Uchaguzi 2020 CHADEMA, TBC TV wanawaharibia kampeni ya mgombea Urais wenu Tundu Lissu; chukueni hatua sasa na haraka kabla hawajaharibu zaidi!

Chadema watu hakuna kwenye mikutano ata nyie wenyewe mnalijua hilo ndio maana kutwa kupost video na picha za ccm.lakini ata hivyo si uwa hamtazami TBCccm leo imekuwaje
Tulitizama TBCCM na tumeona live,jiwe aliambiwa HATUKUTAKII!!!
Hapo mjini Bukoba.

Jamaa alikuwa ametafuta hela za tetemeko na za rambirambi,ndiyo kisa cha kukataliwa.

Kukataliwa kunaumaaa!!!!
 
Hata Millard ayo anafanya the same, namna anavyoandika kichwa cha habari za Lissu mtu timamu lazima ajiulize ninini shida ya Millard, i have nothing against Millard lakini aache huo ujinga wa kuripoti habari za TL kwa mtindo huo. Huyu ni media binafsi hatumlazimishi ila tunamuomba kama hajisikii kuripoti habari za TL aache!
Ni kusaga huyo, utakuta wameshapewa hela ya kutoonyesha habari za cdm.
 
Kumbe mnaangaliaga TBC!?.
hapa ndo unapoonekana utanzania wetu halisi.misimamo na hamasa za wanamitandao ni tofauti na jinsi walivyo kwenye maisha yao ya kilasiku,ni walaini zaidi ya keki ya mayai.

Nilikuwa kwenye utafiti...

Kwa hiyo, leo nimetazama kuona walivyobadilika baada ya kulialia sana baada ya kutengwa na CHADEMA...

Unfortunately, bado wameamua kuwa wajinga. Wameamua kuwa unethical & unprofessional....

In reality Mimi siyo mpenzi wala mtazamaji wa TV hii inayomtukuza mtu mmoja tu, Magufuli...
 
Tibisi ukweli na uhakika, mkuu kauchumi ka bundle kakiyumba tibisi inaangaliwa tu.......

Ni ngumu tibisi kufanya kama mnavyotaka hasa huku africa, ni chadema wenyewe ktk mazingira yaliyopo kuboresha idara ya habari...... Itapunguza hizi kelele
 
å Leo tarehe 16/9/2020 nimejikuta natazama taarifa ya habari ya saa 2usiku huu kwenye TV kupitia channel ya TBC....

å Taarifa ya kwanza ilikuwa ni kuripoti matukio ya kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka huu 2020 ya vyama tofauti tofauti...

å Wa kwanza kuripotiwa ni mgombea wa CCM, John Pombe Magufuli akiwa Bukoba, Kagera. Ripota wa taarifa hii, akatumia back video yenye nyomi kweli kweli na hatua kwa hatua akadadavua ujumbe na tukio alilokusudia hadhira ijue kwa ufasaha kabisa...

å Baadaye ikafuata taarifa ya mgombea Urais wa CHADEMA, Tundu Antipas Lissu akiwa huko mkoa wa Songwe....

å Hapa ndo mtu utachoka na kucheka kuliko kawaida kwa sababu kilichiripotiwa ni tofauti kabisa na hali halisi ilivyokuwa ktk mikutano yote ya leo. Hapa ndo unaiona "NIA OVU" ya TBC TV...

å Wanachofanya TBC ni ili mradi tu habari ya CHADEMA na Tundu Lissu imeonekana kwenye TV yao ikiwa ni kwa shingo upande tu ya kujibu lawama wanazorushiwa za upendeleo wanaoufanya waziwazi kwa CCM na mgombea wao John Magufuli...

å Alichofanya ripota wa TBC kwenye mikutano ya Tundu Lissu si kuripoti kampeni bali ni kupotosha kwa kutumia negative TV broadcasting propaganda....

å Mfano "back up video" aliyotumia ripota wa leo kule Songwe ni ya kuchekesha kuliko kawaida kinyume kabisa na hali halisi....!

