CHADEMA Tanga na Mbeya wapinga Zitto kuvuliwa uongozi. Mapigano yaibuka

utaifakwanza

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
14,193
2,812
Kundi la vijana wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Zitto jijini Mbeya wanadaiwa kurushiana makonde na viongozi wa Chadema katika ofisi ya chama hicho Wilaya ya Mbeya Mjini kwa madai ya kutofautiana msimamo kuhusiana na uamuzi wa Kamati Kuu.

Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mbeya Mjini, David Mwambigija maarufu kwa jina la ‘Mzee wa Upako’, alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo juzi mchana.
Mwambigija alisema kuwa
chanzo cha vurugu hizo ni vijana zaidi ya 18 wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Zitto kuanza kufanya vikao vya siri mjini Mbeya kwa nia ya kupinga uamuzi wa kumvua madaraka zitto na wenzake.

Alisema uongozi wa chama ngazi ya wilaya ulipopata taarifa hizo alizodai kuwa ni za kiintelijensia na kuwa yeye (Mwambigija) ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya chama hicho wilaya, aliamua kuaandikia barua ya kuwaita ofisini kwa lengo la kuwahoji.

Alisema vijana hao walipofika ofisini kwake huku wajumbe wa Kamati Tendaji wakiwa tayari wameketi kwa ajili ya kuwahoji, waliingia ndani ya ofisi na kulazimisha wahojiwe kwa pamoja badala ya kuhojiwa mmoja mmoja.

Alisema walipotakiwa watoke nje ili kila mmoja ahojiwe kwa wakati wake, waligona na kukataa kutoka ofisini na ndipo yeye kama Mwenyekiti alipoamuru kikosi cha ulinzi wa chama hicho maarufu kwa jina la Red Bridged kuwatoa nje kwa nguvu na ndipo vurugu hizo zilipoanza.

“Ni kweli kumetokea vurugu kubwa ofisini kwetu wakati kikao cha kamati ya utendaji kikihitaji kuwahoji vijana wanaoendesha vikao vya siri kutaka kukihujumu chama kutokana na uamuzi wa Kamati Kuu kumvua Zitto madaraka, tumepata taarifa hizi kwa njia zetu za kiintelijensia kuwa vijana hawa wapo kwenye kundi la Zitto,” alisema Mwambigija.

Hata hivyo, Mwambigija alipotakiwa na gazeti hili kuonyesha uthibitisho juu ya tuhuma dhidi ya vijana hao, alisema kuwa ushahidi bado ni siri kwa vile wametumia njia zao za kiintelijensia kubaini mtandao wa vijana hao.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Mkoa wa Mbeya, Joseph Kasambala ambaye ni mmoja wa vijana walioitwa kuhojiwa na kamati ya utendaji alikanusha madai hayo.

Alisema chanzo cha vurugu hizo ni Kamati hiyo kumuita na kutaka kumuhoji kinyume cha katiba ya Chadema yeye (Kasambala) ambaye ni kiongozi wa mkoa, hivyo hawezi kuhojiwa wala kuwajibishwa na kamati hiyo ambayo ni ngazi ya wilaya.

Alisema kuwa Katiba ya Chadema inaeleza wazi kuwa kingozi wa mkoa mamlaka yake ya nidhamu ni Kamati Kuu ya Chadema Taifa, hivyo kitendo cha ngazi ya wilaya kumuita na kutaka kumuhoji ni ukiukwaji wa Katiba.

“Mimi baada ya kupata barua ya kuitwa na Kamati hiyo ikinieleza kuwa nina tuhuma ambazo hazikuandikwa kwenye barua waliyoniletea, nilikwenda ofisini ili nipewe tuhuma zangu kwa maandishi kama ambavyo Katiba inaelekeza, lakini nikashangaa eti wanataka wanihoji, nikakataa walipotaka kunishinikiza vijana wakawajia juu wakipinga nisidhalilishwe na ndipo vurugu zile zilipoanza,” alisema Kasambala.

KATIBU TANGA AHOJI

Baadhi ya viongozi wa Chadema mkoa wa Tanga, wamehoji maamuzi ya kumvua madaraka Zitto na wenzake.

Ka
tibu wa Chadema Wilaya ya Tanga, Harid Rashid, alisema jana kuwa hakubaliani na maamuzi hayo.

Rashid ambaye aliongozana na mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa, Hussein Baruti na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Wilaya ya Tanga, Mohamed Aufi, alisema
kuwavua nyadhifa viongozi hao ni uonevu kwa kuwa hawaoni kosa walilolifanya
.

Alisema kuwa Kamati Kuu ilikuwa na njia nyingi za kulipatia ufumbuzi jambo hilo badala ya kuwavua uongozi.

Alisema kuwa wameamua kuwa wazi kuhusiana na tukio hilo kutokana na ukweli kuwa Zitto ni mtu muhimu katika uongozi wa chama.
 
Hawa wanao mtetea Zitto wanajua ni mara ngapi ameshaleta mtafaruku ndani ya chama au wamekaa tu kupinga? Ni byema wafanye utafiti kwanza badala ya ushabiki usio na tija kwa Chama
 
Kosa kubwa ambalo litakizika chadema ni kuacha wasaliti kupitia kile kinaitwa "suluhu" na "busara" badala ya kufuata katiba na kanuni za chama zinasemaje..huu ni mtazamo wangu
 
Msaliti nambari moja ni Mbowe kwa kusaliti ndoa yake. Pia yumo Dr Slaa kwa kusaliti kanisa, CCM na ndoa yake
 
Ni wazi kwamba Chadema ni chama muhimu kwa wakati tuliopo, lakini pia tukubali kwamba Zitto ni mtu muhimu sana kwa ustawi na uongozi ndani ya wa Chadema. Wasiotaka kuamini hili wana matatizo katika oblangata zao. Kwa sisi tuliokuwa watu wazima wakati wa kupanda na kuanguka kwa NCCR tuna mifano ya dhahiri juu ya hili. Suluhu ya kudumu ni Zitto ndani ya chama si nje ya chama kama wengi wanavyotumia ushabiki.
 
Msaliti nambari moja ni Mbowe kwa kusaliti ndoa yake. Pia yumo Dr Slaa kwa kusaliti kanisa, CCM na ndoa yake

Kusaliti ndoa kuna uhusiano gani na chama...kuna viongozi wangapi ccm wameacha wake zao, waume zao lakini wanachapa kazi....chukulia JK watoto wake wote ni kutoka kwa mam Salma?
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom