Chadema tawi la magadirisho limepata mwenyekiti mpya ijumaa 27.07.2012 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema tawi la magadirisho limepata mwenyekiti mpya ijumaa 27.07.2012

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Emashilla, Jul 28, 2012.

 1. Emashilla

  Emashilla Senior Member

  #1
  Jul 28, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jumamosi tarehe 14 Julai, 2012 Mwenyekiti wa tawi la Magadirisho Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, Nuru Maeda alihamia Chama Cha Mapinduzi. Tawi hili lilimpoteza kiongozi huyu aliyejipatia umaarufu mkubwa baada ya kutekwa na kuteswa na watu waliodaiwa kuwa ni vigogo wa CCM Katika Kitongoji cha Magadirisho, Kata ya Usa-River. Tukio ambalo lilitokea mwezi Machi, 2012.
  Lakini Nuru Maeda ameamua kwenda kwa waliomteka na kudai amefanikiwa kuibomoa ngome ya Chadema katika wilaya ya Arumeru. Jambo hili limebainika kuwa si la kweli, Ijumaa 27 Julai, 2012 wakati CHADEMA walipokutana ili kumtambulisha Mwenyekiti wao mpya wa tawi la Magadirisho kuziba nafasi iliyoachwa wazi. Wanachama wengi walihudhuria kikao cha jana; jambao lililodhihirisha kwamba Ngome ya CHADEMA ni imara.
  Wananchi zaidi ya 200 waliomba kupatiwa kadi za CHADEMA. Watu walishangaa kugundua kuwa watu 15 waliotajwa kujiunga na CCM hivi karibuni walikuwa ni watu waliopewa kadi za CCM ingawa walikuwa na kadi zao za awali za Chama cha Mapinduzi. Mmoja alirudisha kadi mbili za CCM na kumkabidhi Kaimu Mweyekiti wa Kata ya Usa-River ambaye ndiye alikuwa mwenyekiti wa kikao hiki cha ndani cha CHADEMA.
  Mwenyekiti mpya aliwataka wananchi wasisikitike kuondoka kwa Nuru kwani hakuwa mwenye nyumba bali alikuwa ni mwashi(Fundi Ujenzi) ambaye amemaliza kujenga nyumba nzuri iitwayo CDM na kuikabidhi kwa mwenye nyumba ambao ni wanachama wa CDM. Hana anachodai zaidi ya kusifu kazi yake nzuri aliyoifanya ya ujenzi wa nyumba.
  CHADEMA MWENDO MDUNDO

  PEOPLE'S POWER!
   
 2. sodeely

  sodeely Senior Member

  #2
  Jul 28, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Hana lolote ni mnafiki tu, nyie pigeni kazi
   
 3. maria pia

  maria pia JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 516
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  imekula kwake,njaa mbaya
   
Loading...