Arushaone
JF-Expert Member
- Mar 31, 2012
- 15,135
- 13,254
å Leo tarehe 16/9/2020 nimejikuta natazama taarifa ya habari ya saa 2usiku huu kwenye TV kupitia channel ya TBC....
å Taarifa ya kwanza ilikuwa ni kuripoti matukio ya kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka huu 2020 ya vyama tofauti tofauti...
å Wa kwanza kuripotiwa ni mgombea wa CCM, John Pombe Magufuli akiwa Bukoba, Kagera. Ripota wa taarifa hii, akatumia back video yenye nyomi kweli kweli na hatua kwa hatua akadadavua ujumbe na tukio alilokusudia hadhira ijue kwa ufasaha kabisa...
å Baadaye ikafuata taarifa ya mgombea Urais wa CHADEMA, Tundu Antipas Lissu akiwa huko mkoa wa Songwe....
å Hapa ndo mtu utachoka na kucheka kuliko kawaida kwa sababu kilichiripotiwa ni tofauti kabisa na hali halisi ilivyokuwa ktk mikutano yote ya leo. Hapa ndo unaiona "NIA OVU" ya TBC TV...
å Wanachofanya TBC ni ili mradi tu habari ya CHADEMA na Tundu Lissu imeonekana kwenye TV yao ikiwa ni kwa shingo upande tu ya kujibu lawama wanazorushiwa za upendeleo wanaoufanya waziwazi kwa CCM na mgombea wao John Magufuli...
å Alichofanya ripota wa TBC kwenye mikutano ya Tundu Lissu si kuripoti kampeni bali ni kupotosha kwa kutumia negative TV broadcasting propaganda....
å Mfano "back up video" aliyotumia ripota wa leo kule Songwe ni ya kuchekesha kuliko kawaida kinyume kabisa na hali halisi....!
å Yaani badala ya kuonesha umati wa watu waliohudhuria mkutano, kwa makusudi kabisa mwandishi anaelekeza camera yake mlimani eneo tupu lisilo na watu huku kwenye ripoti yake akisema
"....wakimsikiliza mgombea Urais huyo akisema.....!"
å Lengo la mwandishi ni ili kumfanya anayetazama TV ashangae hao watu wanaomsikiliza huyu mgombea wako wapi? Mbona ni mlima mtupu tu?
å Kwa mtazamo wangu, niwashauri CHADEMA kuwa, hakuna haja ya kuendelea kushirikiana na TBC kwenye kampeni zenu. Piga marufuku ripota wote wa TBC. Hawa ni maadui katika kambi yenu ya mapambano....
å Hawastahili kuambatana nanyi ktk mikutano yenu, hawana nia njema dhidi yenu, wako kwa ajili ya kufanya propaganda hasi dhidi mgombea wenu...
å Hawa watangazaji wa TBC ni aidha kwa kutojua au kwa makusudi kabisa na kwa "NIA OVU" dhidi ya CHADEMA na mgombea Urais Tundu Lissu wameamua kuwa unethical & unprofessional ktk tasnia ya habari. Kwanini mshirikiane na watu wa namna hii??
å Kwanini muendelee kuwa na waandishi au chombo cha habari cha namna hii chenye waandishi/watangazaji ambao unethical and unprofessional?
å Kwa hakika, uwepo wao kwenye kampeni zenu hauwaongezei chochote zaidi tu kwamba unawaharibia kwa kutoa picha hasi kwa wapiga kura dhidi ya kampeni na mgombea wenu....!
å Hamchachelewa kuchukua hatua kwa sababu BETTER LATE THAN NEVER...!!
Naunga mkono hoja.
Kwa kuongeza tu, wafanyakazi wa TBC TV walioko field huwa wanachukua matukio yote kama yalivyo ila habari huhaririwa kishetani 100% ikifika srudio na wanaofanya hiyo kazi sio jopo la tbc peke yao...kuna external force (amri kutoka juu) ili kuaminisha watazamaji kuwa wanachokiona ndivyo kilivyo.
Wasichojua ni kuwa technology haidanganyi.
Kabla hawajarusha taarifa ya habari 68% ya watanzania walishaona through mobile phones na YouTube channels na sana share mpaka kesho yake 89% ya watanzania wameshaona kila kitu, so hao TBC ndio wanaonekana wajinga kwa kupotosha habari.
Zama za kudanganyana zilishasahaulika kitambo sana.
Huu uhariri ndio unaotakiwa kumfurahisha mgombea wa chama chao.
Endapo Lissu/CHADEMA watashinda uchaguzi huu Dr Ryoba ataficha wapi USO wake?
This is what they call DICTATORSHIP MENTALITY ya CCM leaders.
Ila wajue tu hakuna marefu yasiyo na mwisho.
Mungu sio kuwa haoni vilio vya watu wake ila the right time is coming soon.