarauliwe lakini muda si mrefu itahamia kwenu mtakapo kuwa ni Chama pinzani dhaifu
   
 13. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #13
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,187
  Likes Received: 4,541
  Trophy Points: 280
  Ukitaka vitu vya wizi hapa Dar kama Loptop, iPhone, Blackberry, iPad, vinatoka South Africa kwa wa Tanzania wanaoshi huko.
   
 14. C

  Curriculum Specialist JF-Expert Member

  #14
  Apr 14, 2012
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 2,736
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Serikali yako ya ccm ndo imewafanya wawe vibaka kuko south kwahiyo si vibaya wakiwekeza mapato yao kuiangamiza ccm!
   
 15. Highlander

  Highlander JF-Expert Member

  #15
  Apr 14, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 3,094
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135


  Naomba kuchangia accademically--siyo politically. Kwa kuwa mimi si mwanasiasa. Wazo la kuichangia Chadema limekaa vizuri sana. Ila wazo la kuwaita watanzania waliopo nje ya nchi kuja kufanya kazi katika serikali itayoongozwa na Chadema linahitaji angalizo:

  ANC ilikuwa na virtual government nje ya nchi. Na asilimia kubwa ya viongozi katika hiyo virtual government walikuwa
  wamekuwa vetted wakiwa katika mapito makali sana yenye lengo la kujenga ukakamavu. Mtu anapokuwa vetted kwa ajili ya kufanya kazi katika serikali maana yake ni kwamba tabia yake imechunguzwa kwa kina sana na anajulikana kupita kiasi. CCM imekuwa ikitoa nafasi kwa watu kufanya kazi katika serikali bila kufanya vetting vizuri. Na hili haswa ndilo sababu kubwa ya kupata vilaza na wezi katika serikali. Nilikuwa karibu na mtu fulani 1995 baada ya uchaguzi uliomuweka Mkapa madarakani. Vyeo vilikuwa vinatolewa kwa kujuana kirafiki tu. Unakuta kilaza mmoja kwa kuwa tu ana mtu karibu na timu ya kampeni kesho huyooo--yupo ofisi ya waziri mkuu! Mwingine kwa sababu tu pengine alitoa uroda kwa mtu katika timu ya uchaguzi, kesho huyoo tayari keshapewa wilaya!

  Angalizo langu ni kwamba watanzania wenye nia njema na nchi yetu wachangie wind of change
  katika nchi yetu, lakini wasifanye hivi kwa tumaini la nafasi katika serikali mpya, kwani kwa kukaa kwao
  nje ya nchi, hiyo process ya vetting inaweza ikawa ngumu kidogo, na hivyo kuwafanya wasiwe candidate wazuri sana kwa uongozi mpya. Lakini pia itakuwa kama kununua nafasi katika serikali; which is NOT advisable.

  toeni bila strings. Na muwe open kuchukulika ama kutokuchukulika katika serikali mpya. Lakini ni vizuri kuweka msisito
  wakati mkifinance change, kuwa mnataka serikali adilifu katika mabadiliko haya. Kufanikisha hili indepth vetting is a must kwa kila mtu atayekuwa katika serikali mpya.
   
 16. k

  kagame Senior Member

  #16
  Apr 14, 2012
  Joined: Dec 6, 2008
  Messages: 159
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Bora yao hao walioamua kwenda kuiba kwa jirani na kuja kuimarisha uchumi wa nchi yao tofauti na wewe uliyechafuka kwa tuhuma za kujitajirisha kwa utajiri usiyo na mapato yakinifu, huna tofauti na kijana anayeiba ndani ya familia yao na kwenda kutawanya nje.
   
 17. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #17
  Apr 14, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,015
  Likes Received: 313
  Trophy Points: 180
  Watanzania wengi na si wote. Basi wachache kati ya hao walioko huko nje watatosha kuchangia. Lakini wizi mzuri ni upi? Wa kuiba kutoka nje kuleta ndani au wa kuiba ndani kupeleka nje kama anavofanya mjomba wako JK na Ngereja? Watanzania wanaiba Laptop na simu South Africa, then Makaburu yanaiba nini Geita kupela South? Iko siku itafika utajiona kuona una damu ya wangapi sababu ya kutetea madhambi labda uwe tayari freemason maada tayari huogopi damu bali ndicho kinywaji chako.
   
 18. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #18
  Apr 14, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,015
  Likes Received: 313
  Trophy Points: 180
  Ukitaka dhahabu nzuri kutoka Buzwagi, Geita, North Mara, yenye kiwango cha juu kutoka Tanzania unaipata wapi? South Africa kule inapelekwa na nani? Kama sio wewe kupiga piga makofi na kuvaa ki headphone kumsikiliza atakayeisema ccm na Jk. Dawa yenu nyie au mtakachoambulia sana sana ni Rambirambi kubwa kwenye familia zenu. Yeye akienda akapewa koleo la dhahabu akajua atakula na familia yake akitoka madarakani.....kimoyomoyo anawaambia Watanzania... to hel with their problems kwani tulizaliwa pamoja?......aaaaghhhh waende.....anaagiza mvinyo anakunywa lakini mwisho hauko mbali. Mungu hakuwa mjinga kutupa raslimali watanzania lakini zikaliwa na unaowatetea kila siku.........lakini sikulaumu sana maana inn most cases a woman is a recipient!.................
   
 19. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #19
  Apr 14, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,659
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  Hoja ni kuchangia CDM!
  Hayo mengine baadae....
  Unatakiwa mfumo mahsusi unaoendana na muendelezo wa M4C!
  Taarifa za muongozo na ufafanuzi wa masuala haya ziletwe na muwakilishi wa CDM hapa JF haraka iwezekanavyo.....
  Kweli kuna maswali mengi jinsi ya kuchangia mabadiliko sio kwa walio nje tu bali hata kwa walio hapa home.
   
 20. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #20
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,328
  Likes Received: 191
  Trophy Points: 160
  Mkuu ujumbe nadhani utawafikia maana Zitto, Mnyika, Michael Aweda, Nanyaro na wengineo ng member humu.

  Otherwise hata mimi nadhani bado cdm hawajaweka nguvu ya kutosha kwenye kuwashirikisha wananchi kuwachangia. Nilifurahi walipozindua M4C lakini iliishia pale na hakuna kilichoendelea! Nadhani wanahitaji kuongeza mbinu na nguvu!
   
Loading...