å Yaani badala ya kuonesha umati wa watu waliohudhuria mkutano, kwa makusudi kabisa mwandishi anaelekeza camera yake mlimani eneo tupu lisilo na watu huku kwenye ripoti yake akisema

"....wakimsikiliza mgombea Urais huyo akisema.....!"

å Lengo la mwandishi ni ili kumfanya anayetazama TV ashangae hao watu wanaomsikiliza huyu mgombea wako wapi? Mbona ni mlima mtupu tu?

å Kwa mtazamo wangu, niwashauri CHADEMA kuwa, hakuna haja ya kuendelea kushirikiana na TBC kwenye kampeni zenu. Piga marufuku ripota wote wa TBC. Hawa ni maadui katika kambi yenu ya mapambano....

å Hawastahili kuambatana nanyi ktk mikutano yenu, hawana nia njema dhidi yenu, wako kwa ajili ya kufanya propaganda hasi dhidi mgombea wenu...

å Hawa watangazaji wa TBC ni aidha kwa kutojua au kwa makusudi kabisa na kwa "NIA OVU" dhidi ya CHADEMA na mgombea Urais Tundu Lissu wameamua kuwa unethical & unprofessional ktk tasnia ya habari. Kwanini mshirikiane na watu wa namna hii??

å Kwanini muendelee kuwa na waandishi au chombo cha habari cha namna hii chenye waandishi/watangazaji ambao unethical and unprofessional?

å Kwa hakika, uwepo wao kwenye kampeni zenu hauwaongezei chochote zaidi tu kwamba unawaharibia kwa kutoa picha hasi kwa wapiga kura dhidi ya kampeni na mgombea wenu....!

å Hamchachelewa kuchukua hatua kwa sababu BETTER LATE THAN NEVER...!!

Mimi kama mimi sikuafiki sana Mbowe kwenda kupatana na TBC,na hata kama wangeopatana angewaambia kuwa wamesameheana, lakini hawako tayari TBC watangaze taarifa zao.
 
Acheni unafki, lini mmeanza kuangalia TBC? si huwa mnaiita tbccm
Sasa mheshimiwa, unataka watu wakiangalia TBC wawe wanakujulisha ili ujue kwamba sasa wameanza kuangalia TBCCM,??
Weka namba yako ya simu hapa, kesho nikiangalia taarifa ya habari ya TBCCM nakujulisha kwa sms.
 
Pembe la ngo'mbe halifichiki!

Ni ujinga kuanzisha malumbano na Vyombo vya habari!

Sasa shida yenu ni nini?
Wakiripoti robo ya mahudhurio ya watu mkutanoni ndio imekuwa hivyo sasa?
Hii ni Sawa na wanandondi mmoja katandikwa ya sikioni Hadi damu inamtoka, halafu aliyepigwa Anasema hajapigwa!
Hicho ndicho mnabishania na TBC,

Chadema wote mnajua mnajaza nyomi, TBC Anasema hamjazi?

Baking na ukweli wenu, shida iko wapi? Au ni kweli kwamba hamjazi?
 
Walishamnunua siku nyingi huyo sasa hivi anatumika ili kutimiza kile maccm wanachokitaka toka kwake.

Hata Millard ayo anafanya the same, namna anavyoandika kichwa cha habari za Lissu mtu timamu lazima ajiulize ninini shida ya Millard, i have nothing against Millard lakini aache huo ujinga wa kuripoti habari za TL kwa mtindo huo. Huyu ni media binafsi hatumlazimishi ila tunamuomba kama hajisikii kuripoti habari za TL aache!
 
Nmeona pia kupitia ITV .

Kwa ufupi huu uhuni Hadi Millard Ayo anao pia.


Unakuta Lissu anapouliza swali anataka mwitikio wa watu... Wao wanaiminya sauti ile, ili ionekane kama ameongea Pumba.


Lissu anaongea, wanaonyesha picha za pembezoni sanaaa ambako unakuta ni mwananchi mmoja mmoja.



NADHANI NI WAKATI MWAFAKA, KUWAFUKUZIA MBALI TBC NA ITV ,AYO .
Sijaona shida kwa ITV, Mabele Makubi anafanya vizuri sana kwenye mikutano ya CDM
 
Back
Top Bottom